ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 18, 2025

AFISA MDHIBITI MKUU UBORA WA SHULE MANISPAA YA KIBAHA ATEMA CHECHE KWA WAZAZI JUU YA WATOTO KUANZA MASOMO

 


AFISA Mdhibiti mkuu Ubora wa shule Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha Asha Kiliza amesema wazazi wanatakiwa kuhakikisha watoto wao wanaohitimu elimu ya awali wanaandikishwa mapema kuanza masomo ya darasa la kwanza kwa mwaka 2026.


Amesema wazazi ambao wanawapeleka watoto wao shule binafsi wanatakiwa kuzingatia zile ambazo zimesajiliwa na zinafuata mtaala ulioboreahwa.

Asha ameyasema hayo aliposhiriki mahafali  ya wanafunzi wanaohitimu elimu ya awali katika shule ya msingi ya The Finest iliyopo Kibaha.

Amesema ofisi yake imekuwa ikitoa semina elekezi masuala ya mtaala uliobireshwa kwa shule za binafsi zilizoanzishwa sambamba na kukagua shule hizo kabla hazijapokea wanafunzi.

Kwa mujibu wa Mdhibiti Ubora huyo semina wanayotoa imekuwa ikijikita katika nyanja nane ikiwemo mtaalaunaotumika, vifaa vya mitaala mazingira ya shule pamoja na maadili kwenye shule hizo.

Awali mkurugenzi wa shule hiyo Abubakar Alawi alisema shule hiyo ulianza Octoba 2023 ikiwa na wanafunzi wawili mwalimu mmoja na sasa wamefikia 362 walimu 15.

Mwenyekiti kamati ya shule hiyo ya The Finest Pro. Mrisho Malipula amewataka wazazi kutoa ushirikiano kwa kuwafuatilia wanafunzi na kulipa ada kwa wakati kuepusha kukwama mipango iliyopangwa.

Ameiomba Serikali kuboresha miundombinu ya barabara hiyo kuondoa changamoto ya magari kuharibika na maeneo mengine kutopitika kipindi cha mvua.

VIONGOZI CWT TUKUBALI KUBADILIKA - DKT. DOTO BITEKO

“ Tumetoka mbali, zamani familia iliyokuwa maarufu na kuheshimika kijijini ni ile iliyokuwa na taa ya chemli na watu walijipanga kuangalia namna inavyofaidi mwanga, Dunia imebadilika kwa kiwango ambacho leo hii kila nyumba ina umeme na watu wanaona umeme kama hitaji la lazima kwenye maisha yao, Nataka niwaombe walimu wote nchini endeleeni kuishi kwa dunia inayobadilika, fikirini upya kila siku. Viongozi mnatakiwa kuwafikia walimu wote, kuwasikiliza na kuwahudumia ili wapate sababu ya kuwapenda ”. amesema Dkt. Biteko


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema hayo Oktoba 16, 2025 katika Manispaa ya Musoma, Mkoani Mara wakati akifungua Semina ya Viongozi wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) kanda ya Ziwa na kanda ya Magharibi iliyoshirikisha viongozi kutoka mikoa minane.

MWANAMKE GEITA ATIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MUME WAKE NA KUMZIKA NDANI YA NYUMBA


Jeshi la Polisi mkoani Geita linamshikilia mwanamke aitwaye Martha Japhet (44), mkazi wa Kitongoji cha Mzalendo, Kata ya Nyarugusu, Wilaya ya Geita, kwa tuhuma za kumuua mume wake na kumzika ndani ya nyumba yao, kisha kufunika kaburi hilo kwa magunia ya muhogo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Safia Jongo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akibainisha kuwa mauaji hayo yalifanyika usiku wa Oktoba 11, 2025, majira ya saa 3:00, na kugundulika Oktoba 16, 2025, majira ya saa 7:00 mchana.

Kwa mujibu wa Kamanda Jongo, uchunguzi wa awali umebaini kuwa mama huyo alimjeruhi mumewe kwa kitu chenye ncha kali baada ya kutokea ugomvi baina yao. Baada ya tukio hilo, watoto wa familia hiyo walianza kumtafuta baba yao bila mafanikio, hali iliyozua mashaka miongoni mwa majirani na hatimaye kufanikisha kugundulika kwa tukio hilo.

Kamanda Jongo ametoa wito kwa jamii kuepuka tabia ya kujichukulia sheria mkononi wanapokumbana na changamoto au migogoro ya kifamilia. Pia, amesisitiza umuhimu wa kutoa taarifa kwa vyombo vya usalama pale mtu anapopotea au kunapotokea tukio linalotia shaka.

“Wakati mwingine matukio ya watu kupotea huchangiwa na watu wa karibu kabisa, hivyo jamii inapaswa kuwa makini na kutoa taarifa mapema,” alisema Kamanda Jongo.

'UCHAPAKAZI UNALIPA' MALUNDE 1 BLOG WANYAKUWA TUZO SHINYANGA.


 Hongera nyingi kwa Malunde 1 Blog kwa ushindi huu wa heshima katika Mdau Awards Shinyanga – kipengele cha Uandishi Bora na Upashaji Habari Bora! 


Gsengo Blog inatoa pongezi za dhati kwa Bwana Kadama Malunde, Mkurugenzi, mmiliki na muasisi wa blogu hiyo, pamoja na timu nzima ya waandishi wanaofanikisha kazi hii kwa bidii na ubunifu.

Tuzo hii ni uthibitisho kwamba kazi nzuri, uaminifu na weledi hulipa.  

Hongereni sana Malunde 1 Blog — endeleeni kung’ara na kuweka historia!



Friday, October 17, 2025

VIDEO;-RC MTANDA AFUNGUKA MAZITO AZINDUA BODI YA NANE YA MAJI BONDE LA ZIWA VICTORIA NA KUKABIDHI MAGARI

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameitaka bodi mpya ya Bonde la ziwa Victoria kusimamia menejimenti ya bonde la ziwa hilo ili iwajibike ipasavyo katika kulinda rasilimali maji kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo. Mhe. Mtanda ametoa rai hiyo jana tarehe 15 Oktoba, 2025 wakati akizindua bodi ya nane ya bonde hilo pamoja na vitendea kazi (Magari) kwa ajili ya matumizi ya bodi hiyo hafla iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya bonde hilo jijini Mwanza. Mhe. Mtanda amesema katika kutekeleza majukumu yao wana wajibu wa kutoa elimu kwa jamii juu ya taratibu na sheria za matumizi ya rasilimali maji na sio kusubiri mwananchi akosee ndipo wamchukulie hatua hususani wanaochimba visima vya maji. Aidha, Mhe. Mtanda ameishukuru Serikali kwa kutoa Tshs.Bilioni 264.8 mkoani humo katika sekta ya maji ambazo zimetumika kuongeza upatikanaji wa maji mjini vijijini kutoka 58% hadi 85% na kutoka 53% hadi 77% kwa mjini huku akibainisha uwepo wa miradi kadhaa vijijini na mijini.

WINNIE ODINGA AFAFANUA KUHUSU KIFO CHA RAILA : "ALIKUFA MIKONONI MWANGU"

 Winnie alifichua kuwa baba yake aliendelea kuwa na nguvu hadi dakika za mwisho. 

Alikuwa amezoea kufanya mazoezi kila asubuhi. Katika siku hiyo ya maafa, Winnie alisema kuwa babake alitembea kwa raundi tano, na Wakenya wanapaswa kujivunia kwamba alikufa kama mwanajeshi. 

"Leo tunaposherehekea maisha yake, nilichagua sio tu kukumbuka kiongozi ambaye kila mtu alijua, lakini baba ambaye nilimpenda kwa kila utu wangu. Sehemu kubwa zaidi ya mimi nilikufa mnamo Oktoba 15. Roho ya simba inanguruma milele. 

Nilikuwa naye India wakati alivuta pumzi yake ya mwisho. Alikufa mikononi mwangu, lakini hakufa kama watu wamekuwa wakisema kwenye mitandao ya kijamii. Kila siku angeamka asubuhi na kutembea kila siku. alisukuma hadi raundi tano alikufa kwa nguvu na kwa heshima na kiburi na lazima ujivunie kwa hilo. 

Winnie pia aligusia kujifunza kuhusu matakwa ya mwisho ya baba yake. 

"Sijui nitamkosa nani zaidi baba yangu au shujaa wangu. Nilikuwa msichana mwenye bahati zaidi duniani kwa sababu ulikuwa baba yangu. Baba, ulikuwa mwepesi, thabiti, mnyenyekevu, na mwanadamu. Ulipokuwa mdogo walikuita Aluo, wakaanza kukuita mtoto wa Jaramogi. Kwangu mimi, ulikuwa baba tu, mtu ambaye uwepo wake ulikuwa wa kawaida." 


Thursday, October 16, 2025

RC MTANDA AZINDUA BODI YA NANE YA YA MAJI BONDE LA ZIWA VICTORIA

 

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda ameitaka bodi mpya ya Bonde la ziwa Victoria kusimamia menejimenti ya bonde la ziwa hilo ili iwajibike ipasavyo katika kulinda rasilimali maji kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Mhe. Mtanda ametoa rai hiyo JANA tarehe 15 Oktoba, 2025 wakati akizindua bodi ya nane ya bonde hilo pamoja na vitendea kazi (Magari) kwa ajili ya matumizi ya bodi hiyo hafla iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya bonde hilo jijini Mwanza.
Mhe. Mtanda amesema katika kutekeleza majukumu yao wana wajibu wa kutoa elimu kwa jamii juu ya taratibu na sheria za matumizi ya rasilimali maji na sio kusubiri mwananchi akosee ndipo wamchukulie hatua hususani wanaochimba visima vya maji.

Aidha, Mhe. Mtanda ameishukuru Serikali kwa kutoa Tshs.Bilioni 264.8 mkoani humo katika sekta ya maji ambazo zimetumika kuongeza upatikanaji wa maji mjini vijijini kutoka 58% hadi 85% na kutoka 53% hadi 77% kwa mjini huku akibainisha uwepo wa miradi kadhaa vijijini na mijini.

Akitoa salamu kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara, Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji Bw. Robert Sande amesema bodi ya nane inaingia rasmi kufuatia kufikia ukomo wa bodi ya saba mwezi juni mwaka huu iliyodumu kwa miaka mitatu kutoka Disemba 03, 2022.

Ameongeza kuwa Dira ya Taifa ya 2050 inalenga kuifikisha nchi kwenye uchumi wa kati na imeelekeza kuwepo kwa rasilimaji maji ya kutosha na usimamizi wa rasilimali maji na eneo oevu hivyo bodi hiyo mpya ina jukumu la kutekeleza hayo pamoja kutekeleza sera mpya ya maji ya mwaka 2002 toleo la 2025.

Naye aliyekuwa Mwenyekiti wa bodi iliyomaliza muda wake Dkt. Boniventura Baya amesema bodi ya saba imepata hati safi mfululizo kutoka kwa CAG na kwamba wamefanya tathmini na ufuatiliaji wa uwingi na kuthibiti ubora na usalama wa rasilimaji za maji pamoja na kulinda vyanzo vya maji.







YANGA SC YAWASILI SALAMA LILONGWE KUIVAA SILVER STRIKERS JUMAMOSI

 

KIKOSI cha Yanga kimewasili salama Jijini Lilongwe, Malawi tayari kwa mchezo wa kwanza wa Raundi ya Pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Silver Strikers Jumamosi.

Msafara wa Yanga ulioondoka Saa 1:40 mapema asubuhi ya leo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam ulifika Lilongwe Saa 4:44 tayari kwa mchezo huo es Oktoba 18 Uwanja wa Taifa wa Bingu Jijini Lilongwe.

Kocha mpya Msaidizi wa Yanga — Mmalawi Patrick Mabedi ni miongoni mwa waliosafiri na timu wiki moja tangu ajiunge na kikosi cha Wananchi kuliongezea nguvu benchi la Ufundi chini ya Kocha Mkuu, Mfaransa Romain Folz.

SIMBA SC YAWAFUATA HOTSPURS ESWATINI BILA KIPA NAMBA MOJA CAMARA

KIKOSI cha Simba SC kimeondoka bila kipa wake namba moja, Mousa ‘Pin Pin’ Camara raia wa Guinea kwenda Eswatini kwa ajili mchezo wa kwanza za Raundi ya Pili Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Nsingizini Hotspurs.

Kuelekea mchezo huo wa Jumapili ya Oktoba 19 Uwanja wa Taifa wa Somhlolo mjini Lobamba — Simba imeondoka na makipa wawili, Yakoub Suleiman na Hussein Abel.
Timu hizo zitarudiana Jumapili nyingine ya Oktoba 26 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na mshindi wa jumla ataingia hatua ya makundi inayohusisha timu 16.

Kikosi cha wachezaji wa klabu ya Simba Sc kuelekea mchezo wake wa Klabu Bingwa utakaochezwa siku ya Jumapili ya Oktoba 19 Uwanja wa Taifa wa Somhlolo mjini Lobamba 


VIDEO;- TANZANIA YAZINDUA MRADI WA DUNIA KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO NA DHARURA ZA KIAFYA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezindua Mradi wa Dunia wa kukabiliana na magonjwa ya Mlipuko nchini na kuzitaka wizara zote tawala za mikoa na serikali za mitaa pamoja na taasisi kutekeleza shughuli za kipaumbele katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na dharura za kiafya. Dkt. Biteko ametoa agizo hilo Oktoba 15, 2025 jijini Mwanza na kusema mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 38.7 unalenga kuboresha huduma za afya kwa watanzania na kuchochea maendeleo ya nchi. Amesisitiza kuwa wizara, taasisi na washirika wa maendeleo wanatakiwa kusimamia utekelezaji katika uwekezaji huo na kuhakikisha yanapatikana matokeo chanya kama ilivyokusudiwa.

Wednesday, October 15, 2025

TANZANIA YAZINDUA MRADI WA DUNIA KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO NA DHARURA ZA KIAFYA


📌 Dkt. Biteko ataka utekelezaji wa kuleta matokeo chanya

📌 Mradi kugharimu Dola za Kimarekani milioni 38.7

📌 WHO, FAO, UNICEF na Pandemic Fund zaipongeza Tanzania

 

Na Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezindua Mradi wa Dunia wa kukabiliana na magonjwa ya Mlipuko nchini na kuzitaka wizara zote tawala za mikoa na serikali za mitaa pamoja na taasisi kutekeleza shughuli za kipaumbele katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko na dharura za kiafya.

Dkt. Biteko ametoa agizo hilo Oktoba 15, 2025 jijini Mwanza na kusema mradi huo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 38.7 unalenga kuboresha huduma za afya kwa watanzania na kuchochea maendeleo ya nchi.


Amesisitiza kuwa wizara, taasisi na washirika wa maendeleo wanatakiwa kusimamia utekelezaji katika uwekezaji huo na kuhakikisha yanapatikana matokeo chanya kama ilivyokusudiwa.

“Wizara zote, Tawala za mikoa na Taasisi , tekelezeni shughuli zote za kipaumbele katika kukabiliana na magonjwa haya ya mlipuko na dharura nyingine za afya kulingana na maeneo yenu na hakikisha kwamba hakuna hata shilingi moja inayopotea au kuchepushwa kando ya malengo yaliyokusudiwa,” amesema Dkt. Biteko.


Amesema kuwa Serikali kwa upande wake itaendelea kushirikiana na wadau wote wa ndani na nje ya nchi kuimairsha mradi huo ili uweze kuleta matokeo chanya katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ambayo yamekuwa tishio kwa maisha ya watu na kurudisha nyuma maendeleo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Ummy Nderiananga amesema uzinduzi wa mradi huo, ni muhimu katika jitihaza za kukabiliana na magonjwa ya mlipuko. 


Amesema mradi huo unatekelezwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia sehemu ya Afya moja pamoja na wadau wa maendeleo likiwemo Shirika la Afya Duniani(WHO), Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) na Pandemic Fund.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya ambaye ni Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe amesema mradi huo utaboresha mwitikio wa mifumo ya afya katika kukabiliana na magonjwa kama Ebola, MPOX, Marburg, ZIKA na magonjwa mengine yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi.


Dkt. Magembe amefafanua kuwa utekelezaji madhubuti utawezesha upatikanaji wa taarifa za haraka kuhusu uwepo au uvumi kuhusu magonjwa ya mlipuko na hivyo kuzifanyia kazi taarifa hizo.


Amesema upatikanaji wa fedha hizo utawezesha pia maboresho ya maabara ya taifa na kikanda ikiwa ni njia ya kupata taarifa za haraka kwa usahihi kutoka kwa wananchi.

Akizungumzia utekelezaji wa mpango huo, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt. Salim Nassor Slim amewashukuru viongozi wa Kitaifa kwa hatua za kuboresha afya za wananchi ili kuwa na afya bora.


Naye Naibu Mwakilishi Mkazi wa UNICEF, Dkt. Patricia Safi ameipongeza Tanzania kwa ushirikiano ulipo kati yake na mashirika ya kimataifa na kuongeza kuwa Shirika hilo litahakikisha linaendeleza mashirikiano katika kutatua changamoto za kijamii.


Amesema UNICEF itahakikisha mchango wake unajikita katika maendeleo ya mtoto na kufanya jitihada za kuwezesha watoto wote wanapata huduma kwa mujibu wa mipango iliyopo.

Tuesday, October 14, 2025

IRAN YAIKAMUA STARS 2-0


 Ni katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliochezwa katika dimba la Al Rashid Stadium pale Dubai ambapo timu ya Iran imeibuka na ushindi wa mabao mawili bila majibu dhidi ya Stars.

Wafungaji wa Iran ni washambuliaji Amirhossein Hosseinzadeh dakika ya 17 kwa njia ya penati baada ya beki wa Stars Ibrahim Baka kufanya madhambi ndani ya 18, na  Mohhamad Mehdi Mohebi katika dakika ya  28 aliyepokea pande kutoka kwa K. Taheri.

'SIMBA YAKATAA UHUNI'

 

UONGOZI wa Simba SC umeweka wazi kuwa haukubaliani na vitendo vya kihuni kwenye mpira wa miguu kwa kuwa unarudisha nyuma maendeleo ya wachezaji na timu kiujumla.

Simba SC inapeperusha bendera katika Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa hatua ya pili inatarajiwa kucheza mchezo wake wa kimataifa dhidi ya Nsiginzini Hotspurs Oktoba 19 2025 pia inaongoza ligi ikiwa na pointi sita baada ya mechi mbili.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa vitendo vya kihuni ambavyo vinatokea uwanjani kwa wachezaji kuchezeana rafu mbaya vinaumiza wachezaji na kudumaza maendeleo ya mpira kutokana na wachezaji kukaa nje muda mrefu wakipambania hali zao.

“Vitendo vya kihuni kwenye mpira wa miguu havifai kwa kuwa vinadumaza maendeleo ya mpira na sio mpira tu hata maendeleo ya mchezaji husika yanadumaa kwa kuwa maisha yake yapo kwenye mpira hapo anaendeleza maisha na familia.

“Inapotokea mchezaji mwingine anamchezea faulo mbaya mchezaji hii inamaana kwamba anahatarisha maisha yake na maisha ya familia yake. Wapo wachezaji ambao wamekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu na hii imetokana na kufanyiwa vitendo vya kihuni.

“Muhimu kila mchezaji kuwa mlinzi wa mchezaji mwengine hili litafanya mpira usiwe wa kihuni na rafu mbaya hazifai kwa kuwa mpira ni maisha na maisha yanatengenezwa kila hatua ambayo inapigwa.”

TAKRIBANI SH BILIONI 245 ZAHITAJIKA KUTEKELEZA MPANGO WA USIMAMIZI MAJI-BONDE LA MAJI ZIWA VICTORIA

 NA ALBERT G. SENGO/ MWANZA

Takribani shilingi Bilioni 245 zahitajika kutekeleza Mpango wa Usimamizi wa Maji – BONDE LA ZIWA VICTORIA. Robert Sunday, ni Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji, akizungumza kwenye Jukwaa la Wadau wa Sekta Mtambuka lililofanyika jijini Mwanza, anasema fedha hizo zinahitajika kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa Usimamizi wa Rasilimali za Maji katika Bonde la Maji la Ziwa Victoria, ikiwa ni pamoja na utoaji elimu ya utunzaji mazingira. Sunday amesema mpango huo unalenga kuboresha matumizi endelevu ya maji, uhifadhi wa vyanzo vya maji, pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na shughuli za usafi wa mazingira kwa jamii zinazozunguka bonde hilo. Aidha, amewataka wadau kushirikiana kwa karibu na serikali katika utekelezaji wa mikakati hiyo ili kuhakikisha upatikanaji wa maji salama, usalama wa mazingira na maendeleo ya kijamii na kiuchumi vinaimarika. Tathmini ya Umoja wa Afrika ikishirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika na Shirika la Global Worker Partnership imeonyesha kuwa ili bara la Afrika lifikie malengo endelevu ya kimataifa ifikapo mwaka 2030, zinahitajika dola za Marekani milioni 30 kwa mwaka kwa ajili ya sekta ya maji.

HUYU NDIYO NYERERE TUNAYEMUADHIMISHA LEO / MIAKA 26 BILA NYERERE


Huyu Ndiyo Nyerere Tunayemuadhimisha leo 


NA DENIS MPAGAZE
__________________

1. Alizaliwa April, 13, 1922, katika familia ya kichifu!
2. Akasoma mpaka Ulaya, akapata ajira, akaiacha na kwenda kupigania Uhuru!
3. Tanganyika tukawa huru, lakini akasema, “Uhuru wetu hauwezi kuwa na maana kama wenzetu bado wanatawaliwa”,
4. Akaelekeza nguvu kuikomboa Afrika, Tanzania ikawa kambi ya Wapigania Uhuru wa nchi za Kusini mwa Afrika!
5. Urafiki Jazz wakamtia moyo Mwalimu kwa vibao murua, Afrika ikawa Huru!
6. Oktoba 1999 Nyerere akapumzika akiwa maskini wa vitu na mali, lakini tajiri wa watu na utu!
7. Siku ile Nyerere amezaliwa, aliitwa Mugendi yaani ‘Mtembezi’ au tuseme *‘Mzurulaji,’!
8. Lakini mizimu ya ukoo wao ikalikataa jina hilo na kuwashauri wamuite “Kambarage”
9. Jina la Spirit wa Mvua, Wazee wakatii maana walijua nguvu ya jina!
10. Mugendi’ akaitwa Kambarage, akaja na mvua ya Uhuru, ikanyesha Tanganyika na Afrika yote. 
11. Katika tumbo la Mama Nyerere walizaliwa watoto nane na katika viuno vya baba yake walitoka watoto 25. 
12. Mzee alikuwa na wake 22 na masuria wanne tu. Wote aliowahudumia kwa umaridadi!
13. Mzee Francis Atwoli anasema mwanaume unakuwa na mke mmoja, SHENZI ðŸ˜€ðŸ˜€
14. Sijui wazee wa zamani walikula nini? Imagine! Baba yake Nyerere alioa kabinti ka mia 15 yeye akiwa na miaka 47, halafu akazaliwa Nyerere, Mkombozi wa Afrika. 
15. Nyerere alitafutiwa kabinti ka miaka minne ili akaoe, akachomoa. Kaliitwa Magori Watiha. Hata mie ningechomoa🤭.
16. Nyerere alipenda kula sana mtama kwa sababu mtama una miujiza kibao walisema wahenga. 
17. Hata Kinjekitile aliutumia kuwatia msukosuko wajerumani kwenye ile vita ya maji maji.
18. Kuleni mtama nyie, shauri lenu!  
19. Nyerere alibarikiwa akili nyingi za darasani na maishani. 
20. Darasani aliwashangaza walimu kwa uwezo wa kujibu maswali kwa haraka na umaridani mkubwa hadi kumrusha darasa.
21. Shuleni hakuwa na muda na michezo. Yeye alikwenda kusoma na akasoma kweli. 
22. Hakuwa na mambo mengi kama wanafunzi wa siku hizi. Wana mambo mengi kama unga wa ngano ati. 
23. Mapenzi wao, michezo wao, uongo wao, utoro wao, uchonganishi wao, wizi wa mitihani wao, uvuvi wao, loh!
24. Bidii ya Nyerere katika masomi ilimg’arisha ndani na nje ya nchi. 
25. Mwaka 1936 alivyohitimu Shule ya Msingi Mwisenge aliongoza kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi katika mtihani wa taifa. 
26. Serikali ya Mkoloni ikampa ufadhili wa kwenda Tabora School, huko nako akapiga na kwenda zake Makerere Uganda. 
27. Makerere aliingia 1943. Huko ndiko Falsafa na Mitazamo ya Nyerere kuhusu binadamu wote ni sawa ilikoanza kuonekana. 
28. Hata kazi alizosoma zilirelate na fikra zake. Alimsoma sana John Stuart Mill. 
29. Huyu John Mill ndiye aliyesema kabla hujafanya maamuzi yoyote zingatia matokeo yatakayozalisha furaha kubwa kwa watu wengi. 
30. Nyerere alimuelewa sana huyu Mzee Mill na kuziishi fikra zake. 
31. Fikra hizi ndo zilimsukuma Nyerere kuacha mshahara mnono kwenda kupigania uhuru Tanganyika ili kuwafurahisha wengi.
32. Lakini pia Nyerere hakuwa mtu wa tamaa ya mali na vitu, bali watu na utu. 
33. Hata serikali ilipomjengea nyumba aliwashushua na kuwaambia jumba lote la nini kwani mie tembo?  
34. Sisi hata kama nyumba unazo, bado ukijengewa nyingine unapokea ðŸ¤­ðŸ¤­
35. Pamoja na kusoma kwake hadi Ulaya hakudharau tamaduni za kwao.
36. Nyerere alikuwa muungwana. Unyenyekevu wake ulimvutia kila mtu kutaka kufanya naye kazi.
37. Halafu tangu shule ya msingi mpaka chuo kikuu kule Scotland, Nyerere alipinga unyonyaji na ubepari kwa dhati. 
38. Akiwa shule ya msingi alipambana na Herman Abdallah, mkuu wa shule baada ya kula fedha za wanafunzi.
39. Aliadhibiwa kwa utovu wa nidhamu lakini ujumbe ulifika. 
40. Nyerere akiwa Makerere alindika barua kwa mhariri wa gazeti la Tanganyika Standard kulaani ubepari. 
41. Katika Barua hiyo ya Julai 1943 alisema ni vigumu sana kupractice ubepari Afrika kwa sababu waafrika ni wajamaa kwa asili.
42. Lakini pia mwaka 1951, wakiwa Scotland yeye na John Keto waliandika makala kwenye gazeti la chuo kupinga mpango wa mkoloni kuingiza Tanganyika katika shirikisho la Rhodesia na Nyasaland.
43. Alipinga pia unyanyasaji wa kijinsia kwa kuandika insha akionyesha application ya falsafa za Mills katika haki za wanawake. 
44. Mara nyingi aliwachallenge wanawake kama wanataka kuondoa unyanyasaji wa kijinsia basi waanze na kupinga mahari.
45. Katika hilo hakueleweka kabisa ndo maana mahari zinaendelea mpaka leo!
46. Pamoja na harakati zote hizo, hakumsahau mama yake mjane. 
47. Hata siku ile ametoka Makerere breki ya kwanza ilikuwa kwa mama yake, kumjengea nyumba.
48. Kitendo hiki kilimfariji sana mama yeke aliyeachwa na mume wake mpenzi . 
49. Mumewe alifariki Machi 1942 Nyerere akiwa mwaka wa mwisho pale Tabora Scholl na alinyimwa ruhusa ya kwenda kumzika mama yake.
50. Nyerere akiwa Tabora, alijiunga na chama cha TAA. Alichaguliwa kuwa mweka hazina wa chama kwa sababu hakuwa mwizi.
51. Alikuwa na kina Chifu Fundikira. Wakafungua Duka la Ushirika na kuuza mahitaji madogo madogo kama sukari, unga na sabuni. 
52. Aprili 1946 alhudhuria mkutanao wa TAA Dar es Salaam, mkutano uliotangaza rasmi kuingia kwenye harakati za kupigania Uhuru.

38. Hata hivyo mwaka 1949 kwa ushauri wa Fr Richard Walsh, Mkuu wa Shule, Nyerere alikwenda Scotland kwa masomo ya juu. 
39. Huko alipiga Master of Arts Degree pale University of Edinburgh.
40. Aliwaza sana angemuachaje mama yake lakini akapiga moyo konde, akaenda Ulaya kwa sababu safari siyo kifo. 
41. Ulaya alipiga vibarua mashambani kujiongezea kipato na kusupport familia yake.
42. Nyerere alimaliza masomo yake Ulaya na Oktoba 1952 alirejea nyumbani, akajenga kijumba pale Musoma, kisha akafunga ndoa na mpenzi wake Maria Gabriel, kutoka kabila tofauti. 
43. Ilikuwa 24 Januari 1953. Alioa kabila lingine kwa sababu hakuamini katika ukabila. 
44. After all Afrika hatukuwa na ukabila, tulikuwa na koo. Ukabila uliletewa na wakoloni kutugawa.
45. Baada ya ndoa walihamia Pugu, St Francis’ College, alikoajiriwa kwa kazi ya ualimu. 
46. Mwaka 1953 wakabarikiwa mtoto wa kiume, wakamuita Andrew Burrito na kufatiwa na Anna Watiku, Anselm Magige, John Guido, Charles Makongoro, Godfrey Madaraka, Rosemary Huria na Pauleta Nyabanane. John tu ndo alifariki.
47. Andrew ndo yule Mzee aliyesema Rais Samia asiende kutembelea kaburi la Baba wa Taifa😀😀! Andrew ana mambo nyie. 
48. Hakuna mtoto wa Nyerere aliyefia kwenye ndege kipindi za Vita vya Kagera kama ulivyokuwa unajua. 
49. April 1953, Nyerere alichaguliwa kuwa Rais wa TAA, kutokana na umahiri wake wa kuongea na kujenga hoja. 
50. Julai 7, 1954 TAA ilibadilishwa na kuwa TANU. Historia ya TAA ni ndefu pia.
51. Agosti 1954, Umoja wa Mataifa ulipendekeza Tanganyika kupata Uhuru miaka 25 ijayo. 
52. Wazee wakasema acheni utoto. Miaka 25 nyie kuweza?
53. Wazee wakamtuma Kambarage kwenda UNO kupinga hoja kwa hoja! 
54. John Rupia ndo alilipa nauli. March 1955, Nyerere akatinga UNO. Akajenga hoja za utayari wa kujitawala mpaka UNO yote ikalegea.
55. Mkoloni akashinikiza Kanisa limfukuze kazi Nyerere asijeleta vurugu kama Mau Mau. 
56. Kanisa ndo lilimuajiri, likamwambia achague siasa au kazi. Nyerere akachagua siasa. 
57. “Mpendwa Fr. Lynch, tayari nimezingatia chaguo ulilonipatia, kati ya ajira yangu shuleni na uanachama wa TANU , na nimefikia uamuzi kwamba ni lazima nijiudhuru kazi yangu ya kufundisha,” aliandika Nyerere katika Barua yake ya 22 Mach 1955. 
58. April 1955 Nyerere akamrudisha mke wake kijijini Butiama, Mwitongo na Oktoba 1955 akarudi Dar es Salaam tayari kwa mashambulizi ya uhuru. Alizunguka nchi nzima akihubiri uhuru. 
59. Alitumia Landrover la TANU. Mikutano ya Nyerere ilikuwa amsha amsha! Watu walifurika hatari.
60. Alihamasisha matumizi ya amani badala ya nguvu katika kupigania Uhuru na watu walimtii. 
61. Alimuiga Mahtma Ghandi, yule mpigania Uhuru wa India aliyeamini amani haiji kwa ncha ya upanga.
62. Upepo wa Nyerere ulimsumbua sana Edward Twining, Gavana wa Tanganyika hadi na yeye akaanzisha chama cha United Tanganyika Party (UTP) ili kupambana na TANU.
63. Twining alimtuhumu Nyerere kwamba anahubiri ubaguzi nchini. 
64. Nyerere akasema, tunapambana dhidi ya ukoloni na siyo wazungu. 
65. Wazungu walifanya mengi mazuri tatizo lao yaliwanufaisha wachache. 
66. Hayo ndo Nyerere aliyapinga mpaka kuwaita wakoloni mashetani na maharamia wakamshitaki na kumpiga faini. 
67. Aliwatukana kupitia gazeti lake la SAUTI YA TANU mwaka 1958. Alipigwa faini ya Sh 3,000.
68. Akazilipa, Bibi Tit Mohammed na wanawake wanzake wakafurahi mzee kukwepa kifungo. 
69. Walipitia changamoto nyingi wakati wa kupigania uhuru. 
70. Kuna wakati walizinguana wao kwa wao, siku nyingine mkoloni akawazingua, tutayaangalia haya katika sehemu ya pili!
.
Pata ofa hizi za Nyerere kwa Sh 10,000 tu. Ni softcopy. Mpesa 0740590451

1. Tunisahihishe by Nyerere
2. Uongozi Wetu by Nyerere
3. Moyo wa Kujitolea by Nyerere
4. Ujamaa; Essays on Socialism
5. Man and Development

Cheers
Mwl. Denis Mpagaze
Muhenga wa Karne ya 21!