ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 4, 2024

WANA CCM TUSIBWETEKE UCHAGUZI HUU HAKUNA KUPITA BILA KUPINGWA

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA Amos Makalla akizungumza na Wanachama pamoja na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni katika Ukumbi wa Kiramuu Hall, leo NOV 04, 2024. Amesema kwenye kipindi cha kampeni hakuna kulala Wana CCM wapambane watafute kura ili kukiwezesha Chama cha Mapinduzi kushinda kwa kishindo kwani Uchaguzi huu hakuna ile kushinda bila kupingwa japo kuwa kuna Mitaa ,Vijiji na Vitongoji wenzetu hawajaweka watu. "Pamoja na kwamba kuna dalili za wenzentu kutosimamisha wagombea kwenye maeneo mbalimbali itakapotea naomba niongee na wana CCM wa Kinondoni na Nchi nzima kwamba Uchaguzi huu hauna kupita bila kupingwa msibweteke kwani mmesikia Chama fulani kimesema kitahakikisha hata kama CCM ndo wameteuliwa tutawapigia kampeni ya kupigiwa kura ya hapana." #CCM #samiasuluhuhassan

ZINGATIENI MISINGI YA UTAWALA BORA KATIKA USIMAMIZI WA RASILIMALI WATU-MAJALIWA


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa wasimamizi wote wa rasilimaliwatu wazingatie misingi ya utawala bora na weledi katika kuisimamia rasilimali hiyo katika Sekta ya Umma Barani Afrika.


Amesema kuwa kufanya hivyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuwezesha kutoa huduma bora na kudumisha imani ya wananchi kwa Serikali zao.


Ametoa wito huo leo (Jumatatu, Novemba 04, 2024) alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Mkutano wa Tisa wa Mwaka wa Mtandao wa Wasimamizi na Mameneja wa Rasilimaliwatu Katika Sekta ya Umma Barani Afrika (APS-HRMnet) jijini Arusha.


“Rasilimaliwatu ina mchango mkubwa katika kuiwezesha Serikali kufikia malengo ya maendeleo iliyojiwekea pamoja na Malengo ya Maendeleo Endelevu. Hivyo ninyi, kwa kuwa ni wataalam katika usimamizi wa Rasilimaliwatu mnao wajibu na dhamana kubwa ya kuhakikisha mnasimamia ipasavyo Rasilimali hiyo muhimu na ya thamani”

Amesema kuwa ili kuimarisha  usimamizi wa kimkakati wa rasilimaliwatu na kukabiliana na changamoto zake, viongozi hao wanapaswa kuendelea kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa  watumishi wao waendane na mabadiliko ya kidunia na waweze kufanya kazi kwa weledi.


Aidha, amewataka Kukuza ujuzi wa watumishi na kuwawezesha kujifunza stadi mpya kulingana na majukumu yao. “Ongozeni kwa maono, ubunifu, uadilifu na kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Nchi husika katika kutumikia wananchi kwenye maeneo yenu”


Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa  amewataka viongozi hao kutafsiri kwa vitendo Dira ya APS-HRMnet ya kuunda mtandao thabiti wa kitaalamu wa mameneja wa rasilimaliwatu katika sekta ya umma kwa kufanikisha malengo ya huduma bora.


Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene amesema kuwa mkutano huo umefanyika katika kipindi ambacho dunia ina changamoto zinazohitaji mijadala, kubadilishana mawazo ili kujibu masuala magumu yanayosababisha watumishi wa umma kutofanya majukumu yao sawasawa.


Naye, Rais wa Mtandao huo Xavier Mrope Daudi amesema kuwa lengo lao ni kukuza ubora, uadilifu na viwango vya taaluma katika utendaji wa usimamizi wa rasilimali watu kwenye sekta ya umma barani Afrika.


“Pia lengo jingine ni kutambua na kushirikisha mbinu bora katika usimamizi wa rasilimali watu ili kusaidia sekta ya umma kuboresha utendaji kazi katika usimamizi wa rasilimali watu.


Kaulimbinu ya mkutano huo ni  “Utawala stahimilivu na Ubunifu: Kukuza Sekta ya Umma ijayo kupitia Uongozi wa Rasilimaliwatu”

WAZIRI MKUU AKUTANA NA BALOZI WA DENMARK NCHINI


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo November 4, 2024 amefanya mazungumzo Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Jespper Kammersgaard, kwenye Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam,


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo November 4, 2024 amefanya mazungumzo Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Jespper Kammersgaard, kwenye Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo November 4, 2024 amefanya mazungumzo Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Jespper Kammersgaard, kwenye Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo November 4, 2024 amefanya mazungumzo Balozi wa Denmark nchini, Mhe. Jespper Kammersgaard, kwenye Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam,

Sunday, November 3, 2024

ADEM YAWAKUTANISHA WALIMU WAKUU 816 MKOANI RUVUMA KUWAPATIA MAFUNZO

 


NA VICTOR MASANGU

Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kukuza sekta ya elimu hapa nchini Walimu Wakuu wametakiwa  kufahamu majukumu,  maono na miongozo inayotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa lengo la kutoa elimu bora kwa wanafunzi.

Aidha wakuu hao wamehumizwa kuweka misingi imara ya kutekeleza  maagizo ambayo yanatolewa na Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) kwa lengo la kuwafundisha watoto kwa kuzingatia misingi ya  weledi ambayo itawafanya waweze kuongeza kiwango cha ufaulu pamoja na kutimiza ndoto zao.


Hayo yamebainishwa na  Mtendaji Mkuu wa ADEM Dkt. Maulid J. Maulid wakati wa  kufunga rasmi  mafunzo ya Walimu Wakuu  wa shule za msingi  wapatao  816 kutoka Mkoani Ruvuma ambayo yamefanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Songea.

“Sekta ya elimu ina jukumu la kuwaandaa Watoto ili kuleta maendeleo katika sekta zingine, hivyo walimu Wakuu mkatekeleze zana ya uongozi bora kwa kuwasimamia walimu shuleni kufundisha kwa ufanisi unaotakiwa ili wanafunzi watimize ndoto zao”. Amesema Dkt. Maulid.


Naye  Afisa elimu Mkoa wa Ruvuma, Bi. Edith Mpenzile akizungumza na walimu wakuu hao amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipa kipaumbele Sekta ya elimu hasa katika eneo la uboreshaji wa miundombinu ya elimu Mkoani Ruvuma. 

Aidha Mwalimu  Mpenzile amewasisitiza Walimu Wakuu hao kwenda kusimamia ustawi na usalama wa wanafunzi shuleni kwani Watoto wanapokuwa shuleni usalama na ustawi wao ni jukumu la mwalimu. 

“Tukawe mfano na chanzo cha mabadiliko ya uongozi na usimamizi wa shule, tusimamie usalama na ustawi wa wanafunzi, nasisitiza tuipe taaluma kipaumbele lakini malezi ya watoto tusiache nyuma”. Amesema Mwl. Mpenzile


Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu-ADEM umeendesha Mafunzo ya Uongozi na Usimamizi wa Shule kwa Walimu Wakuu 816 wa Mkoa wa Ruvuma kwa siku tatu kuanzia tarehe 30 Oktoba hadi tarehe 1 Novemba, 2024 yakilenga kuwajengea uwezo walimu wakuu kuhusu uongozi, usimamizi na uendeshaji fanisi wa shule katika halmashauri zote za Mkoa wa Ruvuma.

Hii ni awamu ya tatu ya mafunzo hayo ambayo yanafanyika katika Mikoa 13 ya Tanzania Bara ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Ruvuma ikihusisha jumla ya Walimu Wakuu 8,551 yakiendeshwa na ADEM chini ya mradi wa BOOST.