ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 14, 2023

MKE WA MWENYEKITI ABAKWA KISHA KUUAWA

 


Mke wa mwenyekiti wa mtaa wa National Housing kata Rwamishenye katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Khadija Ismail (29) amebakwa na kisha kuuawa kwa kupigwa kwa kitu butu kichwani na kijana aliyetambulika kwa jina la Paschal Kagwa (22) aliyekuwa akiishi naye.

Tukio hilo limetokea Februari 13/2023 majira ya jioni.

Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Sima amesema kuwa kijana anayetuhumiwa kumbaka mama huyo alikuwa akiishi nyumbani kwa mwenyekiti baada ya kupewa hifadhi. "Aliishi nao nyumba moja lakini sio ndugu yao alipewa hifadhi tu"

Chanzo - EATV

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.