Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akifurahia jambo na bi Mwaija Ngaga mara baada ya kufanikiwa kumaliza mgogoro wako
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa kwenye meza moja na walalamikiwa pamoja na walalamika wakati wa kutatua mgogoro
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kutatua mgogoro
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela amefanikiwa kutatua mgogoro
wa ardhi baina ya wananchi saba dhidi ya chuo kikuu cha Iringa uliodumu toka
mwaka 1992
Akizungumza kwenye ofisi za mkuu wa chuo hicho,Kasesela alisema kuwa amefanikiwa
kuutatua mgogoro huo kutokana na kuzikutanisha pande mbili ambazo zilikuwa
zinagombana kuhusu ardhi ya chuo hicho ilipochukuliwa mwaka 1992.
“Huu mgogoro ni wa miaka mingi na mimi nimeukuta hivyo leo
nimefanikiwa kuumaliza kwa njia ya busara kabisa kitu ambacho pale zilizokuwa
zinalalamika zimefikia muafaka” alisema Kasesela
Aidha Kasesela alisema kuwa wamefanikiwa kumaliza mgogoro kwa
kuwatafutia kila mmoja kiwanja kimoja ili kufidia maeneo ambayo
serikaliilikipatia chuo kikuu cha Iringa.
“Nimewaagiza uongozi wa chuo kuwa ikifika siku ya jumatatu waje
ofisini kwangu ili wawalipe nauli zao hawa wananchi kwa kuwa wanawajibu kwa
mujibu wa makubaliano yetu ambayo tulikuwa tumefikia kwenye kikao hiki” alisema
Kasesela
“Kwa leo nimefalijika kuona familia hii imeamua kumaliza mgogoro huu
ambao ulikuwa hauna afya katika harakati za kuleta maendeleo kwa wananchi hawa
kwa kuwa walikuwa wanapoteza muda mwingi kupigania mgogoro huu” alisema
Kasesela
Kwa upande wa waliokuwa wanalalamika wakiwakilishwa Mwaija Ngaga pamoja
na Zuhura Balama walisema kuwa wamelidhishwa na maamuzi yaliyofikiwa na kumpongeza
mkuu wa wilaya ya Iringa kwa kumaliza mgogoro huo.
“Kwa kweli mkuu wa wilaya tunaomba ufikishe salamu zetu kwa Rais kwa
kuchagua viongozi kama nyie wenye maono ya kushughulikia kero za wananchi maana
la sivyo tulipanga kwenda Dodoma kumuona Rais” walisema wazee hao
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.