ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 26, 2019

PING YAPANIA KUBORESHA UCHUMI WA MADEREVA WA VYOMBO VYA USAFIRI NCHINI SASA YATINGA RASMI MWANZA


Madereva wa Tax, Bodaboda na Bajaji toka mkoani Mwanza hii ni fursa yao tena kutumia vyombo vyao vya usafiri kupata kipato zaidi, ni kupitia kujiunga na mpango wa usafiri na usafirishaji wa PING. 

Pia wito umetolewa kwa madereva wanawake kuichangamkia fursa hiyo adimu iliyo salama kwa mmiliki wa chombo pamoja na abiria.
Mkurugenzi wa Ping Tanzania Nasoro Halfani Nasoro akizungumza na mamia ya madereva wa Tax, Bodaboda na Bajaji mkoani Mwanza katika mkutano wa uelimishaji ambao pia ulihusika kupokea changamoto za wadau hao wa usafiri.
Kwa umakini ndani ya kusanyiko.
Uelimishaji ukiendelea.
Meza kuu.
Mkurugenzi wa Ping Tanzania Nasoro Halfani Nasoro akifafanua jambo mbele ya mamia ya madereva wa Tax, Bodaboda na Bajaji mkoani Mwanza (pichani chini) katika mkutano wa uelimishaji ambao pa ulihusika kupokea changamoto za wadau hao wa usafiri.
Kwa umakini hatua kwa hatua.
Sehemu ya madereva wa Tax, Bodaboda na Bajaji mkoani Mwanza waliojitokeza katika mkutano wa uelimishaji ambao ulihusika kutoa elimu na kupokea changamoto za wadau hao wa usafiri.

HAFLA YA MAPOKEZI YA NDEGE MPYA BOEING 787-8 DREAMLINER YA AIR TANZANIA



RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AONGOZA WATANZANIA KATIKA MAPOKEZI YA NDEGE MPYA BOEING 787-8 DREAMLINER YA AIR TANZANIA (Karibu Nyumbani)

Friday, October 25, 2019

BREAKING NEWS:- MASHABIKI WA YANGA WAPATA AJALI SAFARINI KUELEKEA MWANZA


"Habari za saa hizi wana Yanga Kuna habari zinaenezwa kuwa majeruhi wamepelekwa Hospitali ya Tumbi, habari hizo sio za kweli, wagonjwa wamepatiwa huduma ya kwanza na Daktari tuliye naye  safarini na sasa tunaendelea na safari baada ya kampuni ya ile gari kutupatia gari nyingine, kwa hiyo tumeamua kuendelea na safari ili kutimiza lengo la kuisapoti timu yetu YANGA, kama kutakuwa na tatizo tutapeana taarifa tunawaomba mtuombee kwa Mwenyezi Mungu ili tufike salama" Han 's Kashata amepenyeza ujumbe 

RAIS Dkt. MAGUFULI NA MKEWE WATOA POLE KWA FAMILIA YA MMOJA WA WAASISI WA VYAMA VINGI NCHINI MAREHEMU JAMES MAPALALA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Mwanasiasa Mkongwe na mmoja wa Waasisi wa Mfumo wa Vyama vingi nchini Marehemu James Mapalala Osterbay jijini Dar es salaam aliyefariki dunia Oktoba 23,2019 katika Hospital ya Kairuki jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Bi. Hannah Mapalala Mke wa Marehemu James Mapalala alipokwenda na Mkewe Mama Janeth Magufuli kutoa pole nyumbani kwa Mwanasiasa Mkongwe na mmoja wa Waasisi wa Mfumo wa Vyama vingi nchini Osterbay jijini Dar es salaam aliyefariki dunia Oktoba 23,2019 katika Hospital ya Kairuki jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakisali Sala maalumu ya kumuombea pamoja na Familia ya Mwanasiasa Mkongwe na mmoja wa Waasisi wa Mfumo wa Vyama vingi nchini Marehemu James Mapalala walipokwenda kutoa pole nyumbani kwake Osterbay jijini Dar es salaam. Marehemu James Mapalala alifariki dunia Oktoba 23,2019 katika Hospital ya Kairuki jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia Benard James  Mapalala (Mtoto wa Marehemu James Mapalala) alipokwenda na Mkewe Mama Janeth Magufuli kutoa pole nyumbani kwa Mwanasiasa Mkongwe na mmoja wa Waasisi wa Mfumo wa Vyama vingi nchini Osterbay jijini Dar es salaam, aliyefariki dunia Oktoba 23,2019 katika Hospital ya Kairuki jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na waombolezaji wengine walipokwenda kutoa pole kwa familia ya Marehemu James Mapalala ambaye ni Mwanasiasa Mkongwe na mmoja wa Waasisi wa Mfumo wa Vyama vingi nchini, nyumbani kwake Osterbay jijini Dar es salaam aliyefariki dunia Oktoba 23,2019 katika Hospital ya Kairuki jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

YANGA WAMALIZA KUZINDIKA KIRUMBA


Kikosi cha Yanga leo kimefanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa CCM kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Pyramids Fc ambao utapigwa keshokutwa Jumapili katika uwanja huo

Wachezaji wote waliokambini mkoani Mwanza walishiriki mazoezi hayo ya mwisho akiwemo mshambuliaji Sadney Urikhob ambaye jana alishindwa kumaliza mazoezi kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mguu
 Wapinzani wao Pyramids Fc ambao tayari wametua leo jijini Mwanza, kesho watautumia uwanja huo kwa mara ya kwanza



SERIKALI YAAGIZA WALIOKIMBIA NA BILIONI 1.2/= ZA WAKULIMA MTWARA WAKAMATWE.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Stendi ya Mabasi wilayani Newala leo, ambapo ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata Viongozi wa Vyama Vya Msingi vya Ushirika ambao wametoroka na fedha za wakulima wa korosho wilayani hapo,Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Newala Aziza Mangosongo .Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Mkuu wa Wilaya ya Newala Aziza Mangosongo akizungumza katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Stendi ya Mabasi wilayani Newala leo, wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia).Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Mwananchi wa Newala,Shadrack Ntesi akimuuliza swali Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(hayupo pichani), wakati wa Mkutano wa Hadhara uliofanyika leo katika Stendi ya Mabasi wilayani hapo.Picha  na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni akisalimiana na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Newala baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi,Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo Aziza Mangosongo.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Na Mwandishi Wetu
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ameliagiza Jeshi la Polisi Mkoani Mtwara kuwakamata  Viongozi wa Vyama vya Msingi vya Ushirika wanaotuhumiwa kukimbia na  Kiasi cha Shilingi Bilioni 1.2/= za wakulima ambazo ni madeni ya Korosho.
Ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Newala  katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika Viwanja vya Stendi Kuu baada ya kupokea Ripoti ya Jumla ya Madeni wanayodai wakulima katika Wilaya za Mtwara, Masasi, Nanyumbu, Newala na Tandahimba.
Nilivyofika hapa Mtwara jambo la kwanza lilikuwa kumuuliza Kamanda wa Polisi wa hapa juu ya utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais alilolitoa siku za hivi karibuni alipokuwa ziara na kuagiza kukamatwa kwa viongozi wawili wa vyama vya msingi vya  ushirika  wanaodaiwa fedha za korosho na wakulima, ameniambia walitekeleza agizo na hao viongozi  wawili tayari wameanza kulipa hizo fedha,” amesema Masauni
Akizungumza baada ya kupokea ripoti ya madeni kwa Wilaya zote za Mkoa wa Mtwara Naibu Waziri Masauni amelitaka Jeshi la Polisi kuwakamata viongozi wengine katika wilaya zilizobakia za Mtwara, Newala, Masasi, Nanyumbu na Tandahimba ambazo katika taarifa ya jumla ya mkoa inaonyesha takribani Shilingi Bilioni 1.2 bado zinadaiwa na wakulima hao kutoka kwa viongozi wa vyama hivyo.
“Mheshimiwa Rais kwenye ziara yake aliishia wilaya ya Masasi lakini katika ripoti hapa inaonyesha katika wilaya zingine wakulima pia wanadai fedha zao ambacho ni kiasi kikubwa,nakuagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara kuwakamata viongozi wengine katika wilaya zilizobakia na hakikisha kiasi hicho cha fedha cha wakulima hao kinalipwa,” amesema Masauni
Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara,Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Blasius Chitanda inaonyesha jumla ya Vyama vya Ushirika 61 bado vinadaiwa na wakulima katika wilaya za Mtwara, Masasi, Tandahimba na Newala kuanzia Msimu wa Korosho wa Mwaka 2015/2016 hadi 2017/2018.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano huo baadhi ya wakulima wanaodai fedha zao waliiomba serikali kuhakikisha wanalipwa haki yao kwani madeni hayo yamechukua muda mrefu hali inayopelekea kuzorotesha shughuli zao za kuchumi huku familia zao zikipata taabu kutokana na fedha zao kutopatikana kwa wakati.

HATUPO SAWA NA UONGOZI WANGU ULIOPITA/NILITAKIWA KULIPA MILIONI 500 NIMEUZA MALI ZANGU ILI NIWALIPE.


#CloudsMedia ipo mubashara kutoka kwenye kipindi cha XXL ya Clouds Fm ikifanya exclusive interview na Konde Boy aka Harmonize, Watangazaji ni BDozen, Kenedy The Remedy, Adamu Mchomvu, Mamy Baby na Perfect Crispin

NAMNA SAHIHI ZA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA KIMAFANIKIO KATIKA MAISHA.


Nafahamu ya kuwa kila mmoja wetu anahitaji mafanikio makubwa sana kwa kile anchokifanya siku zote, ila tatizo  kuna baadhi  changamoto mbalimbali zinasomsonga na kufanya eidha kefeli kabisa kwa jambo anolifanya au kufanikiwa kwa asilimia chache tofauti na alizokuwa anategemea mwanzoni mwa kuanza jambo.

Kuna wakati mwingine tunajikuta tunakata tamaa baada ya kuona baadhi ya changamoto zinatokea na kuzuia mafanikio ambayo tumejipangia. Changamoto hizi zinaweza zikajitokeza katika biashara, elimu, kazi kwa mfano kufukuzwa kazi ambayo ulikuwa unaitegemea, kufiwa na mtu ambaye ulikuwa unamtegemea na changamoto zinginezo.

Pia kuna wakati mwingine changamoto zikitokea tulio wengi  hukataa tamaa na muda mwingine na kujiona  hutafai kuendelea kuishi ,pia wakati mwingine huwa hata tunakufuru kwa kusema baadhi ya maneno kama vile Mungu kampendelea na mengineyo mengi.

Lakini ndugu msomaji wa makala hii tukumbuke ya siku zote changamoto ni njia ya kufikia mafanikio tunayoyahitaji. Pia changamoto hutokea ili kupima imani yako je wewe ni mtu wa aina gani katika kakabilana na changamoto?

Zifutato ni baadhi ya njia ya jinsi ya kukabilaiana na changamoto.

Kubali changamoto zinajitokeza.
Kama nilivyoeleza hapo awali ya kwamba changamoto ni lazima zitokee katika safari yako ya mafanikio, hivyo basi hakikisha ya kwamba unakua ni mtu kwa kuzikubali  changamoto hizo na ujue ni jinsi gani unaweza kupambana nazo ili uweze kutimiza malengo yako, mfano huenda ukawa unafanya biashara mahali fulani ila mwanzoni mwa biashara yako wateja walikuwa wengi ila kwa sasa wamepungua jaribu kufanya taathimini juu hili uone ni sababu zipi zilizochangia kutokea kwa hili na siyokuwa  ni mtu wa kukataa taamaa maana hakuna dhambi kubwa kama kukaata tama.

Tafuta washauri
Nafahamu ya kuwa baadhi yetu huwa tuna watu wa karibu ambao huwa tunaweelezea shida zetu ili kupata ushauri. Mfano wa  watu wa karibu wanaweza kuwa ndugu, marafiki na watu wengine. Pia unaweza kuwatumia viongozi wa dini kwa jambo linalolokukatiza kwani ni watu ambao ni washauri wazuri kwa  jambo linalokukatiza  na kukuzuia kukamilisha malengo yako.

Pia katika utautizi wa changamoto watu wengi huwa tunakosea sana. Huwa tunaangalia effect (madhara) ya jambo fulani kutokea badala ya kualia causes (sababu) ya jambo Fulani kutokea. Huenda ukawa hujanielewa ngoja nikupe mfano ufutao; katika baadhi ya maeneo hapa nchini kuna ugonjwa wa mlipuko ambao umetokea unaitwa kipundupindu lakini katika utatutizi juu ya ugonjwa huu watu huenda kuatibu madhara (effects) sawa ni jambo nzuri lakini ni vyema kuanza kuangalia ni nini chanzo (causes) cha ugonjwa huu kutokea ndipo tuje tuangalie madhara (effect).

Ukifuata kanunu hii ya kuangalia chanzo yaani (causes)  harafu uje kuangalia effect (madhara) itasaidia kupunguza changamoto zingine zinazokutatiza katika kufanikisha malengo yako.

Mwisho naomba nimalize kwa kusema ”usizibe ufa kabla ya kujua chanzo cha ufa kutokea’’

Na. Benson Chonya

BAINA YA CHUO KIKUU CHA IRINGA NA WANANCHI SABA WA KATA YA KIHESA

 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akifurahia jambo na bi Mwaija Ngaga mara baada ya kufanikiwa kumaliza mgogoro wako
 Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye meza moja na walalamikiwa pamoja na walalamika wakati wa kutatua mgogoro
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kutatua mgogoro

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amefanikiwa kutatua mgogoro wa ardhi baina ya wananchi saba dhidi ya chuo kikuu cha Iringa uliodumu toka mwaka 1992

Akizungumza kwenye ofisi za mkuu wa chuo hicho,Kasesela alisema kuwa amefanikiwa kuutatua mgogoro huo kutokana na kuzikutanisha pande mbili ambazo zilikuwa zinagombana kuhusu ardhi ya chuo hicho ilipochukuliwa mwaka 1992.

“Huu mgogoro ni wa miaka mingi na mimi nimeukuta hivyo leo nimefanikiwa kuumaliza kwa njia ya busara kabisa kitu ambacho pale zilizokuwa zinalalamika zimefikia muafaka” alisema Kasesela

Aidha Kasesela alisema kuwa wamefanikiwa kumaliza mgogoro kwa kuwatafutia kila mmoja kiwanja kimoja ili kufidia maeneo ambayo serikaliilikipatia chuo kikuu cha Iringa.

“Nimewaagiza uongozi wa chuo kuwa ikifika siku ya jumatatu waje ofisini kwangu ili wawalipe nauli zao hawa wananchi kwa kuwa wanawajibu kwa mujibu wa makubaliano yetu ambayo tulikuwa tumefikia kwenye kikao hiki” alisema Kasesela

“Kwa leo nimefalijika kuona familia hii imeamua kumaliza mgogoro huu ambao ulikuwa hauna afya katika harakati za kuleta maendeleo kwa wananchi hawa kwa kuwa walikuwa wanapoteza muda mwingi kupigania mgogoro huu” alisema Kasesela
Kwa upande wa waliokuwa wanalalamika wakiwakilishwa Mwaija Ngaga pamoja na Zuhura Balama walisema kuwa wamelidhishwa na maamuzi yaliyofikiwa na kumpongeza mkuu wa wilaya ya Iringa kwa kumaliza mgogoro huo.

“Kwa kweli mkuu wa wilaya tunaomba ufikishe salamu zetu kwa Rais kwa kuchagua viongozi kama nyie wenye maono ya kushughulikia kero za wananchi maana la sivyo tulipanga kwenda Dodoma kumuona Rais” walisema wazee hao

RC ALLY HAPI ATOA SIKU SABA UJENZI WA SOKO LA MLANDEGE KUKAMILIKA

 Mkuu wa Mkoa wa Iringa  Ally Hapi akiongea na waandishi wa habari wa mkoa Iringa juu ya hatma ya soko kuu la Mlandege lililopo katika manispaa ya Iringa.
 Mkuu wa Mkoa wa Iringa  Ally Hapi akimsikiliza kwa makini mkandarasi wa soko la kisasa la Mlandege Manispaa ya Iringa
 Moja ya eneo la soko kuu la kisasa la Mlandege lilopo Manispaa ya Iringa

NA FREDY MGUNDA,IRINGA.

Mkuu wa Mkoa wa Iringa  Ally salumu hapi amefanya ziara ya kutembelea eneo la ujenzi wa soko kuu na la kisasa mlandege mjini Iringa na kuagiza kasi ya ujenzi iongezwe na mkandarasi wa Home Africa Constractions Engineering Ltd anayejenga soko hilo ili hadi kufikia October 31 mwaka huu liwe limekamilika tayari kwa matumizi ya wafanyabiashara.

Katika Ziara hiyo ya Mkuu wa Mkoa na kamati ya ulinzi na usalama ya kutembelea na kukagua ujenzi wa soko jipya unaoendelea hivi sasa mjini Iringa Hapi alionesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi huo huku akitoa agizo la kuhakikisha linakamilika mwishoni mwa mwezi huu Mwaka Huu.

“Ndani ya tarehe 31 mwezi huu kumi taa zote,umaliziaji vitu vyote ya soko hili  viwe vimekamilika,nataka ifikapo mwezi wa 11 tarehe 1 tayari muwe tayari kukabidhi mradi  huu wa kisasa kwa halmashauri   ili iweke utaratibu wa  mzuri wa matumizi   kwa hiyo nawapa siku saba tuu soko hili  liwe imekamirika”alisema hapi.

Aidha Hapi alisema kuwa mradi huo unagharimu shilingi bilioni 3.7 huku akimtaka   mkurugenzi wa halmashauri  ya manispaa ya Iringa  na wataalamu kuhakikisha wanaweka mpangilio mzuri wa watu kupata vibanda na maduka  kwa halali bila manung’uniko na waliokutwa mwanzo ndio wapewe kipaumbele.

Alisema mkoa wa Iringa hauna duka kubwa la kisasa la kuuza bidhaa ,hivyo halmashauri iangalie katika soko hilo eneo wanaloweza kuweka kwajili ya uwekezaji wa duka kubwa litakalokuwa linatoa bidhaa zenye ubora ili kuongeza pato la hamashauri.

“Naomba nitumie fursa hii kuwapongeza sana mkuu wa wilaya ya Iringa Richard kasesela,mkurugenzi na mkandarasi kwa kazi kubwa mliyoifanya kuhakikisha soko hili linakamili hivi karibuni” alisema Hapi 

Simon s. bahegwa ni mkandarasi wa kampuni ya home Africa constractions alimesema kuwa thamani ya mradi ilikuwa shilingi bilioni 3.72 na ifikapo tarehe 31 october watakuwa wamekamilisha kama alivyoagiza mkuu wa mkoa.

“ mheshimiwa kufikia  tarehe 31 mwezi huu tutakuwa tumekamilisha mradi huu kwa asilimia 100 kwa tukimaanisha kufunga taa ,na thamani ya mradi huu ilikuwa ni shilingi bilioni 3.72 na fedha iliyotumika mpaka sasa ni bilioni 2.6 tunategemea kukabidhi mradi  huu mwishoni mwa mwezi huu”alisema bahegwa

Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya iringa HAMID NJOVU alisema kuwa soko hilo la Mlandege linaukubwa wa Squermeter 3182 ambapo wanatarajia likianza kutumika litakuwa likiingiza mapato ya shilingi million 55 mpaka milioni 80 kwa mwezi.

Mradi wa ujenzi wa soko jipya la Mlandege Manispaa ya Iringa  unagharimu taklibani shilingi bilioni 3.7 kwa fedha za serikali unaotarajiwa kuwa na jumla ya  wafanyabiashara 2000 .

Thursday, October 24, 2019

MAREHEMU LAZIMA AZUNGUSHWE MJINI SIKU MBILI KATIKA UREFU USIOPUNGUA KILOMITA 20 ILI AUAGE MJI.


Duniani kumejaa dini na madhehebu yaliyo na imani na desturi mbali mbali ambazo waanzilishi na wafuasi huzifuata ili kuzitosheleza imani zao. Lofty Matambo anatupa tarifa ya mazishi ya ajabu ya dhehebu la Jerusalem church lake Mary Akutsa ambapo wanaamini marehemu lazima azungushwe mjini siku mbili katika urefu usiopungua kilo mita ishirini ili auage mji ndiposa aende peponi kwa amani.

Wednesday, October 23, 2019

BREAKING NEWS: Rais Magufuli afanya uteuzi muda huu


Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Cleopa David Msuya (Waziri Mkuu Mstaafu) kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU).

RAIS MAGUFULIA AKUTANA NA VIONGOZI WA TAASISI YA MASHAURIANO YA KISHERIA KWA NCHI ZA ASIA NA AFRIKA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 23 Oktoba, 2019 amekutana na viongozi wa Taasisi ya Mashauriano ya Kisheria kwa Nchi za Asia na Afrika (AALCO) ambao wanahudhuria mkutano wa 58 unaofanyika hapa nchini kwa siku 5 ukiwakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 49 na mashirika mbalimbali.

Viongozi wa AALCO waliokutana na Mhe. Rais Magufuli ni Rais wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Waziri wa Sheria na Katiba, Tanzania), Makamu wa Rais wa AALCO aliyechaguliwa katika mkutano huu Prof. Mohamad Shalaldeh (Waziri wa Sheria wa Palestina), Katibu Mkuu wa AALCO Prof. Kennedy Gastorn (Tanzania) na Naibu Makatibu Wakuu wa AALCO watatu ambao ni Bw. Yukihiro Takeya (Japan), Bi. Wang Liyu (China) na Dr. Ali Garshasbi (Iran).

Mhe. Rais Magufuli amewashukuru na kuwakaribisha wajumbe wa AALCO nchini Tanzania na amewahakikishia kuwa Serikali inatambua kazi inayofanywa na taasisi hiyo tangu ijiunge nayo mwaka 1965 na kuwa mwanachama kamili kuanzia mwaka 1973.

Mhe. Rais Magufuli amesisitiza umuhimu wa AALCO kutekeleza malengo ya taasisi hiyo kama alivyoelezwa na viongozi hao, na ametoa wito wa kuendelea kuzitetea nchi wanachama hasa zinazowekewa vikwazo mbalimbali.

Ametolea mfano wa Zimbabwe ambayo imewekewa vikwazo kwa miaka mingi hali inayosababisha wananchi wa Zimbabwe kuteseka.

Rais wa AALCO Mhe. Balozi Mahiga na Katibu Mkuu Mhe. Prof. Kennedy Gastorn wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa kupata fursa ya kukutana nae na wameahidi kuwa AALCO itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa maslahi ya Asia na Afrika.

Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba Mhe. Amon Mpanju.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Ndg. Guo Yezhou, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Ndg. Yezhou kwa kutembelea hapa nchini kwa mara ya pili na pia ameishukuru China kwa kuendeleza ushirikiano na uhusiano mzuri na Tanzania ikiwemo mchango mkubwa wa chama cha CPC ambacho kinajenga Chuo cha Uongozi cha Mwalimu Julius Nyerere katika Wilaya ya Kiba

WAZIRI MKUU AMWAKILISHA RAIS MAGUFULI MKUTANO WA UCHUMI KATI YA URUSI NA AFRIKA.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnagangwa na   Rais wa Uganda,  Yoweri Museveni  (kulia) wakimsikilza  Rais wa Urusi, Vladimir Putin  wakati alipohutubia katika  Mkutano  wa uchumi  kati ya  Afrika na Urusi  (Russia -Africa  Economic Forum) kwenye Kituo cha Olympic Park, Sochi nchini Urusi, Oktoba 23, 2019








Rais wa Urusi, Vladimir Putin akihutubia katika Mkutano  wa uchumi  kati ya  Afrika na Urusi (Russia -Africa Economic Forum) kwenye Kituo cha Olympic Park, Sochi nchini Urusi, Oktoba 23, 2019













Mahakama yataka uthibitisho wa maendeleo ya afya ya Tundu Lissu



Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imewataka wadhamini wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwenda na uthibitisho wa maendeleo ya afya yake kesi hiyo itakapotajwa tena Mahakamani hapo

Hayo yameelezwa leo baada ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba kuuliza maendeleo ya Lissu na Mdhamini wake, Robert Katula kudai kuwa Lissu bado anaumwa

Baada ya maelezo ya mdhamini, Wakili wa Serikali, Estazia Wilson alieleza kuwa shauri hilo lilikuja kwa ajili ya kusikilizwa, hawawezi kuendelea na watamsubiri Lissu hadi afya yake itakapoimarika

Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 21, 2019. Lissu na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na sheria ya Magazeti ya mwaka 2002

Tuesday, October 22, 2019

VIDEO:- YANGA YARANDA MBAO KIRUMBA.



YANGA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyeji, Mbao FC 1-0 Uwanja wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Shukrani kwa bao pekee la mshambuliaji kutoka Namibia, Sadney Urikhob Khoetge dakika ya 57 akimalizia krosi ya kiungo, Balama Mapinduzi ‘Kipenseli’ kutoka upande wa kushoto.


Kwa ushindi huo wa pili mfululizo kwenye Ligi Kuu baada ya kuichapa na Coastal Union ya Tanga 1-0 pia kwenye mechi iliyopita, Yanga SC inafikisha pointi saba katika mchezo wa nne, nyingine mbili wakifungwa 1-0 na Ruvu Shooting na kutoa sare ya 3-3 na Polisi Tanzania, zote Dar es Salaam.


Refa Meshack Suda wa Singida aliyesaidiwa na Athumani Rajab na Soud Hussein wote wa Kigoma alikataa bao la kila timu kipindi cha kwanza kutokana na wafungaji wote kukwamisha mpira nyavuni wakiwa wamezidi.

Alianza Yusssuf Athumani wa Mbao FC kuukwamisha mpira nyuma ya kipa Mkenya Faroukh Shikalo dakika ya 37, kabla ya mshambuliaji David Molinga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), naye kutia mpira nyavuni dakika ya 41. 


Lakini kipindi cha pili mambo yakaenda vizuri kwa Yanga SC wakifanikiwa kupata bao bao lao pekee la ushindi.


Yanga inarejea kambini kuendelea na maandalizi ya mchezo wake wa kwanza wa mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pryramids FC ya Misri utakaofanyika Jumapili wiki hii hapo hapo Kirumba.


Kikosi cha Mbao FC kilikuwa; Abdallah Makangana, Datius Peter, Emanuel Charles, Abdulrahman Said, Babilas Chitembe, Chilo Mkama/ Kauswa Benard dk65, Mussa Haji Gabi, Rajab Rashid, Said Junior, Yusssuf Athumani/ Jordan John dk42 na Adili Sultan/ Wazir Junior dk63.


Yanga SC; Farouk Shikhalo, Juma Abdul, Ali Mtoni, Ali Hamad Ali, Kelvin Yondan, Feisal Salum/ Abdulaziz Makame dk77, Mapinduzi Balama, Papy Kabamba Tshishimbi, David Molinga/ Juma Balinya dk77, Sadney Urikhob na Mrisho Ngassa/Patrick Sibomana dk85.

WAATHIRIWA WA MAFURIKO UGANDA WAILAUMU SERIKALI KWA KUCHELEWESHA MIDAADA.



Waathiriwa wa mafuriko Uganda wailaumu serikali kwa kuchelewesha misaada


Raia walioathiriwa na janga la mafuriko mashariki mwa Uganda wameilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kuchelewa kupeleka misaada katika maeneo hayo ambapo mamia ya familia zimebaki bila makazi.
Ripoti mbalimbali kutoka nchini Uganda zinasema kuwa, waathiriwa wengi wa mafuriko hayo yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha wameomba  hifadhi kwenye shule na makanisa.
Wakizungumza na duru za habari, baadhi ya waathiriwa mafuriko hayo wamesema kuwa, hawajapokea msaada wowote kutoka serikalini tangu Ijumaa iliyopita licha ya serikali kufahamu hali hayo na mazingira magumu wanayokabiliwa nayo.
Taarifa zaidi zinasema kuwa, baadhi ya waathiriwa wamechukuliwa na ndugu zao kwa ajili ya kuwapa hifadhi huku wengine wakibaki hawana makazi, chakua wala mavazi.
Tunaiomba serikali itufikishie misaada haraka kwani hali yetu ni mbaya mno, amesema mmoja wa waathiriwa wa mafuriko hayo alipozungumza na vyombo vya habari.

Serikali ya Rais Museveni inalaumiwa kwa kuwatelekeza waathiriwa wa mafuriko

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika Ukanda wa Afrika Mashariki zimekuwa na maafa makubwa pia katika nchi jirani ya Tanzania.
Ripoti zinasema kuwa, idadi ya watu waliofariki dunia kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini Tanzania imepindukia 30 huku baadhi ya maeneo yakiharibiwa vibaya na mafuriko.
Serikali ya Tanzania imewaonya na kuwataka wananchi wanaoishi katika maeneo ya mabonde kuhama maeneo hayo hasa wakati huu ambapo nchi inashuhudia mvua kali ili kuepuka maafa zaidi.

MAELFU YA WATU WAMEKUWA WAKIMBIZI NCHINI NIGER KUTOKANA NA MAFURIKO.

Maelfu ya watu wamekuwa wakimbizi nchini Niger kutokana na mafuriko

Mafuriko yaliyoyaathiri maeneo ya kusini mashariki mwa Niger tangu mwanzoni mwa mwezi Oktoba hadi sasa yamesaabisha watu elfu 23 kukosa makazi.
Ukame wa mwaka jana ulioikumba Niger na mafuriko yaliyoyaathiri maeneo ya kusini mashariki mwa nchi hiyo umezidisha mgogoro wa kibinadamu katika nchi hiyo ambayo mara kwa mara imekuwa ikilengwa na mashambulizi ya magaidi wa Boko Haram. 


Magaidi wa Boko Haram 
Ripoti ya mwezi Septemba mwaka huu ya vyombo vya habari vya serikali ya Niger inaeleza kuwa, kuongezeka kiwango cha maji ambacho hakijawahi kushuhudiwa nchini humo katika kipindi cha miaka 50 iliyopita kumesababisha maafa makubwa katika mji mkuu Niamey. Watu 57 wameaga dunia katika mafuriko hayo. Nigeri inapatikana magharibi mwa Afrika huku asilimia 80 ardhi ya nchi hiyo ikiwa ni jangwa. Niger ilipata rasmi uhuru wake mwaka 1960 kutoka kwa mkoloni Ufaransa. 

WAZAZI WANAWASHINIKIZA WATOTO WA KIKE KUWEKA VIJITI VYA UZAZI?


Suala la ukosefu wa maadili na malezi bora kwa watoto limetajwa kuathiri mienendo ya  wanafunzi katika Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza ambapo inaelezwa kwamba baadhi ya wazazi baada ya kushindwa kuwadhibiti watoto wao sasa wanalazimika kuwapa mbinu za kushiriki ngono bila kupata mimba.

Hayo yalielezwa na Mkurugenzi wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally kufuatia midahalo mbalimbali ya kutoa elimu kwa jamii ili kupinga aina zote za ukatili wa kijinsia wilayani humo nayo jamii ikifunguka kile kinachoendelea.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango mkakati wa kitaifa wa kupambana na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) uliozinduliwa na Halmashauri ya Wilaya Misungwi kwa kushirikiana na Shirika la KIVULINI katika Kata ya Koromije, Oktoba 16, 201 na baadae kuendelea katika Kata zingine.

WAFANYAKAZI WA UMMA WAANZISHA MGOMO ZIMBABWE.


Kuongezeka kwa hali mbaya ya kiuchumi nchini Zimbabwe kumepelekea mamia kwa maelfu ya wafanyakazi wa umma kuanzisha mgomo.

Baraza ka Apex linalojumuisha mashirikisho yote ya wafanyakazi wa umma lenye wanachama wapatao laki 3 limetoa taarifa kwa wanahabari kwamba kutokana na kutolipwa mishahara yao na ongezeko kubwa la mfumuko wa bei maafisa wa serikali wameanzisha mgomo.

Taarifa hiyo ilisema pia kwamba kumekuwepo viwango tofauti katika uongezaji wa mishahara huku katika maeneo mengi pamoja na nyongeza ya mishahara, kwa kiasi kikubwa mishahara hiyo inakuwa imepungua.

Walimu wanaofanya kazi vijijini nchini Zimbabwe walianzisha mgomo kutokana na kulipwa mishahara kidogo.

Ni karibu mwezi 1.5 hivi sasa madaktari wa nchi hio wamegoma.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la kimataifa la fedha (IMF), mfumuko wa bei katika nchi hio kwa mwaka ni karibu asilimia 300.

Katika taarifa ya shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulika na kilimo na chakula, watu milioni 5.5 nchini humo wanahitaji msaada wa chakula.

RWANDA YAPIGA MARUFUKU VYOMBO VYA PLASTIKI VINAVYOTUMIWA MARA MOJA.

Wizara ya mazingira ya Rwanda imetangaza kupiga marufuku vyombo vya plastiki  ambavyo vinatumiwa mara moja na kurejelezwa.

Ni miaka  10 tangu serikali ya Rwanda kupiga marufuku  katika ukanda wa Afrika Mashariki matumizi ya mifuko ya plastiki kwa lengo la kulinda mazingira.

Wizara ya mazingira chini ya uongozi wa waziri Vincent Biruta imetangaza sheria mpya ambayo inapiga marufuku  matumizi ya  vyombo na bidhaa za plastiki ambazo hutumiwa mara moja na kurejelezwa.

Waziri wa mazingira wa Rwanda amenukuliwa na vyombo vya habari nchini Rwanda  akitoa muda wa miezi  mitatu  kwa wafanya  biashara wa bidhaa za plastiki kuwa wawe wamekwishasitisha  biashara hiyo.

Sheria hiyo ina lenga bidaa za plastiki kama  vikombe,  masahani, mirija ya vinywaji na bidhaa nyingine ambazo ni za plastiki.

Adhabu kweli itatolewa kwa mtu yeyote atakaekwenda kinyume na sheria.

Monday, October 21, 2019

AKINABABA NA FEDHA ZA MASHARTI KISA CHA KUWATESA WENGI


Jinsi ya kiume imetajwa kuwa ni moja kati ya watendaji wakubwa wa vitendo vingi vya ukatili dhidi ya Mwanamke na Mtoto katika jamii ambavyo vimekuwa vikiathiri malezi ya watoto na ustawi wa familia.

Hayo yameainishwa na wazazi pamoja na wanafunzi katika mdahalo wa kutoa elimu kwa jamii kupinga aina zote za ukatili wa kijinsia wilayani Misungwi mkoani Mwanza kufuatia swali la majadiliano liliulizwa kwa wanafunzi na aliyekuwa mwendesha mada Mkurugenzi wa Shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la KIVULINI Yassin Ally  kwamba "Kama ikitokea Mungu akakupa nafasi uchague nani abaki duniani kati ya mama au baba utapenda nani abaki?" Nayo majibu mengi yakaelekea kumtetea mama.

Hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa awamu ya pili ya mpango mkakati wa kitaifa wa kupambana na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWWA) uliozinduliwa na Halmashauri ya Wilaya Misungwi kwa kushirikiana na Shirika la KIVULINI katika Kata ya Koromije, Oktoba 16, 201 na baadae kuendelea katika Kata zingine.

PICHA: NDEGE MPYA AIR TANZANIA IKIWA KATIKA HATUA ZA MWISHO KUAMILIKA.


Ndege Mpya Kabisa ya Air Tanzania aina ya Boeing787-8 Dreamliner ikiwa katika hatua zake za mwisho kukamilika kabla ya kuwasili nchini hivi karibuni.