Dr. Upendo Mwingira. |
ASILIMIA 80 ya wananchi wa mkoa wa Mwanza, wamebainika kuwa na ugonjwa wa Minyoo ya tumbo na kichocho, huku wilaya za Kwimba na Magu zikiongoza kwa ugonjwa wa Trakoma ukiwa ni utafiti wa mwaka 2004-2005 kutoka kwa Kituo cha Utafiti wa magonjwa ya Binadamu nchini (NIML)Jijini Mwanza.
Hayo yalibainishwa leo katika semina ya kuhamasisha viongozi wa mkoa, wilaya na Halmashauri za wilaya kuyapa kipaumbele Magonjwa yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele ili kufanikisha zoezi la ugawaji dawa za tiba na kinga kwa jamii walio na magonjwa aliyabainisha kuwa ni Minyoo ya tumbo, Trakona, Kichocho, ukoma, mabusha , tauni ,matende, usubi, homa ya dengi, homa ya ini na homa ya malale.
Akiwasilisha mada na
kujibu maswali mbalimbali ya washiriki wa semina hiyo, Mratibu wa Mpango wa Taifa
kudhibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele, Dr Upendo Mwingira ambapa alieleza
kuwa kutokana na utafiti uliofanyika nchini mwaka 2004-2005 takwimu zinaonyesha
Mkoa wa Mwanza wananchi wake kuathiliwa zaidi na ugonjwa wa miyoo.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo (kulia) na Katibu Tawala wa mkoa wakisikiliza kwa makini wakati wa uwasilishwaji wa mada ya magaonjwa yaliyosahaulika. |
Dr.Mwingira alisema
kwamba semina hiyo imelenga kuwahamasisha Wakuu wa Wilaya, Wakurugrnzi wa
Halmashauri na Maafisa Elimu wa Wilaya kuweka kipaumbele kuhakikisha zoezi hilo
linafanikiwa kwa kuhakikisha wadau wote wanashirikishwa kwenye maeneo yao ili
jamii iweze kushiriki kupata tiba na kinga za dawa hayo.
“Maeneo ya Kando ya Ziwa
Victoria hususani Wilaya za Ilemela, Nyamagana, Ukerewe, Magu na Sengrema ni
sehemu ambayo imetakiwa kuwekewa mkakati maalumu ili kuhakikisha magonjwa ya
miyoo na kichocho yanadhibitiwa kwa kutolewa elimu na mafunzo, dawa za tiba na
kinga”alisema .
Dr.Mwingira alisema
kwamba zoezi la utowaji wa dawa litakuwa la siku mbili kuanzia Agosti 21 hadi
22 mwaka huu na kuwalenga watoto walio shuleni na nyumbani kuanzia umri wa
miaka 5 kwa shule za awali na msingi ambao ndiyo huasiliwa zaidi ambapo kabla
ya kumeza dawa hizo wanatakiwa kuwa wamekula na kushiba ili kuepuka kupata
kizunguzungu na kuanguka hovyo.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Valentino Bangi akitoa ufafanuzi juu ya hali ya afya ya mkoa. |
Mkuu wa wilaya ya Ukerewe Merry Tesha (wa pili kutoka kushoto) akiteta na wataalamu wake. |
Mkuu wa wilaya ya Kwimba Selemani Mzee (kulia) na wadau wa wilaya yake. |
Wagonjwa wa Trakoma
katika Wilaya za Magu na Kwimba wameombwa kujitokeza kwenda katika vituo vya afya
na hospitali za Wilaya kwa lengo la kupatiwa tiba huku wale wa mabusha nao
wakifanya hivyo na kupuuza na kuuondoa hofu ambayo imekuwa ikisambazwa na
baadhi ya watu ambao hawana uwezo wa kitaalamu na kitabibu hasa wa vijijini na
mitaani ili kupata tiba na kinga za magonjwa mbalimbali.
Mdau akichangia. |
Wanahabari wakifuatilia yanayojiri. |
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo akihutubia kusanyiko hilo. |
Naye Mkuu wa mkoa wa
Mwanza Injinia Evarist Ndikilo lisisitiza kwa wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa
Halmashauri na Maafisa Elimu wa Wilaya kuhakikisha wanajiandaa kusimamia na
kutekelezwa kwa zoezi hilo kwenye maeneo yote ya Mkoa wa Mwanza.
Nyuzi bin Nyuzi.... |
Injinia Ndikilo ametoa
wito kwa wananchi wa Mkoa wa Mwanza kujitokeza kuwapeleka watoto wenye umri wa
kuanzia miaka mitano walio majumbani kwenye zahanati, vituo vya afya na
hospitali kwenye maeneo yao ili kupata huduma hiyo huku pia akiwataka viongozi
wa madhehebu ya dini na vyama vya siasa wakiwemo wabunge kuwahamasisha wananchi
kushiriki katika zoezi hilo na wale wanaoanza kujihisi kuwa na magonjwa hayo
yaliyosahaulika.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.