Mhe. Mbowe akikabidhiwa nguo zilizotapakaa damu alizokuwa amevaa Mhe.Tundu Lissu baada ya kupigwa risasi nyingi na watu wasiojulikana mapema leo mjini Dodoma.
Mbowe adhibitisha hali ya Tundu Lissu Ni Mbaya ,Wabunge na viongozi mbalimbali wa serikali wamefika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kufuatia taarifa ya Mbunge Tundu Lissu kupigwa risasi. #Mwananchileo
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu amekimbizwa hospitali
mchana huu baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana leo mchaa
akiwa nyumbani kwake Mkoani Dodoma.
Akizungumza na kituo cha ITV Mwenyekiti wa CHADEMA Freeaman Mbowe amesema Mbowe "Hali ya Tundu Lisu ni mbaya Sana, na msishangae mkasikia lolote kuanzia sasa"
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu amepigwa risasi leo Alhamisi nyumbani kwake na
kwamba hali yake ni mbaya.
Lissu, ambaye ni mwanasheria mkuu wa Chadema kwa sasa amepelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah, wabunge na viongozi wengine wa ulinzi wa Bunge wamefika katika hospitali hiyo kujua kinachoendelea.
Baadhi ya ndugu na wagonjwa wamefurika katika chumba cha upasuaji cha hospitali ya mkoa wakitafakari, huku wengine wakilia.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Charles Kihologwe amewataka watu hao kukaa mbali na chumba cha upasuaji lakini wengi wanakataa wakisema hawamwamini mtu yeyote.
Asubuhi, Lissu alihudhuria kikao cha Bunge na aliomba mwongozo wa Naibu Spika akihoji kuhusu taarifa za kamati zilizoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya Tanzanite na almasi kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu badala ya kujadiliwa na Bunge kwanza.

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.