ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, April 18, 2023

MAJIBU YA MHE MEMBE KWA ASKOFU MWAMAKULA!


Baba Askofu Salaam na Asante kwa barua yako ambayo umenitaka nimsamehe Musiba kwa sababu Amesalimu Amri na kwamba hana hela hata kama atauza kijiji!


Baba Askofu, sababu ulizozitoa hazina mashiko kwa sababu Musiba hajaniomba radhi, hajasalimu amri na amechelewa! Aidha hata kama hana hela kama unavyosema, anazo mali zisizohamishika na hizo zote zitapigwa mnada!

Musiba anajua kuwa siwezi kumsamehe kwa sababu nilimpatia nafasi tatu za wazi za kuomba radhi kwenye Chama, kwa barua ya kumtaka aombe radhi kwenye magazeti yake, na kabla ya kesi kuanza tulipata muda wa kulimaliza jambo hili nje ya mahakama! Nafasi zote hizo alizikataa.

Sitamsamehe kamwe na anastahili adhabu hiyo ili awe na adabu na iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za kijinga kama hizo!
Nawashukuru Majaji wote wa mahakama kuu kwa uvumilivu na kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kunirudishia heshima yangu na kuuthibitishia umma kuwa katika nchi hii kuna uhuru wa Mahakama na uongozi unaoheshimu sheria!
Vinginevyo nakushukuru kwa barua na mawazo yako! Ubarikiwe!

BM

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.