ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 5, 2015

REDD'S ORIGINAL SASA KATIKA MWONEKANO MPYA.

Meneja wa Makao Makuu ya Kiwanda cha Bia Tanzania(TBL), Calvin Martin na Meneja wa Kinywaji cha Redd’s Original, Victoria Kimaro wakionyecha muonekano mpya wa kinywaji cha Redd’s Original wakati wa hafla ya uzinduzi wa kinywaji hicho kwa wafanyakaji iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Wafanyakazi wa Makao Makuu ya Kiwanda cha Bia Tanzania(TBL) wakiburudika na kinywaji cha Redd’s Original wakati wa hafla ya uzinduzi wa muonekano mpya wa kinywaji cha Redd’s Original iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Wafanyakazi wa Makao Makuu ya Kiwanda cha Bia Tanzania(TBL) wakiburudika na kinywaji cha Redd’s Original wakati wa hafla ya uzinduzi wa muonekano mpya wa kinywaji cha Redd’s Original iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Wafanyakazi wa Makao Makuu ya Kiwanda cha Bia Tanzania(TBL) wakiburudika na kinywaji cha Redd’s Original wakati wa hafla ya uzinduzi wa muonekano mpya wa kinywaji cha Redd’s Original iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Wafanyakazi wa Makao Makuu ya Kiwanda cha Bia Tanzania(TBL) wakiburudika na kinywaji cha Redd’s Original wakati wa hafla ya uzinduzi wa muonekano mpya wa kinywaji cha Redd’s Original iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Wafanyakazi wa Makao Makuu ya Kiwanda cha Bia Tanzania(TBL) wakiburudika na kinywaji cha Redd’s Original wakati wa hafla ya uzinduzi wa muonekano mpya wa kinywaji cha Redd’s Original iliyofanyika Dar es Salaam jana.
Picha ya Pamoja.
Picha ya Pamoja.

RITA YAZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUWA NA CHETI CHA KUZALIWA

 Ofisa Uhusiano wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), Jafarri Malema (kushoto), akizungumza na wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo (hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu shughuli zinazofanywa na Rita na umuhimu wa cheti cha kuzaliwa. Kulia ni Ofisa Uhusiano wa Rita, Grace Kyasi.
 Ofisa Uhusiano wa Rita, Grace Kyasi akizungumza katika mkutano na wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo.
Wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo wakiwasikiliza maofisa wa Rita walipokuwa wakizungumza nao.

Dotto Mwaibale

WANANCHI wametakiwa kuwa na vyeti vya kuzaliwa kwani vina umuhimu katika maisha ya kila siku ndani na nje ya nchi.

Mwito huo umetolewa na Ofisa Uhusiano wa Wakala wa  Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), Jafarri Malema wakati  akizungumza na wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu shughuli zinazofanywa na Rita na umuhimu wa kuwa na cheti cha kuzaliwa. 

"Cheti za kuzaliwa ni msingi wa mafanikio ya kila mmoja wetu na ni muhimu kuwa nacho" alisema Malema.

Alisema Rita imekuwa ikifanya shughuli za usajili wa vizazi,vyeti vya kuzaliwa, kuandika wosia, kusajili ndoa na talaka na udhamini kama mali za umma na ile isiyokuwa na mwenyewe.

Alisema faida ya kuandika wosia unasaidia kuepusha watoto, mke au mume kunyang'anywa mali pale kinapotokea kifo na inawezesha kumchagua msimamizi wa mirathi.

Alitaja faida nyingine ya kuandika wosia kuwa ni kuepusha migongano katika familia, ndugu au jamaa na kuwa unampa uhakika wa maisha bora ya baadae warithi wa mali waliziachiwa.

Alisema jambo linalofanyika baada ya kufariki kwa mtu aliyeandika wosia mmoja wa mashahidi anatakiwa kwenda kutoa taarifa Rita ambapo taratibu za wosia kuwasilishwa mahali husika hufanyika.

Naye Ofisa Uhusiano wa Rita, Grace Kyasi alisema umuhimu wa kuwa na cheti cha kuzaliwa ni mkubwa kwani ni nyaraka pekee yenye mamlaka kisheria kuthibitisha tarehe na mahali mtu alipozaliwa na ni nyaraka muhimu kwa kila mwananchi kwani hutumika kupata huduma nyingine za msingi kama elimu, afya na makazi.

Alisema cheti cha kuzaliwa kinawawezesha watoto kujiunga na elimu ya msingi na sekondari na kuwawezesha kupata nafasi ya masomo ya elimu ya juu pamoja na mikopo ya masomo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AADHIMISHA KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI, MKOANI TANGA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga, leo Juni 5, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mazingira wa Ofisi yake, Dkt. Julius Ningu, wakati alipotembelea kwenye banda la maonyesho la Ofisi ya Makamu wa Rais, kwenye Sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamano, mkoani Tanga, leo Juni 5, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya mshindi wa tatu katika usimamizi wa usafi wa mazingira, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga, leo Juni 5, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu utunzaji wa nyaraka kutoka kwa Mkurugenzi wa Msaidizi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Lupi Mwaikambo, wakati alipotembelea kwenye banda la maonyesho la Ofisi ya Makamu wa Rais, kwenye Sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamano, mkoani Tanga, leo Juni 5, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya mshindi wa pili katika usimamizi wa usafi wa mazingira, Mwakilishi wa Manispaa ya Kinondoni, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga, leo Juni 5, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitembelea mabanda wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga, leo Juni 5, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mtoa huduma wa dawa za asili, Karunde Amadi, wakati alipotembelea kwenye banda wafanyabiashara za dawa asili, kwenye Sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamano, mkoani Tanga, leo Juni 5, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya mshindi wa kwanza katika usimamizi wa usafi wa mazingira, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga, leo Juni 5, 2015. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo ya usimamizi wa usafi wa mazingira, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Kpt . Chiku Galawa wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga, leo Juni 5, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhi zawadi ya Pikipiki kwa mmoja kati ya washindi. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua rasmi Jarida la muongozo wa Usafi wa Mazingira, wakati wa sherehe za maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Mazingira Duniani, zilizofanyika kwenye wa Viwanja Vya Tangamani, mkoano Tanga, leo Juni 5, 2015. Kushoto kwake ni Waziri wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Binilith Mahenge, Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, Samia Suluhu, na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Stephen Masele Picha na OMR

MBILINYI NA MUNDI KUZITWANGA KESHO UWANJA WA NDANI WA TAIFA

Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akitunishiana misuli na Said Mundi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpaqmbano wao wa kesho jumamosi utakaofanyika katika uwanja wa ndani wa Taifa mpambano wa raundi sita. 

Bondia Vicent Mbilinyi kushoto akipozi kigagwe na Said Mundi baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao utakaofanyika jumamosi ya juni 6 katika uwanja wa ndani wa taifa.

Bondia Vicent Mbilinyi akipima uzito kwa ajili ya mpambano wake na Said Mundi wa Tanga kushoto ni mratibu wa mpambano uho Antony Rutta.
 
Bondia Said Mundi wa Tanga akipima uzito kwa ajili ya mpambano weke na Vicent Mbilinyi kushoto ni Anton Rutta Picha na SUPER D BOXING NEWS.

SKYLIGHT BAND YAENDELEA KUUNGURUMA NDANI YA KIOTA KIPYA CHA LUKAS PUB MASAKI, USIKOSE LEO

Ilikuwa noma sana siku ya Ijumaa iliyopita maana ilikuwa sio ya kupitwa basi mchuke na ndugu, jamaa au rafiki yako leo uje kuona vitu vitamu kutoka kwenye Bendi ya Skylight
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 akiimba moja ya nyimbo yenye hisia kali sambamba na msanii mwenzake Sam Mapenzi.
Mwimbaji kutoka Bendi ya Skylight, Sony Masamba akitoa burudani ndani ya kiota cha Lukas Pub huku akisindikizwa na wasanii wenzake ambao ni Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47(katikati) na Sam Mapenzi.
Sam Mapenzi pamoja (Kushoto) na Ashura Kitenge wakiimba kwafuraha huku wakiwakonga nyoyo mashabiki wa Skylight Band.
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akishusha mistari na kucheza huku waimbaji wenzake Sony Masamba (wa pili kutoka kushoto), Aneth Kushaba(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sam Mapenzi wakisebeneka Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Lukas Pub jijini Dar.
Sony Masamba akiimba na kucheza pamoja na waimbaji wenzake ambao ni Aneth Kushaba (katikati) pamoja na Sam Mapenzi ndani ya kiota kipya cha Lukas kilichoko Masaki jijini Dar.
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiimba na kusheza pamoja na waimbaji wenzake kwenye kiota cha Lukas Pub ijumaa iliyopita
Ulikuwa ni mwendo wa kuserebuka mbele ya mashabiki wao(hawapo pichani) maana ilikuwa ni noma saanaaaaa.....!!!!
Binti mwenye sauti ya kumtoa Nyoka pangoni, Ashura Kitenge akiimba kwa hisia moja ya nyimbo inayobamba sana nje na ndani ya Tanzania katika kiota cha Lukas Pub jijini Dar.
Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 akiimba sambamba na msanii mwenzake Ashura Kitenge
Waimbaji wa Skylight Band wakiendelea kutoa burudani ya kukata na shoka
Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 akiendelea kutoa burudani huku akisindikizwa na wasanii wenzake ambao ni Ashura Kitenge(wa kwanza kutoka kushoto), Joniko Flower(wa pili kutoka kushoto) pamoja na Sony Masamba

Ulifika wakati wa kuanza kucheza style za bendi ya Skylight hii ni style ya Kikuku inakubidi kanza usugue alafu ufanye ya kwako njoo leo ujionee mambo mapya kutoka katika bendi yako
Mashabiki wa Skylight Band wakijiachia kwa raha zao ndani ya kiota cha Lukas pub
Sam Mapenzi akitoa burudani huku akisindikizwa na wanamziki wenzake waliokuwa wakimpa support ya nguvu kwenye ngoma za Nigeria ambao ni Joniko Flower (wa kwanza kushoto), Ashura Kitenge(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sony Masamba.
Ilikuwa ni furaha maana Fleva zilizokuwa zikipigwa zilikuwa zinawapagawisha mashabiki
Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 akiimba