Friday, April 21, 2023
TAASISI YA GOODWILL&HUMANITY FOUNDATION YALAANI NDOA ZA JINSIA MOJA
MKURUGENZI wa Kituo cha Kulea Watoto cha Goodwill and Humanity Foundation Sayyed Muhdhar Idarusi akizungumza wakati wa hafla ya Iftari aliyoaiandaa kwenye Kituo hicho
Mwakilishi wa Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Mwanaidi ambaye ni Afisa Tarafa wa Ngamiani Kati akizungumza
Msimamizi wa Casa Della Giaio Sista Consolata Mgumba akizungumza wakati wa halfa hiyo ambapo aliiasa jamii ipunguze ubinafsi na kurudisha moyo wa kujali kuwaangalia wengine na kuwajaali.
MKURUGENZI wa Kituo cha Kulea Watoto cha Goodwill and Humanity Foundation Sayyed Muhdhar Idarusi akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho mara baada ya futari
MKURUGENZI wa Kituo cha Kulea Watoto cha Goodwill and Humanity Foundation Sayyed Muhdhar Idarusi akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho mara baada ya futari
MKURUGENZI wa Kituo cha Kulea Watoto cha Goodwill and Humanity Foundation Sayyed Muhdhar Idarusi akiwa kwenye picha ya pamoja na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho mara baada ya futari
Na Oscar Assenga,TANGA
MKURUGENZI wa Kituo cha Kulea Watoto cha Goodwill and Humanity Foundation Sayyed Muhdhar Idarusi amesema kwamba taasisi hiyo inalaani vikali ndoa ya jinsia moja ikiwemo vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wakina mama.
Muhdar alitoa kauli hiyo wakati wa Iftari iliyoandaliwa na Taasisi hiyo kwa lengo la kueleza namna walivyopingana na vitendo hivyo na kuitaka jamii kutokubali kushiriki kwenye mambo hayo
Alisema kwamba wanataka kuiambia dunia kwamba taasisi hiyo ina laani ndoa za jinsia moja na inakemea vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikifanywa kwa watoto na wakina mama kwa kuitaka jamii kubadilika na kuachana navyo.
“Taasisi hii tuna laani ndoa za jinsia moja na hatuviungi mkono kwani sisi ni moja ya huduma tunazotoa ni kuhifadhi watoto waliopotea na waliofanyiwa ukatili na Tuna Afisa Ustawi maalumu wa kuambatana na maafisa wa serikali kuwapelekea mahakamani wanaowafanyia ukatili watoto wenye kesi zinayowakandamizi watoto tunaokuwa nao kwenye makazi yetu”Alisema
“Kwani tumekuwa tukipokea watoto wamekatwa masikio,watoto wamekatwa mikono,wamemiminiwa nailoni iliyochomwa moto,waliocopmwa midomoni ,waliovuliwa nguo na kumiminiwa nailioni na kuwababua ngozi hizo ni changamoto kubwa wanazokumbana nazo watoto”Alisema
Aidha alisema kwamba wao wanaungana na kauli ya Serikali ya kukataa ukatili dhidi ya watoto na leo wametoka kuiambia dunia ukatili dhidi ya watoto haiwezekani ikiwemo ndoa ya jinsia moja haikubaliki na hawapo tayari kuwa na taifa ambalo limejaa mashoga na lenye wanawake wasagaji .
“Tumewaita kuja kufuturu pamoja ni kuthamini mchango wenu kwenye taasisi hii ambayo imeundwa kwa lengo la kusaidia mayatima,wazee, walemavu na makundi yasiyojiweza”Alisema
Awali akizungumza Msimamizi wa Casa Della Giaio Sista Consolata Mgumba aiasa jamii ipunguze ubinafsi na kurudisha moyo wa kujali kuwaangalia wengine na kuwajaali.
“Tujiulize watoto yatima kwanini zamani hayakuwepo familia tuacha kukimbia maajukumu yetu na tuwapeleka watoto kwenye vituo hivyo ikiwa hakuna msaada wowte kwenye jamii kwani wana jamii zao “Alisema
Aidha aliwataka wazingatie maadili huku akieleza kwamba mambo ya ushoga inatokana na wakina mama kutokutaka kuishi na wanaume badala yake wanalea watoto pekee yao na hivyo kuwajenga watoto kwenye mitazamo isiyosawa hivyo wao wataendelea kulipigia kelele jambo hilo.
Naye kwa upande wake akizungumza wakati wa iftari hiyo Mwakilishi wa Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga Mwanaidi ambaye ni Afisa Tarafa wa Ngamiani Kati alitoa wito kwa wazazi na walezi kutoa taarifa kuhusu vitendo vya ukatili kwenye jamii zao kutokana na kwamba hali sio nzui
Mwanaidi alisema kwamba wazazi watoe taarifa na wae na kauli kuhakikisha wanashirikiana kwa pamoja kuweza kutokomeza vitendo vya ukatili kwenye jamii
DR CHINGUILE ATATUA CHANGAMOTO YA MAJI NA BARABARA KIJIJI CHA MCHANGANI.
Tuesday, April 18, 2023
MWANAMUME MMOJA WA CHINA AMEFARIKI BAADA YA KUPIGWA RISASI NA MWINDAJI AMBAYE ALIDHANI KUWA NI SUNGURA POLISI WASEMA.
Wanaume wanne wamekamatwa kwa kifo cha Wang Moujin, ambaye alianguka kwenye shimo baada ya kupigwa risasi kichwani na bunduki ya anga.
Tukio
hilo lilitokea Ijumaa iliyopita jioni wakati wanne hao walipoenda kuwinda
katika Mji wa Shaxi, mkoa wa Jiangxi.
Matukio
yanayohusisha bunduki ni nadra nchini Uchina.
Polisi
kutoka wilaya ya Xinzhou walisema mmoja wa watu hao alifyatua risasi baada ya
kuona msogeo kwenye nyasi kando ya mtaro, ambapo Bw Wang aliripotiwa kuwa
akivua samaki.
Polisi
waliitwa kwenye eneo la tukio na kuwakamata wanaume hao wanne, ambao baadhi yao
wanafikiriwa kuwa na umri wa miaka 30.Uchunguzi unaendelea.
Uchunguzi
wa maiti ulibaini kuwa Bw Wang alikufa kwa kuzama.
Uchina
ina baadhi ya sheria kali zaidi za bunduki duniani, ambazo zinaweza kutumika hata
kwa bunduki za kuiga au za kuchezea.
Tukio
hilo limejadiliwa sana kwenye mitandao ya kijamii ya China."Inawezekanaje
kwamba watu katika nchi hii wana bunduki?"Alisema mtoa maoni mmoja kwenye
Weibo.
SUNGUSUNGU WASAKWA KWA KUPIGA KUMJERUHI MWANAMKE
Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linawatafuta sungusungu zaidi ya 30 waliohusika kumcharaza viboko hadharani na kumsababishia majeraha mbalimbali mwilini, Manka Mushi (26) mkazi wa Kijiji cha Ikoma Kata ya Itilima Halmashauri ya Kishapu kwa madai ya kuiba Sh 420,000/= za mteja wake.
Akizungumzia
tukio hilo lilitokea Aprili 14, 2023 na kumsababisha binti huyo kulazwa Hospitali
ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Janeth Magomi
amesema baada ya sungusungu hao wa jeshi hilo la jadi kufanya tukio hilo kwenye
uwanja uliopo katika kijiji hicho walikimbia.
Akisimulia mkasa
uliomkuta, Manka aliyekuwa akifanya kazi baa na nyumba ya kulala wageni
kijijini humo amesema ilikuwa Saa sita usiku ambapo mteja aliyefahamika kwa
jina la Julius Tarimo aliagiza kupelekewa shuka, baada ya kumpelekea ghafla
alimkaba koo akimtaka kurudisha Sh420, 000 alizohisi binti huyo kachukua.
Manka amesema
alikataa kuhusika na wizi huo na kupiga kelele za kuomba msaada kisha Julius
kumtishia kuwa atamtambua baada ya binti huyo kumkataa kimapenzi na baadaye
alifanikiwa kutoka ndani ya chumba hicho.
“Kufuatia
hatua hiyo niliambiwa na kamanda wa sungusungu twende uwanjani na baada ya
kufika nilikuwa mwanamke pekee yangu nikaambiwa ni lale chini katikati ya
wanaume zaidi ya 30 ukaletwa mzigo wa fimbo wakaanza kunicharaza viboko kwa
zamu nikijaribu kuinuka wengine wanapiga mgongoni na kichwani,” amesema Manka
Amesema aliwapa
namba ya mama yake mzazi ambaye anaishi jijini Arusha, walimpigia na kuzungumza
naye kisha kumtaka atume hela lakini aliwaomba wampeleke polisi na baada ya
kuona hali inazidi kuwa mbaya walimpeleka ofisi ya Kata kutoa maelezo
hakupokelewa.
“Namshukuru Mungu
kwa sasa naendelea vizuri tofauti na awali ambapo sehemu ya makalio na mgongoni
kulikuwa kumejaa vidonda, Naomba Serikali iwachukulie hatua kali sungusungu
walionifanyia kitendo hicho,”amesema
Muhudumu wa wodi
namba saba ya wanawake na upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga, Weru Kiula amesema walimpokea Manka Aprili 14 mwaka huu akiwa na
hali mbaya na vidonda kwenye makalio na mgongoni lakini kwa sasa anaendelea
vizuri.
Ofisa Ustawi wa
Jamii Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga, Prisila Mushi amesema matukio ya
wanawake kupigwa na sungusungu yamekuwa yakitokea mara kwa mara na kuiomba
Serikali ichukuwe hatua kali kwa watu waliohusika na ukatili huo.
MAJIBU YA MHE MEMBE KWA ASKOFU MWAMAKULA!
Baba Askofu Salaam na Asante kwa barua yako ambayo umenitaka nimsamehe Musiba kwa sababu Amesalimu Amri na kwamba hana hela hata kama atauza kijiji!
Baba Askofu, sababu ulizozitoa hazina mashiko kwa sababu Musiba hajaniomba radhi, hajasalimu amri na amechelewa! Aidha hata kama hana hela kama unavyosema, anazo mali zisizohamishika na hizo zote zitapigwa mnada!
Musiba anajua kuwa siwezi kumsamehe kwa sababu nilimpatia nafasi tatu za wazi za kuomba radhi kwenye Chama, kwa barua ya kumtaka aombe radhi kwenye magazeti yake, na kabla ya kesi kuanza tulipata muda wa kulimaliza jambo hili nje ya mahakama! Nafasi zote hizo alizikataa.
Sitamsamehe kamwe na anastahili adhabu hiyo ili awe na adabu na iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za kijinga kama hizo!
Nawashukuru Majaji wote wa mahakama kuu kwa uvumilivu na kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kunirudishia heshima yangu na kuuthibitishia umma kuwa katika nchi hii kuna uhuru wa Mahakama na uongozi unaoheshimu sheria!
Vinginevyo nakushukuru kwa barua na mawazo yako! Ubarikiwe!
BM
Monday, April 17, 2023
WENJE ATOA YA MOYONI KUHUSU SUALA LA AJIRA NCHINI.
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza Mhe. Ezekiel Wenje ametoa ya moyoni kuhusu suala la ajira nchini.
Wenje ameyasema hayo akiwa kwenye ziara yake kuangalia na kutathimini hali ya biashara katika soko la Mchafukuoga lililopo kata ya Igogo jijini hapa. . . . #jembefmkimewaka2023🔥🔥🔥RAIS SAMIA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA YA CHIMBAJI MADINI MUHIMU NA MADINI YA KIMKAKATI, IKULU DODOMA.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mikataba baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni tatu (3) za Uchimbaji Madini Muhimu na Madini ya Kimkakati kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 17 Aprili, 2023.
Picha namba 2. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Eliezer Mbuki Feleshi wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Msingi (Framework Agreement) baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Uchimbaji Madini ya EcoGraf Limited ya Australia iliyowakilishwa na Mtendaji Mkuu wake Andrew Spinks pamoja na Christer Mhingo kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 17 Aprili, 2023. Mkataba huu unahusu mradi wa Epanko, Ulanga Mkoani Morogoro.
Picha namba 3. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu akisaini Mkataba wa makubaliano ya Wanahisa baina ya Serikali na Kampuni ya Uchimbaji Madini ya EcoGraf Limited ya Australia iliyowakilishwa na Mtendaji Mkuu wake Andrew Spinks pamoja na Christer Mhingo kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 17 Aprili, 2023.
Picha namba 4. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Eliezer Mbuki Feleshi wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Msingi (Framework Agreement) baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Evolution Energy Minerals ya Australia iliyowakilishwa na Mtendaji Mkuu wake Phillip Hoskins, pamoja na viongozi wengine Michael Bourgnoin pamoja na Heavenlight Kavishe kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 17 Aprili, 2023. Mkataba huo ni wa Chilalo, Ruangwa Mkoani Lindi
Picha namba 5. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu akisaini Mkataba wa makubaliano ya Wanahisa baina ya Serikali na Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Evolution Energy Minerals ya Australia iliyowakilishwa na Mtendaji Mkuu wake Phillip Hoskins, pamoja na viongozi wengine Michael Bourgnoin pamoja na Heavenlight Kavishe kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 17 Aprili, 2023.
Picha namba 6. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Eliezer Mbuki Feleshi wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Msingi (Framework Agreement) baina ya Serikali ya Tanzania na Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Peak Rare Earth Limited ya Australia iliyowakilishwa na Mwenyekiti Mtendaji wake Russell Scrimshaw wapili (kulia) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bardin Davis kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 17 Aprili, 2023.
Picha namba 7. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishuhudia Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu akisaini Mkataba wa makubaliano ya Wanahisa baina ya Serikali na Kampuni ya Uchimbaji Madini ya Peak Rare Earth Limited ya Australia iliyowakilishwa na Mwenyekiti Mtendaji wake Russell Scrimshaw wapili (kulia) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo Bardin Davis kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 17 Aprili, 2023. Mkataba huo unahusu Mradi wa Ngualla uliopo Mkoani Songwe
WAZIRI AWESO ATOA AGIZO KWA MKURUGENZI WA IDARA YA USAMBAZAJI MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA CPA MSIRU
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akisisitiza jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Korogwe Jokate Mwogelo leo wakati wa ziara yake katika Mji wa Korogwe ambaye ilikuwa na lengo la kuangalia tatizo la upatikanaji wa maji katika mji huo
Waziri wa Maji Jumaa Aweso akizungumza leo wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani Korogwe
Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji Mji Korogwe Mhandisi Sifael Masawa akieleza jambo wakati wa ziara hiyo
MKUU wa wilaya ya Korogwe Joketi Mwogelo akizungumza wakati wa ziara hiyo kushoto ni Waziri wa Maji Jumaa Aweso
Waziri wa Maji Jumaa Aweso kushoto akimsikiliza kwa umakini Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Timotheo Mzava wakati wa ziara hiyo anayewafuatia kwa nyumba ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM)
Waziri wa Maji Jumaa Aweso katikati akiwa na Mkuu wa wilaya ya Korogwe Joketi Mwogelo kushoto wakati wa ziara yake wilayani Korogwe
Na Oscar Assenga, KOROGWE
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amemuagiza Mkurugenzi wa Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira ,Wizara ya Maji CPA Joyce Msiru kuziangalia Mamlaka za Maji Usafi wa Mazingira katika Miji mbalimbali nchini ili wakurugenzi wao waendane na mazingira ya elimu yao kuliko ilivyo sasa.
Sambamba na hilo akaagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Maji wa Korogwe mjini Mhandisi wa Maji Korogwe Mji Sifael Masawa kupangiwa kazi nyengine kutokana na kushindwa kutatua changamoto ya maji kwenye kwenye eneo lake
Aweso aliyasema hayo jana wakati wa ziara yake katika Mji wa Korogwe ambaye ilikuwa na lengo la kuangalia tatizo la upatikanaji wa maji katika mji huo licha ya kuwepo kwa vyanzo vya maji ikiwemo Mto Pangani ambao unapita katikati ya mji huo.
Hatua hiyo ni baada ya kufika wilayani humo na kupata taarifa kuhusu miradi ya maji inayotekeleza kwenye mji huo ambapo alionyesha kutokuridhishwa na namna mtendaji huyo anavyoshughulia jambo hilo ili liweze kupata majawapo yake.
Alisema haiwezekani mji huo kukosa huduma hiyo muhimu wakati kuna vyanzo ambavyo vinaweza kutumika kuweza kuondosha changamoto hivyo lakini kutokana na usimamizi mbovu unapelekea kuwepo wa hali hiyo na wao kama wizara hawawezi kukubali kuona jambo hilo.
“Mkurugenzi wa Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira ,Wizara ya Maji CPA Joyce upo hapa naagiza Mamlaka zote hapa nchini aina ya Korogwe tuangalie wakurugenzi wao taaluma zao ziendane na mazingira yao sambamba na elimu mimi sitamtoa kwenye kazi lakini huyo wa hapa Mkurugenzi wa Maji Korogwe Mji Mhandisi Sifale Masawa ni mzuri lakini apelekwe sehemu ambayo inaendana na mazin gira yta elimu yake”Alisema Waziri Aweso.
“Umeshakuwa Mkurugenzi hapa jiendeleze kielimu…fursa zipo nyingi za vyuo hatuwezi kwenda hivi lakini Katibu Mkuu wa Wizara leo mkae mpange mje muona namna ya kufanya hapa Korogwe kama ni suala la kutoa miundombinu ya zamani tuona tunafanyaje”Alisema
“Lakini sio tunakaa na kulalamika wakati mto Pangani upo hapa tunaendelea kuteseka lakini hitaji hilo liendane na miji ya 28 na fedha za awali zimeshatolewa”Alisema
Katika hatua nyengine,Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameagiza kupelekwa Mkurugenzi mwengine Korogwe na yeye kupangiwa sehemu nyengine ufanye kazi ambayo itaendana na mazingira ya hapa kwenye mji wa Korogwe kutokana na kwamba wanahitaji kusaidiwa hivyo hapoa wataona namna ya kumuweka mtu mwengine .
“Hapa tutamuweka mtu mwengine atusaidie kwani hata mazingira haya ushindwe hata ofisi kuboresha ndio maana hata huna kujiamini lakini ninachojua mtaalamu wa maji ni mtu ambaye amesomea maji ndio mtu anasema mambo yanakuwa safi hakuna kipaumbele nini kifanyike kuondosha tatizo la maji bado umeendelea kukaa kimya bila kupatikana kwa suluhu”Alisema Aweso
Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji Mji Korogwe Mhandisi Sifael Masawa alisema kuwa mamlaka hiyo imakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa miundombinu ya maji hali ambayo inasababisha kuwepo na uhaba wa maji.
Alisema kuwa licha ya kuwa na vyanzo vingi vya maji hali ya upatikanji wa maji kwa sasa ipo katika asilimia 70 lakini changamoto ya uhaba wa umeme mdogo pamoja na kutokuwewepo na mtambo wa kusafisha maji kumesababisha uwepo wa changamoto hiyo.
“licha ya jitihada za serikali kutuletea mitambo kwa ajili ya uchimbaji wa visima saba tunauhitaji wa fedha takribani sh Mil 825 kwa ajili ya uwekaji wa miundombinu ya usambazaji wa maji baada ya maji kupatikana .