ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, February 26, 2010

MUSOMA WAMEGEWA PANDE LA RAHA ZA UKWELI.


HAYAWI HAYAWIZ SASA ISHAKUWAZ!
ILE KIU YA MUDA MREFU YA BURUDANI KWA WAKAZI WA MUSOMA MJINI NA MKOA MZIMA WA MARA SASA IMEPATA TIBA, NI BURUDANI YA MTAKATO ILIYOKOSHWA IKATAKASIKA NAYO NI YA KUKATA NA ULIMI KWANI NI KURAMBA TUUU AAAHMMM- AAHMM!
NI NDANI YA UKUMBI ULIOKARABATIWA NA KUWA WAKISASA ZAIDI PENINSULA BEACH MUSOMA.
UFUNGUZI NI JUMAMOSI HII 27FEB2010
KIINGILIO SHILINGI 3,000/= TU!
SOUND SAFI
LIGHT SAFI
NGOMA SAFI
MISOSI SAFI
WEWE NA MIMI SAFI
KAMA WE BARUTI LIPUKA NAMI PALE.

USIKOSE...

Thursday, February 25, 2010

KABAGO WA PASSION FM AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI.

MTANGAZAJI MAHIRI WA PASSION FM YA JIJINI MWANZA AMBAYE PIA NI MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA PHILBERT KABAGO AMEMPOTEZA MAMA YAKE MZAZI ROSEMARY FELICIAN KABAGO ALIYEFARIKI DUNIA TRH 24 FEB 2010 KATIKA HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO KWA TATIZO LA PRESHA, MWILI UNASAFIRISHWA LEO KUELEKEA BUKOBA KWA MAZISHI. "BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE"

WADAU WA MO RECORDS YA JIJINI MWANZA WALIOHUDHURIA IBADA HIYO KUTOKA KUSHOTO MRS. MANYAGA,DJ SOUND, FILM PRODUCER HANS, MASANJA, PRODUCER TIDDY NA PRODUCER Q.THE DON.
HATUA CHACHE KUTOKA OFISI ZA JIJI LA MWANZA MAENEO YA ISAMILO KUNA KITOFALI HIKI KIKALI KINACHOMEA, NOW KINAPACHIKWA VIOO, KINAKWENDA KWA KASI HOPE SOON KITAKAMILIKA.

UWANJA WA NYAMAGANA SAKATA LAKE JUU YA KUBADILISHWA MATUMIZI NA KUJENGWA HOTEL KIPINDI KIREFU KIMEPITA LIMEKUWA KIMYA LIMEFUKIWA AU LIMEZIKWA? SIDHANI...

HUYU JAMAA ANAYETAJWA KWAMBA NI CHIZI AKIRANDARANDA MITAA MBALIMBALI JIJINI MZ ANAKAMTINDO UKIMPITIA KARIBU ANAKUTWANGA MANGUMI AU KUKUZABA KIBAO NA UKIPITA MBALI AKIKUMAINDI ANAKUPIGA MAWE, AMESUMBUA SANA WATU HUSUSAN AKINA DADA WALOVAA FRESH NA WAKIPITA NA MIONDOKO YA MAPOZI. PICHA HII NILIMPIGA JANA MCHANA. NASKIA JIONI YAKE VIJANA WALIJIPANGA WAKAMZINGIRA NA KUMPA KICHAPO KITAKATIFU, ALIEJE?! HAKUNA RANGI ALIACHA ONA ILIBIDI POLISI WAINGILIE KATI KUMNUSURU. SIJUI KAMA ATARUDI...

Tuesday, February 23, 2010

MWANZA LEO.

ROCK CITY MPAKA ZIWANI KIMTINDO.

ROCK CITY PANDE HII UNAUONA JINSI MJI TARATIBU UNAVYOJENGEKA HUDUMA MUHIMU ZIKIBORESHWA SAMBAMBA NA MAKAZI. JE!UNAWEZA PATIA PICHA HII IMEPIGWA TOKA SEHEMU GANI?

MJENGO MPYA SIMPLE WA PPF ULIOKO BARABARA YA KENYATA UKITIZAMANA NA MWANZA HOTEL MOJA KATI YA MAJENGO YALIYO KATIKA MTINDO WA KISASA YANAYOTIA CHANGAMOTO KWA WAMILIKI WA MAJENGO YAKIZAMANI KUBOMOA MAJENGO YAO NAKUJENGA MAPYA.

JENGO LA CCM MKOA WA MWANZA KAMA LINAVYOONEKANA LEO. HUMO NDANI SI SHUGHULI ZA CHAMA PEKEE BALI KUNA MAKAMPUNI BINAFSI NA YAKISERIKALI YAMEPANGISHA HUMU. OFISI ZA CLOUDS FM 88.1 MWANZA ZIKO JENGO HILI GHOROFA YA 5, KARIBU SANA.