VICTOR MASANGU/BAGAMOYO PWANI
SAUTI BY GSENGO.
Shirika lisilokuwa la kiserikali la Organization for Community Development (OCODE) katika kushirikiana na serikali ya awamu ya sita kuwakomboa vijana limeamua kutoa mafunzo ya stadi za maisha na maadili kwa viongozi wa dini,wajumbe wa kamati za umoja wa walimu na wazazi (UWAWA) pamoja na kamati za shule Wilaya ya Bagamoyo lengo ikiwa ni kwenda kutoa elimu zaidi kwa vijana hao.
Hayo yamebainishwa na mratibu wa stadi za maisha Wilaya ya Bagamoyo kutoka Shirika hilo la Ocode Tunu Sanga wakati wa mafunzo hayo ambayo yamefanyika kwa siku moja katika shule ya msingi Nia Njema iliyopo Wilaya ya Bagamoyo na kuwashirikisha washiriki wapatao 37 ambao wamepatiwa uelewa juu ya umuhimu wa stadi za maisha.
Katika mafunzo hayo ya siku moja ambayo yameandaliwa na shirika la Ocode washiriki hao wapatao 37 kutoka Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani wameweza kupatiwa elimu hiyo juu ya stadi za maisha pamoja na maadili ili wawe mabalozi wa kwenda kuwaelimisha vijana wao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.