KITU CHA MAHINDI UTAMU ZAIDI KINASHUKA NA NDIMU, PILIPILI NA CHUMVI AKA NTUMVI (swaga za POWER BREAKFAST), NASKIA, ETI MGAMBO WA JIJI WAKIKUKAMATA, WANABEBA MAHINDI,MIHOGO, JIKO, MKAA KISHA WANATIMUA, ALAFU DK SIFURI WANAREJEA "TUMEKAMATA VYOTE CHUMVI HATUJAIONA, SI ULIKUWA NA CHUMVI WEYE! LETE NTUMVI!". LOOH!
KARIAKOO HAPA NI KAMVUA KADOGO TU!
TEGETA KIBAONI USPAPIMIE! PAONE HIVI HIVI, MISOSI YA MAHALA HAPA MITAMU KINOMANOMA!
MIKIKI HAPA NA PALE KARIAKOO.
KWA HILI LILILO KITHIRI SIKAI KIMYA. KIUKWELI HALMASHAURI YA JIJI SIDHANI KAMA WAKO DUNIANI.
Wednesday, June 09, 2010
BANGO
PICHANI RAIS JAKAYA KIKWETE AKIPIGA NGOMA ALIPOTEMBELEA ENEO LA MAKUMBUSHO YA KABILA LA WASUKUMA BUJORA NJE KIDOGO YA JIJI LA MWANZA. PEMBENI YAKE MWENYE JOHO NI PADRI SANDU NICASIUS AMBAYE NI KIONGOZI WA MAKUMBUSHO HAYO AKITOA MAELEZO.
HABARI KAMILI:-
ZOMEAZOMEA ya viongozi wa serikali imeendelea kuwakumba viongozi waandamizi, baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Mwanza, Wilson Kabwe, kuzomewa na wananchi mbele ya Rais Jakaya Kikwete.
Kabwe alikumbwa na mkasa huo baada ya Rais kumwita jukwaani na kumtaka atoe maelezo ya kina kuhusu kuwekewa alama za X kwenye baadhi ya nyumba za wananchi wa kata ya Mkolani jijini Mwanza.
Rais Kikwete ambaye yuko ziarani mkoani Mwanza, alitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkolani ambapo pia alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi huku akiwataka waeleze kero zao.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkolani A, Mathias Kihamba, alipewa nafasi na Rais Kikwete kueleza matatizo yanayowakabili ambapo mwenyekiti huo alisema kuwa wanaishi kwa wasiwasi katika nyumba zao kwa kuwa zimewekwa alama ya X pasi sababu za msingi.
Hata hivyo kinyume na matarajio ya wengi mkurugenzi huyo alishindwa kueleza sababu ya kuwekwa alama hizo za X zaidi ya kusema kuwa inawezekana kwa sababu watu wamejenga kiholela au ndani ya hifadhi ya barabara.
Rais Kikwete kusikia zomeazomea ikizidi kushika kasi, aliamua kumuokoa mkurugenzi huyo kwa kumtaka kulifanyia kazi haraka jambo hilo ili kupunguza malamiko ya wananchi.
Rais Kikwete yuko mkoani Mwanza kwa ziara ya siku mbili ambapo alikagua ujenzi wa barabara ya lami ya kutoka Usagara hadi Geita na kusema hakuna barabara itakayosimama kujengwa kwa sababu ya kukosa fedha . Leo Jumapili ametembelea makumbusho ya kabila la wasukuma na baadaye kufungua sherehe za Bulabo.