ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 24, 2017

KATIBU MKUU MAMBO YA NDANI AENDESHA KIKAO CHA IDARA ZA WIZARA HIYO JIJINI DAR ES SALAAM


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akiongoza kikao cha ndani kilichoshirikisha Idara zilizopo ndani ya wizara.Kikao hicho kimefanyika  katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamishna wa Jeshi la Magereza Divisheni ya Utawala na Fedha,Gaston Sanga, akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, wakati wa  kikao cha ndani kilichoshirikisha Idara zilizopo ndani ya wizara.Kikao hicho kimefanyika  katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kamishna  wa Fedha Jeshi la Polisi  Albert Nyamuhanga.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke na Afisa Tawala wa Idara hiyo,Jenita  Ndone(Kulia), wakifuatilia kwa makini kikao cha ndani cha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Regasira (hayupo pichani) .Kikao hicho kimefanyika  katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Maafisa kutoka idara ya Uhamiaji wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakitolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira(hayupo pichani) wakati wa  kikao cha ndani kilichoshirikisha Idara zilizopo ndani ya wizara. Kikao hicho kimefanyika  katika ukumbi wa wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


WEMA SEPETU RASMI AHAMIA CHADEMA KUTOKA CCM

Lady Super Star wa Bongo movie @wemasepetu leo rasmi amekihama Chama cha Mapinduzi CCM na kutinga CHADEMA.

Star huyo mwenye ushawishi kwa jamii aliyetumikia CCM kwa kipindi kirefu hasa kampeni za uchaguzi mkuu 2015 kupitia Movement ya 'Mama Ongea na Mwanao' iliyokuwa na jukumu la kutia ushawishi kwa wanawake kukimini kwa muhula mwingine, Wema amewaambia waandishi wa habari kuwa kuhama kwake hakujashawishiwa na fedha wala rushwa ya aina yoyote zaidi ya maamuzi binafsi na namba moja ya yote ni suala la Demokrasia kuminywa. Zaidi cheki na #www_gsengo_blogspot_com

MKUU WA KAMPUNI INAYOUNDA SIMU ZA BEI NAFUU INDIA AKAMATWA.

Bw Mohit Goel

MKURUGENZI wa kampuni ya Ringing Bells, kampuni ya India ambayo imedai kwamba inauza simu ya bei nafuu zaidi duniani, amekamatwa kwa madai ya ulaghai.

Mohit Goel alikamatwa baada ya kampuni moja inayosambaza simu hizo kwa wauzaji kudai kwamba ilikuwa haijapokea simu ambazo ilikuwa imelipia.

Simu hiyo ya Freedom 251, ambayo bei yake ni rupia 251 ($3.70; £3), ilianza kuuzwa Februari 2016.



Lakini ingawa wateja wengi walipokea simu walizoagiza, Ringing Bells imedaiwa kutotimiza maombi yote ya ununuzi wa simu hizo.

Kampuni ya Ayam Enterprises, imesema ililipa rupia 3m ($45,000; £35,800) baada ya Bw Goel kuishawishi ifanye biashara ya kusambaza simu hizo.

Lakini inadai ilipokea simu za thamani ya rupia 1.4m pekee na wafanyakazi wake walitishiwa walipodai "pesa tena na tena".

Msemaji wa polisi Rahul Srivastava amethibitishia BBC kwamba Bw Goel amekamatwa na atafikishwa kortini baadayek Ijumaa.

"Malalamiko mengine kadha sawa na hayo yamewasilishwa kutoka maeneo mengine ya jimbo. Tunataka kuyachunguza kwa kina," amesema.

"Ni muhimu kwetu kufichua sakata hizi kwa sababu watu wasio na hatia hupoteza pesa zao walizotolea jasho."

UTAFITI WA VIASHIRIA NA MATOKEO YA UKIMWI KUFANYIKA MKOANI GEITA.

Afisa mawasiliano na umasishaji wa jamii la haika,Mihayo Bupamba akitoa maelekezo kwa wajumbe wakati wa Mkutano huo.

Afisa mawasiliano na umasishaji wa jamii la haika,Mihayo Bupamba,akitoa elimu kwa wajumbe juu ya zoezi la utafita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akitoa takwimu za Ukimwi zilivyo katika hapa nchini.

Wajumbe wakifatilia Mkutano.

Mkuu wa Mkoa wa Geita akiendelea kutoa maelezo.

Wajumbe wakikao wakifatilia.


IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE 

Wananchi Mkoani Geita,wametakiwa kutoa ushirikiano wa karibu kwa watafiti wa  viashiria na matokeo ya ukimwi kwa mwaka 2016 ambao watafika kwenye maeneo  12 ambayo yamepangwa kufanyiwa utafiti.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga wakati wa Mkutano wa wadau wa utafiti  wa viashiria na matokeo ya ukimwa ya mwaka 2016 uliofanyika kwenye ukumbi wa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa alisema  kiwango cha maambukizi kuwa kwasasa maambukizi yamepungua kwa asilimia mbili hali ambayo imesaidia kuhifanya Tanzania kuonekana kuwa chini katika ukanda wa jangwa la sahara.

“Kiwango cha maambukizo ya VVU katika tafiti zilizopita kinaonekana kupungua kutoka asilimia 7 mwaka 2003 mpaka asilimia 5.1 mwaka 2011. Taarifa hii inaonyesha kuwa juhudi hizo za Serikali zimeiwezesha Tanzania kupunguza kiwango cha maambukizo ya VVU kwa asilimia mbili na kuifanya Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi zenye kiwango cha chini cha maambukizo kati ya nchi za kusini mwa jangwa la Sahara ambapo nchini nyingi za ukanda huu zina kiwango cha maambukizo cha zaidi ya asilimia 10”Alisema Kyunga

Kwa upande wake afisa mawasiliano na umasishaji wa jamii la haika,Mihayo Bupamba ameelezea kuwa katika mikoa ambayo wamepita wamepata ushirikiano wa mwitiko mkubwa kutoka kwa wananchi ambao walikuwa wakiwafikia kwaajili ya shughuli ya upimaji.

“Kiukweli mikoa ambayo tumepita kwaajili ya zoezi hili tumepata ushirikiano mkubwa sana changamoto hazikosekani tulikutana na changamoto baadhi ya watu ambao walikuwa wameandikishwa kukosekana kwenye makazi yao kwa maana ya kwamba wameama makazi"Alisema Bupamba.

Pamoja na hayo utafiti huo utasaidia kukusanya taarifa za upatikanaji  na utumiaji wa huduma zitolewazo katika kudhibiti maambukizo ya  VVU na Ukimwi na vile vya tabia hatarishi vinavyochangia maambukizo ya VVU.

Utafiti wa namna hiyo ni wa awamu ya nne kufanyika nchini ,unaoangalia zaidi maswala ya afya ambapo utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2003/2004,wa pili ulifanyika 2007/2008 na utafiti wa tatu ulifanyika 2011/2012

VYUO VIKUU VYAISHANGAA TCU, NI BAADA YA KUTANGAZA WANAFUZI WASIO NA SIFA,

SIKU moja baada ya Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) kutangaza majina ya wanafunzi zaidi ya 8,436 wa elimu ya juu wasio na sifa ya kusoma kiwango hicho cha elimu, baadhi ya wakuu wa vyuo hivyo wameishukia tume hiyo kwa kusema yenyewe ndiyo iliyodahili wanafunzi huku yenyewe ikisema iliratibu tu zoezi hilo.

Taarifa ya tume hiyo iliyotolewa Februari 20 mwaka huu na kuwekwa kwenye tovuti yake, ilisema majina hayo yanatoka kwenye vyuo 52 ambavyo uhakiki wa wanafunzi wake umekamilika na kwamba wanafunzi hao wanatakiwa kuthibitisha sifa zao kabla ya 28 Februari, 2017.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, wanafunzi ambao hawatafanya hivyo hawatatambuliwa na tume hiyo na  hivyo kukosa sifa za uanafunzi.

CBE

Mkuu wa Chuo cha Biashara (CBE), Profesa Emmanuel Mjema, alisema wao walipelekewa taarifa  na TCU kwamba  kunatakiwa kufanyika kwa uhakiki wa wanafunzi wao na miezi miwili iliyopita wakaandaa taarifa hizo na kuziwasilisha kwao.

Alisema alishangaa  kuona idadi ya wanafunzi  476 kuambiwa kuwa  hawana sifa,  jambo ambalo alisema ni la kushangaza.

Alisema ni makosa  kusema wanafunzi hao hawana sifa  wakati  wanakidhi vigezo, huku akisema kuwa  hali hiyo inatilia shaka.

“Yani ni hivi wewe umeniletea wanafunzi  na  nimewapokea halafu tena  unasema huwatambui. Hayo ni makosa yao nafikiri katika kuhakiki mambo yao kwa ufasaha ,’’alisema Profesa Mjema .

Alisema taarifa zao wanazo miezi miwili iliyopita na hakuna hata mwanafunzi mwenye matatizo katika hayo majina waliyoyataja huku akihoji na kushangaa kuwa sijui imekuwaje.

Naibu Makamu  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)  Taaluma, Prof.  Frolence Luoga, alisema chuo chake hakina tatizo na kwamba wanatoa elimu kwa kiwango cha ubora unaotakiwa.

Alisema wanaprogramu zilizothibitishwa na TCU na wanafunzi wao wamedahiliwa na kuthibitishwa pamoja na kufanyiwa ukaguzi, hivyo ameishangaa TCU kuja na taarifa hiyo.

Alisema lakini kuna wanafunzi ambao walidahiliwa pia siku za nyuma mfumo wa udahili haukuwa wa kupitia TCU  na kabla hawajaanza udahili wa pamoja waombaji  walikuwa wakifika chuoni hapo moja kwa moja  wakitokea kidato cha sita na wengine  vyuoni moja kwa moja na kujiunga .

Alisema wanafunzi wengine pia  waliingia vyuoni hapo kwa kutumia program maalum ambazo zilikuwepo zaidi ya miaka 40 iliyopita.

SAUT
Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Agustino  (SAUT) Dk. Padre Thadeus Mukamwa, kilichotajiwa wanafunzi wake 1,046  kukosa sifa amesema huo ni uonevu mkubwa na kuharibiana sifa za vyuo.

Alisema TCU  ina sheria zake na kabla ya kuwatangaza wanafunzi hao walitakiwa kuweka bayana kwamba wamekosa wao  kwa kuwa udahili wote umefanywa na wao wenyewe.

Alisema walikuwa na utaratibu hata kabla majina hayo hayajapitishwa na TCU wanakutana wakuu wote wa vyuo  vyote nchini, Dar es Salaam, wanafanya mkutano wa pamoja na majadiliano kwa kuangalia historia ya vyuo vyao nakisha kudahili wanafunzi.

JEMBE FM Kupitia kipindi cha KAZI NA NGOMA imezungumza na Afisa Habari wa Chuo Cha SAUT Living Komu na hapa anajibu swali kwanini watu wasikilaumu chuo hicho kwa kuchukuwa wanafunzi wasio na sifa. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.
Na hapa anatoa rai kwa wanafunzi walioainishwa majina yao wakitajwa kuwa hawana sifa. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA
.


Kwa mujibu wa Dr. Mukamwa anasema kuwa walipata  taarifa kutoka TCU wakiambiwa  vigezo vya wanafunzi hao ni questionable kwa kudai kuwa namba za wanafunzi hao hazieleweki  wengine kuonyesha walisoma nje.

Alisema inawashangaza  kwa kuwa TCU ndio wanaofanya utaratibu wote na hata kwa kupokea kiasi cha shilingi 50,000 kutoka kwa wanafunzi hao kwa ajili ya uhakiki.

“Sasa sijui fedha walizokuwa wakipokea ilikuwa rushwa au laa na kama waliwapitisha wanafunzi hao walitoa rushwa kwanini walipokea fedha hizo,” alisema.

Alisema kuna wanafunzi  wengine tayari wamemaliza kama kuna matatizo walitakiwa kuwa wanasema na kufanyiwa marekebisho  lakini si kuwaambia  kuwa hawana vigezo.

“TCU  inakusanya data sasa wanashindwa kufanya uhakiki matokeo yao wanaharibu sifa za vyuo, kutoa lawama , wanaharibu muda wa wanafunzi ,fedha za mikopo pia,” alisema.

Alisema chuo hata siku moja hakitoi mikopo ni wao bodi ya mikopo  ambao baada ya kuona wanastahili waliamua kuwapa mikopo hiyo leo kusema hawana sifa hawaoni kwamba wanaharibu sifa za vyuo  na kuwachanganya  wanafunzi bila kujali na wao ni binadamu pia.

Akizungumzia kauli za wakuu wa vyuo hivyo,  Ofisa Habari wa TCU, Erdward Mkaku, alisema hakuna mahali wamesema kuwa  wanafunzi hawana sifa bali tangazo limesema kwamba zoezi la uhakiki wa sifa limekamilika.

“Hakuna mahali tumesema  wanafunzi hawana sifa, tangazo  letu linasema zoezi la uhakiki limekamilika  na kuna wanafunzi ambao wamedahiliwa katika  programu  ambazo hawana sifa nazo,’’ alisema.

Alisema orodha yote iliwasilishwa vyuo husika na kwamba kilichobakia sasa ni kwamba watakaojiona waende kwa kiongozi wao wa taluuma wa chuo chake kwa uhakiki .

Ofisa huyo alisema TCU inafanya kazi ya kuhakiki, lakini vyuo ndivyo  vinavyodahili.

DEMOCRATS: TUTAANZISHA MCHAKATO WA KUMNG'OA MADARAKANI TRUMP.






WABUNGE na wanasiasa wa chama cha Democrat nchini Marekani wanasema mienendo ya Rais wa nchi hiyo Donald Trump katika muda wa wiki tatu zilizopita imeibua uwezekano kuanzishwa mchakato wa kumng'oa mamlakani rais huyo.

Katika mahojiano na shirika la habari la CNN jana usiku, Mwakilishi wa Minnesota wa chama cha Democrat, Keith Ellision, alisema mienendo ya Trump yakiwemo matamshi yake ya kugongana ni baadhi ya mambo aliyoyafanya rais huyo wa Marekani chini ya mwezi mmoja, ambayo yanatia nguvu hoja ya kuanzishwa mchakato wa kumuondoa ofisini mara moja.


Sheria ya kibaguzi dhidi ya Wahajiri ni moja ya hoja za Democrat.
Ellison, ambaye anawania kuwa kinara wa Chama cha Democratic nchini Marekani amesema lengo lao la kuweka wazi suala la kuanzishwa harakati za kumbandua mamlakani Trump limetokana na ukweli kuwa, mfanyabiashara huyo tajiri amekiuka mara kadhaa misingi ya katiba na hivyo hafai kuendelea kuongoza.

Amesema kimsingi jambo ambalo limewafanya waanzishe mchakato huo, ni kwa ajili ya kuinusuru hadhi na heshima ya Ofisi ya Rais.

Wiki iliyopita, Kevin Barrett, mchanganuzi wa masuala ya siasa na mwandishi wa habari wa Marekani alisema matamshi ya kukinzana yanayotolewa mara kwa mara na Rais Donald Trump na hususan matamshi aliyoyatoa hivi karibuni dhidi ya Iran yanadhihirisha kuwa bilionea huyo ana matatizo ya kiakili.

Mijadala na minong'ono inaendelea kufanyika katika kona mbali mbali za nchi kuhusu hali ya kiafya ya Trump, baadhi ya wanasaikolijia wakisema kuwa rais huyo wa Marekani anahitaji matibabu ya haraka kabla ya mambo kuharibika zaidi. 

7 WAKAMATWA NA DAWAZA LULEVYA MWAZA.

WATU saba (07) wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kupatikana wakiwa na dawa za kulevya zinazodhaniwa kuwa ya heroine kiasi cha kete 32, bhangi kilo mbili na nusu na misokoto 75 ya bangi, wilayani Nyamagana, Mkoani Mwanza.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Naibu Kamishina wa Polisi Ahmed Msangi amesema tukio hilo limetokea tarehe 22.02.2017 majira ya saa 4 asubuhi katika maeneo ya katikati mwa jiji la Mwanza.

Kamanda Msangi amesema kuwa polisi bado wapo katika mahojiano na watuhumiwa wote saba, ili kuweza kubaini mtandao wa watu wanaoshirikiana katika biashara hiyo haramu ya dawa za kulevya na kuwa uchunguzi ukikamilika watuhumiwa wote saba watafikishwa mahakamani kwa ajili ya hatua stahiki za kisheria.

Aidha Kamanda Msangi amesema kuwa oparesheni ya dawa ya kulevya ni endelevu katika maeneo yote ya jiji na mkoa Mwanza na kuwataka wananchi waendelee kutoa taarifa mapema polisi kuhusu watumiaji, wauzaji na wasafirishaji wa dawa hizo, ili waweze kukamatwa kisha wafikishwe katika vyombo vya sheria.

RAIS MSTAAF DKT. KIKWET AKUTANA NA RAIS WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA JIJINI ABDJAN.

Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya ELimu, Dkt. Jakaya Kikwete akikaribishwa kwa furaha na mwenyeji wake Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Akinwumi Adesina ofisini kwake jijini  Abidjan, Ivory Coast>



RAIS Mstaafu na  Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Kupendekeza Namna Bora ya Kugharamia Fursa za ELimu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amekutana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Akinwumi Adesina alipomtembelea katika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Abidjan, Ivory Coast.

Katika mazungumzo yao, Rais Mstaafu Kikwete amewasilisha kwa Rais Adesina ripoti ya Kamisheni ya Elimu na kuwasilisha rai ya Kamisheni hiyo ya kuiomba Benki ya Maendeleo ya Afrika kusaidia nchi za Afrika kugharamia miradi na mageuzi ya sekta ya elimu katika nchi zao. Rai hiyo ya Kamisheni inatokana na ripoti kubaini kuwa misaada na mikopo inayotolewa kwa sekta ya elimu imekuwa ikishuka ikilinganisha na zile zinazotolewa kwa miradi ya afya na miundombinu. Kamisheni inaamini kuwa bila kuongeza uwekezaji katika sekta ya elimu, watoto wapatao milioni 223 duniani (takribani milioni 160 wakiwa Afrika) watakosa fursa ya kupata elimu ifikapo mwaka 2030.
Kwa upande wake, Rais Adesina ameupokea ujumbe huo na kusema kuwa takwimu zilizoibuliwa na Ripoti ya Kamisheni 'zinakatisha tamaa na pia zinatoa changamoto'. Rais Adesina ameahidi kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika itaitizama Ripoti hiyo na mapendekezo yake na iko tayari kufanya kazi kwa karibu na Kamisheni katika kutafuta majawabu ya changamoto zilizopo katika elimu barani Afrika. Amesema kuwa Benki yake inatambua kuwa kuwekeza katika vijana na nguvu kazi ya Afrika ndio jawabu la maendeleo ya uhakika huko mbeleni.
Katika hatua nyingine, Rais Mstaafu amekutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Makhtar Diop pembezoni mwa mkutano wake na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika. Ziara ya Rais Mstaafu nchini Ivory Coast itahitimishwa kwa kukutana na Rais wa Ivory Coast Mhe. Alassane Ouattara.

 Rais Mstaafu na Mjumbe Maalum wa Kamisheni ya Kimataifa ya Elimu  Dkt. Jakaya Kikwete akiwasilisha ripoti ya Kizazi cha Elimu kwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Adesina
 Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Adesina katika picha ya pamoja na wajumbe wa Mkutano.
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akibadilishana mawazo na  Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Dkt. Akinwumi Adesina na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia  Dkt, Makthar Diop pembezoni mwa mkutano huo.

RAIS MSTAAFU ALHAJ ALLY HASSAN MWINYI KATIKA SHEREHE YA UHURU WA KUWAIT USIKU HUU JIJINI DAR ES SALAAM

 Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akipokea zawadi ya mchoro toka kwa Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem al Najem katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Andrew Mahiga
  Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akikata keki na  Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem al Najem katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Andrew Mahiga
 Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akikata keki na  Balozi wa Kuwait nchini Mhe. Jasem al Najem katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kushoto ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Andrew Mahiga
Keki ya hafla hiyo  ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. 
Rais Mstaafu Alhaj Ally Hassan Mwinyi akiwa katika hafla ya kusherehekea Miaka 54 ya Uhuru wa nchi ya Kuwait na miaka 26 ya mapambano ya ukombozi katika ubalozi wa nchi hiyo Oysterbay jijini Dar es salaam usiku huu. Kulia kwake  ni waziri wa mambo ya nchi za nje Dkt. Andrew Mahiga.

Thursday, February 23, 2017

CCM YAANGUKA KESI YA UBUNGE ARUSHA.


Mahakama ya Rufaa nchini imetupilia mbali rufaa ya kupinga hukumu ya kesi ya uchaguzi katika jimbo la Longido mkoani Arusha, yaliyompa ushindi Onesmo Ole Nangole (Chadema), iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Dk. Stephen Kiruswa,

Uamuzi huo umesomwa leo (Alhamisi) na msajili wa Mahakama ya Rufaa nchini, Amir Msumi na kusema kwamba wakata rufaa waliwasilisha rufaa mpya badala ya kurekebisha baadhi ya vipengele kama walivyoagizwa na mahakama.

Msumi amesema badala ya kuwajumuisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali na  msimamizi wa uchaguzi kwenye rufaa hiyo, wakata rufaa walifanya kitu ambacho hawakuruhusiwa kukifanya na mahakama na hivyo rufaa hiyo imetupwa na wanapaswa kulipa gharama za uendeshaji wa kesi hiyo.

ZINGATIENI SHERIA MUEPUSHE AJALI MIGODINI CHATO

Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye machimbo ya dhahabu ya Musasa yaliyopo kwenye Kata ya Makurugusi, Wilayani Chato. Nyuma yake ni baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini.
Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini kwenye machimbo ya dhahabu ya Musasa katika Kata ya Makurugusi, Wilaya ya Chato wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani).
Baadhi ya wachimbaji wadogo wa madini kwenye machimbo ya dhahabu ya Musasa katika Kata ya Makurugusi, Wilaya ya Chato wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani).
Muonekano wa baadhi ya maeneo ya machimbo ya dhahabu ya Musasa katika Kata ya Makurugusi, Wilaya ya Chato.
WACHIMBAJI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA KUEPUSHA AJALI MIGODINI

WACHIMBAJI wadogo wa madini nchini wametakiwa kufanya shughuli za uchimbaji kwa kuzingatia sheria na kanuni za usalama migodini ili kuepusha ajali.

Wito huo umetolewa hivi karibuni na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani alipokuwa akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu kwenye mgodi wa Musasa uliopo Kata ya Makurugusi, wilayani Chato.

Dkt. Kalemani alisema njia bora ya kuepukana na ajali migodini ni kufanya shughuli za uchimbaji kwa kutii sheria za uchimbaji madini bila shuruti na kuzingatia kanuni za usalama kwenye maeneo ya machimbo na wakati wa shughuli za uchimbaji.

Aliwaasa wachimbaji wadogo wa madini kote nchini kujifunza kutokana na ajali mbalimbali zilizotokea migodini ili kuepuka sababu zilizopelekea kutokea kwa ajali hizo kutojirudia tena kwenye maeneo mengine.

Aidha, Dkt. Kalemani aliwasisitiza wachimbaji wa madini kote nchini kuhakikisha wanafanya shughuli za uchimbaji kwa kutunza mazingira na afya zao pamoja na afya za wengine wanaozunguka machimbo husika.

Alisema suala la mazingira linapaswa kupewa kipaumbele wakati wa shughuli husika, na kwamba ni jukumu la kila mchimbaji na kila anayeishi ama kufanyia shughuli zake maeneo ya machimbo kuhakikisha anaboresha mazingira ili kuepusha majanga mbalimbali ikiwemo ya magonjwa ya mlipuko.

“Chimbeni madini kwa kutunza mazingira na afya zenu ili mpate kufaidi matunda yatokanayo na shughuli hii, alisema Dkt. Kalemani.

Kwa wakati huohuo, Naibu waziri huyo aliwakumbusha wachimbaji wadogo wa madini kulipa kodi na ushuru stahiki ili kuepuka usumbufu.

Aliwahakikishia wachimbaji wadogo wa madini kufanya shughuli zao bila kubughudhiwa endapo watafuata maelekezo ya sheria.

“Mkitaka kuishi salama na kufanya shughuli zenu bila kubughudhiwa, hakikisheni mnalipa kodi na tozo mbalimbali mnazopaswa kulipa,” alisema.

Dkt. Kalemani alizipongeza kampuni za watanzania zinazomiliki leseni kwenye machimbo hayo ya Musasa ambazo ni Godfrey and Partners, Kilimo Kwanza Group na Hapa Kazi Tu Group kwa kuonesha njia na kutunza usalama kwenye machimbo hayo na hivyo kuwataka wachimbaji wengine kuiga mfano huo.