ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 29, 2017

MICHUANO YA COPA -UMISSETA YAZINDULIWA KWA KISHINDO DODOMA

 Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Selemani Jaffo akisalimiana na baadhi ya wachezaji wa timu zilizoshiriki uzinduzi wa michezo ya shule za sekondari nchini (Copa-UMISSETA) katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jana, mara baara ya uzinduzi rasmi wa michuano hiyo itakayoendeshwa nchini kote kwa udhamini wa kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola. Hafla ya uzinduzi ilihudhuriwa na wanafunzizaidi ya elfu 20 kutoka shule mbalimbali za sekondari mkoani Dodoma. (Picha na Mpiga Picha Wetu, Dodoma).
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Selemani Jaffo akipiga penati kuashiria uzinduzi wa michezo ya shule za sekondari nchini (Copa-UMISSETA) katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jana, mara baara ya uzinduzi rasmi wa michuano hiyo itakayoendeshwa nchini kote kwa udhamini wa kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola. Hafla ya uzinduzi ilihudhuriwa na wanafunzizaidi ya elfu 20 kutoka shule mbalimbali za sekondari mkoani Dodoma. (Picha na Mpiga Picha Wetu, Dodoma).
Vifaa vya michezo.
* Wanafunzi zaidi ya elfu 20 kutoka sekondari wahudhuria
Na Mwandishi wetu, Dodoma
Kiu ya wanafunzi na wadau wa michezi nchini kote kuhusiana na mashindano ya michezo na sanaa kwa shule za sekondari nchini imekatwa rasmi siku ya jana, baada ya kufanyika uzinduzi wa michuano hiyo kwenye uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Akifungua michuano hiyo kwa mkoa wa Dodoma,Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Selemani Jaffo alitoa pongezi kwa mchango wa kampuni ya Coca-Cola kuendeleza michezo mashuleni, huku akiwataka wakurugenzi wa halmashauri kote nchini kuhakikisha kuwa wanatenga viwanja vya michezo.
Vile vile, aliwaelekeza maafisa elimu ngazi ya tarafa, kata, wilaya, mikoa pamoja na wakurugenzi wa halmashauri nchini kuhakikisha kuwa vipindi vya michezo mashuleni vinaimarishwa na kutumika kwa ajili ya shughuli za michezo na si kufundisha masomo mengine.
“Mtoto anayekosa kushiriki michezo, hata akili yake huweza kufubaa. Michezo hujenga na kuimarisha afyaya mwili na akili, upendo, ushirikiano na uzalendo”, alisema Jaffo.
Aidha, aliongeza kuwa wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa na makaibu tawala wa mikoa kuhakikisha kuwa kila shule ina viwanja vya michezo vyenye vipimo sahihi na kusimamia sharia ya elimu inayotaka shule inaposajiliwa lazima kuwa na eneo la viwanja vya michezo.
Ofisi ya Rais Tamisemi haitowaangusha walimu wote wa michezo nchini katika kutekeleza majukumu yao.
Kwa upande wake, wakati akihutubia hafla ya ufunguzi wa michuano hii, mwakilishi wa kampuni ya Coca-Cola nchini, Pamela Lugenge aliwahakikishia washiriki kuwakampuni hiyo itaendelea na dhamira yake ya kuunga mkono jitihada ya vijana mbalimbali nchini kote katika kuwasaidia kudhihirisha vipaji vyao kupitia mashindano mbalimbali ya michezo, ikiwa ni pamoja na uendelezaji wa udhamini wa michuano ya Copa-UMISSETA.
“Dhamira yetu katika kudhamini mashindano haya na kushirikiana TAMISEMI ni endelevu, tukiwa tumejidhatiti kuhakikisha tunaendelea kuunga mkono jitihada za kutambua na kuinua vipaji vya vijana ambao watakuja kuifikisha nyanja ya michezo nchini katika kiwango cha juu zaidi”, alisema Pamela.
Mbali na hayo, aliongeza kuwa “Pamoja na kuwepo changamoto ndogondogo za hapa na pale, tutaendelea kufanya kazi bega kwa bega na washirika wetu serikalini, pamoja na wadau wengine wote wa michezo nchini, ili kwa pamoja tuweze kufanikisha na kusaidia kukua kwa sekta ya michezo nchini, hususani mashindano ya mpira wa miguu pamoja na mpira wa kikapu kwa vijana”.
Alimalizia kwa kuwahakikishia wadau wa michezo nchini ya kwamba kwa mwaka huu kampuni ya Coca-Cola imejipanga kwa dhati, kudhihirisha ya kwamba michezo ni zaidi ya ushindani, kwa kuweza kuambatanisha mashindano haya na kujenga mshikamano wa timu shindani, urafiki na hata nidhamu kwa wachezaji na timu zinazoshiriki.

MBUNGE WA BUKOMBE AWATAKA WANANCHI KUVUNJA MAKUNDI YA VYAMA NA KUWA WAMOJA.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko akiwa kwenye Mkutano wa kutatua na kusikiliza Kero za wananchi kijiji cha Bwenda Kata ya Kantente.

Meza Kuuu hakiwepo Mbunge wa Jimbo la Bukombe pamoja na viongozi wa Kijiji cha Bwenda na wa kata ya Kantente.

Wananchi wakitoa kero zao mbele ya Mbunge wa Bukombe.


Mbunge wa Jimbo la Bukombe Dotto Biteko akikabidhi mpira kwa Mwenyekiti wa Kijiji ambayo ilikuwa imeombwa na vijana kwaajili ya kujiandaa na Kombe la Dotto Cup
Diwani wa Kata ya Bulangwa Yusuf Mohamedi akielezea wananchi juu ya serikali ambavyo imejipanga kutatua Kero za wananchi juu ya Elimu pamoja na Huduma ya Afya.


Wananchi wa jimbo la Bukombe Mkoani Geita,wametakiwa kuachana na siasa ambazo  zinaweza kusababisha  kutokuwa wamoja katika kuleta maendeleo.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Jimbo  la hilo Dotto Biteko wakati akizungumza na wananakijiji wa kijiji cha Bwenda Namba 9 Kata Ya Kantente ambao ulikuwa na lengo la kusikiliza Kero za wananchi na kutatua changamoto walizo nazo.

Amesema kuwa maendeleo ya sehemu yoyote hile hayawezi kuletwa kwa watu kutokuwa na umoja na upendo.

"Wana Bwenda inahitajika nguvu ya pamoja ili kuhakikisha tuna maliza  changamoto za eneo letu, zikiwemo ukosefu wa miundo mbinu ya barabara, kituo cha Afya, miradi ya maji na kuzorota kwa ufaulu wa wanafunzi na niombe  wazazi mshirikiane  na walimu kwa kufuatilia kwa ukaribu zaidi maendeleo ya vijana mashuleni" Alisisitiza Dotto .

Hata hivyo ameongezea kuwa  kwa vijana wameanza kutenga  asilimia kumi ya mapato na tayari vikundi kumi vimekwisha kupatiwa Mkopo  na kwamba ameshapata fedha nyingine ambazo ni milioni hamsini na moja kwaajili ya maendeleo na mikopo kwa vijana na wanawake.

Pia amewataka wanakijiji hao kutokuwaogopa viongozi wao na 
kuwaambia kama wameshindwa kutekeleza majukumu yao ambayo waliyahaidi wakati wakiomba Ridhaa ya kuongoza kwani ni wajibu wao kuakikisha wanawatumikia wananchi ambao waliwaomba kura wakati wa kampeni.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE.

SUNDERLAND YAONESHWA NGAZI YA KUSHUKA NA FC BOURNEMOUTH.Baada ya kuandamwa na matokeo mabovu kwa muda mrefu, hatimaye Sunderland wameshuka daraja kwa mara ya nne katika ligi kuu ya Uingereza Epl.

Sunderland walikuwa uwanja wao wa nyumbani wa Stadium of Light wakati wakiikaribisha timu ya Fc Bournemouth na mashabiki wao waliamini wanaweza pata matokeo katika mchezo huo.

Alikuwa Joshua King aliyeweka machozi kwenye mashavu ya mashabiki wa Sunderland kwani bao lake dakika ya 88 liliwaonesha Sunderland mlango wa kutokea Epl.

Baada ya mchezo huo, kocha wa Sunderland David Moyes alisema hana mpango wa kuondoka katika klabu hiyo bali anataka kupambana ili kuirudisha tena ligi kuu.

“Sunderland watapambana tena na nina uhakika katika hilo, kwa sasa inatupasa kuwa kitu kimoja kuanza kuweka mipango yetu pamoja ili turudi tena msimu ujao” alisema Moyes

Katika michezo mingine goli la Jamie Vardy aliwapa ushindi Leicester dhidi ya Westbrom, Southampton na Hull City wakatoka suluhu ya bila kufungana kama ilivyo kwa Stoke City na West Ham.

SIMBA YAIFUMUA AZAM 1-0 YATINGA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO.

SIMBA SC imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), linalojulikana kama Azam Sports federation Cup baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam FC jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Sifa zimuendee mfungaji wa bao hilo pekee dakika ya 48, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim ambaye hata hivyo hakumaliza mchezo baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu baadaye.

Kwa ushindi huo, Simba itasubiri kukutana na mshindi kati ya wenyeji Mbao FC na Yanga SC zinazomenyaa kesho Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Mathew Akrama wa Mwanza, Azam FC ilipata pigo dakika ya 15 baada ya kiungo wake mchezeshaji, Salum Abunakar ‘Sure Boy’ kutolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumchezea rafu mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Hajib.

Ilionekana kama wachezaji hao wamegongana kwa kawaida mno, lakini kwa namna Hajib alivyojirusha huku akipiga yowe la kuugulia maumivu Akrama aliingia kwenye mtego wa kumtoa kwa kadi nyekundu Sure Boy.

Friday, April 28, 2017

Thursday, April 27, 2017

MUUNGANO WA UPINZANI KENYA WAMTANGAZA RAILA ODINGA KUWA MGOMBEA WAKE WA URAIS.


Muungano mkuu wa upinzani nchini NASA, hatimaye leo umemtangaza mgombea wake wa urais aliyekuwa akisubiriwa kwa muda mrefu. Muungano huo umemtangaza kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti 8 mwaka huu.
Hii itakuwa ni mara ya nne kwa Odinga, mwenye umri wa miaka 72 kuwania urais wa Kenya.
Katika hafla iliyofanyika kwenye uwanja wa kihistoria wa Uhuru Park jijini Nairobi na kuhudhuriwa na maelfu ya wafuasi wa muungano huo, Raila alitajwa kuwa mgombea urais wa NASA na Kalonzo Musyoka mgombea wake mwenza ili kuchuana na Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu wa Agosti 8.
Katika hotuba aliyotoa baada ya kuteuliwa, Raila Odinga ameahidi kushusha bei za vyakula na kupambana na ufisadi. Aidha ameahidi kuifanyia mabadiliko sekta ya umma na kuwepo serikali za mitaa zenye nguvu zaidi.
Hata hivyo kutokana na muundo wa mgao wa madaraka uliopangwa na muungano wa NASA, Raila hatokuwa na madaraka mutlaki endapo atachaguliwa kuwa rais mpya wa Kenya katika uchaguzi mkuu wa tarehe 8 Agosti.
Vinara wa NASA. Kutoka kushoto: Moses Wetangula, Raila Odinga, Kalonzo Musyoka na Musalia Mudavadi.

Katika muundo huo, kiongozi wa chama cha Amani Musalia Mudavadi atakuwa Waziri Kiongozi anayehusika na Uratibu wa Serikali. 

Naye kiongozi wa chama cha Ford Kenya Moses Wetangula atakuwa Naibu Waziri Kiongozi anayehusika na uratibu wa sekta ya uchumi. Kiongozi wa Chama cha Mashinani Isaac Ruto, atakuwa Naibu mwengine wa Waziri Kiongozi, atakayehusika na utawala na uratibu wa sekta ya huduma za jamii.

Muundo huo wa makubaliano yaliyofikiwa baina ya vyama tanzu vinavyounda muungano wa upinzani wa NASA unaonyesha kuwa rais atagawana madaraka na washirika wake wakuu ikiwemo katika suala la uteuzi wa baraza la mawaziri kupitia mashauriano na makubaliano

*WABUNGE KUTOKA KENYA WAMTEMBELEA MH. EDWARD LOWASSA MONDULI MCHANA WA LEO* Wageni kutoka Jamuhuri ya Kenya wakiongozwa na wabunge 13, Madiwani, Machifu na Maleigwanan kutoka kenya mchana wa leo wamemtembelea Waziri Mkuu Mstaafu Mh. Edward Ngoyai Lowassa nyumbani kwake kijijini Ngarash, jimbo la Monduli wakiongozana na vikundi mbalimbali vya Wajasiriamali kutoka Wilaya mbalimbali za Mikoa ya Arusha na Manyara..

UNYANYASAJI WA WAFANYAKAZI MIGODINI NI MOJA YA MASUALA YALIYOJADILIWA HII LEO BUNGENI.


Kampuni binafsi za migodi zimekuwa zikikiuka mikataba ya kazi na pia zikiwakandamiza na kuwanyanyasa wafanyakazi. 

- Jeh ni lini Serikali itafanya ukaguzi wa mikataba kwa kampuni zinazofanya kazi migodini?

- Jeh kwanini Serikali isiamue kuwaondoa nchini waajiri wakorofi kwa unyanyasaji wanaofanya?

DIAMOND, ALIKIBA WAGOMA KUIMBA WIMBO WA KUISAPOTI SERENGETI BOYS.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Maulidi Kitenge ameandika hivi... "Kiba na Diamond wameshindwa kuonesha uzalendo kwa Serengeti Boys wamegoma kuimba wimbo wa hamasa licha kuwepo kamati ya hamasa.inasikitisha"

MSUKUMA AIBUA SUALA LA MELI MPYA ZIWA VICTORIA.

Swali la mbunge Msukuma kuhusu serikali kuboresha meli zinazofanya kazi katika ziwa Victoria hasa zinazokwenda katika kisiwa cha Ukerewe.

MWANZA AJITOKEZA JAMAA ATAKAYEMPIKU HUSSEIN BOLT KATIKA KUFUKUZA UPEPO.

 Mwanariadha kutoka jijini Mwanza, Yusuph Mwilongo akionyesha uwezo wake wa kukimbia mita 100 kwa sekunde 9 hadi 11 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa juzi huku rekodi ya dunia inashikiliwa na Usain Bolt kwa kukimbia mita 100 kwa sekunde 9.12.
 Yusuph akionyesha uwezo wake kwenye uwanja wa CCM Kirumba  picha zote na Annastazia Maginga
 Afisa Michezo wa Jiji la Mwanza, Mohamed Bitegeko akizungumza na waandishi wa habari CCM Kirumba jijini hapa juzi  baada ya kushuhudia mbio za Mwanariadha Yusuph Mwilongo(kushoto) mwenye uwezo wa kukimbia mita 100 kwa sekunde 9 hadi 11.

Airtel YATUMIA TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO KUBORESHA ELIMU YA SEKONDARI

Wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lolangulu iliyopo kijiji cha Mbola mkoani Tabora wakisoma kwa kupitia njia ya mtandao baada ya Airtel kwa kushirikiana na Erickson pamoja na taasisi ya Earth iliyoko nchini Marekani kuwawezesha wanafunzi hao kupata nyenzo za masomo kupitia mtandao kwa kupitia mpango ujulikanao kama “Studi Academy”.
Airtel yatumia teknolojia ya mawasiliano kuboresha elimu ya sekondari Tabora Aprili 26, 2017 katika kutimiza dhamira ya kutumia teknologia ya mawasiliano katika kuendeleza jamii kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kushirikiana na taasisi ya Earth iliyoko nchini Marekani imeanzisha mpango utakaowawezesha wanafunzi wa sekondari kupata nyenzo za masomo kupitia mtandao wao wa intaneti

Mafunzo hayo kwa kupitia mtandao yanayojulikana kama“Studi Academy” yanapatikana kupitia mtandao wa Airtel wa 3G. ambapo katika kijiji cha Mbola Mkoani Tabora Airtel kwa kushirikiana na Erickson wameboresha zaidi mawasiliano ya intaneti ya kasi ya 3G ili kuhakikisha kuwa shule na vituo vya huduma za afya zinafaidika na mpango huu kabambe kwa kuinua upatikanaji wa huduma za masomo kupitia mtandao na kuanza kuwafaidisha wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lolangulu.

Akiongelea ujio na mafanikio ya mradi huo Mwalimu mkuu wa shule ya sekodari ya Lolangulu , Cleophas Bugomba alisema” Shule yetu imekuwa na changamoto ya walimu wa kutosha kwa masomo ya sayansi hivyo kuwepo kwa masomo haya kupitia mtandao kumesaidia kupunguza changamoto hii kwa kiasi kikubwa.

Mafanikio haya tumeyaona kupitia matokeo ya mitihani ya kitaifa ya kidato cha pili ambapo ufaulu wa wanafunzi hususani katika masomo ya sayansi ikiwemo hesabu na fizikia umekuwa wa kiwango kikubwa pamoja nakuwepo kwa changamoto hizi za walimu wa kutosha wa masomo hayo”.

 Kwa upande wake mwanafunzi wa kitado cha tatu mwaka 2017 Irene Tamson ambayo pia ni mwanafunzi bora wa kike aliyefanya vizuri katika masomo ya sayansi kwa mkoa wa Tabora alisema” mpango huu wa “Studi Academy” unaowezeshwa na intaneti ya Airtel umenisaidia sana kufanya maswali mbalimbali na kupata majibu sahihi hapo hapo, kujifunza vitu vipya na kupata nyezo muhimu pindi nikijisomea binafsi au kwa makundi.

Tunafurahi kuweza kunganishwa na mtandao na kujifunza kutoka kwa wengine kutoka nchi za ulaya lakini pia kupata nyenzo muhimu za kujifunzia kwanjia ya technologia ya kisasa.” Nae Meneja wa huduma kwa Jamii wa Airtel , Bi Hawa Bayumi alisema, “tunajisikia fahari kuwa na mtandao bora unaotuwezesha kutoa huduma kwa jamii ikiwemo mpango huu wa Studi Academy, lengo letu Airtel ni kutoa suluhisho kupitia teknolojia ya mtandao ili kuwafikia watanzania wengi zaidi ili wapate mafunzo kwa njia ya mtandao hasa kwa maeneo ya pembezoni”.

 Mipango na dhamira yetu Airtel ni kuendelea kushirikiana na wadau wetu kama Ericsson na Health kutumia fursa ya mawasiliano kuiwezesha jamii kwa kurahisisha baadhi ya changamoto za elimu na afya,”.

Alieleza Bi Bayumi Airtel Tanzania pia kupitia mpango wake wa kuendelea kutoa mawasiliano bora kwa kuzingatia ubunifu mwaka jana ( 2016) walishirikiana na VETA na kuzindua Applikesheni kabambe ya VSOMO ili kuwawezesha watanzania nchini kote kujisomea kozi za ufundi stadi kutoka kwenye vyuo vya Ufundi VETA kupitia simu za mkononi ili kutoa fursa kwa watanzania nchini kujiendeleza kielimu bila kujali changamoto zinazosababishwa na mazingira au ukosefu wa vifaa vyakujisomea karibu nao.

RAIS WA ANGOLA AAFIKI UCHAGUZI MKUU UFANYIKE AGOSTI 23


Rais Jose Eduardo dos Santos wa Angola amesaini dikrii inayoruhusu tarehe 23 Agosti mwaka huu kuwa siku ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini humo. 
Taarifa iliyotangazwa na idhaa ya serikali hapo jana imesema kuwa, uchaguzi mkuu utafanyika Agosti 23, ambapo Dos Santos anatazamiwa kuachia ngazi baada ya kuwa rais wa nchi hiyo kwa karibu miongo minne.

Hata hivyo taarifa hiyo imesisitiza kuwa, Dos Santos ambaye ameiongoza nchi hiyo ya Kiafrika yenye utajiri wa mafuta ghafi atasalia kuwa kinara wa chama tawala cha MPLA


Angola ni mzalishaji namba 2 wa mafuta ghafi Afrika, na uchumi mkubwa wa 3 barani humo
Uamuzi huu wa Dos Santos unajiri chini ya saa 48 baada ya Baraza la Uongozi la Rais wa Angola ambalo hutoa ushauri kuhusu maamuzi ya nchi kupendekeza tarehe 23 Agosti kuwa siku ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini.


Itakumbukwa kuwa, chama tawala nchini Angola cha MPLA mwezi Disemba mwaka jana kilimchagua Joao Lourenco mwenye umri wa miaka 63 kuwa mgombea wa kiti cha urais wa chama hicho.

Jose dos Santos aliye na umri wa miaka 74 ni kiongozi wa pili barani Afrika aliyesalia madarakani kwa muda mrefu zaidi, na mwezi Februari mwaka huu alisema kuwa hatagombea tena kiti cha urais katika uchaguzi ujao.

TGGA YAZINDUA UPANDAJI MITI 600 KILA MKOA TANZANIA.

 Wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari Mtumba Manispaa ya Dodoma wakiwa na miche ya miti kila mmoja wao kabla ya kuipanda kwenye uzinduzi wa upandaji miti uliofanywa kitaifa na Girl Guides Tanzania mkoani humo. 
PICHA NA JOHN BANDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG


John Banda, Dodoma

CHAMA cha Tanzania Girl Guides (TGGA) kimezindua mradi wa upandaji miti kitaifa katika Shule ya Msingi ya Mtumba Manispaa ya Dodoma kwa lengo la kuifanya nchi kuwa ya kijani ili kuweza kuepukana na mabadiliko ya tabia nchi.

Akizungumza katika uzinduzi huo Kamishna Mkuu wa Tanzania Girl Guides nchini, Simphorosa Hangi  alisema wanakamilisha uzinduzi huo  wa kitaifa huku tayari shirika hilo likiwa limeshaanza upandaji wa miti hiyo katika mikoa mingine ya  Arusha, Lindi na Mwanza

Hangi alisema kuwa kwa sasa wapo katika mikoa 22 na wanaendelea kufanya juhudi ili waweze kukamailisha mikoa yote ikiwemo Zanzibar ambapo kila mkoa watapanda miti 600 huku wakiacha kila mkoa kuendelea na zoezi hilo ili kulifanya Taifa kuwa la kijani.

Naye Mwenyekiti wa Shirika hilo kitaifa, Martha Qorro  Alisema zoezi hilo linafanyika mashuleni na kuachwa kwa viongozi wa Girl Guides wa mkoa husika ambao watahakikisha wanapeleka na kupanda miti katika shule ambazo maji yapo yakutosha ili kuifanya miti hiyo kukua.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma, Aziza Mumba katika uzinduzi huo alisema juhudi hizo zinazofanywa na Shirika hilo zinafaa kuigwa ili kusaidia kurejesha uoto wa kijani ambao utasaidia kuyaweka mazingira kuwa mazuri yenye rutuba ya kutosha kutokana na mvua zitakazokuwa zikinyesha kila mahali   


 Wanachama wa Tanzania Girl Guides wakichimba moja ya mashimo ya kupanda mti katika Shule ya Msingi Mtumba Manispaa ya Dodoma wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupanda miti katika shule mbalimbali nchini.

 Wanafunzi wanachama wa TGGA
 Wasanii wakitumbuiza kwa ngoma ya kabila la Wagogo wakati wa uzinduzi wa upandaji miti shuleni hapo
 Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Dodoma, Aziza Mumba akipanda mti katika Shule ya Msingi Mtumba wakati wa uzinduzi wa upandaji miti uliofanyika kitaifa shuleni hapo juzi.

 Mwenyekiti wa TGGA, Marha Qorro akimwagilia mti baada ya kuupanda

 Viongozi na wanachama wa TGGA wakiwa katika picha ya pamoja
 Viongozi wa TGGA Makao Makuu Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mkoa wa Dodoma
 Viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wanachama wa TGGA
Wanafunzi wanachama wa TGGA wakiwa na miche ili waendelee na zoezi la kupanda miti shuleni hapo

MAGAZETI YA LEO:- RAIS AAPA KUULINDA MUUNGANO, MAJUMBA YA KIFAHARI YA KUGUMI YAKAMATWA, LISU KABUDI WATOANA JASHO, HALIMA MDEE AMWANGUKIA SPIKA NDUGAI


Rais aapa kuulinda Muungano, Majumba ya kifahari ya Lugumi yakamatwa, Lissu na Kabudi watoana jasho dk 20.
 
Halima Mdee amwangukia spika Ndugai, JPM: Atakayejaribu  kuvunja Muungano atavunjika yeye, CUF Lipumba yawakuta makubwa. Habarika na dondoo hizi za magazeti ya leo hapa;

Wednesday, April 26, 2017

SHEREHE ZA MUUNGANO MKOANI MWANZA ZATOA ONYO KWA WANAOJIHUSISHA NA MIHADARATI.

HABARI KWA KINA NA SAUTI KUKUJIA HIVI PUNDE.....