ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 17, 2010

STONE CLUB HAIPO TENA.................................WHY?

HEY GUYZ INABIDI MUWE WAPOLE KWANI MTAKOSA MARAHA NA BURUDANI YA UKWELI KWA MUDA KWA MAANA ILE CLUB YETU ILOKUWA “IKIMWAGAGA’ RAHA ROCK CITY "STONE CLUB" IMEDE.......! BUT KUNA TAARIFA ZA KAPETINI TENA ZA UHAKIKA... V.SOON KUNA KIOTA KINGINE “BOMBA ILE KINYAMA’ KINAKWENDA KUTANABAISHWA RASMI! MA BROTHERZ AND SISTERZ KAA CHONJO....!

BONGE ASITISHA ZIARA KANDA YA ZIWA... ILIKUWA AKAE SIKU 10, AKAA SIKU 3 TU! KERO ZAMZINGUA.

SEHEMU YA KIPANDE CHA ENEO LA KIWANJA CHA WAZI CHA MICHEZO FURAHISHA KIRUMBA JIJINI MWANZA KILICHOMEGWA NA HALMASHAURI YA JIJI, KIMEENDELEA KUTUMIKA KUHIFADHIA TAKA NA KUWA KERO KWA WANAMICHEZO WANAO TUMIA KIWANJA HICHO NA WAKAZI WAISHIO KARIBU NA ENEO LA UWANJA HUO. BONGE WA PB AKIRIPOTI....
AWALI WANAMTAA WALILIOMBA JIJI KUWATENGENEZEA KIPANDE HICHO KUWA ENEO LA BUSTANI YA MAPUMZIKO KISHA ENEO LINALOBAKI KUTUMIKA KAMA ILIVYO SASA KWA MICHEZO NA MIKUTANO YA HADHARA, JIJI LIKADAI KUWA HALINA FEDHA, WANAMTAA HAWAKUCHOKA WAKAOMBA KUPEWA BARUA TOKA JIJI ILI WAPATE IDHINI YA KUTAFUTA WENYEWE WAFADHILI, JIJI LIKAKATAA... NA KUDAI KUWA LITATEKELEZA.... DUH KILICHOFUATA NDIYO HIKI.....
ENEO LIMEKUWA KERO, HARUFU KALI YA TAKA, INZI, HATARI KWA MLIPUKO WA MAGONJWA..

NIMEKUWA NIKIJIULIZA IWEJE TAKA ZIKUSANYWE HAPA KUNGOJA KUPELEKWA DAMPO KUU ILE HALI MAGARI YA USOMBAJI TAKA YANAUWEZO WA KUSOMBA TAKA MOJA KWA MOJA TOKA KTK MASOKO NA VYANZO VINGINE NA KUPELEKA MOJA KWA MOJA DAMPO KUU DUH KUMBE KUNA MENGINE... CHEKSHIA HIIII.... GARI LA USOMBAJI TAKA PINDI LILIPOKUTWA NA MNYETISHAJI LIKISOMBA MCHANGA ENEO MAARUFU LA NTENDE, NYASHISHI NJE KIDOGO YA JIJI LA MWANZA.

SHIMO HILI LILILOKO MAENEO YA ASPEN HOTEL KWENYE KONA YA BARABARA YA UHURU INAYOINGIA MLANGO MMOJA NA KUTOKEA NYERERE ROAD, LIME KUWA KERO INAYOSABABISHA MSONGAMANO HUKU LIKIHARIBU VYOMBO VYA USAFIRI VINAVYOTHUBUTU KUPITA ENEO HILO. BARABARA HII IMEKUWA MUHIMU SASA KWA EXPRESS ZIENDAZO NYAKATO, IGOMA ZILIZOPIGWA MARUFUKU KUTUMIA BARABARA NYINGINE KATIKATI YA MJI.


HAKUNA JINSI KWA MAGARI MADOGO YENYE UVUNGU MDOGO, KWANI ILI KUPITA HUSUBIRI MAGARI YANAYOPITA UPANDE WA KULIA ILI KUTUMIA UPANDE HUO USIO NA SHIMO.

Thursday, April 15, 2010

KWEA PIPA YAPATA WENGINE MWANZA.

SAFARI HII TIKETI IMEKWENDA KWA BWANA MDOGO RICHARD BOAZ WA WILAYA YA GEITA MWANAFUNZI WA ST ALOYCE SEC.SCHOOL. SIIPATI PICHA SIMULIZI SHULENI EH BANAAEEEH!

SALUM SALUM KULIA MKAZI WA KAHAMA YEYE KAJISHINDIA FLAT SCREEN TOKA KWEA PIPA NA COCA COLA NA HAPA AKIKABIDHIWA MZIGO.

Wednesday, April 14, 2010

TAHARIRI: usimamizi thabiti utapunguza ajali za wachimbaji wadogo.


Tumepokea kwa masikitiko na mjonzi makubwa vifo vya wachimbaji madini wadogo wadogo 16 katika machimbo ya dhahabu yasiyo rasmi katika kijiji cha Sabola, kata ya Kasame, wilaya ya Geita, mkoani Mwanza.
Huu ni msiba mkubwa mwingine ndani ya mwezi mmoja kutokea ktk machimbo ya dhahabu kanda ya ziwa, ambapo wachimbaji wengine watatu walifunikwa na kifusi katika mgadi wa dhahabu Buzwagi, wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga.
Hili ni tatizo na linakuwa tatizo kubwa zaidi pale wachimbaji wadogo wadogo ambao hawana mafunzo yoyote ya usalama ktk migodi wanapofikwa na ajali kama hizo, kwani msaada unakosekana hata ule wa huduma ya kwanza.
Inavyoonekana, wachimbaji wadogo wadogo wa dhahabu mbali ya kutokuwa na ujuzi wa masuala ya usalama migodini, hawana chama chao, kama kipo basi uongozi una mapungufu.
Nasema hivyo kwa sababu, siyo rahisi idadi kubwa ya wachimbaji madini ikaendesha shughuli zake bila kuwa na uongozi wa kuhakiki taratibu, kanuni na sheria za usalama kama zinazingatiwa kwenye maeneo hatari kama hayo.
Mazingira ya vifo vya wachimbaji hao katika shimo walimofia ni kwamba, mara baada ya taarifa kuenea kuwa shimo hilo lilikuwa likitoa dhahabu nyingi, wachimbaji walikimbilia humo kiasi kwamba hakuna aliyejali usalama wa mwenzake.
Ufumbuzi unatakikana haraka ili wakati mwingine hali kama hii isije jirudia, kwani suala zima la uchimbaji si baya kwa kuwa dhahabu ni madini yenye thamani kubwa ambayo yanaboresha maisha ya wachimbaji.
Hiyo ni rasilimali yao, ni mali ambayo Serikali kupitia Wizara inayohusika inapaswa kuwasaidia kwa mafunzo, uwezeshwaji katika kuunda vikundi vinavyoweza kuweka taratibu za jinsi ya kupata maeneo na uchimbaji kwa ujumla.
Yote haya yamekuja kutokana na kukosekana kwa taratibu za uchimbaji na kama zipo basi kutosimamiwa vilivyo na watendaji wake ndiko kumepelekea wachimbaji kujiendesha bila kuwepo mipaka ya uchimbaji.
Tunawapa pole wananchi wa kijiji cha Sabola, familia za wachimbaji waliopoteza maisha yao kwani Taifa limeondokewa na nguvu kazi muhimu katika ujenzi wake. Mungu azilaze mahala pema peponi Roho za marehemu wote. Amina.

HAPA NA PALE...

MJENGO HUU ULIOATHIRIWA NA MVUA ZILIZO NYESHA HIVI KARIBUNI UNAPATIKANA MITAA YA MABATINI MWANZA.

MAKOROBOI MOJA YA MITAA MAARUFU JIJINI MWANZA, MIAKA YA NYUMA UMAARUFU WAKE NA SIFA ZAKE ULISABABISHA MWIMBAJI MAARUFU DR, REMMY ONGALA KUTOUSAHAU MTAA HUU WAKATI ALIPO KAA CHINI NA KUTUNGA WIMBO KUHUSU MJI WA MWANZA.

ACHA TU! MIAKA YA ZAMANI WENYEJI WANANIAMBIA KILA KITU DUNIANI KILIKUWA KINAPATIKANA HAPA(MAKOROBOI).

Tuesday, April 13, 2010

BONGE NDANI YA MWANZA EH BANA WACHAA!

MOJA YA MAENEO YA KITALII KATIKATI YA JIJI LA MWANZA CAPRIPOINT MWANZA NA UONEKANO WA BISMARCK ROCK.
PICHANI MR.JACK FISH KATIKA OFISI YAKE (ALIYE MEZA KUU) AKITOA MAELEZO YA SHUGHULI ZA UENDESHAJI WA KAMPUNI IMARA YA ULINZI VICTORIA SUPPORT SERVICE (VSS), BONGE WA KIPINDI CHA POWER BREAKFAST CLOUDS FM ANAONEKANA KUSHOTO KABISA.

KUMBE BONGE NAYE NI MDAU WA VSS MWANZA!

KIKAO KIMEISHA.

TWENDE TUKAKAMATE SAMAKI BANIKA CAPRIPOINT.