ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 9, 2017

AZAM Vs SIMBA HAKUNA ALIYECHEKA.

Timu ya Simba imeshindwa kuonyesha ubabe wake mbele ya wana 'lambalamba' Azam Fc, kwa kutoka bila bila kwenye game yao ya leo iliyofanyika nyumbani kwa Azam Fc uwanja wa Chamazi.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara ni wa pili kwa timu ya Simba ambayo mpaka sasa ndio inaongoza kwenye msimamo wa ligi kwa kuwa na point 4 na magoli 7, ikijumlishwa na moja ya leo ambayo wamegawana na timu ya Azam kwa kutoa sare.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo mchezaji wa Azam Himid Mao ambao nao wameshindwa kujitunisha misuli kwa mnyama SImba, amesema mchezo ulikuwa mgumu kwa timu zote mbili.


"Kutoka sare sio kitu kizuri ingawa matokeo yalistahili kwa timu zote mbili, mchezo ulikuwa mgumu lakini kila timu ilicheza vizuri, tunawashukuru mashabiki na wadau waliokuja kutusuport", alisema Himid Mao.


Pamoja na mechi hiyo katika uwanja wa Sokoine Mbeya timu ya prisons imemaliza mchezo wake kwa kutoka sare ya magoli 2-2dhidi ya Majimaji ya Songea.

KADI NYEKUNDU YA SADIO MANE KWA KUMTANDIKA BUTI KIPA WA MAN CITY YAIGHARIMU LIVERPOOL KUPOKEA KICHAPO CHA MKONO.

Buti la Sadio Mane dhidi uso wa Ederson limeigharimu Liverpool hii leo katika mchezo dhidi ya Manchester City.

Gabriel Jesus akishangilia baada ya kuifungia mabao mawili Manchester City dakika za 45 na Ushei na 53 katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England leo mchana Uwanja wa Etihad. 

Leroy Sane alitokea benchi kuchukua nafasi ya Jesus dakika ya 57 naye akafunga mabao mawili dakika za 77 na 90 na Ushei, wakati bao la kwanza leo lilifungwa na Sergio Aguero dakika ya 24.
  • Sergio Agüero24'
  • Gabriel Jesus45+6'
  • Gabriel Jesus53'
  • Leroy Sané77'
  • Leroy Sané90+1'


Sadio Mane went off in pursuit of Joel Matip’s long pass on 37 minutes with honest intentions, and his eyes were looking nowhere but at a ball that his speed and athleticism took him within a whisker of controlling. That does not, however, absolve him of the responsibility for the safety of the advancing Ederson Moraes who took Mane’s right boot to the side of his face and looked in trouble even before he got his hands out to break his fall.Sadio Mane protests his innocence as Ederson clutches his face
Sadio Mane akijisalimisha baada ya madhambi kwa Ederson.

Another red card that divided opinion and demonstrated that there are still so many in football who see the game on the terms that they remember it, or once played it. Which is fine for the post-match debate but when it comes to the difficult real-time decisions in the heat of the moment, all the referee can do is interpret the law as it is today and Jonathan Moss was correct to dismiss Mane.
TANZANIA NA KENYA ZAONDOLEANA VIKWAZO VYA KIBIASHARA.

Nchi za Tanzania na Kenya zimetimiza agizo la maraisi wake na kukubaliana kuondoa vikwazo vya biashara katika bidhaa za unga wa ngano na gesi ya kupikia kutoka Kenya na zile za Maziwa na Sigara kutoka Tanzania.

Aidha masuala mengine 15 kutoka Tanzania na 16 ya Kenya bado yako mezani na majadiliano yanaendelea.


Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakati wa kuhitimisha mazungumzo ya kibishara baina ya nchi hizo ya Siku mbili, Katibu Mkuu wa biashara na uwekezaji nchini Tanzania Adolph Mkenda amesema wamefikia makubaliano hayo ya kibiashara ili kuhakikisha wanatimiza matakwa ya viongozi  wakuu, Rais John Pombe Magufuli na Uhuru Kenyata, yaliyoyowataka wafanye kazi na kuondoa vikwazo vya  biashara mara moja katika nchi hizoi mbili kubwa ndani ya jimuiya ya Africa Mashariki,


Amesema, baada ya maagizo yao, kwa kushirikia na Katibu Mkuu wa biashara wa Kenya, Dr Chris Kiptoo walianza kuwasiliana kwa karibu ambapo kwa kuanzia walifanya mkutano katika mpaka wa Namanga kuangalia biashara inavyokwenda na vikwazo vilivyopo katika nchi hizo ambavyo vilitatuliwa baada ya kupitia masuala mbali mbali,


 Aidha amesema kupitia majadiliano hayo, wameweza kupatia ufumbuzi mambo mengi ikiwemo biashara ya ngano, ambapo amesema wamekubaliana kifungua biashara ya ngano katika nchi hizi na kuhahakikisha wanaiboresha zaidi ikiwamo kutoa kipaumbele kwa wakulima wa zao hilo.


"Tulipata fursa ya kukaa na wadau wa biashara ya unga na ngano yenyewe kutoka nchi hizi mbili, wakiwemo wadau wenye viwanda vya kusaga ngano, wakulima na maafisa wa wizara za kilimo kutoka nchi zote ambao tumekubakiana kufungua biashara ya unga wa ngano kati ya Kenya na Tanzania, na sasa hivi unga wa ngano unapita unavuka mpaka bila vikwazo vyovyote." Amesema Mkenda


Kenya sasa hivi inazalisha ngano nyingi kuliko Tanzania na Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuzalisha ngano kuliko Kenya hivyo tukiunganisha biashara na uwezeshaji,ngano ya Kenya itaongezeka na maeneo mengi Tanzania ambayo yanauwezo wa kuzalisha ngano yataongeza uzalishaji wa ngano


Aidha alisema wamekubaliana na wenye viwanda waanze kutumia ngano za kutoka nchini kabla kuagiza kutoka nje ya nchi hizi mbili na waonyeshe nia nzuri ya kujenga ushirikiano Wa jumuiya hii ya Africa Mashariki..


Kwa upande wake, katibu Mkuu Wa Kenya, Dr Chris's Kaptoo amesema, Kenya imewekeza zaidi dola bilioni moja na nusu nchini Tanzania kwa ajili ya masuala mbali mbali ya kibiashara na viwanda ambapo watu zaidi ya elfu 50 wameajiriwa.


 Ameogeza katika kuendeleza biashara katika nchi hizi mbili, watatumia Uchumi na Nakumati supermarket na kuhakikisha zinafanya kazi inavyopaswa na wale wanaopeleka bidhaa zao wanalipwa kwa wakati.


"Tunafanya bidii kuona Uchumi Supermarket inaimarika, tunataka matawi yake yote yaliyokuwepo Tanzania yanaendelea kama yalivyokuwa awali na pia wale wote watakao kuwa wanapeleka bidhaa zao huko wanalipwa kwa wakati" amesema Dr Kiptoo"

Amesema, siyo wajibu wake yeye katibu kuingilia biashara za watu binafsi kama Nakumat na Uchumi lakini kwa umuhimu wa biashara wanaingilia kati kuhakikisha iko salama na inatimiza matakwa ya nchi.

Friday, September 8, 2017

KUPIGWA RISASA KWA TUNDU LISSU KUMEIBUA MENGINE NDANI YA BUNGE.

Mbunge Hussein Bashe ameiomba Mwongozo wa Spika kufuatia tukio la Mbunge wa Singida Mashariki Mh. Tundu Lissu kupigwa risasi na watu wanaodaiwa kutojulikana.

SUMAYE AFUNGUKA YA MOYONI.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Fredrick Sumaye amedai endapo serikali ingekuwa inawajibika ipasavyo, matukio ya kiuhalifu yasingekuwa yanaendelea kujitokeza mara kwa mara nchini.
Mhe. Sumaye ameeleza kupitia mkutano wa chama hicho na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo ikiwa imepita siku moja tokea kwa tukio lililompata Mhe. Tundu Lissu kushambuliwa kwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma 'Area D' na watu wasiofahamika.

"Katika serikali yeyote ambayo inawajibika ipasavyo kazi ya kwanza ya serikiali ni kulinda uhai wa wananchi wake, hiyo ndiyo kazi ya msingi ya serikali. Kwa hiyo kama ni serikali inayowajibika ipasavyo, basi haya matukio yanayoendelea kutokea yasingekuwepo kabisa au basi tukio linapotokea wahusika wangekuwa wanakamatwa kwa haraka na kupelekwa sehemu husika lakini unapokuwa huoni hatua zinazoridhisha zikichukuliwa basi kuna ulakini katika nchi", amesema Sumaye.

Pamoja na hayo, Sumaye ameendelea kwa kusema "kwa sababu serikali ni yetu sote bila ya kujali itikadi ya chama husika. Kwa hiyo mimi nasema kama kweli serikali inawajibika inavyotakiwa basi haya mambo yote ambayo yanatokea yalitakiwa yapatikane majibu ya uhakika na kwani yanapoachwa baadhi ya maeneo yapo gizani basi wengi tunaanza kufikili kwamba utawala unaowajibika unakosekana ama kwa makusudi au kwa uwezo".

Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti  wa chama hicho Prof. Abdallah Safari amesema kabla ya Mhe. Tundu Lissu kupigwa risasi alikuwa mtu mwenye wasiwasi mkubwa juu ya maisha yake kutokana na baadhi ya watu waliokuwa wanamfuatilia kwa ukaribu kila kukicha.

"Kabla ya tukio hili kutokea Mhe. Lissu alishawahi kusema katika mkutano wake na waandishi wa habari alikuwa na hofu na maisha yake kutokana na kufuatiliwa na watu wenye gari aina ya Nissan Premier yenye namba za usajili T460 CQV hapa hapa Dar es Salaam. Kwa hiyo maisha ya Lissu yamekuwa yapo hatari kwa kipindi kirefu", amesema Prof. Safari.

Kwa upande mwingine, Prof. Safari amevitaka vyombo vya usalama vitekeleze kazi zake kwa uweledi kama ambavyo wanaweza kufanya katika matukio mengine ya kiuhalifu.

MAGHOROFA YA LUGUMI KUPIGWA MNADA KESHO.

Kampuni ya Udalali ya Yono kesho itapiga mnada maghorofa yanayomilikiwa na kampuni ya Lugumi.

Maghorofa hayo mawili ambayo yapo sehemu tofauti moja likiwa mtaa wa Mazengo Upanga na lingine likiwa Mbweni jijini Dar es Salaam..

Mkurugenzi wa Yono, Scolastica Kevela amesema leo Ijumaa kuwa wametumia njia mbalimbali ili kufanikisha mnada huo kufanyika hasa kwa kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Amesema hawezi kutaja gharama halisi ya mali hizo na deni ambalo kampuni hiyo inadaiwa na Mamlaka ya Mapato(TRA) hivyo hao ndio wanaoweza kutoa majibu hayo.

"Kazi yetu sisi ni kupiga mnada tu, gharama ya deni na thamani ya mali hizo TRA ndio wanatakiwa kutolea majibu,"amesema Kevela.

Amesema fedha watakazozipata zitakwenda kusaidia nchi katika shughuli mbalimbali za maendeleo.

Thursday, September 7, 2017

KILA ALHAMISI MWANZA YOTE HUKUTANA NDANI YA THE CASK BAR & GRILL KWENYE KARAOKE.

Welcome on Sing! Karaoke. Sing your favorite songs with lyrics and duet with lovers, friends and celebrities, eneo ni moja tu Kanda ya Ziwa The Cask Bar & Grill place ipo ndani ya Rock City Mall Kirumba Mwanza Tanzania.
Beautiful one akifanya yake eneo la tukio.
Haya ndiyo mashairi anayo husika nayo jeh...ni mashairi ya wimbo gani?
DeejayKflip ndiye Mc wa Karaoke Night ndani ya The Cask Bar & Grill at Rock City Mall Mwanza.
I wanna be down
With what you're going through
I wanna be down
I wanna be down with you
No matter what time of day or night it's true
I wanna be down
Heee heeee heeee..................!!
Ni zaidi ya afya....
Hip Hop in na de area..........!!
Flowers classic.com
"Hongera sana Fatma" says DeejayKflip
Hapa ni mziki gani zaidi ya reggae?
Wow.......The smile.
Mansour Jumanne kutoka Jembe Fm (L) akiwa na Naziru (R)
Marafiki.
 Kulia na kushoto ni Mapacha Classic na pale kati Mansour Jumanne.
Kulia kwa picha akaongezeka G.sengona likagongwa selfie.
Find karaoke song lyrics, watch music videos and listen to recordings kisha ukiiva jumuika nasi hapa tuone ufundi wako.
Karibu sana.

POLISI WAFUNGUKA HAYA JUU YA TUKIO LA KUPIGWA RISASI LISSU.

CHANZO:- Mwananchi: 
Dodoma. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amezungumzia tukio la kupigwa risasi mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, akiwaomba wananchi wenye taarifa kulisaidia jeshi hilo.

Muroto amesema leo Alhamisi kuwa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na wameshafika eneo la tukio nyumbani kwa Lissu.

“Tunaomba mwananchi mwenye taarifa atusaidie. Jeshi la Polisi tumeanza uchunguzi, tumefika eneo la tukio na tunaendelea,” amesema.

Kamanda Muroto amesema taarifa za awali zinaonyesha kuna gari aina ya Nissan lenye rangi nyeupe lilikuwa likimfuatilia Lissu.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana amewataka wananchi kuwa watulivu wakisubiri taarifa za Jeshi la Polisi na madaktari wanaoendelea na matibabu ya mbunge huyo, ambaye pia ni mwanasheria mkuu wa Chadema.

Akizungumza maendeleo ya matibabu ya mwanasiasa huyo ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma James Charles amesema Lissu yu hai na imara.

Amsema mbunge huyo amepigwa risasi tumboni na kwamba timu ya madaktari inaendelea na matibabu.

“Tumempokea Lissu mchana, kanuni za matibabu haziruhusu mtu mwingine asiye mtumishi kuingia chumba cha matibabu. Tuna uwezo wa kutosha wa kutoa huduma ya dharura,” amesema.

Amsema kwa sasa wanaendelea na huduma na wakikamilisha watatoa taarifa.

BREAKING NEWS MBUNGE WA SINGIDA MASHARIKI TUNDU LISSU APIGWA RISAS, ZITTO, MBOWE WATHIBITISHA,

@Regrann from @jembefm - #BreakingNews Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, amepigwa risasi Tano na watu wasiojulikana na amekimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma. Taarifa zaidi zitakujia punde! #Jembefm
Mhe. Mbowe akikabidhiwa nguo zilizotapakaa damu alizokuwa amevaa Mhe.Tundu Lissu baada ya kupigwa risasi nyingi na watu wasiojulikana mapema leo mjini Dodoma.

Mbowe adhibitisha hali ya Tundu Lissu Ni Mbaya ,Wabunge na viongozi mbalimbali wa serikali wamefika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kufuatia taarifa ya Mbunge Tundu Lissu kupigwa risasi. #Mwananchileo

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu amekimbizwa hospitali mchana huu  baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana leo mchaa akiwa nyumbani kwake Mkoani Dodoma.

Akizungumza na kituo cha ITV Mwenyekiti wa CHADEMA Freeaman Mbowe amesema Mbowe "Hali ya Tundu Lisu ni mbaya Sana, na msishangae mkasikia lolote kuanzia sasa"

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi nyumbani kwake na kwamba hali yake ni mbaya.
Lissu, ambaye ni mwanasheria mkuu wa Chadema kwa sasa amepelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.

Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari, huku wengine wakilia.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Charles Kihologwe amewataka watu hao kukaa mbali na chumba cha upasuaji lakini wengi wanakataa wakisema hawamwamini mtu yeyote.

Asubuhi, Lissu alihudhuria kikao cha Bunge na aliomba mwongozo wa Naibu Spika akihoji kuhusu taarifa za kamati zilizoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya Tanzanite na almasi kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu badala ya kujadiliwa na Bunge kwanza.

TANZIA: KAMISHNA MSTAAFU WA OPERESHENI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI AFARIKI DUNIA MAPEMA LEO JIJINI DAR ES SALAAM.


Kamishna   Jenerali wa Jeshi   la   Zimamoto   na Uokoaji Nchini   – Thobias  Andengenye   anasikitika   kutangaza   kifo   cha   aliyekuwa Kamishna   wa   Operesheni   Mstaafu   wa   Jeshi   la   Zimamoto   na Uokoaji CF (OPS) Rogatius Peter Kipali, kilichotokea mapema leo Semptemba 7, 2017 akiwa nyumbani kwake Mombasa, Ukonga jijini Dar es Salaam.


Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji anatoa pole kwa Maafisa, Askari na Watumishi wote wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Nchini, familia ya Marehemu na wale wote walioguswa na msiba huu kwa namna tofauti tofauti.


Jeshi   la   Zimamoto   na   Uokoaji   kwa   kushirikiana   na   familia   ya Marehemu linaendelea kuratibu shughuli za msiba huo na taarifa za Mazishi zitatolewa baadaye baada ya taratibu zote kukamilika.


Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi Amina.


IMEANDALIWA NA KITENGO CHA HABARI NA ELIMU KWA UMMA-JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

TANESCO YAKABIDHI NYUMBA MBILI ZA WALIMU SHULE YA SEKONDARI MTERA DAM


Mkuuwa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mhe.Jabir Shekimweri, (kushoto), akifungua pazia ikiwa ni ishara ya kuzindua nyumba mpya ya Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Mtera DAM, iliyoko jirani na Kituo cha Kufua Umeme wa maji, Mtera, katikati ya mikoa ya Dodoma na Iringa, Septemba 6, 2017. Nyumba hiyo na nyingine iliyokarabatiwa zimejengwa kwa msada wa TANESCO kwa thamani ya shilingi milioni 35. Wengine pichani, ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia usambazaji umeme na huduma kwa wateja mama Joyce Ngahyoma,(wakwanza kulia), aliyemwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, , (kulia) na Naibu Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia Ufuaji umeme, Mhandisi Abdallah Ikwasa. (kushoto), na Mkuu wa shule hiyo, Bw. Simon Dissa.

 Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia usambazaji umeme na huduma kwa wateja, Mama Joyce Ngahyoma,(aliyesimama), akitoa hotuba kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Dkt. Tito Mwinuka.
 Mama Joyce Ngahyoma
 Mkuuwa wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mhe.Jabir Shekimweri, (aliyesimama), akitoa hotuba yake kwenye hafla hiyo.
 Nyumba mpya ya Mawlimu Mkuu shule ya sekondari Mtera DAM, iliyojengwa na TANESCO na nyingine iliyokarabatiwa kwa thamani ya shilingi milioni 35.
 Mkuu wa Wilaya Mhe. Shekimweri, (kulia), na Mama Joyce Ngahyoma, wakiwa mbele ya nyumba hiyo baada ya kuizindua na kuikabidhi kwa Mkuu wa shule.
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumzia utaratibu wa kukabidhi nyumba hizo.
 Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo wakiwa na furaha.
 Mkuu wa shule ya sekondari Mtera DAM, Bw. Simon Dissa, akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo aliishukuru TANESCO kwa kupunguza uhaba wa nyumba za walimu na sasa bado wanahitaji nyumba 15.
  Baadhi ya wananchi waliohudhuria hafla hiyo wakiwa na furaha.
 Wananchi wakifurahia hotuba
 Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa TANESCO wakiongozwa na Mama Joyce Ngahyoma.
Meneja wa Kituo cha Kufua Umeme wa Maji Mtera, Mhandisi John Skauki, akielezea ushirikiano baina ya TANESCO na wana jamii ya Mtera ambao alisema ni mzuri.
Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO
Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO walio katika Kituo cha Kufua umeme wa maji Mtera, wakifuatilia hafla hiyo.


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), limekabidhi majengo mawili ya nyumba za walimu, shule ya sekondari Mtera DAM, iliyoko jirani na Bwawa la kufua umeme wa maji Mtera, (Mtera Hydro Power Plant), lililoko katikati ya mikoa ya Dodoma na Iringa.
Nyumba hizo zilizogharimu shilingi milioni 35, moja ikiwa mpya na nyingine imekarabatiwa, zimekabidhiwa kwa uongozi wa Wilaya ya Mpwapwa Septemba 6, 2017 na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia usambazaji umeme na huduma kwa wateja, Bi. Joyce Ngahyoma, ambaye alimwakilisha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi, Dkt. Tito Mwinuka.
Akizungumza kabla ya kukabidhi nyumba hizo, Bi. Joyce Ngahyoma alisema, wakazi wa kata ya Mtera ni wadau na washirika wakubwa wa TANESCO katika kulinda miundombinu ya umeme ya kituo cha kufua umeme cha Mtera ambayo ina gharama kubwa kwa hivyo walipowasilisha maombi ya kujengewa nyumba ya mwalimu Mkuu, TANESCO ilikubali ombo hilo bila kusita.
Alisema, uongozi wa TANESCO baada ya kupokea maombi hayo ulifanya tathmini na kutoa kiasi cha fedha shilingi Milioni 35 ambazo zilitumika kujenga nyumba jipya na kukarabati nyumba nyingine.
Nyumba mpya iliyojengwa na TANESCO kwa ajili ya makazi ya Mwalimu Mkuu, ina vyumba vinne, choo, bafu na jiko, alisema.
“Napenda nichukue fursa hii kuwashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa mnaotupatia na niwaahidi tu kwamba Shirika litaendelea kushirikiana na serikali na jamii kwa ujumla katika kuhakikisha sekta ya elimu, afya na huduma nyingine zinaimarika kwa kutoa michango ya hali na mali.” Alisema Bi. Ngahyoma.
Alisema, sambamba na msada huo, TANESCO imekuwa ikisaidia jamii ya wana Mtera, katika kuwapatia huduma ya afya kwenye zahanati ya wafanyakazi, huduma ya elimu ya awali(chekechea), kwenye shule ya chekechea iliyojengwa kuhudumia watotot wa wafanyakazi, na pia usafiri, ambapo mabasi yanayochukua wafanyakazi kwenda na kutoka kazini, huwasaidia pia wananchi.
Aidha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, anayeshughulikia ufuaji umeme, Mhandisi Abdallah Ikwasa, alisema, Kituo cha kufua umeme wa maji Mtera, kilijengwa kuanzia mwaka 1984 na kukamilika mwaka 1988 na kuwa na uwezo wa kufua umeme Megawati 80 na tangu kipindi hicho hadi hivi sasa, TANESCO imekuwa ikishirikiana na wananchi katika kulinda miundombinu ya kituo hicho.
Mnamo mwaka 2005 na 2006, Shirika lilichangia kiasi cha shilingi milioni 34 kujenga madarasa mawili mapya na ujenzi wa ofisi ya walimu, alisema Mhandisi Ikwasa.
Akizungumza katika hafla hiyo kabla ya kupokea majengo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Mhe. Jabir Shekimweri, amewataka wananchi wa Kata ya Mtera,  kuendelea kushirikiana na TANESCO, katika kulinda miundombinu ya Shirika hilo kwenye bwawa la kufua umeme wa maji la Mtera, (Mtera Hydro Power Plant).
“Ndugu zangu msada huu umekuja kutokana na faida inayopatikana kutokana na miundombinu hiyo, kwa hivyo niwaombe muendelee kushirikiana na TANESCO na viongozi wa serikali ya kijiji katika kuhakikisha usalama wa miundombinu hiyo unaendelea kuwepo kwani wafanyakazi wa TANESCO pekee hawawezi kulinda miungdominu hiyo peke yao kwa sababu eneo ni pana sana.” Alifafanua.
Mhe. Shekimweri alisema, msada wa majengo hayo, utasaidia kutatua changamoto ya nyumba kwa walimu ambao kutokana na uhaba mkubwa wa nyumba walimu wanaishi maeneo ya mbali na shule na hivyo inapelekea utendaji kazi wao kuwa wa chini.
“Nimeambiwa kuwa ufaulu kwenye shule hii ni mzuri na walimu wakiishi maeneo ya karibu na shule, basi ufaulu huo bila shaka utaongezeka sana.” Alisema.
Lakini pia niwaombe wananchi, umeme unaopatikana hapa unategemea sana uwepo wa maji, kwa hivyo nitoe rai, ni lazima tutumie maji haya kwa busara kubwa naelewa zipo shughuli za uvuvi lakini uvuvi mwingine ni ule haramu wa uharibifu, niwajulishe tu hivi karibuni tutakaa kikao ili kuweka matumizi bora ya maji haya ili kuzuia athari zinazoweza kupelekea uharibifu wa vyanzo vya maji yanayoletwa kwenye bwawa hili, alisisitiza.
Mkuu huyo wa wilaya aliishukuru TANESCO kwa kuisaidia serikali katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii kwenye eneo hilo na .
“ Nimeambiwa kuwa sio tu mmesaidia ujenzi wa nyumba moja mpya na kukarabati nyingine lakini pia mmekuwa mkisaidia wananchi katika kuwapatia huduma za afya kwenye zahanati ya wafanyakazi, hali kadhalika mmekuwa mkiwasaidia wananchi katika usafiri ambapo wamekuwa wakitumia usafiri wa wafanyakazi wenu, hili ni jambo jema katika kujenga mahusiano mema baina yenu na wananchi.” Aliongeza Bw. Shekimweri.