LEO TARHE 11/06/2022 Mkuu wa Wlaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi amezindua Mkutano maalum wa maandalizi ya Sensa inayotarajia kufanyika kuanzia usiku wa Tarehe 23 mwezi wa 8 mwaka huu. Baada ya kusanyiko hilo kumalizika Jembe Fm imepata nafasi ya kuzungumza na baadhi ya wawakilishi wa makundi mbalimbali katika jamii ambao walihudhuria kusanyiko hilo na kubaini haya.
Saturday, June 11, 2022
Friday, June 10, 2022
MNEC SALIM ASAS AKERWA NA WATU WENYE NIA OVU NA CCM IRINGA
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC), Salim Asas ameshauri miaka mitano ijayo ya chama hicho iwe ya ‘Siasa na Uchumi,’ kauli mbiu itakayoinua hali kwa wanachama wake kufanya siasa sambamba na kujijenga kiuchumi.
Asas aliyasema hayo wakati akifunga Baraza la Wanawake Tanzania (UWT) la chama hicho Iringa Vijijini lililofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo, mjini Iringa.
“Siasa ndiyo maisha yetu, kwa vyovyote huwezi kukwepa siasa kwenye maisha yako hata kama utaamua kutojihusisha na siasa. Sasa kwa kuwa siasa ni maisha, tuangalie namna bora ya kuwafanya wanachama wetu wawe na hali ya kujiinua kiuchumi,” alisema.
Alishauri uanzishishwaji wa vyama vya ushirika wa kuweka na kukopa akisema vinaweza kusaidia kufufua fursa za kiuchumi kwa jamii na hususani wanawake na hivyo kuwafanya wafaidike na misaada mbalimbali.
“Tanzania ina mipango mbalimbali ya kuwajengea uwezo wa kiuchumi wanawake na makundi mengine ya kijamii ili kuchochea usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake na wasichana,” alisema.
Katika hatua nyingine, Asas amewapongeza viongozi wa UWT Iringa Vijijini wanaokaribia kumaliza muda wao akisema CCM itawakumbuka kwa kazi kubwa ya kukiimarisha chama hicho waliyoifanya kwa miaka mitano iliyopita.
Kutokana na mchango wao huo, ameahidi kuchangia ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT wa wilaya hiyo akisema mpango huo unaolenga kuwaondoa watendaji wa chama na jumuiya zake kutoka katika nyumba za kupanga na kuishi katika nyumba za chama nchi nzima.
Ahadi ya Asas ya ujenzi huo iliungwa mkono na Mbunge wa Kalenga Jackson Kiswaga aliyeahidi kutoa mchango wa awali wa Sh Milioni moja huku akiwahakikishia wanawake hao kwamba atachanga zaidi.
Katika taarifa yake ya utekelezaji Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Bi Lena Hongole ametaja mafanikio yaliyopatikana kuwa ni kuundwa kwa Vikundi 1500 kutoka vikundi 82 vya awali, ambapo pia vikundi 80 vinapata mkopo. Pia ametaja kuanzishwa kwa viwanda 68 vinavyomilikiwa na wanawake sambamba na kufufua shamba la jumuiya na viwanja vitatu vimenunuliwa kwa ajili ya uwekezaji.
Changamoto iliyotajwa katika taarifa hiyo ni ukosefu wa mabweni kwa wasichana mbunge wa jimbo hilo Mhe. Jackson Kiswaga amesema utekelezaji wa ujenzi wa mabweni kwenye jimbo hilo unaendelea.
Kuhusu mikopo kwa wanawake mbunge anasema miongoni mwa sifa za wanawake wanaostahili kupatiwa mikopo kupitia mfuko wa jimbo ni vikundi vya maendeleo visivyo vya kisiasa
Katika kipindi hiki ambacho chama hicho kinaendelea na uchaguzi wake wa ndani wa ngazi mbalimbali, Asas alitoa mwito kwa wana CCM kuwaogopa wajasiriamali hao kama ukoma ili kukinusuru kisipate viongozi wa ovyo, wasio na uwezo na dhamira ya dhati ya kukitumikia kwa kujitolea.
“Tuwe waangalifu sana katika uchaguzi huu, tusichague viongozi kwa Sh 5,000 au Sh 10,000. Tujiepushe na aina yoyote ya rushwa katika uchaguzi huu, vinginevyo tutapata viongozi watakaotugharimu kwa miaka mitano ijayo,” alisema.
RC SENDIGA AAGIZA KUKAMILIKA KWA UJENZI WA BWENI SHULE YA IPOGOLO NDANI YA MIEZI MINNE
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe Queen Sendiga ameagiza uendelezaji wa mradi wa shule ya msingi maalum ya ipogolo ifikapo Augost mwaka huu.
Amesema mkwamo wa jengo la bweni la watoto wenye ulemavu katika shule hiyo unatakiwa kukamilika ndani ya miezi minne na kuitaka Halmashauri ya Manispaa Iringa kuweka mkakati wa kukamilisha mradi huo sambamba na ujenzi wa uzio.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo alipokea msaada wa vitanda na magodoro 35 yenye thamani ya shilingi M.4 kwa ajili ya kusaidia watoto wenye uhitaji maalum katika shule hiyo na kuahidi ukamilishaji wa miundo mbinu ya mabweni hayo ili watoto waweze kuhamia katika mabweni Jambo litakalosaidia wazazi kuendeleza shughuli za kiuchumi na hasa ukizingatia kuwa baadhi yao wametelekezwa na waume zao.
Bi. Elizabeth mmoja wa wazazi wa mtoto anayeosoma katika shule hiyo amesema kutokana na changamoto zinaziwakabili ukiwemo. usafiri na miundombinu mibovu kwa watoto majumbani na mazingira yasiyo salama yanasobabishwa na wao kuwaacha watoto wao walemavu
majumbani pindi wanapokwenda kutafuta mahitaji yao ndiko kunakosababisha shauku yao ya kuiomba Serikali kukamilisha ujenzi huo ili kuwanusuru watoto wao ambao hata huko nyumbani watoto wengine wanalala chini.
Kitengo hicho cha watoto wenye ulemavu wa akili shule ya msingi maalum Ipogolo kilianzishwa Mwaka 2001 ukiwa ni mpango wa Serikali kuwezesha watoto wenye ulemavu wa akili kupata Elimu ambapo kwa Sasa kuna Jumla ya wanafunzi 90, wavulana 66 na wasichana 24 ambapo kati ya hao wengine wako katika elimu jumuishi.
Hata hivyo Afisa Elimu msingi Manispaa Ndugu Charles Mwakalila amesema kwa bajeti inayo anza Julai Mwaka huu zimetengwa milioni 30 kwa ajili ya ukamilishaji wa mabweni na uzio na kwa sasa wadau mbalimbali wameandikiwa barua kuomba kuchangia ujenzi wa jiko na bwalo.
RAS SENEDA AFUNGUA MAFUNZO YA MAAFISA MAENDELEO YA JAMII MAFINGA
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Happiness Seneda amefungua mafunzo ya mfumo wa usimamizi wa mikopo inayotokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri ya Mji Mafinga.
Alisema mfumo utaanza rasmi kutumika tarehe 1/7/2022 ambapo utarahisisha vikundi vyote kuingizwa kwenye mfumo huo, usimamizi wa marejesho, utoaji w mikopo utakuwa wa haki na hakuna mtu atakopa kwenye vikundi viwili kwa kufanya udanganyifu kwani mfumo utamkataa.
Seneda ameongeza kuwa lengo la serikali ni kuona wananchi wanaondokana na umaskini na wanaweza kusimamia uchumi wao, hivyo anatarajia mafunzo hayo yalete matokeo chanya na kuondokana na changamoto zilizokuwepo hapo nyuma katika ukopeshwaji, urejeshaji na usimamizi wa mikopo hiyo ya makundi ya Wanawake, Vijana na watu wenye Ulemavu.
Aidha Kuhusu zoezi la Kitaifa la SENSA ya watu na makazi, Katibu Tawala amesema Elimu iendelee kutolewa kwa wananchi ili waweze kushiriki zoezi hilo kikamilifu tarehe 23 Agosti kwani litasaidia kupanga mipango ya Serikali kwa sekta zote.
Mafunzo hayo, yametolewa na wawezeshaji ngazi ya mkoa wa Iringa na kuhudhuriwa na baadhi ya Wakuu wa Idara pamoja na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Mji Mafinga Ndugu, Charles Tuyi Afisa Mazingira
MKURUGENZI MNDOLWA AWAASA WAKULIMA MVOMERO KUTUNZA VYANZO VYA MAJI.
Picha ikionesha sehemu za kingo za mto Mvomero zilivyoharibiwa vibaya na shughuli za binadamu. |
· KUNUSURU MIUNDOMBINU YA KILIMO CHA UMWAGILIAJI.
Na; Mwandishiwetu -Mvomero
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mndolwa, amewaasa wakulima nchini kutunza vyanzo vya maji kwa kutokufanya shughuli za kibinadamu hususani za kilimondaniyamitasitini (60) ilikunusuru kuharibika kwa kingo za mito unaopelekea uharibifu wa Miundombinu ya kilimo cha Umwagiliaji.
Bw.Mndolwa ameyasema hayo mapema alipokuwa akizungumza na wakulima wa skimu ya Umwagiliaji Msufini iliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro, inayotumia maji kutoka mto Mvomero kama chanzo cha maji ya kilimo cha Umwagiliaji, ambapo ameshuhudia uharibifu mkubwa uliofanyika kutokana na shughuli za kilimo zisizorasmi.
Aliwashauri viongozi wa S erikali yakijiji kushirikiana kulinda vyanzo hivyo vya maji kwa manufaa ya kila mwananchi na aliendelea kusema “Hatulindi vyanzo vya maji yakunywatuu, hata vya kilimo na kuzuia uharibifu unaofanywa na binadamu wenzetu, asili inaharibiwa na binadamu.”Alisisitiza
Bw. Mndolwa aliagiza wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji nawataalam kutoka Halmashauri kufanya mapitio ya mto na chanzo nakuona athari iliyotokana na mafuriko yaliyopita katika mto huu.
Katika zoezi hilo wataalam watatakiwa kuja na mapendekezo yanini kifanyike ili kurekebisha athari za mafuriko hali itakayopelekea skimu ya Msufini kuanza kufanya kazi.
Aliongeza kuwa, kitachofanyika kwa sasa nikutengeneza chanzo kinachopeleka maji katika skimu hiyo matengenezo ambayo yataridhisha pande zote ikiwa ni pamoja na serikali na watumiaji wa skimu hiyo.
“siwezi ruhusu mkandarasi aliyefanya kazi kwa kiwango cha chini upande mwingine aje tena hapa,sababu kuna mahali kaharibu na nitamfukuza, kama kaharibu kwingine na hapa ataharibu.”Alibainisha Mndolwa.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miundo mbinu kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Mhandisi Ntonda Kimasa alisema, kuwa mradi huo umetengewa fedha kwa mwaka wafedha 2022/2023 kwa ajili yakuboresha miundombinu yake, hivyo mara baada ya kukamilika mapendekezo ya timu kazi ya ukarabatiwa miundombinu itaanza mara moja.
Awali, Bw. Mndolwa aliwakumbusha wakulima swala zima za kulipa Tozo na ada za matunzo ya skimu za Umwagiliaji baada ya kujengewa na kukarabatiwa kwa miundombinu hiyo.
Kwa upande mwingine aliwashauri wadau husika akitolea mfano wadau wa barabara, kilimo na wadau wengine wakae kwa pamoja ili yafanyike maamuzi sahihi na kuona namna ya kuunusuru mto mvomero kutokuacha njia yake ya asili na kupelekea kuvamia makazi ya watu.
Skimu ya kilimo cha Umwagiliaji Msufini, iliyopo Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro pamoja na kuathiriwa na athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabia nchi,imeharibiwa vibaya nashughuli za kibinadamu zinazofanyika ndani ya mita sitini, bila kuzingatia sheria.
Thursday, June 9, 2022
KUNA WANAUME WENGINE MIZIGO - IGP SIRRO
Na Albert G.Sengo Kufuatia kukithiri kwa mikasa ya mauaji na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake , akiwa kama mzazi, mlezi na kiongozi IGP Simon Sirro anaamua kuzama mtaani ambapo hapa anateta na baadhi ya madereva wa bodaboda wanao wakilisha kundi la wanaume katika jamii. #JembeHabari #JeshiLaPolisiTanzania #MauajiTanzania #TokomezaUkatili #HabariZilizoTufikia
TANGA UWASA YATUMIA ZAIDI YA MILIONI 150 KUAGIZA MITA MALIPO KABLA NCHINI UFARANSA
KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga-Uwasa) Mhandisi Rashid Shaban akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani
kuhusiana na tuzo walizopata katika maonyesho ya 9 ya Biashara yaliyofanyika Jijini hapa
KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga-Uwasa) Mhandisi Rashid Shaban katikati akiwa amebeba Kombe la Ushindi na tuzo ikiwa chini akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mamlaka hiyo kwenye Banda lao mara baada ya kukabidhiwa
NA OSCAR ASSENGA,TANGA.
KAIMU Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga-Uwasa) Mhandisi Rashid Shaban amesema mamlaka hiyo imetumia zaidi ya Shs Milioni 150 kwa ajili ya kuagiza mita za malipo ya kabla (pre-paid)toka Nchini Ufaransa.
Mhandisi Shabani aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tuzo walizopata katika maonyesho ya 9 ya Biashara yaliyofanyika Jijini hapa.
Mhandisi Shabani alisema kumekuwepo na malalamiko kwa wateja yanayohusu madai ya kuongezewa gharama za malipo(bili) ambapo mita hizo ndio zitakuwa muarobaini wa malalamiko hayo.
Aidha alisema Mamlaka hiyo imefanya tafiti za kutosha na kubaini kwamba wananchi wengi hawajatambua tatizo la ongezeko la bili ya maji hivyo kuanza kutafuta mbinu mbadala ya kumaliza tatizo hilo.
Alisema lengo ni kukidhi hitaji la Serikali la kutaka wananchi waweze kupata huduma ya maji katika maeneo yote kwa Mijini na Vijijini.
“Tumeanza kufanya tathmini kama tulivyoagizwa na Wizara kuhusiana na mita hizi za malipo ya kabla(pre-paid) na tathmini yetu iko vizuri na matarajio yetu tutafanikiwa”Alisema Mhandisi Shaaban.
Alisema matarajio kuanza na mita 500 ambapo Mamlaka hiyo imepanga kuzifunga kwa baadhi ya wateja kama sehemu ya majaribio na mafanikio yake ndio yatakayopelekea kufungwa kwa mita hizo Mkoa Mzima.
“tumeshaanza majaribio ya mita hizo na zinaonekana kuwa na tija lengo letu sasa ni kuhakikisha tunazisambaza Mkoani kote ”Alisema Mhandisi Shaaban.
Mhandisi Shabani alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi Mkoani Tanga kupokea huduma hiyo na watakuwa na uwezo wa kununua maji kutokana na uwezo wa mteja kama inavyofanyika katika huduma nyingine za kijamii.
Hata hivyo alisema Mamlaka hiyo imepokea tuzo ya watoa huduma bora dhidi ya Mamlaka za Serikali zilizokuwepo kwenye maonyesho hayo kwa kupatiwa cheti na ngao na ile ya ushindi wa Jumla.
FAMILIA YAGOMA KUONDOA KABURI KATIKATI YA BARABARA BARIADI..MKUU WA MKOA DAVID KAFULILA AINGILIA KATI
Wednesday, June 8, 2022
MABORESHO YA MAPANGO YA AMBONI KUIUNGANISHA TANGA NA ZANZIBAR KIUTALII
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga Burhan Yakub akiuliza jambo wakati wa semina hiyo |
Mwandishi wa habari wa Kituo cha ITV na Radio One Mkoa wa Tanga Wiliam Mngazija akiuliza swali katika semina hiyo |
Sehemu ya washiriki wa semina hiyo wakifuatilia matukio mbalimbali
Sehemu ya washiriki kwenye semina hiyo
NA OSCAR ASSENGA, TANGA.
TANZANIA NA MAREKANI ZAJADILI USHIRIKIANO KATIKA MICHEZO NA SANAA
Na John Mapepele
Sunday, June 5, 2022
Picha : RC ROBERT GABRIEL AONGOZA SHEREHE MAALUMU ZA 'USIKU WA WAANDISHI NA WADAU WA HABARI KANDA YA ZIWA
Tazama Picha hapa chini