ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 16, 2013

WANAOTUKANA KWENYE SIMU KUKIONA: TIGO YABORESHA HUDUMA ZAKE MWANZA

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Tawi la Tigo Mwanza lililopo barabara ya stesheni ambapo tawi hilo lilifungwa kwa muda kupisha ukarabati mkubwa kuendana na mahitaji ya huduma bora na za kisasa.


"Moja kati ya sababu za wawekezaji kukimbilia jijini Mwanza iwe ni shughuli za kibenki, mahoteli au shughuli za mawasiliano: kwanza kupitia sensa ya mwaka jana jiji la Mwanza ni la pili kuwa na idadi kubwa ya watu baada ya jiji la Dar es salaam, ni jiji la pili kuchangia pato la Taifa.

Na ukisema jiji la Mwanza unazungumzia wakulima, wafanyabiashara, wavuvi, wachimbaji madini na wasafirishaji, hivyo kwa mwekezaji yeyote akishawekeza Dar es salaam fikra zake humtuma kuja kuwekeza Mwanza ambako vilevile shughuli za kiuchumi zinaenda kwa kasi." alisema Konisaga. 


Sehemu ya wafanyakazi wa Tigo tawi la Mwanza wakifuatilia kinachojiri kwa umakini.


Wakuu wa idara mbalimbali Tigo wakifurahia yanayojiri.


Engo na engo....


"Tulifunga ofisi zetu takribani mwezi mmoja na nusu ili kufanya ukarabati kubadilisha muonekano na pia kuongeza huduma mbalimbali ambazo zitarahisisha shughuli za mawasiliano ya kila siku kwetu sote" Mwangaza Matotola ambaye ni Service Excellence manager wa Tigo 


Engagement wa kampuni ya Mawasiliano ya simu za mkononi Tigo akimkabidhi zawadi Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, kadi maalum ya 'Kipaumbele'.


Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga, naye alipata fursa ya kukabidhi wateja wa kwanza wa jiji la mwanza kupata kadi maalum ya 'Kipaumbele' na hapa alikuwa akimkabidhi bwana Alan Seif Said.






Jackson Jerry ambaye ni Engagement Specialist wa Tigo akiwa na zawadi ya smart phone ambayo ilikabidhiwa kwa rafiki mkubwa wa Tigo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.


Mkuu wa wilaya ya Nyanagana jijini Mwanza Baraka Konisaga akimkabidhi Jackson Kabeza zawadi ya smartphone kwa kuwa rafiki mkubwa mfuatiliaji wa Tigo kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.


Wananchi wa Kanda ya Ziwa wategemee kupata huduma bora za mawasiliano kutoka Tigo.


Ndani ya tawi hili mteja atapata fursa kuona na kujaribu bidhaa.


Mkuu wa wilaya akiendelea kukagua tawi la Tigo Mwanza.


Mazingira mapya ya ofisi ya Huduma kwa mteja na Tigo tawi la Mwanza.


Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga akizungumza na wadau wa Tigo juu ya kuridhishwa kwake na ubora wa mazingira ya ofisi za Tigo tawi la Mwanza, kulia ni Retail Operation Manager wa Tigo Charles Sardina. 


Wafanyakazi wa Tigo wakishea taarifa.


Picha ya pamoja Wafanyakazi wa Tigo Tawi la Mwanza na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Baraka Konisaga.
WANAOTUKANA KWENYE SIMU KUKIONA

WATU wanaotumia simu za mkononi kutoa lugha za matusi kwa kuongea au kuandika ujumbe mfupi dhidi watumiaji wengine watachukuliwa hatua za kisheria.

Onyo hilo lilitolewa leo na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Baraka Konisaga, alipozungumza kwenye ufunguzi wa tawi la ofisi ya Kampuni ya simu za mkononi ya Tigo.

Alisema kumekuwapo na baadhi ya watu wanaotumia vibaya teknolojia ya mawasiliano ya simu kwa kuwatukana wenzao, na bahati nzuri Serikali imehimiza na kufanikisha kwa asilimia kubwa zoezi la usajili wa laini za simu za wateja wa makampuni yote hivyo suala la utambuzi limerahisishwa ambapo hatua kali zitachukuliwa kwa watakao kiuka maadili.

Kwa mujibu wa DC Konisaga, Kampuni ya Tigo ina wajibu wa kuhakikisha inadhibiti hali hiyo kwa wateja wake, kwani kufanya hivyo italeta tija kwa wateja wa kampuni hiyo.

“Kwanza naupongeza sana uongozi wa Kampuni ya Tigo kwa kufungua ofisi hapa jijini Mwanza. Huu ni uwekezaji mzuri sana katika maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

“Lakini kuna baadhi ya watu wanatumia vibaya mawasiliano ya simu kwa kuwatukana wenzao. Serikali inataka Tigo idhibiti hali hii na wahusika wachukuliwe hatua,” alisema Konisaga.

Kwa upande wao, Meneja Huduma na Ubora wa Kampuni ya Tigo, Mwangaza Matotola, kutoka makao makuu, Jackson Jerry na Operesheni Meneja wa Tigo Mwanza, Charles Sardina, walisema wateja wa kampuni hiyo watanufaika na kadi maalumu za ‘Kipaumbele.’

“Kwa kutambua na kuthamini michango ya wateja wetu, Tigo tumeboresha huduma zetu maradufu, wateja wetu watanufaika na kadi za Kipaumbele, watapata huduma bure kwenye matawi yetu 33 nchi nzima,” alisema Jerry.

MKUTANO WA CHADEMA WA KUJADILI YA RASIMU YA KATIBA JINSI ULIVYOKUWA JIJINI MWANZA

Helikopta iliyowabeba viongozi wa CHADEMA ikiwa angani tayari kushuka kwaajili ya kuwahutubia maelfu ya wananchi waliofurika kwenye viwanja vya Magomeni kirumba jijini Mwanza kwa ajili ya mkutano wa hadhara wa kukujadili Rasimu ya Maoni ya Katiba. 

Mbunge wa Nyamagana Ezekiel Wenje akimtambulisha kijana ambaye anatajwa kuingizwa matatani akishinikizwa kukisaliti chama hicho kuwataja viongozi waandamizi wa chama hicho kuhusika katika mauaji mbalimbali na unyanyasaji nchini.

Chadema wameamua kuzunguka nchi nzima kwa lengo la kutoa elimu ya Katiba kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kutoa ufafanuzi wa maana ya Katiba na kujibu hoja za wananchi.

Wakishuka kuelekea jukwaani..

Mbunge wa Ubungo John Mnyika, alisema kuwa maadili ya uongozi na utawala bora, vinatikiswa kama siyo kuyumbishwa. Aliwataka wananchi kuhakikisha misingi ya taifa inarekebika kupitia marekebisho ya katiba mpya.
Mnyika alisema kuwa katika kupitisha maoni ya katiba, wanataka haki, uwazi na usawa katika masuala ya madini na rasilimali za nchi ambazo kimsingi zinapaswa kutajwa kwenye katiba. Tunataka Katiba pia impunguzie rais madaraka, alisema.
Alisema gharama za maisha ya wananchi zinazidi kupanda kila kukicha kutokana na rais kuwa na mlimbikano wa madaraka, hivyo kufanya maamuzi bila kutambua kuwa wananchi walio na kima cha chini ndio wanaoumia.
Aidha alisema kuwa anashangazwa na serikali ya CCM inavyokataa mfumo wa serikali tatu kwa madai kuwa,serikali tatu ni gharama kubwa sana kuendesha huku wakisahau baraza kubwa la mawaziri lisilo na meno.

Ni mikono kuonyesha idadi ya watu ambao hawajapata fursa ya kushiriki kuchangia mapendekezo ya rasimu ya katiba.

Red Brigade mkutanoni.

Mnyika alisema kuwa katika kuzungumzia Katiba hakuna vyama vya siasa, polisi wala mtu wa kada nyingine yoyote. Katiba ni mali ya Watanzania wote, hivyo kila mmoja ana wajibu wa kutoa maoni yake juu ya mambo anayoamini kuwa yatalisaidia taifa kama yataingizwa kwenye katiba.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema, kukusanya maoni ya wananchi kwa ajili ya kupata Katiba Mpya siyo kazi rahisi, ni kazi inayohitaji nia ya dhati ya taifa zima, kwa kuwa katiba ni mali ya wananchi na rasilimali za taifa.

Red brigade wakimzuia jamaa ambaye alikuwa akitaka kumfikia Mbowe huku akiwa na mabango yake wakihofia kuwa katumwa na watu wasiojulikana.

"Nataka nifike jukwaani..!!" Ilisikika sauti ya jamaa huyo.

Ilibidi nguvu zaidi iongezwe kutokana na jamaa huyo kung'ang'ania kufika jukwaani ili atimize azma yake.

Mbowe aliwasihi walinzi hao kumwachia, naye hatua kwa hatua akaelekea jukwaani akiwa amebeba mabango yake, mfukono akiwa amebeba vitu vizito.

Bango la Kwanza linamaanisha: 'Ona Chadema karibu mweshimiwa mkombozi wa haki zetu Mwanza, No Matata.'

Bango la pili lasema 'Hatumtaki Matata, Shashi No Matata...'

Mmenusurika Bukoba...!! Ndiyo ujumbe uliochomoza...

Acha wapigwe tu!! Ndiyo ujumbe uliochomoza...

Chadema imekuwa ikifanya mikutano ya hadharani nchini kuzungumzia mchakato wa katiba. Wamekuwa wakitoa elimu na kuwaeleza wananchi umuhimu wa kazi hiyo kwa taifa ambapo leo itakuwa ni zamu ya wakazi wa Mkoa wa Geita na wilaya zake.

MKAZI WA BUHEMBA ANASWA NA VIPANDE 10 VYA MENO YA TEMBO VYA THAMANI YA MILIONI 23.2 AKISAFIRISHA JIJINI MWANZA.

 MKAZI wa Kijiji cha Buhemba Wilaya ya Butiama Mkoani Mara Yohana Jackison (27) amekamatwa na Askari Polisi wa dolia akiwa na vipande 10 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya zaidi shilingi milioni 23.2 Jijini Mwanza.
Gunia lililokamatwa na nyaraka hizo za serikali (meno ya Tembo).

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Evarist Mangu jana alieleza kuwa mtuhumiwa huyo aliyekuwa akisafirisha meno ya tembo kutoka kijiji cha Buhemba kuja Jijini Mwanza alikamatwa na askari wa dolia katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Buzuruga majira ya saa 3:15 asubuhi kwenye kilichopo eneo la Nyakato baada ya kushitukiwa na askari hao.
Kamanda Mangu alisema kwamba baada ya kushuka kwenye basi dogo mali ya Kampuni ya JOHANVIA Express linalofanya safari zake kati ya Butiama na Mwanza akiwa ameficha vipande vya meno hayo ya Tembo kwenye gunia la mkaa ambapo baada ya kutelemka na kuonyesha wasiwasi ndipo askari hao waliamua kumsimamisha.
Vipande vya meno ya Tembo vikikaguliwa mara baada ya kutolewa kwenye gunia.


Yohana Jackison (27)

 “Baada ya kumsimamisha walimhoji kabla ya kuanza kumpekuwa na ndipo walipogundua kuwa katika gunia la mkaa kunavitu vingine na walipozidi kuumwaga mkaa walikuta kifurushi kikiwa kimefungwa ndani yake kukiwa na vipande 10 vya meno ya Tembo ikiwa ni Nyara za Serikali ” alisema Kamanda Mangu na kuongeza kuwa.
  
Gunia la mkaa ambamo kulikuwa na fuko la pembe za ndovu.

Mtuhumiwa Yohana Jackison (27) akivirejesha vipande vya ndovu kwenye fuko lake alilolificha ndani ya mkaa.


 Baada ya askari hao kuona vipande hivyo waliendelea kumshikilia na kumpeleka katika Kituo cha Polisi Kati ili kumhoji zaidi na kuwatafuta Maafisa wa wanyama pori wa Idara ya Maliasili ili kufanya utambuzi zaidi wa meno hayo ambapo ilithibitishwa  kuwa ni meno ya tembo.
  
 Kwa upande wake Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia ujangili Mikoa ya Kanda ya Ziwa Benjamin Kijika alisema kwamba vipande hivyo ni vya tembo wawili na ni meno manne ambavyo vilikatwa vipande vipande na kutoka 10 ili kumrahisishia katika ubebaji wake na tembo hao waliuwawa kwa Ujangili.
“Vitendo vya ujangiri ambavyo vimekuwa vikishika kasi ya kushamili kwenye maeneo mbalimbali ya Hifadhi za Mbuga za Wanyama Pori na maeneo tengefu hapa nchini kwa sasa vimepewa kipaumbele kwa kuwasaka wahalifu na majangiri na  watu ambao wamekuwa wakijihusisha na biashara ya meno ya tembo hapa nchini” alisema Kijika.
Kamanda Kijika amelipongeza Jeshi la Polisi maeneo yote ya Mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchini kwa kuweka kipaumbele kupambana na wahalifu wakiwemo majangili wa wanyama pori ambao ni rasilimali kubwa ya Taifa  na kuitendea haki nchi yetu na wanyama pori kwa kuendelea kukuza sekta ya utalii ambayo imekuwa ikituingizi mapato ya fedha za kigeni.
Kamanda huyo amewataka wananchi pia kuanza kuwafichua majangiri kwa kuwataja na kutoa taarifa za siri kwa wakuu wa polisi wa Wilaya na Mikoa yote ili kuwakamata kabla ya kufanya uhalifu wa kuuwa wanyama pori na hata kufanya ujambazi wa unyang’anyi wa kutumia silaha ili kudhibiti wimbi la vitendo vya uhalifu kwenye maeneo yao.

Thursday, August 15, 2013

ASILIMIA 80% YA WANANCHI MKOA WA MWANZA WANA MINYOO: MKUTANO WA KUHAMASISHA UGAWAJI DAWA ZA TIBA NA KINGA WABAINI

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akifunguwa Mkutano wa Semina elekezi kuhusu zoezi la ugawaji wa dawa tiba na kinga kwa magonjwa yaliyosahaulika kama minyoo ya tumbo,kichocho, trakoma, na usubi ambayo yamekuwa yakiathiri jamii na kuidhoofisha mkoani Mwanza. 

Dr. Upendo Mwingira.
ASILIMIA 80 ya wananchi wa mkoa wa Mwanza, wamebainika kuwa na ugonjwa wa Minyoo ya tumbo na kichocho, huku wilaya za Kwimba na Magu zikiongoza kwa ugonjwa wa Trakoma ukiwa ni utafiti wa mwaka 2004-2005 kutoka kwa Kituo cha Utafiti wa magonjwa ya Binadamu nchini (NIML)Jijini Mwanza.


Hayo yalibainishwa leo katika semina ya kuhamasisha viongozi wa mkoa, wilaya na Halmashauri za wilaya kuyapa kipaumbele Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele ili kufanikisha zoezi la ugawaji dawa za tiba na kinga  kwa jamii walio na magonjwa  aliyabainisha kuwa ni Minyoo ya tumbo, Trakona, Kichocho, ukoma, mabusha , tauni ,matende, usubi, homa ya dengi, homa ya ini na homa ya malale.

Akiwasilisha mada na kujibu maswali mbalimbali ya washiriki wa semina hiyo, Mratibu wa Mpango wa Taifa kudhibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele, Dr Upendo Mwingira ambapa alieleza kuwa kutokana na utafiti uliofanyika nchini mwaka 2004-2005 takwimu zinaonyesha Mkoa wa Mwanza wananchi wake kuathiliwa zaidi na ugonjwa wa miyoo. 
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo (kulia) na Katibu Tawala wa mkoa wakisikiliza kwa makini  wakati wa uwasilishwaji wa mada ya magaonjwa yaliyosahaulika.
Dr.Mwingira alisema kwamba semina hiyo imelenga kuwahamasisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugrnzi wa Halmashauri na Maafisa Elimu wa Wilaya kuweka kipaumbele kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa kuhakikisha wadau wote wanashirikishwa kwenye maeneo yao ili jamii iweze kushiriki kupata tiba na kinga za dawa hayo.


“Maeneo ya Kando ya Ziwa Victoria hususani Wilaya za Ilemela, Nyamagana, Ukerewe, Magu na Sengrema ni sehemu ambayo imetakiwa kuwekewa mkakati maalumu ili kuhakikisha magonjwa ya miyoo na kichocho yanadhibitiwa kwa kutolewa elimu na mafunzo, dawa za tiba na kinga”alisema .
Dr.Mwingira alisema kwamba zoezi la utowaji wa dawa litakuwa la siku mbili kuanzia Agosti 21 hadi 22 mwaka huu na kuwalenga watoto walio shuleni na nyumbani kuanzia umri wa miaka 5 kwa shule za awali na msingi ambao ndiyo huasiliwa zaidi ambapo kabla ya kumeza dawa hizo wanatakiwa kuwa wamekula na kushiba ili kuepuka kupata kizunguzungu na kuanguka hovyo.
Katibu Tawala wa mkoa Doroth Mwanyika (kulia) akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Masenza huku wadau wengine kama Mkurugenzi wa Wilaya ya Ilemela Zuberi Mbiana na wadau wengine wa elimu wakifurahia jambo.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Valentino Bangi akitoa ufafanuzi juu ya hali ya afya ya mkoa.

Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Merry Tesha (wa pili kutoka kushoto) akiteta na wataalamu wake.


Mkuu wa wilaya ya Kwimba Selemani Mzee (kulia) na wadau wa wilaya yake.
Wagonjwa wa Trakoma katika Wilaya za Magu na Kwimba wameombwa kujitokeza kwenda katika vituo vya afya na hospitali za Wilaya kwa lengo la kupatiwa tiba huku wale wa mabusha nao wakifanya hivyo na kupuuza na kuuondoa hofu ambayo imekuwa ikisambazwa na baadhi ya watu ambao hawana uwezo wa kitaalamu na kitabibu hasa wa vijijini na mitaani ili kupata tiba na kinga za magonjwa mbalimbali.
Mdau akichangia.

Wanahabari wakifuatilia yanayojiri.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akihutubia kusanyiko hilo.
Naye Mkuu wa mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo lisisitiza kwa wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Maafisa Elimu wa Wilaya kuhakikisha wanajiandaa kusimamia na kutekelezwa kwa zoezi hilo kwenye maeneo yote ya Mkoa wa Mwanza.

“Mkisimamia vyema na zoezi likaenda kama ilivyokusudiwa tutakuwa tutakuwa tumetekeleza kwa vitendo sera ya kupata misaada ambayo imekuwa ikitolewa na wafadhili mbalimbali kwa serikali na Mkoa wetu ili kuona jinsi gani tunavyothamini na waokuendelea kutusaidia tena kila wakati”alisema 

Nyuzi bin Nyuzi....

Injinia Ndikilo ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza kujitokeza kuwapeleka watoto wenye umri wa kuanzia miaka mitano walio majumbani kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali kwenye maeneo yao ili kupata huduma hiyo huku pia akiwataka viongozi wa madhehebu ya dini na vyama vya siasa wakiwemo wabunge kuwahamasisha wananchi kushiriki katika zoezi hilo na wale wanaoanza kujihisi kuwa na magonjwa hayo yaliyosahaulika.