ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 24, 2017

WASOMI WAZUNGUMZIA UTEUZI MAOFISA WA TRA.


Rais John Magufuli akimuapisha Alphayo Kidata kuwa Katibu Mkuu Ikulu wakati wa hafla ya kuwaapisha mawaziri na mabalozi jijini Dar es Salaam, jana.

Dar es Salaam. Baadhi ya wasomi wamezungumzia uteuzi wa aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alphayo Kidata kuwa Katibu Mkuu wa Ikulu kwamba kunaonyesha kuwa Rais John Magufuli anaitumia taasisi hiyo kama kipimo cha watu anaowaamini kuwapa dhamana kubwa zaidi.

Kidata alikuwa mteule wa pili kuongoza TRA, tangu Rais Magufuli alipoingia madarakani mwishoni mwa mwaka 2015.

Novemba 27, 2015, Rais Magufuli alimsimamisha kazi Kamishna Mkuu wa TRA, Rished Bade baada ya kuibuliwa kwa upotevu wa makontena 349 yenye thamani ya Sh80 bilioni katika bandari ya Dar es Salaam pasipo TRA kuwa na kumbukumbu zozote.

Katika mabadiliko hayo, Rais alimteua Dk Philip Mpango kukaimu nafasi hiyo, lakini hakukaa muda mrefu kwani Desemba 23, 2015, alimteua Dk Mpango kuwa mbunge na kisha Waziri wa Fedha na Mipango.

Wiki moja baada ya uteuzi huo wa Dk Mpango, Desemba 30, 2015 Rais Magufuli alimteua Eliakimu Maswi, kuwa Kaimu Naibu Kamishna wa TRA lakini naye hakukaa muda mrefu na Januari 2016, alirejeshwa mkoani Manyara kuendelea na kazi yake ya katibu tawala wa mkoa. Kuhusu Maswi, Rais alifafanua kuwa amekamilisha kazi aliyokwenda kuifanya katika taasisi hiyo.

Kutokana na uteuzi wa Maswi, Rais Magufuli alimteua Kidata kuwa Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA ambaye baadaye alithibitishwa na kuwa Kamishna Mkuu. Kabla ya uteuzi huo, Kidata alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Akizungumzia mabadiliko hayo, Profesa wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Humphrey Moshi alisema haoni athari za kuyumba kwa TRA kutokana na mabadiliko hayo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.