Kwa mujibu wa tafsiri aliyokuwa akiitoa Vick Mtetema kuwasilisha taarifa ya Muasisi wa Shirika la Under The Same Sun ambalo limekuwa likijibidiisha katika kuibua yale yaliyofichika yanayohusu changamoto, manyanyaso na ukatili kwa watu wenye albinism, Bw. Peter Ash, baada ya kufanya ziara kwenye kijiji cha Ndame wilayani humo (Kwimba) na kukutana na mama yake Pendo aitwaye Sofia Juma, amepokea malalamiko toka kwa mama huyo ambaye amelelemika kuwa tangu apate tatizo hakuna kiongozi yeyote wa Kisiasa aliyethubutu kumtembelea kujua hali yake au kutafuta ufumbuzi akiwemo yule wa jimbo lake aliyempigia kura.
Wanahabari kusanyikoni. |
Hiyo ni hali ambayo imekuwa ikijirudia, Peter Ash akikutana na malalamiko kama hayo pindi anapozitembelea baadhi ya familia zinazokumbana na masahibu kama hayo yanayohusisha watu wenye ulemavu wa ngozi (wenye albinism).
"Hata familia ya mtoto Karim Kasimu (4) anayeishi na wazazi wake Nyakato jijini Mwanza ambaye pia alinusurika kutekwa nyara tarehe 6 Januari 2015 akiwa karibu na nyumbani kwao, ile familia haijaona kiongozi yoyote wa kisiasa aliyethubutu kutembelea kuona jinsi gani anaweza kuisaidia kushiriki kwa namna moja au nyingine kuwalinda watu wenye albinism" KUMSIKILIZA BOFYA PLAY
Wanahabari kikazi zaidi. |
AMRI BILA VITENDO NI KAZI BURE.
Hoja imewasilishwa kwa njia ya swali:- Hivi hiyo amri ya kupiga marufuku upigaji ramli iliyotolewa na Waziri wa mambo ya ndani inatofautiana nini na amri iliyotolewa na Waziri Mkuu mnamo Januari 2009,amri ambayo hata hivyo ilikuja kufutwa tarehe 30 September 2010 mwezi mmoja kabla ya UCHAGUZI MKUU?
Kwa sasa hivi tunaelekea kwenye UCHAGUZI MKUU mwingine, nayo amriimetolewa. Jeh hii amri itakuwa na uzito, itafanya kazi, itatimiza malengo yaliyokusudiwa? BOFYA PLAY KUSIKILIZA.
Mwanahabari Albert G. Sengo akitafakari mara baada ya kutoka chumba cha mkutano na wadau wa Under the same sun uliofanyika katika ukumbi wa Hotel Ryans Bay wilayani Nyamagana jijini Mwanza. |
UMOJA WA MATAIFA WAAMUA KUHUSU WATU WENYE ALBINISM
Zaidi ya matukio 152 ya mauaji yametokea ndani ya kipindi cha miaka 14 nchini Tanzania lakini ni asilimia 5 tu ya kesi zake zimefikishwa mahakamani.
Umoja wa Mataifa umetambua Umuhimu wa kuliangalia hili suala la watu wenye albinism, hali yao na ukatili unaofanywa dhidi yao na sasa umeitenga kuanzia mwaka huu tarehe 13 mwezi JUNI ya kila mwaka kuwa 'SIKU YA ALBINISM DUNIANI'
BOFYA PLAY SIKILIZA