ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 25, 2017

H BABA ASHUHUDIA JEMBE MEDIA GROUP IKIICHANACHANA SAHARA MEDIA GROUP 5-2 NDANI YA DIMBA JIPYA LA NYAMAGANA.Wachezaji wa Jembe Media Group wakimwagia maji mfungaji wa goli la nne na la tano Mbaba Vc mara baada ya ushindi wa kishindo goli 5-2 dhidi ya Sahara Media Group mchezo uliochezwa dimba la Nyamagana jijini Mwanza.

Michezo siku zote imekuwa sehemu ya kuunganisha watu mbali mbali hasa wale watu ambao wanaonekana kuwa na ushindani wa kikazi, kibiashara au kazi nyingine,Michezo imekuwa ikitumika kuwa chanzo cha kusogeza ukaribu baina ya vyombo hivi.
Kikosi Cha Jembe Media Group.
Kikosi cha Sahara Media Group.
 Katika zama hizi kutoka Jijini la miamba .....Mwanza ni wazi kila mtu anafahamu mapinduzi makubwa katika tasnia ya Habari ambayo yamekuja baada ya radio Jembe Fm chini ya Mkuu wake Dr. Sebastian Ndege kutia maguu katika uwekezaji eneo hilo, Pia ni wazi kila mtu anafahamu ukongwe wa Chombo cha Habari cha Sahara Media Group ambayo inamiliki Radio Free, Kiss Fm, Star Tv na vyombo vingine chini ya mtaalamu Dkt. Anthony Diallo.

Vijana wakali wasio na maneno saaaana zaidi ya vitendo Dr. Ndege wamefanya yao.
 
Leo katika uwanja wa Nyamagana uwanja ambao umewekewa Nyasi Bandia na kukamilika hivi karibuni, leo umeweka moto ambapo Jembe Media Group ilikuwa ikicheza dhidi ya Sahara Media Group ambapo mpaka dakika Tisini za mchezo zinakamilika Jembe Media Group ikaibuka na ushindi wa Magoli (5 -2).
Juma Ayo alikuwa wa kwanza kufungua lango la magoli kwa Jembe Media Group ikiwa ni dakika ya 18 tu ya mchezo.
Kasi ya mchezo wa leo ilinogeshwa na team kapten wa Jembe Medi Group Juma Ayo ambeye alikuwa akilinyanyasa mwa-mwi lango la Sahara Media Group ya Jijini Mwanza.
Sahara Media hapa walikuwa wameweka kambi katika lango la Jembe Media kiasi cha kusababisha upatikanaji wa goli la pili wakiiacha Jembe Media waliokuwa nyuma muda huo kwa tofauti ya goli 1-2
Si kwa service hizi mchezaji lazima upone....Mshambuuliaji machachari wa Jembe Media Group Juma Ayo akipata usaidizi chini ya team ya huduma ya kwanza Jembe Family.
Kama mtu anabazidEi hivi...........
Pasha pasha ....kutoka kulia Dj Scorpion, Mbaba Vc na Chomo.


Emma The Gooner (L) na Sisco (R)
Pasha pasha......
Chini ya kocha wa Wakata Umeme.Mfungaji wa goli la 4 na la 5 Mbaba Vc akiwa juu ya mikono ya wana-Jembe Media Group mara baada ya kuibuka washindi.

HureeeeeeEeeeee......!!

Kocha wa Sahara Media akifanya mazungumzo na wandishi wa habari mara baada ya mchezo.

Kocha mchezaji wa Jembe Media Group Albert G. Sengo akitoa tathimini ya mchezo dhidi ya Sahara Media Group, baada ya ushindi wa 5-2.

Ilikuwa ahadi hatimaye imekuwa ukweli mmoja kati ya wasanii nembo ya mkoa wa Mwanza HBaba (katikati mwenye ndevu style) amesafiri toka makazi yake ya sasa jijini Dar es salaam hadi Rock City kwaajili ya ku-show love kwa kipute hiki.
Chriss The Dj on the ball.
Mapemaaa........
Hatariiiiii..
Mpaka kieleweke.
Mshambuliaji wa Sahara Media Group akimtoka beki wa Jembe Media Ramadhani (aliyelala chini)
Halo halo.....
Benchi la timu ya Sahara Media Group likiongozwa na Kocha Abdalah Tilata.
Mchezo ni undugu kocha wa Sahara, Abdalah Tilata (L) na Kocha wa Jembe, Albert G. Sengo
Kila Kitu balaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!
 

CHINBEES KUKISANUKISHA HII JUMAMOSI 25 MARCH JEMBE BEACH RESORT MWANZA.

 LEO NDIYO LEO #amshaaaa 
Mwanza Mko tayari,!!!

Baada ya kuibamiza bila huruma SAHARA Media 5-2 CLUB JEMBE Na WANENE ENTERTAINMENT wanakuangushia bonge la bata LEO jumamosi ya tarehe 25/3/2017, ambapo atadondoka mkali wa chorus anae trend na Goma lake la PEPETA @chinbees akidondoka na team nzima ya @waneneentertainment kuamsha popo kwenye #PEPETA NIGHT hii si yakukosa KIINGILIO NI BUKU 5 tu mlangoni.

 ENEO la tukio ni ndani ya jembe beach resort, kuanzia saa kumi na mbili jioni #twasemaaaaa amshaaaaa @mbabavc@johnjackson_jj@dj_mike_beats ENEO la tukio ni #JembeBeachResort CC:- @jembenijembe

 Mahojiano ndani ya kipindi cha Hit Zone jana kulia ni mtangazaji Babajuti na Natty E (pale kati) na kushito ni ChinBees toka Arusha.
 ChinBees kwenye mic ndani ya Jembe Fm Mwanza.
 Mzigo wa Leo.
 We inaDe area.
 The Crew ya ChinBees akiwa na WANENE ENTERTEINMENT.
 Kuelekea eneo la stage na mambo ya sound check.
Si vibaya kureluX.

MAGAZETI YA LEO:- 'ONYO KALI' SASA MAGUFULI AGEUKIA VYOMBO VYA HABARI, RPC KINONDONI AKANA KUZUIA MKUTANO WAKE, MWANDISHI WA HABARI KITENGE ALIVYO MUOKOA NAPE

Magufuli asisitiza uzalendo kwanza, atoa onyo kali, Mwigulu Nape si jambazi,nyundo 5 za JPM mtego wa vigogo,pata dondoo za magazeti hapa.

UN YAANZISHA KAMPENI MPYA YA KUTOKOMEZA POLIO AFRIKA.


Kampeni hiyo ambayo itafanywa kwa wakati mmoja na wahudumu wa kujitolea 190,000 kwa kutembea kwa miguu, baiskeli na njia zingine zozote, ni katika harakati za kuutokomeza kabisa ugonjwa huo katika nchi zilizobakiwa na waathirika wa ugonjwa huo ambao WHO inasema bado ni tishio kubwa kwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano.
Mashirika hayo yamesema mapigano katika jimbo la Borno nchini Nigeria yalisababisha watoto wanne kupooza mwaka 2016 kutokana na ukosefu wa chanjo, eneo pekee ambalo kirusi cha Polio bado kinatishia maisha, na iwapo hakitashughulikiwa haraka, eneo hilo na maeneo yaliyo jirani yatakuwa hatarini kuambukizwa. Jimbo la Borno ni ngome ya kundi la kigaidi la magaidi wakufurishaji wa Boko Haram.

Mtoto aliyepooza kutokana na polio
Ili kufanikisha kampeni hiyo, mashirika hayo yamesema ushirikiano wa serikali kuu hadi za mashinani unahitajika ili kuweza kumfikia kila mtoto.
Nchi hizo 13 ni Benin, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, Chad, Côte d'Ivoire, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Guinea, Liberia, Mali, Mauritania, Niger, Nigeria na Sierra Leone.

CHADEMA KUTUMIA BUNGE KUFAFANUA HALI YA SIASA NCHINI.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara, John Mnyika

Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kitautumia Mkutano wa Saba wa Bunge la Bajeti utakaoanza Aprili 4 kufafanua hali ya kisiasa ilivyo nchini.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alisema jana kuwa chama chake ndicho kinachoongoza kambi rasmi ya upinzani bungeni na kitautumia mhimili huo kuikosoa Serikali.

“Haki inapovunjwa mahali popote pale, hata inapovunjwa juu ya mwanaCCM na juu ya raia yoyote wa Tanzania hatusiti kutoa kauli ya kukemea na kutaka hatua kuchukuliwa, ”alisema Mnyika.

Alisema katika Bunge lijalo, wabunge wa upinzani na wa CCM watakuwa kitu kimoja katika kuchukua hatua hivyo Watanzania watarajie Bunge litakalokuwa limechangamka.

Alisema kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilichofanyika  Machi 22 na 23 kilijadili hali ya kisiasa na vyombo vya habari nchini.

“Matukio yaliyojitokeza hivi karibuni yanagusa uhuru wa vyombo vya habari, jambo kubwa linaloonekana bayana ni matumizi mabaya ya wazi ya madaraka yanayofanywa na baadhi ya viongozi,” alisema

Alisema katika siku za karibuni kumekuwa na matumizi mabaya ya silaha. “Tunalaani kwa kiwango kikubwa sana matumizi mabaya ya madaraka na matumizi mabaya ya vyombo vya dola hasa yanapofanyika hadharani.”

Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Kibamba, alimpa pole mbunge wa Mtama Nape Nauye kwa tukio la juzi la mtu anayedaiwa kuwa ni askari kanzu kumtolea bastola hadharani. Alisema upinzani umekuwa ukikilalamika kuhusu matumizi mabaya ya silaha na kuonekana unapiga kelele, lakini sasa kila mmoja anaona hali ilivyo na inamgusa.

Friday, March 24, 2017

WASOMI WAZUNGUMZIA UTEUZI MAOFISA WA TRA.


Rais John Magufuli akimuapisha Alphayo Kidata kuwa Katibu Mkuu Ikulu wakati wa hafla ya kuwaapisha mawaziri na mabalozi jijini Dar es Salaam, jana.

Dar es Salaam. Baadhi ya wasomi wamezungumzia uteuzi wa aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu kwamba kunaonyesha kuwa Rais John Magufuli anaitumia taasisi hiyo kama kipimo cha watu anaowaamini kuwapa dhamana kubwa zaidi.

Kidata alikuwa mteule wa pili kuongoza TRA, tangu Rais Magufuli alipoingia madarakani mwishoni mwa mwaka 2015.

Novemba 27, 2015, Rais Magufuli alimsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade baada ya kuibuliwa kwa upotevu wa makontena 349 yenye thamani ya Sh80 bilioni katika bandari ya Dar es Salaam pasipo TRA kuwa na kumbukumbu zozote.

Katika mabadiliko hayo, Rais alimteua Dk Philip Mpango kukaimu nafasi hiyo, lakini hakukaa muda mrefu kwani Desemba 23, 2015, alimteua Dk Mpango kuwa mbunge na kisha Waziri wa Fedha na Mipango.

Wiki moja baada ya uteuzi huo wa Dk Mpango, Desemba 30, 2015 Rais Magufuli alimteua Eliakimu Maswi, kuwa Kaimu Naibu Kamishna wa TRA lakini naye hakukaa muda mrefu na Januari 2016, alirejeshwa mkoani Manyara kuendelea na kazi yake ya katibu tawala wa mkoa. Kuhusu Maswi, Rais alifafanua kuwa amekamilisha kazi aliyokwenda kuifanya katika taasisi hiyo.

Kutokana na uteuzi wa Maswi, Rais Magufuli alimteua Kidata kuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA ambaye baadaye alithibitishwa na kuwa Kamishna Mkuu. Kabla ya uteuzi huo, Kidata alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Akizungumzia mabadiliko hayo, Profesa wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Humphrey Moshi alisema haoni athari za kuyumba kwa TRA kutokana na mabadiliko hayo.

"NAPE KARIBU UPINZANI" HIZI NI KAULI ZA WADAU.

WADAU KUTOKA JUKWAA LA MABADILIKO NA KAULI ZAO.
Nape Moses Nnahuye,  mtoto wa Brigedia Moses Nnahuye.
Umelinda heshima ya baba yako mwanamapinduzi, umeonyesha damu ya mjali utu, naam kizazi cha haki, kikao cha hekima. Busara si mlima lakini pia siyo mtelemko.
Jina lako halitafutika katika nchi takatifu Tanzania. Kama kwa baba na mwana.
Cheo ni nini?
Hofu ni nini?
Aibu ni kitu gani?
Naam umetenda kiutu, umeonysha ujemedari. Wewe ni mjenga nchi, popote ulipo, kwanafasi yoyote, kwa jina lolote.
Zile siku na zije, majemedari wamekuja na wapo tayari.

Nawaende washibao kwa dhuruma, ghiliba, choyo, ubinafsi, visasi, ukatili, tamaa mbaya, fitina, huzushi na laghai.

Kila mwenye mapenzi mema, aonaye sasa na hata halfajiri atasimama na wewe.
Asubuhi njoo, umande wa kesha utaondoka..........
Lucas Haule.


Nape hongera.
Heri kufukuzwa uwaziri kuliko  kukanyaga sheria na Katiba ya Tanzania,
Mungu wetu aliye juu yetu wote hatakuacha. 
Kumbuka umewekwa pembeni  kutokana na kusimamia heshima ya serikali.
Umetunguliwa uwaziri kutokana na kupigania haki, utu na heshima ya  Watanzania.
Kazi yako imekujengea heshima ya  pekee mbele ya wanahabari na Watanzania   
Umekuwa  Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo wa kupigiwa mfano katika zama hizi.
Ananilea Nkya

LIVE: Hafla ya Kuapishwa kwa Mawaziri Wapya, Dk Mwakyembe na Kabudi

Rais Magufuli, leo anawaapisha mawaziri wawili aliowateua siku chache zilizopita. Rais Magufuli amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri na kumteua waziri mpya wa habari na michezo. Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Harrison George Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Nape Moses Nnauye ndiye aliyekuwa anashikilia wadhifa huo.

Aidha, Dkt Magufuli amemteua Prof Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.


Mawaziri hao wanaapishwa Ikulu ya Magogoni, jijini Dar es Salaam
Bw Nauye amevuliwa majukumu yake siku moja baada yake kupokea ripoti ya kamati ya uchunguzi kuhusu uvamizi uliotekelezwa na mtu anayedaiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika studio za kituo cha habari cha kibinafsi cha Clouds mwishoni mwa wiki.

SHEIN AMTUMIA SALAMU MAALIM SEIF.

RAIS WA ZANZIBAR, DK. ALI MOHAMMED SHEIN.

RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, amesema hakuna mabadiliko yoyote yatakayotokea Zanzibar kama inavyoelezwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad.

Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu jana kuadhimisha mwaka mmoja wa uongozi wake wa muhula wa pili, alisema mabadiliko hayawezi kutokea bila kufanyika kwa uchaguzi au mapinduzi.

Alisema ni vyema Maalim Seif awaeleze wananchi na wafuasi wake mabadiliko hayo yatakuja kwa njia gani wakati uchaguzi umeshafanyika na yeye ndiye aliyechaguliwa na wananchi na kushinda kwa asilimia 91.4 katika uchaguzi wa marudio wa Machi 20, 2016, baada ya uchaguzi wa Oktoba 25, 2015 kufutwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

“Kama Maalim Seif anasema mabadiliko yanakuja, mimi siwezi kumzuia kusema hivyo mwache aseme maana mdomo ni nyumba ya maneno, lakini mimi nasema mabadiliko hayaji ng’oo, mimi ndiye rais wa Zanzibar hadi mwaka 2020, baada ya tume ya uchaguzi kutangaza uchaguzi mwingine,” alisema Dk. Shein.

Alisema hakuna njia ya kupata serikali kama sio kufanyika uchaguzi au kufanyika kwa mapinduzi, hivyo anayesema atapewa serikali bila uchaguzi na kushinda ni kujidanganya.

“Mwenye ubavu wa kiniondoa madarakani mimi nasema aje kuniondoa, hivyo wanaosema huko waache waseme ilimradi hawavunji sheria wala kuibugudhi serikali kupita kiasi.”

Dk. Shein alihoji kuwa huyo anayedai kuwa atapewa serikali atapewa na nani na kwa njia ipi na nani ambaye atamuapisha na kusisitiza kuwa maneno yanayosemwa hayamkoseshi usingizi kwani urais amepewa na wananchi kwa kupigiwa kura.

Aidha, Dk. Shein alisema katika awamu yake ya kwanza ya uongozi ambayo aliongoza serikali ya umoja wa kitaifa akishirikiana na CUF, hakukuwa na mivutano mikubwa kati yake na mawaziri kutoka CUF pamoja na Maalim Seif ambaye alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais, ingawa ziliibuka tofauti wakati serikali hiyo ikimaliza muda wake.

Alisema tofauti hizo zilianza Mawaziri na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CUF walipotoka nje ya vikao vya baraza hilo wakati baraza likijadili bajeti ya serikali ya 2015/2016, kutokana na wajumbe wa CUF kutokubaliana na hoja.

“Hapo ndipo tulipoanza kuvutana, lakini mwanzoni mwa muhula wangu wa kwanza wa uongozi tulikuwa tukienda vizuri, tukizungumza, tukicheka na kufurahi na hata tulikuwa tukikaa pamoja kula chakula cha mchana,” alisema Dk. Shein.

Thursday, March 23, 2017

NILIIKUTA CCM IKO SHIMONI NIKAITOA HUKO, VIJANA SIMAMIENI HAKI YENU - NAPE.


NAPE Nnauye amezungumza na Waandishi wa habari akiwa juu ya gari lake leo maeneo ya St. Peter Osterbay Dar es salaam ikiwa ni saa chache kabla ya taarifa kutoka IKULU kutangaza kwamba nafasi yake ya Waziri wa Habari amepewa Dr. Mwakyembe, hii ni Sentensi hapa chini ya jinsi ilivyokua.

"Nataka aliyeinua bastola hapa aje aseme ameiinua kwa sababu gani" - Nape Nnauye
"Nia ya mkutano wangu haikuwa mbaya. Nilitaka kuzungumza na waandishi wa habari lakini Polisi wanakuja kunizuia."- Nape  
ZAIDI BOFYA PLAY KUSIKILIZA

 "We have nothing to fear, but fear itself."- Nape
"Mnajua ni kiasi gani nimepigana kuirudisha CCM madarakani? Miezi 28 nimelala porini leo mtu anakuja kunitolea bastola. Jana nilisema kuwa kuna gharama za kulipa wakati unatetea haki za watu. Na nilisema kuwa nipo tayari kuilipa gharama hiyo. Sina kinyongo na serikali wala chama changu. Sikumuuliza Rais siku aliniteua na sitamlaumu kwa kuamua kuniondoa."- Nape

"Niliikuta CCM iko shimoni nikaitoa huko. Uzalendo wangu ndani wa CCM si wa kutiliwa shaka. Kina Kawawa walikuwepo wakapita, sisi tutapita, lakini tujiulize tutawaachia watoto wetu Tanzania ya namna gani?"- Nape

"Namshukuru Rais kwa mwaka mmoja alioniamini. Nampongeza kaka yangu Dkt Mwakyembe. Nawaomba mumuunge mkono Waziri Mwakyembe. Nawaomba mtulie maisha yaendelee. Nape ni mdogo sana kuliko nchi. Kuna mambo mazuri mbele hivyo tuiunge mkono serikali."- Nape

"Vijana naomba msimamie haki yenu"- Mbunge Nape Nnauye
"Mimi niliwahi kufukuzwa CCM kwa kusimamia nilichokiamini. Ili mbegu iote na kuchanua, sharti ioze kwanza."- Nape

"Namshukuru Rais kwa mwaka mmoja alioniamini. Nampongeza kaka yangu Dkt Mwakyembe. Nawaomba mumuunge mkono Waziri Mwakyembe. Nawaomba mtulie maisha yaendelee. Nape ni mdogo sana kuliko nchi. Kuna mambo mazuri mbele hivyo tuiunge mkono serikali."- Nape

"Nilitamani sana kuendelea kufanya kazi na ninyi waandishi wa habari lakini muda wa aliyeniweka umefika akaamua niondoke."-Nape

"Mimi niliwahi kufukuzwa CCM kwa kusimamia nilichokiamini. Ili mbegu iote na kuchanua, sharti ioze kwanza."- Nape

KAULI YA TFF BAADA YA MWAKYEMBE KUPEWA UWAZIRI WA MICHEZO.


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limempongeza Mheshimiwa Dk. Harrison Mwakyembe kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Katika taarifa iliyotolewa leo kwa wana habari, imesema kuwa shirikisho hilo linaamini chini ya uongozi wake mahiri Tanzania itapiga hatua kubwa zaidi katika maendeleo ya michezo.

Naye Rais wa TFF, Jamal Malinzi kupitia mtandao wa twitter amesema "TFF inampongenza Dkt. Harrison Mwakyembe kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo.Tunakuombea mafanikio makubwa.Amina."

KIPINDUPINDU CHATISHIA MAISHA YA WATU ZAMBIA, SHULE ZAFUNGWA KWA KUHOFIA MAAMBUKIZI.


MSEMAJI wa Wizara ya Afya ya Zambia amesema kuwa maafisa wa wizara hiyo wamewataka wananchi kutilia maanani usafi na taratibu za kinga ili kuzuia maambukizi zaidi ya ugonjwa wa kipindupindu. Ameongeza kuwa, watu walisiopungua 70 wameambikizwa ugonjwa huo na kwamba kuna uwezekano ukaenea zaidi katika maeneo mengine.

Wakati huo huo serikali ya Zambia imetangaza kwamba imefunga shule kadhaa na vituo vya uvuvi katika mkoa Luapula ili kuzuia maambukizi ya kipindupindu.

Waziri wa Afya wa Zambia, Chitalu Chilufya amesema kufungwa kwa shule hizo ni sehemu ya hatua za kudhibiti mlipuko wa kipindupindu katika mkoa wa Luapula ambapo makumi ya kesi za ugonjwa huo zimeripotiwa katika wiki nne za hivi karibuni.
Usafi ni muhimu kwa ajili ya kupambana na kipindupindu.

Hali duni ya usafi na mazingira machafu vinatajwa kuwa sababu ya mlipuko wa kipindupindu katika maeneo yenye watu wengi nchini Zambia.
 
Ripoti iliyotolewa jana na UNICEF kwa mnasaba wa Siku ya Maji Duniani imeonyesha kuwa, watoto zaidi ya 800 wanapoteza maisha kila siku katika sehemu tofauti za dunia kutokana na ugonjwa wa kipindupindu unaosababishwa na mazingira machafu na ukosefu wa maji safi ya kunywa.