ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 21, 2018

KUKATIKA UMEME KWENYE CHANZO CHA MAJI CAPRI-POINT

TAARIFA KWA UMMA

KUKATIKA UMEME KWENYE CHANZO CHA MAJI CAPRI-POINT

MWAUWASA inawataarifu wateja na wakazi wa Jiji la Mwanza kuwa mnamo Saa 7:00 Usiku wa kuamkia leo umeme ulikatika kwenye chanzo cha maji cha Capripoint na hivyo kusababisha mitambo kuzimika na uzalishaji wa maji kusimama. 

Kufuatia hali hiyo, kutakuwa na upungufu wa maji kwenye maeneo yote ya Jiji la Mwanza na viunga vyake.

Hata hivyo, Mamlaka inaendelea kuwasiliana na TANESCO ili kubaini hatua zinazochukuliwa kurejesha huduma ya nishati ya umeme katika hali yake ya kawaida.

Mamlaka inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza. Hali itarejea kama kawaida mara baada ya huduma ya nishati kurejea.

Imetolewa Tarehe 21 Novemba, 2018* na: 
………………………………….
OFISI YA UHUSIANO
MWAUWASA

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.