Saturday, November 29, 2014
HII HAPA NGOMA MPYA YA LADY JAYDEE FT DABO - FOREVER
ULIKUWA ukiisubiri kwa hamu ngoma mpya ya Lady Jaydee, au pengine ukijumuika na wengi waliokuwa na maswali kuhusu maisha yake ambapo kwa kinywa chake hivi majuzi alipohojiwa na chombo kimoja wapo cha habari Bongo Tz alinukuliwa akisema kuwa majibu ya baadhi ya maswali ya wengi yatapatikana ndani ya ngoma yake mpya.
Sasa mwanamama Lady Jaydee kaachia kichupa cha wimbo Forever akimshirikisha mshindi wa tuzo za Kilimanjaro katika muziki wa Reggae na Ragga namzungumzia Dabo. Chekshia video hapo juu.
RAIS KIKWETE ASEMA AMEPONA SARATANI
![]() |
Rais Kikwete akizungumzia afya yake. |
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema amepona saratani baada ya kufanyiwa upasuaji mapema mwezi huu nchini Marekani.
Kiongozi huyo wa Tanzania mwenye umri wa miaka 64 ametoa hotuba kwa taifa kuelezea afya yake..
"Niligundulika kuwa na hatua ya pili ya saratani ya kibofu, ambayo baadaye ikaonekana kuwa ni hatua ya kwanza," alisema Kikwete katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja kupitia televisheni akiwa uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam baada ya kurejea kutoka Marekani.
Aliongeza kuwa madaktari wamesema sasa hali yake shwari: "Madaktari walisema saratani haikuenea katika sehemu nyingine za mwili na baada ya upasuaji sasa wamesema nimepona saratani."
Alisema aligundulika kuwa na saratani ya kibofu zaid ya mwaka mmoja uliopita na alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Johns Hopkins Hospital tarehe nane Novemba.
Kikwete ambaye anamaliza muhula wake wa pili mwakani amesema wananchi wajenge tabia ya kupima afya zao ili wagundue maradhi mapema.
CHANZO: BBC SWAHILI.Friday, November 28, 2014
LAMUDI TANZANIA KUTANGAZA HUDUMA ZA MADALALI BURE.
Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam. |
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi leo jijini Dar es Salaam, Meneja Huduma kwa Wateja wa Lamudi Tanzania, Godwin Lemma amesema kwa sasa madalali wanaweza kutangaza nyumba, viwanja na magari yaliyoko sokoni kupitia mtandao wa kampuni hiyo bila malipo yoyote.
Akifafanua zaidi Lemma alisema dalali anayependa kupata huduma hiyo anatakiwa kufika katika ofisi za Lamudi Tanzania zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam (Garden Road) na kujaza fomu ambayo itaelezea huduma yake na kuanza kuitangaza kwenye tovuti www.lamudi.co.tz bila malipo yoyote. “…Kimsingi huduma hii inawasaidia sana madalali kutangaza kazi walizonazo, bei zao na hata eneo ilipo. Mfano kama ni nyumba au kiwanja baada ya dalali kutoa taarifa za kutosha sisi tunamtangazia bure kazi hiyo kupitia tovuti yetu (www.lamudi.co.tz),” alisema Lemma.
Alisema mbali ya kuwasaidia madalali kutangaza bidhaa zao wameanza kutoa pia mafunzo ya kuwajengea uwezo madalali kuweza kufanya kazi zao kiuaminifu zaidi ili kujenga heshima ya kazi zao. “Wakati mwingine tumekuwa tukifanya kazi ya kuchukua baadhi ya madalali na kuwajengea uwezo, kuwapa mafunzo ya namna ya kufanya kazi zao kiuaminifu zaidi na masuala mengine ya msingi katika shughuli zao,” alifafanua Meneja huyo wa Huduma kwa Wateja.
Pamoja na hao alisema kwa sasa kampuni ya Lamudi Tanzania imezinduwa huduma mpya ya kumwezesha mteja kupata taarifa za uuzaji au ukodishaji nyumba ama viwanja kupitia simu za mkononi hivyo kumrahisishia kupata taarifa kwa wakati. *Imeandaliwa na www.thehabari.com
NJOO TUAGE MWEZI NOVEMBA KWA STAILI YA AINA YAKE NA SKYLIGHT BAND IKIWEMO RED CAPET TREATMENT, LEO THAI VILLAGE
IJUMAA 28.11.14: Kama kawaida tunaaga mwezi aina yake, skylight friday ndani ya Thai village masaki,special show ya mwisho wa mwezi kuwashukuru wadau wetu, Kutakua na Red carpet treatment, kutakua free shots of tequilla mlangoni, zawadi kwa dancers na shabiki wetu wa mwezi atapatikana#si ya kukosa ijumaa hii
JUMAMOSI 29.11.14:Hii ni siku ya bata na bata litaendelea, ni Pale Azura Beach Club Kawe Darajani kwenye siku kuu ya bata#Bata day# muziki na bata, usikosee hii
JUMAPILI 30.11.14: Ni bonanza letu la kistaarabu la kumalizia weekend, Skylight Sunday bonanza#Escape1 beach club# tutamaliza weekend yetu na mziki wa nguvu hii itakua ki africa zaidi#miziki mbalimbali toka barani africa#piga ki africa upate zawadi
Meneja wa bendi Aneth Kushaba AK47 akiwapa raha mashabiki wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar. |
Mashabiki wa Skylight Band nao wajisakata sebene la vijana wa Skylight Band Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Thai Village Masaki jijini Dar. |
Rappa Sony Masamba wa Skylight Band akishusha mistari Ijumaa zao za kila Ijumaa ndani ya viunga vya Thai Village Masaki jijini Dar huku akipewa sapoti na Joniko Flower pamoja na Sam Mapenzi. |
Kipaji kipya ndani ya Skylight Band anafahamika kwa jina la Alice. |
Diva Digna Mbepera akitoa burudani kwa mashabiki wa Skylight Band huku akipewa back up na Sony Masamba pamoja na Hashim Donode. |
Mashabiki wa Skylight Band wakipata burudani kutoka kwa Digna Mbepera (hayupo pichani).
|
Twende kazi hakuna kulala hapa.!
|
Mashabiki nao walijibu mashambulizi hawajakubali kushindwa. |
Mashabiki wa Skylight Band wakijibu mashambulizi kwa kusebeneka. |
Joniko Flower akiwaduarisha mashabiki wa Skylight Band.
|
Mashabiki wa Skylight Band wakipata ukodak Ijumaa iliyopita. |
Mashabiki wa Skylight Band wakifurahia ukodak. |
Bella Kombo na Emma Beyz wakishow love back stage. |
Mratibu wa Skylight Band, Dean Nyalusi wa ZIFF pamoja na Blogger wa Vijimambo... |
Mashabiki na wadau wa ukweli wa Skylight Band. |
Thursday, November 27, 2014
BONUS TRACK- MTOTO WA FISADI BY KINGKAPITA
YULE KIJANA HATARI WA MISEMO ANAETESA NA TRACK YAKE YA 'KUNA TATIZO KWANI' ALIYOMSHIRIKISHA GODZILA, BAADA YA MAMBO YANAYOIENDELEA NCHINI KINGKAPITA AINGIA STUDIO NAKUANDIKA WIMBO HUU NA KUAMUA KUIACHIA KAMA BONUS KUFUNGIA MWAKA - MAALUM KAMA SALAMU KUTOKA GHETO - KITAANI KWA WALE WOTE WANAOKULA HELA ZA JASHO LA WANANCHI - WIMBO UNAITWA MTOTO WA FISADI VS MTOTO WA MTANII.
AKIONGELEA MAISHA YA WATOTO WA MAFISADI NA MAISHA YA MTOTO WA MTAA ALIO RECORD MIAKA MITATU ILIOPITA.
HII NI BONUS TRACK MUDA WOWOTE MTASIKIA NGOMA MPYAAA NA PROJECT KIBAO BAADA YA KUMALIZA MASOMO YAKE NJE YA NCHI. BOFYA PLAY KUUSIKILIZA HAPO JUU.
WAFANYAKAZI WA AIRTEL KUWAUNGANISHA WADAU KATIKA KUSAIDIA SHULE YA MSINGI KUMBUKUMBU-Dar
![]() |
Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi |
Wafanyakazi wa Airtel kuwaunganisha wadau katika kusaidia shule ya msingi Kumbukumbu-Dar
· Wafanyakazi wa Airtel kutembea ili kukusanya jumla ya zaidi ya milioni 10
· Wafanyakazi wa Airtel kukarabati darasa na kununa madawati shule ya kumbukumbu.
Wafanyakazi wa Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake maalumu wa “Airtel tunakujali”imeandaa matembezi ya hisani huku ikialika wadau wote wenye wito wa kuchangia elimu kuungamkono jitiada hizo ili kukamilisha lengo la kuikarabati shule ya msingi kumbukumbu iliyopo kinondoni jijini Dar es Saalam.
Matembezi hayo yanayoandaliwa na wafanyakazi wa Airtel yatashirikisha wadau mbalimbali na yatafanyika siku ya Jumamosi tarahe 29/11/2014 kuanzia saa moja asubuhi katika viwanja vya ofisi ya Airtel Makao makuu Morocco.
Akiongea kuhusu Matembezi haya Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema “wafanyakazi wa Airtel nao wameona mapungufu yaliopo shuleni hapo na kuamua kujitosa kwa kutumia sehemu ya kipato chao kuihudumia jamii kwa njia hii, kila mfanyakazi wa airtel ambae amehamasika tayari ameshachangia.
Na sasa tumeona ni vyema kuishirikisha jamii pia wakiwemo wanafamilia, marafiki na wote wenye wito wa kuchangia elimu kuungana nasi kuhakikisha watoto wanaosoma shule ya kumbukumbu wanasoma katika mazingira mazuri
“Lengo ni kukusanya zaidi ya shilingi milioni 10 ili kukarabati darasa moja na kununua madawati kwa ajili ya darasa la wanafunzi wa darasa awali”
Tutafanya Matembezi ya Kilomita 5 ambapo ni ya wazi ili kila mtanzania aweze kushiriki na kuchangia, pia kutakuwa na Tshirt maalumu zinapatikana katika ofisi ya Airtel Makao Makuu kwa gharama ya shilingi 15,000. Kwa kununua lengo ni kumfanya kila mmoja aweze kuchangia.
Tunatoa wito kwa wadau mbalimbali kujitokeza na kuungana nasi katika matembezi haya kwa kununua tshirt hizi maalumu na kwa kujitokeza kutembetea nasi ili kuwezesha vijana wetu ambao ni taifa la kesho kupata elimu bora ,katika mazingira mazuri na yaliyoboresha zaidi. Aliongeza Hawa
Airtel chini ya mpango wa”Airtel Tunakujali” unaoendeshwa na wafanyakazi katika vitengo mbalimbali umeshika kasi ambapo kitengo cha huduma kwa wateja kilifanya burudani na kumshirikisha banana zoro na mzee king Kikii na sasa kitengo cha rasilimali watu na ofisi ya mkurugenzi imeandaa matembezi ya hisani lengo likiwa ni kukusanya fedha kwa ajili ya kusaidia maeneo mbalimbali yanayozunguka jamii hususani kwenye elimu ambapo utekelezaji wake unategemea kutafanyika mapema mwakani.
WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA KUWA MGENI RASMI KWENYE UZINDUZI WA ALBAMU ‘USILIE’ DESEMBA 7/2014
![]() |
Mkurugenzi wa kwaya ya ‘Family Singers’ Daniel Misheto (kulia). Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog. |
Na Mwandishi Wetu.
WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda ametajwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa albamu ‘Usilie’ ambayo itapatikana kwenye DVD Desemba 7, mwaka huu.
Akizungumza Dar es Salaam jana kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa kwaya ya ‘Family Singers’ Daniel Misheto, alisema hafla hiyo itafanyika kwenye Ukumbi wa PTA uliopo Uwanja wa Sabasaba, Dar es Salaam.
Mbali ya uzinduzi huo Misheto alisema pia wasanii mbalimbali wa filamu watanogesha siku hiyo.
Aliwataja waimbaji wa injili ambao watakuwepo siku hiyo kuwa ni Leah Mudy, AIC (T) Vijana Chang’ombe, Accasia Singers, Papson Mastaki kutoka Kenya na Frank Hume kutoka Boston nchini Marekani watatumbuiza.
Uzinduzi huu umeratibiwa na Misheto Promotion, ambapo kabla ya uzinduzi huo kutafanyika huduma za bila malipo za kiafya na kitabibu kutoka kwa madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali, ambayo yamekuwa yakiikabili jamii.
Misheto ameyataja magonjwa hayo kuwa ni moyo, figo, kisukari na mengineyo ambapo huduma hiyo itatolewa na madaktari bingwa nchini.
“Huduma hii itaanza saa mbili asubuhi na itatolewa bure, ikiwemo ushauri na kwa wale ambao wataweza kutibika watatibiwa, ila ambao watakuwa kesi zao zimekuwa ni kubwa zaidi watapewa ushauri wa bure wa kuendelea na matibabu katika hospitali kubwa na hakutakuwa na kiingilio," alisema Misheto.
Wednesday, November 26, 2014
KIMENUKA BUNGENI.
PAMOJA na maneno mengi yaliyosemwa, shutuma lukuki zilizotolewa na mbinu za kila aina kutaka kuzuia mjadala wa ripoti ya uchunguzi wa kashfa ya IPTL, hatimaye hii leo kila kitu toka kwenye uchunguzi wa kamati kimewekwa wazi jioni hii.
Taarifa ya kamati imeainisha nani mkweli na nani mwongo wakati Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), lilipowasilisha bungeni maoni yake kuhusu ripoti ya kuchotwa kwa Sh306 bilioni katika Akaunti ya Tegeta Escrow.
Uchunguzi huo ulifanywa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa maelekezo ya Serikali baada ya kuombwa na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila alipolalamikia ufisadi huo bungeni.
Pamoja na juhudi za kampuni ya IPTL na PAP kufungua kesi kuzua mjadala huo bungeni, hukumu iliyotolewa jana na majaji watatu ilisema kila kitu kiendelee kama kilivyo na kitakachoendelea kisiathiri kesi iliyopo mahakamani ambapo sasa mambo hadharani.
Moja kati ya MAPENDEKEZO MAKUU yaliyotolewa mara baada ya Taarifa hiyo kusomwa ni:-
- Kufilisi mali zote za waliohusika ikiwa ni pamoja na hata wale waliohusishwa kwa nia njema.
-Baadhi ya walionufaika na fedha hizo ni viongozi wa Umma ambao wanapaswa kuzingatia sheria ya maadili ya viongozi wa Umma ikiwemo sheria namba 13 ya mwaka 1995 ambayo inawataka kutoa taarifa ya Zawadi wanazopata au Malipo wanayolipwa. Vyombo vya uchunguzi vitafanya kazi yake kuona kama Matakwa ya Sheria yalifuatwa....
BOFYA PLAY KUSIKILIZA TAARIFA YA KAMATI
HUYU NDIYE MSHINDI WA NDOVU GOLDEN EXPERIENCE.
NA MWANDISHI WETU
MSHINDI wa pili ya shindano la Ndovu Golden Experience Amand Kimario amewapiga kumbo washiriki wenzake katika shindano hilo na kujinyakulia nafasi ya kutembelea hifadhi ya Selous mwakani.
MSHINDI wa pili ya shindano la Ndovu Golden Experience Amand Kimario amewapiga kumbo washiriki wenzake katika shindano hilo na kujinyakulia nafasi ya kutembelea hifadhi ya Selous mwakani.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa bia ya Ndovu Special Malt ambao ndio waratibu wa shindano hilo Pamela Kikuli alisema, lengo la kuandaa shindano hilo ni kwa ajili ya kuwapa fursa Watanzania kutembelea hifadhi na kujivunia utalii wao wandani.
Pamela alisema, mshindi huyo amepatikana baada ya kuchezeshwa droo ambapo yeye aliwabwaga wenzake waliojitosa katika shindano hilo, ambapo atatarajiwa kuwana mwenzake ambaye wataongozana katika hifadhi hiyo.
Alisema, kwa kutambua bia yao ya Ndovu inabebwa na nembo ya mnyama Tembo, wanatumia nafasi hiyo kumlinda mnyama huyo kama kampeini yao inavyosema 'Ndovu Defance', ilikunusuru mauaji yake.
"Utalii ni sekta muhimu sana katika kukuza uchumi wa Tanzania, ila utalii mkubwa unaofanyika hapa Tanzania niwa wageni wa nje, hivyo basi tunaamini kwa kuendeleza kampeini yetu hii ya Ndovu Golden Experience, inayoendeshwa kwa kutumia namba za chini ya kizibo, itawapa fursa muhimu watanzania kujivunia utalii wao,"alisema Pamela.
Aidha Pamela alisema, baada ya kumalizika kwa droo ya shindano hilo Disemba 18, washindi wataenda kutembelea hifadhi hiyo Januari mwakani huku wao Ndovu wakigharimia malazi, chakula pamoja na usafiri na kuwataka watanzania kuhakikisha wanatumia vyema fursa hiyo kwa kuandika namba chini ya kizibo kwenda namba 15499 au katika mtandao wa www.ndovuspecialmalt.com.
MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA KONGAMANO LA KIMATAIFA DAR
![]() |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo mara baada ya ufunguzi. Picha na OMR |
![]() |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo mara baada ya ufunguzi. Picha na OMR |
![]() |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo mara baada ya ufunguzi. Picha na OMR |
![]() |
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya viongozi waratibu wa kongamano hilo, baada ya ufunguzi. Picha na OMR |
KAMPUNI YA KONYAGI YANYAKUWA TUZO MBILI ZA ULIPAJI KODI BORA NCHINI
Mkurugenzi wa Fedha wa TDL, Bwana Michael Brown (KUSHOTO) akipokea Ngao ya ushindi kwa TDL baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kama Mlipa Kodi Bora katika kundi la Viwanda, na Naibu Waziri wa viwanda na Biashara Bw Kigoma malima ndie anaemkabidhi tuzo hiyo. KONYAGI ilinyakuwa tuzo mbili za ulipaji kodi bora. |
Waziri Kiongozi mstaafu Vuai Nahodha akimkabidhi Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya TDL watengenezaji wa KONYAGI bw. Michael Brown Tuzo ya Mshindi wa Jumla ya Mlipa Kodi Bora katika hafla iliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Convention centre Wengine katika Picha ni Joseph Chibehe meneja mauzo na Edward Mashingia meneja wa Fedha. |
Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni ya TDL watengenezaji wa KONYAGI bw. Michael Brown akiwa na tuzo aliyoipokea. |
Maofisa mbalimbali wa makampuni mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa tuzo za ulipaji kodi bora nchini. |
Joseph Chibehe meneja mauzo wa kampuni ya KONYAGI kushoto akibadilishana mawazo na Ofisa wa TBL ambao nao walinyakuwa tuzo. |
Baadhi ya washiliki walionyakua tuzo za ulipaji kodo bora wakitoka ukumbini na tuzo zao. |
Tuesday, November 25, 2014
Subscribe to:
Posts (Atom)