Saturday, February 18, 2023
MSD YAGAWA VYANDARUA KWA WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI
Na Oscar Assenga,Tanga
Mkoa wa Tanga umezindua zoezi la ugawaji vyandarua kwa wanafunzi wa shule ya msingi kuanzia darasa la kwanza hadi la saba kwa shule 1083.
"Usambazaji wa vyandarua hivi mashuleni utatekelezwa kwa siku 45 na utaendelea katika Halmashauri za Korogwe,Muheza,Mkinga,Pangani,
Pia RC Mgumba amewataka vingozi wa serikali,dini na jamii kwa ujumla kusimamia matumizi ya vyandarua kwa usahihi vitakavyogawiwa kwa wanafunzi wa shule za msingi,na jamii ielimishwe juu ya matumizi sahihi ya vyandarua.
Naye Meneja wa MSD Mkoa wa Tanga,Sitti Abdulrahaman ameitaja mikoa itakayofaidika na vyandarua hivyo kuwa ni Iringa,Dodoma,Tanga,Manyara pamoja na Kilimanjaro.
"Bohari ya Dawa MSD ina majukumu manne ambayo ni uzalishaji,ununuzi,utunzaji na usambazaji wa bidhaa Afya,kwenda kwenye vituo vya afya ya Umma na vile vya binafsi zilizoidhinishwa na Wizara ya Afya,na imepewa jukumu la kusambaza vyandarua 529,641 vyenye thamani ya Shilingi Billioni 2.9 kwenye shule zote za msingi 1083 katika mkoa wa Tanga" alisema Meneja wa MSD Sitti.
MLIMBWENDE MPYA WA MKOA WA PWANI KUSAKWA APRIL 28 MWAKA HUU.
Na Victor Masangu,Pwani
DC MOYO ATOA MSAADA WA CHAKULA KILO 400 KWA WAZEE WENYE ULEMAVU WA KUONA
Na Fredy Mgunda, Nachingwea
MKUU wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo ametoa msaada wa chakula kilo 400 kwa wazee wenye ulemavu wa kuona katika Kijiji cha Mwenge kata ya Mitumbati kutoka na kukabiliwa na uhaba wa chakula kwa wazee hao.
Akizungumza wakati wa kutoa msaada huo mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa ametoa msaada huo kufuatia ombi la wazee wenye ulemavu wa kuona kumuomba awasaidie chakula.
Alisema kuwa akiwa wananchi wa wilaya ya Nachingwea anapaswa kuchangia misaada pale inapowezekana hivyo aliguswa na wazee hao ndio maana akatafuta chakula hicho na kuwapelekea walemavu hao wa macho katika Kijiji cha Mwenge kata ya Mitumbati.
Moyo aliishukuru benki ya NMB kwa kuchangia msaada wa chakula kwa wazee wenye ulemavu wa kuona kwa kumuunga mkono Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo kusaidia chakula ambacho walikuwa na uhitaji nacho.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alimazia kwa kuwaomba wadau wengine kuwasaidia wazee wenye ulemavu wa kuona chakula na huduma nyingine kwa kila mtu ni mzee ajaye .
Kwa upande wao baadhi ya wazee wenye ulemavu wa kuona walimshukuru mkuu wa wilaya ya Nachingwea na benk ya NMB kwa msaada wa chakula kilo 400.
Friday, February 17, 2023
LIVE:- KUMBUKUMBU YA KUAGWA KWA MWANAMUZIKI KIERNAN "AKA" FORBES
MEMORIAL SERVICE OF THE LATE KIERNAN "AKA" FORBES
RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI MKUTANO MAALUM WA WAKUU WA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (EAC), ADDIS ABABA, ETHIOPIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika katika Jengo la Usalama na Amani la Julius Nyerere lililopo katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 17 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika katika Jengo la Usalama na Amani la Julius Nyerere lililopo katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 17 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika katika Jengo la Usalama na Amani la Julius Nyerere lililopo katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 17 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika katika Jengo la Usalama na Amani la Julius Nyerere lililopo katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 17 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika katika Jengo la Usalama na Amani la Julius Nyerere lililopo katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 17 Februari, 2023.
VIDEO MPYA YA MKALI KUTOKA NCHINI KENYA ALIYEMSHIRIKISHA HARMONIZE HII HAPA.
“BENKI NI SimBanking” KUONGEZA UTUMISHI WA HUDUMA ZA FEDHA, MOSHI
Wakazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro wameonekana kuipokea vyema promosheni ya “Benki ni SimBanking” ikiwa ni sehemu ya jitihada za Benki ya CRDB kuongeza ujumuishi wa Watanzania kwenye huduma za kibenki. Wakazi hao waliojitokeza kwa wingi katika uzinduzi wa promosheni hiyo mkoani Moshi walionyesha kufurahia huduma zinazopatikana katika huduma ya SimBanking ambazo kwa kiasi kikubwa zimeondoa ulazima wa mteja kutembelea matawi ya benki iwe kufungua akaunti au kufanya miamala.
Akizungumza na mamia ya wateja waliojitokeza katika uzinduzi wa promosheni hiyo, Kaimu Meneja wa Kanda ya Kaskazini wa Benki ya CRDB, Emmanuel Kafui ameeleza kuwa anatamani kuona huduma ya SimBanking inakua sehemu ya maisha ya kila siku ya wakazi wa Moshi wanapohitaji kufanya malipo, kutuma fedha pamoja na huduma nyingine za kifedha.
“Pamoja na kuwa na zawadi mbalimbali ambazo zitatolewa kwa watumiaji wazuri wa SimBanking katika kipindi cha promosheni ya Benki ni SimBanking, lengo letu kuu ni kufikisha huduma hii kwa kila Mtanzania jambo ambalo litakwenda kuongeza ujumuishi wa huduma za fedha na kuondoa utamaduni wa kufanya malipo kwa fedha taslimu” alisisitiza Kafui.
Takwimu za robo ya mwisho wa mwaka 2022 za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zinaonyesha kuwa kuna watumiaji wa simu zaidi ya Milioni 58 huku watumiaji wa intaneti wakiwa zaidi ya Milioni 31. Ikiwa idadi hii yote itaweza kufikiwa na huduma za benki kwa njia ya simu basi Tanzania itakua imepiga hatua kubwa katika ujumuishaji wa huduma za benki kwa wananchi wake.
Kwa upande wake Meneja wa Tawi la Benki ya CRDB Moshi, Pamela Mushi amesema kuwa zawadi zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 565 zitatolewa kwa wateja ambao watafungua akaunti kwa njia ta SimBanking na kufanya miamala mingi zaidi katika kipindi cha promosheni.
“Promosheni ya Benki ni SimBanking inakwenda kuwazawadia wateja wetu ambao ni watumiaji wazuri wa huduma ya SimBanking ambapo fedha taslimu zaidi ya Milioni 350, simu janja 200 sambamba na magari sita (Toyota Crown tano na Toyota Vanguard moja) yanakwenda kutolewa kwa wateja wetu" alisema Pamela.
Promosheni ya Benki ni SimBanking inakuja ikiwa ni kipindi kifupi kimepita baada ya Benki ya CRDB kutangaza taarifa ya fedha ya mwaka 2022 inayoonyesha kuongezeka kwa miamala ya kidigitali ambapo kwa mwaka 2022 zaidi ya asilimia 86% ya miamala ya wateja ilifanywa kwa njia za kidigitali hususan huduma ya SimBanking.
Meneja wa Tawi la Benki ya CRDB Moshi, Pamela Mushi akichukua alama za vidole katika zoezi la kuwafungulia wateja akaunti kupitia huduma ya SimBanking wakati wa promosheni ya kampeni ya 'Benki ni SimBanking' iliyofanyika leo Moshi, Kilimanjaro.
ULEGA: MSOMERA YAZIDI KUNG’ARA MIRADI YA WAFUGAJI YAPAA
Na. Edward Kondela
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) amesema anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo serikali inahakikisha kila sekta inafikiwa katika maendeleo wakiwemo wafugaji na wavuvi.
Naibu Waziri Ulega amebainisha hayo (16.12.2023) wakati alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja katika Kijiji cha Msomera kilichopo Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali inayowahusu wafugaji, yakiwemo mabwawa ya maji, minada ya mifugo, majosho na malambo ili kusogeza huduma karibu kwa wakazi wa kijiji hicho.
Amesema mbali na wafugaji ambao serikali imekuwa ikiwafikia kwa kuwapatia huduma mbalimbali za miundombinu kwa ajili ya shughuli za mifugo, wavuvi na wafugaji wa samaki pia wanafikiwa.
“Hakuna lililosimama yote yanasonga mbele makandarasi waendelee kushirikisha vyema wenyeji ambao wanajua mazingira ya hapa na wenyeji kushirikiana na makandarasi na wenyewe kuwashirikisha viongozi kila hatua.” Amesema Mhe. Ulega
Ameongeza kuwa anaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa imetenga fedha Shilingi kwa mwaka wa fedha 2022/23 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji kwa wafugaji, ikiwemo minada takriban Shilingi Bilioni 5.9 kwa ajili ya kujenga minada mipya na kukarabati ya zamani na Shilingi Bilioni 5.9 kwa ajili ya kutengeneza majosho.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Albert Msando akitoa taarifa ya wilaya kwenye kikao cha Kijiji cha Msomera ambacho Naibu Waziri Ulega alikuwa mgeni rasmi, amesema hadi sasa serikali imeshajenga majosho saba kwa ajili ya kuoshea mifugo, miradi kwa ajili ya malisho ya mifugo ambapo maandalizi yamekamilika yakiwemo ya upatikanaji wa mbegu.
Mhe. Msando ameongeza kuwa idadi ya mifugo iliyopo katika kijiji hicho ni mingi kuliko idadi ya wakazi wake ambapo inafikia zaidi ya 86,234 ikiwemo ng’ombe 28,049 mbuzi 32,743 kondoo 24,795 na punda 647.
Nao baadhi ya wanakijiji cha Msomera katika kikao hicho walipata fursa ya kutoa maoni na maswali kwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) ambapo moja ya maoni yao ni kuwepo kwa vikundi vinavyojumuisha wanakijiji hao ili wapatiwe mashamba darasa na ng’ombe wa maziwa ili wafuge kisasa, ambapo Naibu waziri Ulega ameielekeza Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB) kufika katika kijiji hicho na kutoa elimu juu ya mikopo kwa wafugaji hao ili waweze kufuga kwa tija na kibiashara kwa kuwa wana makazi ya kudumu.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) yuko Mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kujionea namna maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya sekta za mifugo na uvuvi.
MAELEKEZO YA DKT. SAMIA YAWAVUTIA VIJANA KUJIAJIRI KWENYE UFUGAJI
Na. Edward Kondela
Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeamua kukuza sekta ya mifugo kupitia unenepeshaji wa mifugo ili wananchi waweze kufuga kibiashara na kwa tija zaidi.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amebainisha hayo (15.02.2023) Mkoani Tanga, wakati alipotembelea vijana waliojiunga kwenye vituo atamizi vilivyopo Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI) na Wakala ya Vyuo vya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) ili kupata mafunzo ya vitendo ya ufugaji kibiashara na unenepeshaji bora wa mifugo.
Mhe. Ulega amefafanua kuwa kupitia dira na maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia, serikali imeonelea kuichangamsha Sekta ya Mifugo, kupitia unenepeshaji na ufugaji wenye tija hivyo wizara kuja na programu ya Samia Ufugaji kwa Tija (SAUTI).
“Tunataka kutengeneza matokeo chanya kwa vijana katika maendeleo yao Rais Dkt. Samia anataka vijana wachakarikaji, wenye kasi ya maendeleo.” Amesema Mhe. Ulega
Nao baadhi ya vijana ambao wanapata mafunzo hayo wamemwambia Naibu Waziri Ulega kuwa wamejiwekea mikakati ya kufanya ufugaji wenye tija mara wakapomaliza mafunzo yao ambayo yanadumu kwa mwaka mmoja.
Wamebainisha kuwa ni wakati wao saa kufikiria kujiajiri na hata kutoa mafunzo kwa wafugaji wengine wa asili ili wafuge kisasa na kuingia katika biashara ya unenepeshaji wa mifugo
Programu ya SAUTI ambayo imeanzishwa kutokana na maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyotoa wakati wa kuhitimisha sherehe za wakulima (Nanenane) Mwaka 2022, imelenga kuwabadilisha vijana kifikra kwa kuwapatia mbinu mbalimbali za ufugaji wa kisasa na kibiashara ikiwa ni pamoja na kuwaonyesha fursa zilizopo kupitia Sekta ya Mifugo.
Thursday, February 16, 2023
RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AWASILI JIJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA KWAAJILI YA KUHUDHURIA MKUTANO WA 36 WAKUU WA NCHI NA SERIKALI AU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) tarehe 16 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) tarehe 16 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) tarehe 16 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ngoma za asili za Taifa la Ethiopia mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) tarehe 16 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ngoma za asili za Taifa la Ethiopia mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) tarehe 16 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia ngoma za asili za Taifa la Ethiopia mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole Jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) tarehe 16 Februari, 2023.
RUBY: 'BADO NAWASILIANA NA EX WANGU' AFUNGUKA KUHUSU KUHARIBIWA SHOW.
Akizungumza kwa upole na utulivu tofauti na nyuma (mwezi February 2022) ambapo Ruby kwenye ukurasa wake wa Instagram, aliandika kwa ghadhabu na hasira juu ya mahusiano yake ya zamani na Kusah, This time ikiwa ni February 2023, Ruby anazungumza na mtangazaji wetu Suzuki 'Drum Drum', bila kuacha hata chembe ya swali.......
TETEMEKO KUBWA LA ARDHI LILILOTIKISA SYRIA NA UTURUKI WAHANDISI WA MAJENGO NCHINI WAMEJIPANGA VIPI?
NA ALBERT G. SENGO
Kupitia kipindi cha Mchakamchaka ndani ya Jembe Fm Mwanza ukiwa na watangazaji wako George Kimini pamoja naye Pascal Kadushi. - Ni wiki chache zilizopita dunia imeshuhudia tetemeko kubwa la ardhi likitikisa Syria na Uturuki na kuua maelfu ya watu, swali kuu hapa tulishuhudia nyumba na maghorofa makubwa yakianguka na kumomonyoka kama biskuti au kama yalijengwa kwa udongo. Watu wakithubutu kusema hayakujengwa kwa uimara kwa Tahiti zenu hili linaukweli kiasi gani? - Jeh mmeweka mikakati gani kunusuru majanga kama hayo yakipita hapa nchini yasijeacha madhara kama hayo ya wenzetu? Hasa ukizingatia Kanda ya ziwa hususani mkoa wa Mwanza kwa eneo kubwa umezungukwa na eneo kubwa la maji? Pamoja na hayo lekini Jeh........ - Majukumu ya ERB ( bodi ya usajili wa wahandisi) ni yapi hasa? - Hatua zipi mnazichukua kwa wahandisi wasiofata taratibu? - Usajili wa wahandisi una maana gani?WHO YAUNGANA NA WIZARA YA AFYA KUUNDA KAMATI ZA KUPAMBANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO KIBAHA.
Na Victor Masangu,Pwani
DKT. SAMIA AMWAGA MABILIONI KUINUA FURSA ZA UCHUMI WA BULUU.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), (wa nne kushoto) akiwa kwenye boti ya uvuvi iliyopewa jina la Mv. Blue Economy na kubainisha mambo kadhaa juu ya uwekezaji wa serikali kwenye Uchumi wa Buluu, mara baada ya kutembelea kikundi cha ushirika cha Mchukuuni kilichopo jijini Tanga ambacho kinajishughulisha na kilimo cha mwani na ufugaji tango bahari ama jina lingine la zamani jongoo bahari.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), (wa kwanza kushoto) akiwa kwenye kikundi cha ushirika cha unenepeshaji kaa kiitwacho Jifute kilichopo Wilaya ya Pangani, Mkoani Tanga kujionea namna wanavyojishughulisha na unenepeshaji wa kaa hao pamoja na vizimba vilivyojengwa mahsusi kwa ajili ya kufuga kaa 600 kwa wakati mmoja
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb), (aliyesimama) akiwa kwenye mazungumzo mara baada ya kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Omary Mgumba (aliyekaa), kabla ya Naibu Waziri Ulega kuanza ziara ya kikazi mkoani humo.
Na. Edward Kondela
Serikali imeendelea kutekeleza bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 katika uwekezaji wa uchumi wa buluu kupitia maji ya Bahari ya Hindi, maziwa na mito ikiwemo kuhamasisha ufugaji wa viumbe maji.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) amebainisha hayo (15.02.2023) wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Tanga ambapo katika siku ya kwanza ya ziara hiyo, kwenye Sekta ya Uvuvi ametembelea vikundi vya ushirika vya ukuzaji viumbe maji vya Jifute kinachonenepesha kaa pamoja na Mondura na Mchukuuni vinavyojishughulisha na ufugaji wa tango bahari ama kwa jina lingine la zamani jongoo bahari pamoja na ukulima wa mwani.
Ili kukuza uchumi wa buluu, Naibu Waziri Ulega amesema serikali imeweka Shilingi Bilioni 2.5 kwa ajili ya kuendeleza zao la mwani ambapo tayari Shilingi Milioni 447 zimeshatolewa kwa vikundi mbalimbali, Shilingi Bilioni 11.5 zimetengwa kwa ajili ya kutengeneza boti za kisasa za uvuvi na Shilingi Bilioni 20 kwa ajili ya ujenzi wa vizimba vya kufugia samaki aina ya sato kwenye Ziwa Victoria.
Mhe. Ulega amesema serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejizatiti kuinua uchumi wa buluu kwa kutenga fedha nyingi huku wadau mbalimbali wa sekta hiyo wakikaribishwa kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia kuweka mazingira mazuri ya ukuzaji viumbe maji.
Aidha, amewataka wadau wa Sekta ya Uvuvi hususan vikundi vya ushirika vya wavuvi kuchangamkia fursa ambayo serikali imetoa fedha ili kuongeza mahitaji ya ukuzaji viumbe maji kutokana na masoko yaliyopo ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe. Zainabu Abdallah amesema anafurahishwa na namna Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inavyoweka juhudi za kuwasaidia vijana katika uwekezaji kwenye viumbe maji kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kutaka uwekezaji wa kisasa kwa kuongeza mnyoyoro wa thamani, huku akibainisha kuwa wilaya yake iko tayari kutenga maeneo mengi zaidi kwa ajili ya shughuli za ukuzaji viumbe maji.
Akisoma risala ya kikundi cha ushirika cha kilimo cha mwani na ufugaji tango bahari cha Mchukuuni kilichopo jijini Tanga, Bw. Abdallah Mtondo amelalamikia kitendo cha baadhi ya watu ambao siyo waaminifu kuiba matango bahari katika mashamba yao hususan nyakati ambapo maji yamefunika mashamba hayo.
Kutokana na hali hiyo wameiomba serikali kuwachukulia hatua za kisheria watu hao ambao wamekuwa wakiwarudisha nyuma katika shughuli za ufugaji ili kujiongezea tija jambo ambalo Naibu Waziri Ulega amelitolea kauli kali na kutaka mamlaka husika kuingilia kati jambo hilo huku akisisitiza wanunuzi wa mwani na tango bahari kununua mazao hayo kwenye vikundi vinavyotambulika na kusajiliwa.
Awali kabla ya kuanza ziara ya kikazi Mkoani Tanga, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) amefika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Omary Mgumba na kufanya naye mazungumzo juu ya namna serikali kupitia wizara hiyo inavyofanya jitihda mbalimbali za kufungua fursa kwa wadau wa sekta za mifugo na uvuvi kwa kufuga na kuuza mazao yanayotoka katika sekta hizo.
Tuesday, February 14, 2023
AJINYONGA KISA KAACHWA KWENDA KUMZIKA BIBI YAKE
Picha ya Philimon Shukrani. |
Kijana Philimon Shukrani (19) mkazi wa mtaa wa Mnubi, Kata ya Kwangwa Manispaa ya Musoma mkoani Mara amekutwa amejinyonga ndani baada ya wazazi wake kuondoka na kwenda msibani Ukerewe huku chanzo cha kujinyonga kikisadikiwa kuwa ni kuachwa kwenda kumzika bibi yake wilayani Ukerewe.
MKE WA MWENYEKITI ABAKWA KISHA KUUAWA
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ashuhudia utiaji Saini Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9, Ikulu Jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9. Hafla ya utiaji saini Mikataba ya kuimarisha Gridi ya Taifa na usambazaji wa umeme Vijijini imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akishuhudia Mkurugenzi wa Shirika la Umeme nchini TANESCO Maharage Chande akiwa pamoja na Mwanasheria wa Shirika hilo Zaharani Kisilwa wakati wakitia saini Mikataba mbalimbali ya Gridi Imara na Wakandarasi mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Umeme Vijijini REA Eng. Hassan Saidy pamoja na Mwanasheria wa REA Mussa Muze wakati wakitia saini Mikataba ya kupeleka Umeme maeneo mbalimbali nchini kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023.
Wageni mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9 Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023.
Wageni mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9 Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023.
Wageni mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9 Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9, Ikulu Jijini Dar es Salaam.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
TOIO YAWATAKA VIJANA JIJINI TANGA KUCHANGAMKIA FURSA YA MAFUNZO YA UBUNIFU NA UJASIRIAMALI.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Ufundi Tanga (Tanga School) wakiendelea na ubunifu wa Incuber aambacho ni maalumu kwa ajili ya kutotoleshea mayai ya kuku kupitia katika mradi mafunzo ya ubunifu na ujasiriamali ambayo yanaendelea shuleni hapo kupitia Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) yenye Makazi yake Jijini Tanga na Dar chini ya fadhilwa na Shirika la Foundation Botnar ambao wamelenga kuhakikisha Vijana wanajifunza masuala mbalimbali ya ubunifu ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Na Oscar Assenga,TANGA