ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 18, 2015

MAPOKEZI YA MAGUFULI YAVUNJA REKODI YA CCM MWANZA.

Dkt John Pombe Magufuli akiwasili jijini Mwanza na makaribisho ya wana CCM wakiongonzwa na Mwenyekiti wa mkoa Anthony Dialo (kushoto mwenye mbele mwenye shati la kijani)
Msafara ukitoka Airport Mwanza.
Watoa huduma, wafanyabiashara na abiria walio kwenye uwanja wa ndege Mwanza wakipunga mikono kwa msafara wa mteule wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
Baadhi ya Wananchi wakilikimbiza gari la  Mgombea Uraisi CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli kwa shangwe kama waonekanavyo pichani ,wakati Magufuli lipokuwa akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla jioni ya leo.
Msafara.
Msafara wa mapokezi Mwanza.
Msafara wa mapokezi Mwanza.
Msafara na shangwe za hapa na pale toka kwa wananchi.
Barabara ya Airport - Makongoro jijini Mwanza.
Msafara wa mapokezi Mwanza.
Msafara wa mapokezi Mwanza.
Msafara wa mapokezi Mwanza.
Mhe.Jonh Mombe Mgufuli, alisimama sehemu mbalimbali nakuongea na wananchi alisema hakuja kufanya kampeni bali  amekuja kwaajili ya utambulisho tu na sio vingine, aidha mgombea huyo amesema wakati ukifika watanzania wote wajitokeze kupigakura na kuchagua Chama cha mapinduzi CCM, kuanzia nafasi ya Rais, Wabunge na Madiwani. Magufuli amewashukuru wanachama wa CCM na wananchi wa jiji la Mwanza kwakujitokeza kwa wingi kumpokea yeye na mke wake akiongeza neno moja "Watanzania Mniombe"
 Baadhi ya Wananchi wa jiji la Mwanza wakiwa wamefunga barabara kwa muda wakishangilia ujio wa  Mgombea Uraisi wa CCM,Mh.Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwasili jijini Mwanza kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi kwa ujumla jioni ya leo.
kuna wengine waliacha kazi kwa muda kama hizi na kuja kwenda kushangilia ujio wa Mh.Dkt John Magufuli.

Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi alipokuwa akiwasili jijini Mwanza jioni ya leo akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa juu wa chama cha CCM,Magufuli yuko jijini Mwanza kujitambulisha kwa Wananchi.
Amsha amsha.
 Wananchi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi mbele ya jengo la CCM Mkoa kwaajili ya kumpokea Dkt John Pombe Magufuli .
Dkt John Pombe Magufuli akiwasili katika viwanja vya jengo la CCM Mkoa wa Mwanza.
Mke wa Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi Dkt.John Pombe Magufuli,Mama Janeth Magufuli akiwasalimia Wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake waliojiotokeza kwa wingi kuwapokea,Pichani kulia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Shangwe za wananchi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.Dkt John Pombe Magufuli kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake,nje ya ofisi za CCM mkoa wa Mwanza.
Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake,nje ya ofisi za CCM mkoa,ambao walijotokeza kumlaki kwa shange na furaha kubwa.Dkt Magufuli amewasili jana jijini Mwanza akitokea jijini Dar kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi kwa ujumla.
Mgombea Uraisi kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Mh.Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wanachama wa chama hicho pamoja na Wananchi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake,nje ya ofisi za CCM mkoa,ambao walijotokeza kumlaki kwa shange na furaha kubwa.Dkt Magufuli amewasili jana jijini Mwanza akitokea jijini Dar kwa ajili ya kujitambulisha kwa wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi kwa ujumla.
Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia Wananchi wa jiji la Mwanza waliojitokeza kwa wingi jioni ya jana.
Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na kada wa CCM mara baada ya kusalimiana na MNEC wa Tarime Mzee Gachuma.
Dkt John Pombe Magufuli akiweka saini katika kitabu cha wageni kwenye ofisi ya CCM Mkoa wa Mwanza, Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza Anthony Diallo, Katibu wa CCM Mkoa Miraji Mtaturu na Mbunge wa Jimbo la Titus Kamani.
PICHA ZOTE NA ZEPHANIA MANDIA WA GSENGO BLOG.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AJUMUIKA NA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU KATIKA SWALA YA EID EL FITRI KITAIFA MKOANI GEITA.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwahutubia waumini wa dini ya Kisslamu wakati wa swala ya Sikukuu ya Eid El-Fitri iliyofanyika Kitaifa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kalangalala, katika Halmashauri ya Mji wa Geita, leo Julai 18, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwahutubia waumini wa dini ya Kisslamu wakati wa swala ya Sikukuu ya Eid El-Fitri iliyofanyika Kitaifa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kalangalala, katika Halmashauri ya Mji wa Geita, leo Julai 18, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijumuika na Baadhi ya Viongozi wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, (BAKWATA) na wananchi katika swala ya Sikukuu ya Eid El-Fitri iliyofanyika Kitaifa kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi  Kalangalala, katika Halmashauri ya Mji wa Geita, leo Julai 18, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir Ally, baada ya kumalizika kwa swala ya Sikukuu ya Eid El-Fitri kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi, Kalangalala, mkoani Geita, leo Julai 18, 2015. Picha na OMR
baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria Swala hiyo ya Sikukuu ya Eid El-Fitri Kitaifa Mkoani Geita leo Julai 18, 2015. Picha na OMR
baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria Swala hiyo ya Sikukuu ya Eid El-Fitri Kitaifa Mkoani Geita leo Julai 18, 2015. Picha na OMR
baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria Swala hiyo ya Sikukuu ya Eid El-Fitri Kitaifa Mkoani Geita leo Julai 18, 2015. Picha na OMR
baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu waliohudhuria Swala hiyo ya Sikukuu ya Eid El-Fitri Kitaifa Mkoani Geita leo Julai 18, 2015. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akishiriki swala ya Sikukuu ya Eid El-Fitri na waumini wa Dini ya Kiislamu iliyofanyika Kitaifa wa Mkoani  Geita  leo Julai 18, 2015. Picha na OMR
Kaimu Mufti  Mkuu wa Tanzania, Sheikh, Abubakar Zubeir Ally, akitoa neno la shukrani baada ya swala hiyo ya kitaifa mkoani Geita. Picha na OMR
Maagano.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Masheikh kutoka mikoa mbalimbali walioalikwa kuhudhuria swala ya Sikukuu ya EidEl-Fitri baada ya swala hiyo iliyofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi, Kalangalala, Mkoani Geita. Picha na OMR

DADA ANTU MANDOZA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE WA VITI MAALUM,VIJANA - BUKOBA LEO

Mgombea Ubunge Viti Maalum Vijana Bukoba Bi. Antu Mandoza(Kulia) akirejesha Fomu ya Kuomba Ridhaa kuteuliwa kugombea Ubunge wa Viti maalum Vijana Bukoba katika ofisi za umoja huo Mjini Bukoba, ahaidi kuinua Vijana Kiuchumi endapo atapata nafasi ya kuwa Mbunge wa Vijana.(Habari Picha na Faustine Ruta/bukobasports).
Mcheza kwao hutunzwa, Vijana wazidi kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi. Binti Antu Mandoza mwenye kuonekana kuwa na umri miaka 22-25 Amerudisha Fomu za kuwania nafasi ya Ubunge Vijana Viti Maalumu kupitia CCM. 

Kwa Mahojiano mafupi ameongelea jinsi anavyopanga kuinua Maisha ya Vijana kwa kuwatengenezea Fursa na mbinu mbalimbali za kujiajiri pia kuwaonya kutokukubali kutumika vibaya na MAKUNDI ya Kisiasa tunapoelekea Uchaguzi kwani ni wajibu wetu Vijana kuilinda Amani yetu. 

Mgombea huyo pia amesema kuwa shauku yake kubwa ni kuwatumikia Vijana kwa kutatua changamoto ya Ajira na pia ametoa ahadi ya kushirikiana na Vijana bega kwa bega kuleta maendeleo katika Mkoa wa Kagera.

Binti Antu Mandoza akiweka sawa Kumbukumbu zake katika kitabu mbele ya karani Bi. Jasinta Benedicto wa Umoja wa Vijana Kagera.

Dada Antu Mandoza akiwa kwenye Ofisi za Umoja wa Vijana Bukoba.
Mgombea Ubunge Viti Maalum Vijana Bukoba Dada Antu Mandoza (kulia) akiptia Fomu yake ya Kuomba Ridhaa kuteuliwa kugombea Ubunge wa Viti maalum Vijana. Kushoto ni Bi. Jasinta Benedicto karani wa Umoja wa Vijana Kagera.

Mgombea Ubunge viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi dada Antu Mandoza akitoka katika ofisi za umoja wa vijana wa ccm Mkoa wa Kagera baada ya kuchukua fomu