Huyu Ndiyo Nyerere Tunayemuadhimisha leo
NA DENIS MPAGAZE
__________________
1. Alizaliwa April, 13, 1922, katika familia ya kichifu!
2. Akasoma mpaka Ulaya, akapata ajira, akaiacha na kwenda kupigania Uhuru!
3. Tanganyika tukawa huru, lakini akasema, “Uhuru wetu hauwezi kuwa na maana kama wenzetu bado wanatawaliwa”,
4. Akaelekeza nguvu kuikomboa Afrika, Tanzania ikawa kambi ya Wapigania Uhuru wa nchi za Kusini mwa Afrika!
5. Urafiki Jazz wakamtia moyo Mwalimu kwa vibao murua, Afrika ikawa Huru!
6. Oktoba 1999 Nyerere akapumzika akiwa maskini wa vitu na mali, lakini tajiri wa watu na utu!
7. Siku ile Nyerere amezaliwa, aliitwa Mugendi yaani ‘Mtembezi’ au tuseme *‘Mzurulaji,’!
8. Lakini mizimu ya ukoo wao ikalikataa jina hilo na kuwashauri wamuite “Kambarage”
9. Jina la Spirit wa Mvua, Wazee wakatii maana walijua nguvu ya jina!
10. Mugendi’ akaitwa Kambarage, akaja na mvua ya Uhuru, ikanyesha Tanganyika na Afrika yote.
11. Katika tumbo la Mama Nyerere walizaliwa watoto nane na katika viuno vya baba yake walitoka watoto 25.
12. Mzee alikuwa na wake 22 na masuria wanne tu. Wote aliowahudumia kwa umaridadi!
13. Mzee Francis Atwoli anasema mwanaume unakuwa na mke mmoja, SHENZI 



14. Sijui wazee wa zamani walikula nini? Imagine! Baba yake Nyerere alioa kabinti ka mia 15 yeye akiwa na miaka 47, halafu akazaliwa Nyerere, Mkombozi wa Afrika.
15. Nyerere alitafutiwa kabinti ka miaka minne ili akaoe, akachomoa. Kaliitwa Magori Watiha. Hata mie ningechomoa
.
.16. Nyerere alipenda kula sana mtama kwa sababu mtama una miujiza kibao walisema wahenga.
17. Hata Kinjekitile aliutumia kuwatia msukosuko wajerumani kwenye ile vita ya maji maji.
18. Kuleni mtama nyie, shauri lenu!
19. Nyerere alibarikiwa akili nyingi za darasani na maishani.
20. Darasani aliwashangaza walimu kwa uwezo wa kujibu maswali kwa haraka na umaridani mkubwa hadi kumrusha darasa.
21. Shuleni hakuwa na muda na michezo. Yeye alikwenda kusoma na akasoma kweli.
22. Hakuwa na mambo mengi kama wanafunzi wa siku hizi. Wana mambo mengi kama unga wa ngano ati.
23. Mapenzi wao, michezo wao, uongo wao, utoro wao, uchonganishi wao, wizi wa mitihani wao, uvuvi wao, loh!
24. Bidii ya Nyerere katika masomi ilimg’arisha ndani na nje ya nchi.
25. Mwaka 1936 alivyohitimu Shule ya Msingi Mwisenge aliongoza kanda ya Ziwa na Kanda ya Magharibi katika mtihani wa taifa.
26. Serikali ya Mkoloni ikampa ufadhili wa kwenda Tabora School, huko nako akapiga na kwenda zake Makerere Uganda.
27. Makerere aliingia 1943. Huko ndiko Falsafa na Mitazamo ya Nyerere kuhusu binadamu wote ni sawa ilikoanza kuonekana.
28. Hata kazi alizosoma zilirelate na fikra zake. Alimsoma sana John Stuart Mill.
29. Huyu John Mill ndiye aliyesema kabla hujafanya maamuzi yoyote zingatia matokeo yatakayozalisha furaha kubwa kwa watu wengi.
30. Nyerere alimuelewa sana huyu Mzee Mill na kuziishi fikra zake.
31. Fikra hizi ndo zilimsukuma Nyerere kuacha mshahara mnono kwenda kupigania uhuru Tanganyika ili kuwafurahisha wengi.
32. Lakini pia Nyerere hakuwa mtu wa tamaa ya mali na vitu, bali watu na utu.
33. Hata serikali ilipomjengea nyumba aliwashushua na kuwaambia jumba lote la nini kwani mie tembo?
34. Sisi hata kama nyumba unazo, bado ukijengewa nyingine unapokea 



35. Pamoja na kusoma kwake hadi Ulaya hakudharau tamaduni za kwao.
36. Nyerere alikuwa muungwana. Unyenyekevu wake ulimvutia kila mtu kutaka kufanya naye kazi.
37. Halafu tangu shule ya msingi mpaka chuo kikuu kule Scotland, Nyerere alipinga unyonyaji na ubepari kwa dhati.
38. Akiwa shule ya msingi alipambana na Herman Abdallah, mkuu wa shule baada ya kula fedha za wanafunzi.
39. Aliadhibiwa kwa utovu wa nidhamu lakini ujumbe ulifika.
40. Nyerere akiwa Makerere alindika barua kwa mhariri wa gazeti la Tanganyika Standard kulaani ubepari.
41. Katika Barua hiyo ya Julai 1943 alisema ni vigumu sana kupractice ubepari Afrika kwa sababu waafrika ni wajamaa kwa asili.
42. Lakini pia mwaka 1951, wakiwa Scotland yeye na John Keto waliandika makala kwenye gazeti la chuo kupinga mpango wa mkoloni kuingiza Tanganyika katika shirikisho la Rhodesia na Nyasaland.
43. Alipinga pia unyanyasaji wa kijinsia kwa kuandika insha akionyesha application ya falsafa za Mills katika haki za wanawake.
44. Mara nyingi aliwachallenge wanawake kama wanataka kuondoa unyanyasaji wa kijinsia basi waanze na kupinga mahari.
45. Katika hilo hakueleweka kabisa ndo maana mahari zinaendelea mpaka leo!
46. Pamoja na harakati zote hizo, hakumsahau mama yake mjane.
47. Hata siku ile ametoka Makerere breki ya kwanza ilikuwa kwa mama yake, kumjengea nyumba.
48. Kitendo hiki kilimfariji sana mama yeke aliyeachwa na mume wake mpenzi .
49. Mumewe alifariki Machi 1942 Nyerere akiwa mwaka wa mwisho pale Tabora Scholl na alinyimwa ruhusa ya kwenda kumzika mama yake.
50. Nyerere akiwa Tabora, alijiunga na chama cha TAA. Alichaguliwa kuwa mweka hazina wa chama kwa sababu hakuwa mwizi.
51. Alikuwa na kina Chifu Fundikira. Wakafungua Duka la Ushirika na kuuza mahitaji madogo madogo kama sukari, unga na sabuni.
52. Aprili 1946 alhudhuria mkutanao wa TAA Dar es Salaam, mkutano uliotangaza rasmi kuingia kwenye harakati za kupigania Uhuru.
38. Hata hivyo mwaka 1949 kwa ushauri wa Fr Richard Walsh, Mkuu wa Shule, Nyerere alikwenda Scotland kwa masomo ya juu.
39. Huko alipiga Master of Arts Degree pale University of Edinburgh.
40. Aliwaza sana angemuachaje mama yake lakini akapiga moyo konde, akaenda Ulaya kwa sababu safari siyo kifo.
41. Ulaya alipiga vibarua mashambani kujiongezea kipato na kusupport familia yake.
42. Nyerere alimaliza masomo yake Ulaya na Oktoba 1952 alirejea nyumbani, akajenga kijumba pale Musoma, kisha akafunga ndoa na mpenzi wake Maria Gabriel, kutoka kabila tofauti.
43. Ilikuwa 24 Januari 1953. Alioa kabila lingine kwa sababu hakuamini katika ukabila.
44. After all Afrika hatukuwa na ukabila, tulikuwa na koo. Ukabila uliletewa na wakoloni kutugawa.
45. Baada ya ndoa walihamia Pugu, St Francis’ College, alikoajiriwa kwa kazi ya ualimu.
46. Mwaka 1953 wakabarikiwa mtoto wa kiume, wakamuita Andrew Burrito na kufatiwa na Anna Watiku, Anselm Magige, John Guido, Charles Makongoro, Godfrey Madaraka, Rosemary Huria na Pauleta Nyabanane. John tu ndo alifariki.
47. Andrew ndo yule Mzee aliyesema Rais Samia asiende kutembelea kaburi la Baba wa Taifa
! Andrew ana mambo nyie.

! Andrew ana mambo nyie. 48. Hakuna mtoto wa Nyerere aliyefia kwenye ndege kipindi za Vita vya Kagera kama ulivyokuwa unajua.
49. April 1953, Nyerere alichaguliwa kuwa Rais wa TAA, kutokana na umahiri wake wa kuongea na kujenga hoja.
50. Julai 7, 1954 TAA ilibadilishwa na kuwa TANU. Historia ya TAA ni ndefu pia.
51. Agosti 1954, Umoja wa Mataifa ulipendekeza Tanganyika kupata Uhuru miaka 25 ijayo.
52. Wazee wakasema acheni utoto. Miaka 25 nyie kuweza?
53. Wazee wakamtuma Kambarage kwenda UNO kupinga hoja kwa hoja!
54. John Rupia ndo alilipa nauli. March 1955, Nyerere akatinga UNO. Akajenga hoja za utayari wa kujitawala mpaka UNO yote ikalegea.
55. Mkoloni akashinikiza Kanisa limfukuze kazi Nyerere asijeleta vurugu kama Mau Mau.
56. Kanisa ndo lilimuajiri, likamwambia achague siasa au kazi. Nyerere akachagua siasa.
57. “Mpendwa Fr. Lynch, tayari nimezingatia chaguo ulilonipatia, kati ya ajira yangu shuleni na uanachama wa TANU , na nimefikia uamuzi kwamba ni lazima nijiudhuru kazi yangu ya kufundisha,” aliandika Nyerere katika Barua yake ya 22 Mach 1955.
58. April 1955 Nyerere akamrudisha mke wake kijijini Butiama, Mwitongo na Oktoba 1955 akarudi Dar es Salaam tayari kwa mashambulizi ya uhuru. Alizunguka nchi nzima akihubiri uhuru.
59. Alitumia Landrover la TANU. Mikutano ya Nyerere ilikuwa amsha amsha! Watu walifurika hatari.
60. Alihamasisha matumizi ya amani badala ya nguvu katika kupigania Uhuru na watu walimtii.
61. Alimuiga Mahtma Ghandi, yule mpigania Uhuru wa India aliyeamini amani haiji kwa ncha ya upanga.
62. Upepo wa Nyerere ulimsumbua sana Edward Twining, Gavana wa Tanganyika hadi na yeye akaanzisha chama cha United Tanganyika Party (UTP) ili kupambana na TANU.
63. Twining alimtuhumu Nyerere kwamba anahubiri ubaguzi nchini.
64. Nyerere akasema, tunapambana dhidi ya ukoloni na siyo wazungu.
65. Wazungu walifanya mengi mazuri tatizo lao yaliwanufaisha wachache.
66. Hayo ndo Nyerere aliyapinga mpaka kuwaita wakoloni mashetani na maharamia wakamshitaki na kumpiga faini.
67. Aliwatukana kupitia gazeti lake la SAUTI YA TANU mwaka 1958. Alipigwa faini ya Sh 3,000.
68. Akazilipa, Bibi Tit Mohammed na wanawake wanzake wakafurahi mzee kukwepa kifungo.
69. Walipitia changamoto nyingi wakati wa kupigania uhuru.
70. Kuna wakati walizinguana wao kwa wao, siku nyingine mkoloni akawazingua, tutayaangalia haya katika sehemu ya pili!
.
Pata ofa hizi za Nyerere kwa Sh 10,000 tu. Ni softcopy. Mpesa 0740590451
1. Tunisahihishe by Nyerere
2. Uongozi Wetu by Nyerere
3. Moyo wa Kujitolea by Nyerere
4. Ujamaa; Essays on Socialism
5. Man and Development
Cheers
Mwl. Denis Mpagaze
Muhenga wa Karne ya 21!
Tupe maoni yako

0 comments:
Post a Comment