ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 25, 2022

MAGANYA AMBWAGA DR. MNDOLWA UENYEKITI WAZAZI CCM.

Wajumbe 578 kati ya 835 wa mkutano Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa wamemchagua Fadhil Maganya kuwa mwenyekiti mpya wa jumuiya hiyo. Maganya ameibuka kidedea akimshinda aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Dk Edmund Mdolwa aliyepata kura 64. 

Matokeo hayo yametangazwa usiku wa kuamkia leo Ijumaa Novemba 25, 2022 baada ya wasimamizi wa uchaguzi kuhesabu kura kwa zaidi ya saa saba.

 Wagombea walimaliza kuomba kura saa 12 jioni na kisha kufuata upigaji na uhesabuji wa kura ambalo ambapo shughuli hiyo ilidumu hadi za saa saba usiku na ndipo msimamizi wa uchaguzi alipotangaza matokeo.

 Akitangaza matokeo hayo jijini Dodoma, msimamizi wa uchaguzi huo, Maalim Kombo Hassan amesema Maganya ameibuka kidedea kwa kupata kura 578 kati ya kura 835 zilizopigwa huku kura mbili zikiharibika. 

 Maganya aliwashinda wagombea wengine saba akiwemo Dk Mndolwa. Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Msimamizi huyo amemtangaza Doto Iddi Mabrouk kuwa mshindi kwa kupata kura 530 kati ya 736 zilizopigwa akiwashinda wagombea wengine wanne. 

 Katika nafasi ya wajumbe watatu wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) Tanzania Bara, Mwenyekiti huyo amewatangaza Hamoud Abuu Jumaa, Waziri wa Madini, Dk Doto Biteko na George Gandye kuwa washindi.

 Jumaa alipata kura 569, Biteko 535 na Gandye 238 kati ya kura 825 zilizopigwa huku kura saba zikiharibika. Katika nafasi hiyo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angelina Mabula alipata kura 232 huku Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima akipata kura 195. 

 Kwa upande wa Baraza Kuu kundi la Zanzibar, Msimamizi huyo aliwatangaza Christina Antony aliyepata kura 325, Ally Issa Ally, kura 397 na Time Bakari kura 441. 

 Baraza Kuu Bara walioshinda ni Ally Kassim Mandai aliyepata kura 220, Lulu Abas Mtemvu kura 248 na Saad Mohammed Khimji kura 298. 

Peter Kasera aliibuka mshindi wa uwakilishi UVCCM kwa kupata kura 264 na kwa upande wa Uwakilishi wa UWT mshindi akiwa ni Asha Juma Ferouz aliyepata kura 287 akiwashinda wagombea wengine watatu.

ALIZWA BAADA YA MKEWE KUTOROKA NA PESA ZAKE MILIONI 28.1AKIWA NA MCHEPUKO.

Manit na wanawe wakiwa katika kituo cha polisi baada ya mkewe kutoroka na pesa zake. 

Furaha ya mwanamume nchini Thailand aliyetambulika kama Manit, kushinda bahati na sibu iligeuka na kuwa ndoto mbaya baada ya mkewe kuchukua pesa hizo na kutoroka na mpenziwe.

 Mwanamume huyo wa miaka 49 alichanganyikiwa na kuvunjika moyo baada ya mkewe mwenye umri wa miaka 45, Angkanarat, kutoroka na shilingi milioni 28.1. 

Kwa mujibu wa ripoti ya shirika la habari ya The Thaiger, Manit alikuwa ameshinda pesa hizo kujpitia bahati na sibu mnamo Novemba 1, na kuweka hela hizo katika akaunti ya benki ya mkewe. 

Manit alipiga ripoti kwa polisi, ila maafisa hao walisema hawangemsaidia kwani pesa hizo zilikuwa kwenye akaunti ya benki ya Angkanarat.

 Isitoshe, wawili hao hawakuwa wameoana kihalali, kwa sababu hawakuwa na cheti cha ndoa. 

Wawili hao wameishi pamoja kam mke na mume kwa miaka 26, na wana watoto watatu, ila Manit alisema hakujuwa kama mkewe alikuwa na mpango wa kando. 

Angkanarat aliaambia shirika la habari la Thai kwamba hana mpenzi mwingine, ila alimkimbia mumewe kwa sababu alichoka na malalamiko yao na ya mwanao wa kiume. 

Pia alisema kwamba alitaka kuwa mtawa na sehemu ya pesa hizo alipeana kama ufadhili katika mashirika tofauti za msaada. 

Baada ya kupata habari kwamba anasakwa na polisi kufuatia ripoti ya mumewe, mwanamke huyo alirejea nyumbani siku ya Jumapili, Novemba 20, ili kufafanua yaliyojiri. 

GOODLUCK GOZBERT ASHIRIKISHWA NA MKALI MWINGINE TOKA KENYA.

 Hello, Praise Jesus

This is a New Song From Deus Derrick (Kenya) featuring Goodluck Gozbert (Tanzania)

May God Bless You as You are Listening To It And Share With Friends and Believers.

................................................................................................................


Habari, Tumsifu Yesu Kristo

Huu ni Wimbo Mpya Kutoka kwa Deus Derrick (Kenya) akimshirikisha Goodluck Gozbert (Tanzania) Mungu Akubariki Unapoisikiliza na Kushiriki na Marafiki na Waumini.

"KILA UHAI UNA THAMANI TOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE NA WATOTO" SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI.

Tumekusanyika hapa leo tukiungana na mataifa mengine kote duniani kuadhimisha Kampeni ya Siku 16 za Uanaharakati Dhidi ya Ukatili wa Kijinsia ambapo kitaifa unaizindua wewe mwenyewe leo hapa katika viwanja vya Klabu ya Viongozi (Leaders Club) . 

Leo ni siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake ambayo ndio siku ya kwanza katika kuadhimisha kampeni ya siku 16 za Uanaharakati. Anna Kulaya(Mratibu wa WiLDAF) 

Ingawa tunafuraha kuona umati mkubwa huu na wewe mwenyewe mgeni rasmi ukijumuika nasi kwenye uzinduzi huu, mioyoni tumejaa machungu tele. Ni hali yakusikitisha kuwa karne hii ya 21 ya ulimwengu uliostaarabika, bado kuna matukioya ukatili wa kijinsia kwani tunaamini yanazuilika

Kauli mbiu ya kampeni ya mwaka huu ni “Kila Uhai Una Thamani! Tokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto.” Anna Kulaya (Mratibu wa WiLDAF) #PingaUkatiliOkoaMaisha #16DaysOfActivism 

Kauli mbiu hii imelenga kuhamasisha kila mtu, jamii, taasisi na serikali kuwa sehemu ya kuwajibika kutokomeza vitendo vyote vya ukatili kwani madharayake ni makubwa na mwisho hupelekea vifo hasa kwa wanawake nawasichana

Miaka ya hivi karibuni kumekuwa na vitendo vya ukatili wa kijinsia,Mathalani ripoti ya mwaka 2021 jeshi la polisi lilionyesha jumla ya watu 29,737 walifanyiwa ukatili wa kijinsia kati yao 20,897 ni wanawake, 8,476 wanaume. 

Ambapo kati yao mauaji ya vikongwe ni 118. Asilimia 68.6 ya mauaji yaliyoripotiwa yalikuwa ni dhidi ya wanawake. Mwaka 2020, mauaji yaliyotokana na migogoro ya majumbani na wivu wa mapenzi ni asilimia 26% ya mauaji yote yaliyoripotiwa katika Jeshi la Polisi. 

Naye Waziri wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalumu Dkt Dorothy Gwajima Ameiongeza WiLDAF na Mkuki kwa uratibu na kufanikisha uzinduzi wa siku 16 za unaharakati vile vile amepongeza wazo la msafara wa kupinga ukatili wa kijinsia vilevile amesema atashiriki kwenye baadhi ya mikoa.

Wana MKUKI  tumejipanga kutumia kampeni hii kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo Msafara wa kampeni wa kupinga ukatili wa kijinsia ambao utapita mikoa (Pwani,Morogoro,Dodoma,Shinyanga,Geita,Mara na Arusha) 

Msafara huu utatembelea jamiii, mashuleni, kwenye vituo vya mabasi na maeneo ambayo yanaonesha Kombe la Dunia na kwa kutumia njia hii tutaweza kufikia wanaume wengi zaidi na kuhamasisha mabadiliko ya kifikira, kimtazamo namatumizi mabaya ya mamlaka/power walizonazo katika kulinda wanawake nawatoto. 

Tarehe 8 Desemba tunategemea kuwa na tuzo maalum kwa vinara wanaolinda wanawake, watoto na kuzuia ukatili wa jinsia.Tuzo hii imeanzishwa na wana MKUKI kwa kushirikiana na wadau wa maendeleowakiwemo UNFPA na LSF ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa watukatika jamii zetu wanaofanya kazi kubwa ya kuzuia na kutokomeza vitendo vyaukatili wa kijinsia. Anna Kulaya(Mratibu wa WiLDAF)#PingaUkatiliOkoaMaisha 

MRADI WA BILIONI 12 WA MAJITAKA WASAINIWA MWANZA

 

Mkataba wa upanuzi wa mfumo wa majita ukisainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele (kushoto) na Katibu Mtendaji wa LVBC, Dkt. Masinde Bwire (kulia). Wanaoshuhudia ni viongozi wa Wizara ya Maji na MWAUWASA.
Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele (kushoto) akibadilishana mkataba na Katibu Mtendaji wa LVBC, Dkt. Masinde Bwire mara baada ya kusaini.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira, Mhandisi Charles Mafie (kushoto) akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa upanuzi wa mfumo wa majitaka

Wawakilishi wa LVBC, Wizara ya Maji, Bodi na Menejimenti ya MWAUWASA mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa upanuzi wa mfumo wa majitaka. 

Na Mohamed Saif

Serikali kupitia Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) imesaini mkataba wa shilingi bilioni 12.7 na Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria (‘LVBC’) kwa ajili ya upanuzi wa mfumo wa majitaka utakaonufaisha wakazi 7,360 Jijini Mwanza.

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira, Mhandisi Charles Mafie akimuwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga kwenye hafla ya utiaji saini Novemba 23, 2022 alipongeza jitihada za LVBC kwenye utunzaji wa Ziwa Victoria.

Mhandisi Mafie alisema wananchi wanahitaji maji safi na salama na kwamba jitihada za makusudi za utunzaji wa vyanzo vya maji zisipofanyika, maji salama hayotapatikana.

“Kwa mkataba huu na program hii kwa Mwanza tunakwenda kuhakikisha kwamba Ziwa Victoria linakwenda kulindwa na sio suala la maji pekee kwani Ziwa likichafuka maana yake hata samaki hatutapata kwahiyo hapa tunazungumzia suala la lishe pia,” amesema Mhandisi Mafie.

Hata hivyo aliisisitiza LVBC kutazama namna ya kutanua program hiyo na kuifikisha kwenye miji mingine inayozunguka Ziwa Victoria ikiwemo mji wa Musoma na Bukoba ili kusiwe na uchafuzi kutoka kwenye maeneo yote yanayozunguka Ziwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Mhandisi Leonard Msenyele amebainisha kuwa utanufaisha wakazi wa Kata za Igogo, Kitangiri, Kirumba, Pasiansi na Nyamanoro.

Amebainisha kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha maji ya Ziwa Victoria yanaendelea kuwa salama na kwamba jitihada, mikakati na hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na uwepo wa mradi huo.

“Tunaishukuru sana Serikali yetu kwa kutuletea mradi huu, sisi pia kama taasisi tutanufaika kwani kulinda uchafuzi wa Ziwa maana itasaidia kupunguza gharama ya kutibu maji kabla ya kuyapeleka kwa wananchi,” amesema Mhandisi Msenyele.

Mhandisi Msenyele ameihakikishia Serikali kuwa MWAUWASA itasimamia vyema utekelezaji wa mradi na kwamba kila kipengele kwenye mkataba kitasimamiwa kwa weledi na kwa kuzingatia miiko ya kitaaluma ili kuleta tija iliyokusudiwa.

“Serikali kupitia Wizara ya Maji, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Fedha na Mipango imetuamini kusimamia mradi huu, tunaahidi kutekeleza kwa uaminifu mkubwa ili manufaa yaliyokusudiwa yapatikane,” amesema Mhandisi Msenyele.

Naye Katibu Mtendaji, Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria (LVBC), Dkt. Masinde Bwire amesema chimbuko la mradi unatokana na mradi wa kwanza wa Uhifadhi wa Mazingira ya Ziwa Victoria (‘LVEMP’) ambao haukuweza kutatua changamoto zote kwa wakati huo ikiwemo ya uchafuzi wa Ziwa.

“Mradi huu umeainisha changamoto zilizoshindwa kutatuliwa na mradi wa kwanza (LVEMP) kwani hadi sasa uchafuzi wa Ziwa Victoria bado ni mkubwa kutoka kwenye miji inayozunguka ikiwemo Mwanza, Kampala, Kisumu, Musoma na Bukoba,” anabainisha Dkt. Bwire.

Amesema jukumu kubwa la LVBC ni kusimamia matumizi endelevu ya Rasilimali za Maji na rasilimali zingine ndani ya ukanda wa Ziwa Victoria na kwamba ni wajibu wao kutafuta fedha kwa kushirikiana na Serikali za Jumuia sambamba na wadau wa mazingira na maendeleo.

“Kwa sasa tumefanikiwa kupata kiasi cha shilingi za Kitanzania Bilioni 12.7 kwa ajili ya mradi huu ambao unatekelezwa kupitia Mpango Jumuishi wa Usimamizi wa Rasilimali za Maji katika Bonde la Ziwa Victoria (‘LVB IWRMP’) na usimamizi wake utakuwa chini ya MWAUWASA,” amesema Dkt. Bwire

Amesema utakamilika mwishoni mwa Mwaka 2025 na kwamba jitihada za kutafuta fedha zaidi kutoka kwa wadau zinaendelea kwani uchafuzi wa Ziwa Victoria bado ni mkubwa.

“Rai yetu kwa Mamlaka za Miji inayozunguka Ziwa Victoria ni kuendelea kuhimiza usafi wa mazingira na kufanya matumizi endelevu ya Rasilimali za Maji na vyanzo vya maji,” amesisitiza Dkt. Bwire.

Thursday, November 24, 2022

WAKULIMA IRINGA WAMPONGERA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN

 


Mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego akiongea na wakulima waliofika ofisi kwake kwa ajili ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha sekta ya Kilimo.

Baadhi ya wakulima waliofika ofisi kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego kwa ajili ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha sekta ya Kilimo
Baadhi ya wakulima waliofika ofisi kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego kwa ajili ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha sekta ya Kilimo.



Na Fredy Mgunda, Iringa.
WAKULIMA mkoa wa Iringa  wamefanya matembezi ya  kumpongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  Samia Suluhu Hassan kwa kuwapunguzia bei ya mbolea.

Wakizungumza Mbele ya Mkuu wa mkoa wa Iringa,wakulima hao wamesema kuwa  walikuwa wakinunua mbolea kwa shilingi  150,000 lakini sasa wananunua kwa shilingi  60,000  hadi 70000

“Tunampongeza na kumshukuru sana rais samia kwa kutuona sisi wakulima kwa sababu mwanzo tulikuwa tukinunua mbolea kwa laki moja elfu thelathini lakini saizi tunapata kwa elfu 60000 hadi sabini ni hatua nzuri tunampongeza mama na sasa tunaamini kila mwananchi wetu atalima"walisema

Akisoma risala Mbele ya Mkuu wa mkoa wa Iringa Abeid Kiponza alisema kuwa  wana kila sababu ya kumpongeza Rais Samia kutokana na kupunguza gharama za pembejeo za kilimo hususani upande wa mbolea

 “sisi wakulima wa mkoa wa Iringa tumefanya matembezi maalumu ya kumshukuru na kumpongeza mheshimiwa rais kutokana  na upendo wake kwetu kutokana na mambop makubwa anayoendelea kutufanyia kwenye kilimo tanzania nzima inajua wakulima wa nyanda za juu kusini tumekuwa tukizalisha viazi,mahindi,ngano,alizeti na mazao mengine ya chakula na hatuwezi zalisha mazo vizuri bila kuungwa mkono na serikali na tumwambie usiwasikilize wanasiasa ambao wamekuwa kama wasemaji wetu wakati sio wasemaji wetu usiwasikilize"alisema

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amesema kuwa  Serikali ya awamu ya sita imeamua kutatua matatizo ya msingi kwa kuwekeza kwenye kilimo na miradi umwagiliaji.

“Sisi wote ni mashuhuda mheshimiwa rasi ameweza kutoa pikip[iki kwa maafisa ugani wote na wanatakiwa wahikikishe wanafika kama kuna maswali muulize wawahudumie nyinyi na zimetoka billion 55 mradi wa pawaga umwagiliaji kwa hiyo tunaposema mama ameupiga mwingi na ametuletea ruzuku ambayo ndio tunategemea sisi wakulima"

Hata hivyo lengo la serikali ya Rais Samia Suluhu  awamu ya sita ni kuhakikisha inaboresha sekta ya kilimo na maslahi ya wakulima kwa ujumla.

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Burundi aipongeza Benki ya CRDB Burundi kwa miaka 10 ya Mafanikio

 

Mwenyekiti wa Bodi ya kampuni Mama ya Benki ya CRDB, Dkt. Ally Laay (watatu kulia) akikabidhi tuzo maalumu ya shukrani ya maadhimisho ya miaka 10 ya kampuni tanzu ya Benki ya CRDB Burundi kwa Naibu Gavana wa kwanza Benki Kuu ya Burundi, Desire Musharitse (katikati) pamoja na Naibu Gavana wa pili, Marie Goreth Ndayishimiye. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Burundi, Hosea Kashimba (wapili kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (wapili kushoto), Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Burundi, Fredrick Siwale (kushoto) pamoja na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Burundi, Menard Bucumi.

=========   ========   ========

Bujumbura, 24 Novemba 2022 – Benki Kuu ya nchini Burundi (BRB) imeipongeza Benki ya CRDB Burundi kwa mafanikio makubwa iliyopata katika kipindi cha miaka 10 ya uwepo wake nchini Burundi. 

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu ya Burundi kwa niaba ya Gavana katika mkutano na ujumbe wa Benki ya CRDB ulioongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela aliyeambatana na wajumbe wa Bodi ya kampuni Mama ya Benki ya CRDB pamoja na kampuni tanzu ya Benki ya CRDB Burundi. Ujumbe huo umetembelea Benki Kuu ya Burundi kutoa shukrani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya utoaji huduma za kibenki ya kampuni tanzu ya Benki ya CRDB Burundi.
Akizungumza katika mkutano, Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Burundi, Desire Musharitse alisema Benki Kuu ya nchi hiyo inafurahia sana kwa uwepo wa Benki ya CRDB nchini Burundi kwani imekua sehemu ya uwezeshaji wa miradi mingi ya kiuchumi kwa nchi lakini pia imechangia uwezeshaji wa wafanyabiashara.

“Tulipata matatizo yaliyopelekea changamoto kubwa ya upatikanaji wa fedha za kigeni mwaka 2015 lakini tulipata msaada mkubwa sana kutoka Benki ya CRDB na hakika hilo limedhihirisha ule usemi wa rafiki wa kweli hujulikana wakati wa shida” alisema Musharitse.
Tangu ilipoingia katika soko la Burundi mwaka 2012, Benki ya CRDB imekua ikifanya vyema sokoni na katika kipindi cha miaka 10 tu imeweza kushika nafasi ya tatu kati ya benki kumi na tatu zinazotoa huduma za kibenki nchini Burundi. Katika kipindi hiko Benki imeweza kufungua matawi manne huku tawi la tano likitarajiwa kufunguliwa mapema mwaka 2023.

“Kutokana na kufanya vizuri kwa Benki ya CRDB Burundi tunatamani kuona ikifungua matawi mengi zaidi nje ya Bujumbura lakini pia kuweza kufanikisha upatikanaji wa mikopo kwa njia za kidigitali kama ambavyo wamekua wakitoa huduma nyingine kidigitali” aliongeza Musharitse.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela ameishukuru Benki Kuu ya Burundi kwa ushirikiano mkubwa kwa Benki ya CRDB Burundi uliopelekea kampuni tanzu hiyo kupata mafanikio makubwa ndani ya kipindi kifupi cha miaka 10. Sambamba na hilo Nsekela ameishukuru Serikali ya nchi hiyo chini ya Rais Evariste Ndayishimiye kwa kuipatia eneo Benki ya CRDB Burundi katika makao makuu mapya ya nchi ya Gitega ili kufanikisha ujenzi wa tawi jipya.

“Maraisi wetu wanatamani kuona ushirikiano wa sekta binafsi za Tanzania na Burundi lakini pia wamezungumza juu ya miradi ya kimkakati kati ya nchi hizi mbili ikiwemo mradi wa SGR na sisi tuko tayari kuisadia kampuni yetu tanzu kushiriki katika mradi huu kwa upande wa Burundi kama ambavyo tumeshiriki kwa upande wa Tanzania” alisema Nsekela.
Aidha, alisema Benki ya CRDB inatarajia kuingia nchini DRC hivi karibuni jambo ambalo litachangia kukuza biashara kati ya Burundi na DRC lakini pia ushirikiano wa biashara kati ya nchi hizo na Tanzania ambazo kwa pamoja ni sehemu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Adhma yetu katika masoko tunayohudumia sio tu kutoa huduma bora bali kutoa mchango katika uchumi na kubadilisha maisha ya watu tunaowahudumia hivyo tunaahidi kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na Benki Kuu ya Burundi ili kuleta mageuzi ya kiuchumi nchini Burundi” aliongeza Nsekela.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB Burundi, Hosea Kashimba na yeye alitoa shukrani za bodi kwa Benki Kuu ya Burundi kwa ushirikiano mkubwa uliochangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Benki ya CRDB Burundi katika kipindi cha miaka 10 tangu kuingia katika soko la Burundi. 

“Tunaona muelekeo mzuri wa nchi na tunaamini ndani ya kipindi kifupi kijacho tutaweza kuwa Benki kiongozi hapa nchini Burundi hivyo basi tunaomba ushirikiano huu uendelee kwani hatuwezi kufikia malengo yetu bila ushirikiano wenu” alisema Kashimba ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma PSSSF.
Maadhimisho ya miaka 10 ya Benki ya CRDB Burundi yameambatana na shughuli mbalimbali zenye lengo la kushukuru jamii ya watu wa Burundi kuiwezesha Benki ya CRDB Burundi kufanya vizuri sokoni.  Sehemu ya shughuli zilizofanyika ni pamoja na kutoa misaada kwa makundi yenye uhitaji maalum, uandaaji wa shindano la mchezo wa mpira wa kikapu kwa vijana pamoja na ujenzi wa mradi wa usafi kwa jiji la Bujumbura.

Benki ya CRDB Burundi ilianzishwa nchini Burundi mnamo mwaka 2012 chini ya sheria ya makampuni nchini Burundi.  Benki ya CRB Burundi inatoa huduma kwa wateja wa taasisi na makampuni pamoja na wateja binafsi huku ikimilikiwa na kampuni Mama ya Benki ya CRDB kwa asilimia 100. Benki ya CRDB Burundi inatoa huduma kupitia matawi manne sambamba na mawakala wa benki zaidi ya 600. Hadi kufikia robo ya tatu ya mwaka 2022, Benki ya CRDB Burundi imetoa mikopo ya zaidi ya Faranga Bilioni 300 za Burundi kwa sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, viwanda na utalii.

TRA TANGA YAKUSUDIA KUKUSANYA ZAIDI YA BILIONI 232 MWAKA WA FEDHA 2022/2023

 

Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza na waandishi wa habari baadaa ya kuzungumza na walipa kodi katika hafla fupi ya kuwapongeza kwa ulipaji wa kodi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 waliovuka lengo ambapo waliibuka kidedea katika mikoa yote Tanzania. 

Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza na waandishi wa habari baadaa ya kuzungumza na walipa kodi katika hafla fupi ya kuwapongeza kwa ulipaji wa kodi kwa mwaka wa fedha 2021/2022 waliovuka lengo ambapo waliibuka kidedea katika mikoa yote Tanzania. 
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kanda ya Kaskazini Selestini Kiria  akizungumza 

Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure akikata keki 
Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure kushoto akimsikiliza mfanyabiashara Wilbard Mallya
Sehemu ya wafanyabiashara wakiwa kwenye halfa hiyo

Na Oscar Assenga,TANGA.


MAMLAKA ya Mapato Tanzania Mkoani Tanga (TRA) leo wamekutana na kuzungumza na walipa kodi Mkoani Tanga katika halfa iliyokwenda sambamba na kuwapongeza kwa ulipaji kodi wao wa mwaka wa Fedha 2021/2022 ambao uliiwezesha kuvuka lengo na kuibuka kidedea katika mikoa yota nchini.

Halfa hiyo ilikwenda sambamba na kuwatembelea wateja wakubwa mkoani Tanga ikiwemo wafanyabiashara katika eneo la barabara ya 14 Jijini Tanga na Kiwanda cha PPTL ambako walizungumza nao.

Akizungumza wakati wa halfa hiyo Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure alisema kwamba mamlaka hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 inakusudia kukusanya kodi kiasi cha shilingi Billioni 232.69 ikiwa ni malengo ya serikali sawa na ongezeko la asilimia 37 ya mwaka wa fedha uliopita.

Alisema kutokana na uwepo wa Kutokana na ongezeko hilo alitumia fursa hiyo kuwataka wafanyabiashara mkoa humo kuendelea kushirikiana kikamilifu na mamlaka ya mapato katika kuhakikisha wanalipa kodi kwa wakati na kwa hiari ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa ya kuendelea kung’ara katika ukusanyaji wa kodi hapa nchini

Meneja huyo alisema mamlaka hiyo kuibuka kidedea ni kutokana na walipa kodi wa mkoa wa Tanga kulipa kodi na hivyo kuwawezesha kufanya vizuri katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 .

Alisema kwa mkoa wa Tanga walikuwa wamepangiwa lengo la kukusanya billion 169.68 lakini wao wameweza kukusanya billioni 207.52 ikiwa ni sawa na asilimia 121.6% hivyo waliwashukuru kwa kuwawezesha kufikia lengo hilo.

Meneja huyo alisema pia katika mwaka wa fedha 2022/2023 lengo lao la ukusanyaji limeongezeka na kufikia bilion 63 ambayo ni sawa la ongezeko la asilimia 37% ya lengo la mwaka huu ni bilion 232.69 kwa hiyo wana kazi kubwa ya kufanya.

Alisema kwa sababu mwaka uliopita waliweza hatua ambayo imepelekea mwaka huu wameongezewa lakini katika hayo yote hatukuweza pekee yetu bali ni ushirikiano wenu wadau na hivyo kuweza kulipa kodi kwa hiari

Hata hivyo Meneja huyo aliwataka wafanyabiashara katika mkoa huo kuhakikisha wanaendelea kulipa kodi pamoja na kutekeleza maagizo ya serikali ya kulipa kodi kupitia mfumo wa kielektroniki.

“Lakini pia niwatake kutoa taarifa kwa mamlaka ya mapato pale panapotokea changamoto yoyote ikiwemo ya kusitisha biashara au kuhama”alisema

Awali akizungumza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kanda ya Kaskazini Selestini Kiria aliipongeza mamalaka hiyo kwa mafanikio waliyoyapata kwa mwaka wa fedha uliopita.

Sambamba na hilo pia amewaomba kuendelea kuboresha huduma zao ili kuzidi kuwavutia wateja kuweza kulipa kodi kwa wakati.

Akizungumza wakati alipotembelewa kwenye duka lake Mfanyabiashara Wilbard Mallya aliipongeza mamlaka hiyo kwa huku akiiomba Serikali kuwaangalia wafanyabiashara kwenye suala la kodi pamoja na kurahisisha utoaji wa huduma.

MWANAMKE WA KWANZA KUCHEZESHA KOMBE LA

 


Salima Mukansanga wa Rwanda amekuwa Mwamuzi wa kwanza wa kike Mwafrika kuchezesha mchezo wa Kombe la Dunia la FIFA akiwa Rasmi wa Nne.

Pia amehudumu katika Olimpiki, AFCON, Kombe la Dunia la FIFA la Wanawake, Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake na Ligi ya Mabingwa ya Wanawake ya CAF.

POLISI WALAUMU PANYA KULA KILO 200 ZA BANGI ILIYOKAMATWA.

 


Polisi nchini India wamewalaumu panya kwa kuharibu karibu kilo 200 (lbs 440) za bangi iliyonaswa kutoka kwa wachuuzi na kuhifadhiwa katika vituo vya polisi.


"Panya ni wanyama wadogo na hawana hofu na polisi. Ni vigumu kulinda dawa dhidi yao," mahakama katika jimbo la Uttar Pradesh imesema.


Mahakama iliwataka polisi kuwasilisha siri hiyo kama ushahidi katika kesi za ulanguzi wa dawa za kulevya.


Hakimu alitaja kesi tatu ambapo bangi iliharibiwa na panya.

Jaji Sanjay Chaudhary alisema katika agizo kwamba mahakama ilipowataka polisi kuwasilisha dawa hiyo iliyokamatwa kama ushahidi, iliambiwa kuwa kilo 195 za bangi “ziliharibiwa” na panya.


Katika kesi nyingine inayohusu kilo 386 za dawa hiyo, polisi waliwasilisha ripoti wakisema "baadhi" ya bangi hiyo "ililiwa na panya". Jaji Chaudhary alisema baadhi ya kilo 700 za bangi zilizokamatwa na polisi zilikuwa zimelazwa katika vituo vya polisi wilayani Mathura na kwamba "zote ziko katika hatari ya kuvamiwa na panya".


Alisema polisi hawana utaalamu wa kushughulikia suala hilo kwani panya hao ni “wadogo mno”. Njia pekee ya kulinda bidhaa zilizokamatwa kutokana na "panya hao wasio na woga", aliongeza, ilikuwa ni kuzipiga mnada dawa hizo kwa maabara za utafiti na makampuni ya dawa, huku mapato yakienda kwa serikali.


Mbunge Singh, afisa mkuu wa polisi wa wilaya ya Mathura, aliwaambia waandishi wa habari kwamba baadhi ya mirungi iliyohifadhiwa katika vituo vya polisi vilivyo karibu naye "imeharibiwa kutokana na mvua kubwa" na haikuharibiwa na panya.


Mnamo 2018, maafisa wanane wa polisi wa Argentina walifutwa kazi baada ya kuwalaumu panya kwa kutoweka kwa nusu tani ya bangi kutoka kwa ghala la polisi.


Lakini wataalamu walipinga madai hayo wakisema kwamba wanyama hao hawakuweza kuchanganya dawa hiyo kwa chakula na “kama kundi kubwa la panya wangekula, maiti nyingi zingepatikana kwenye ghala hilo”.


Utafiti uliochapishwa mnamo 2019 uligundua kuwa panya wa maabara walipopewa unga uliotiwa bangi, "walizoea kufanya kazi kidogo na joto la mwili wao pia lilipunguzwa".


Mnamo mwaka wa 2017, polisi katika jimbo la mashariki la Bihar walikuwa wamewalaumu panya kwa kunywa maelfu ya lita za pombe iliyochukuliwa, mwaka mmoja baada ya serikali kupiga marufuku uuzaji na unywaji wa pombe.


Mnamo mwaka wa 2018, mafundi waliofika kurekebisha mashine ya pesa iliyoharibika katika jimbo la Assam waligundua kuwa noti za thamani ya zaidi ya rupia 1.2m ($14,691; £12,143) zilikuwa zimechanwa - na washukiwa wa hatia walikuwa panya.

WATOTO WATATU WAFARIKI BWENI LIKITEKETEA SHINYANGA.

 

Muonekano wa Bweni lililoteketea kwa moto na kusababisha vifo vya wanafunzi watatu katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhangija mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde
Moto ambao haujajulikana chanzo chake umeunguza bweni la Kituo cha Kulelea Watoto wenye ulemavu cha Buhangija Mjini Shinyanga na kusababisha vifo vya watoto watatu wa kike wenye ulemavu wa macho.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema moto huo umetokea jana Novemba 23,2022 majira ya saa 2 na nusu usiku katika bweni B lililokuwa na watoto 32 katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu (watoto wenye ualbino, viziwi na wasioona).

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linafanya uchunguzi wa tukio la moto ambao haujafahamika chanzo chake na kuteketeza bweni katika kituo cha kulelea watoto walemavu Buhangija kilichopo mkoa wa Shinyanga na kusababisha vifo vya watoto watatu wa kike”,amesema Kamanda Magomi.

Amewataja watoto waliofariki dunia kuwa ni Niliam Limbu (12), Caren Mayenga (10), Catherine Paulo (10) wote ni walemavu wa macho (wasioona), wanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya Msingi Buhangija.

Amesema kufuatia tukio hilo mali mbalimbali za wanafunzi na za shule zimeharibika ambazo bado thamani yake haijafahamika na hakuna majeruhi yeyote.

“Baada ya taarifa za tukio hili kupatikana Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio, Pia jeshi la zimamoto na uokoaji nalo lilifika katika eneo la tukio na kufanikiwa kuzima moto ule pamoja na TANESCO kufanikisha uzimaji wa umeme haraka katika eneo lile ili kuzuia madhara makubwa ambayo yangeweza kutokea kutokana na moto ule”,ameeleza Kamanda Magomi.
.
Muonekano wa Bweni lililoteketea kwa moto na kusababisha vifo vya wanafunzi watatu katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhangija mkoa wa Shinyanga.


Amefafanua kuwa kituo cha kulelea watoto Buhangija kilikuwa na watoto 163 waliolala bwenini kituoni hapo siku ya tukio ambapo watoto wenye ualbino ni 77 kati yao wa kike 38, wa kiume 39, wasioona 20 wa kiume 9, kike 11 ambapo watatu wamefariki dunia na Viziwi 66 kati yao wa kiume ni 31 na wa kike 35.

Akizungumza na Malunde 1 blog, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila amethibitisha kupokea miili mitatu ya watoto waliofariki dunia kutokana na ajali ya moto katika kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhangija.

MWANAMKE ASTUKIA MCHUMBA AMEKUWA AKICHEPUKA NA JIRANI SIKU MOJA BAADA YA KUJIFUNGUA.


Mwanamke mmoja amesimulia kwa mshtuko kugundua kuwa mpenzi wake, mwalimu wa kupiga mbizi, ni tapeli wa mapenzi. 

Claire Barnes Northcott aligundua kuwa mchumba wake amekuwa akimchiti na jirani yake siku moja baada ya kujifungua mtoto wao.

 Claire Barnes Northcott alifichua kwamba aligundua kuhusu tabia mbaya ya mchumba wake baada ya kujifungua mtoto wao. 

Kulingana na gazeti la The Sun, mama huyo wa mtoto mmoja alisema yeye na mpenzi wake, aliyetambulika kwa jina la Leury, walikuwa wachumba na walikuwa wamebakish miezi michache kabla ya harusi yao. Northcott alisema: 

 "Siku moja baada ya kujifungua mtoto wetu wa kwanza Mickayley, ndiyo siku ambayo niligundua kuwa mchumba wangu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi wa zaidi ya miaka miwili." Alibaini kuwa uhusiano wao umekuwa hadithi ya mapenzi, na mchumba wake amekuwa akimuonesha mahaba matamu. 

"Leury alikuwa mtu wa mahaba sana hata sikujua kwamba alifanya chochote isipokuwa kunipenda. Nilidhani tulikuwa na uhusiano wa hadithi tamu. Nilipogundua kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na jirani yake kwa miezi kadhaa niolishtuka sana," Northcott alisema.

 Northcott na mpenzi wake walikutana wakati wa harusi ya rafiki yake katika Jamhuri ya Dominika, ambako anafanya kazi kama mwalimu wa kupiga mbizi. 

Alieleza kwamba walioneshana mahaba, na walianza kuchumbiana, na mwaka mmoja baadaye, alimuomba awe mkewe na mama wa watoto wake. 

Alipojifungua, moyo wake ulivunjika vipande vipande baada ya jirani wa mpenzi wake kutuma picha zake akiwa na jamaa huyo. 

Mwanamke huyo alikiri kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Leury na alitaka kumwambia lakini alisubiri baada ya kujifungua kwake.

Alipomkabili Leury na taarifa hizo, alikiri bila kusita kuwa alikuwa akimhiti na kumfanya afutulie mbali harusi yao. "Alituchezea akili, familia yangu, na marafiki zangu," alisema. 

 iliripoti kwamba jamaa alifutilia mbali harusi yake baada ya kugundua mkewe alikuwa na watoto wawili na mwanamume mwingine. 

Katika video ya kusikitisha, alielezea uchungu wake alipofuta mipango ya harusi na kuvua viatu vyake vya harusi na suti. Licha ya juhudi kadhaa ya walioshuhudia kumtuliza, bwana harusi aliyekuwa amepandwa na mori alikataa kuendelea na harusi. 

Pia alidai kurejeshewa mahari aliyolipa. "Watoto 2? Nirudishie mahari yangu nachukua mahari yangu," alisema. 

RAIS WA BRAZIL AKIMBILIA KORTINI KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI AKITAKA UFUTWE

 


Rais wa Brazil anayeondoka Jair Bolsonaro amewasilisha ombi katika mamlaka ya uchaguzi ya Brazil kupinga rasmi matokeo ya kura ya urais ya Uchaguzi Mkuu wa 2022. Rais wa Brazil anayeondoka Jair Bolsonaro ataka matokeo ya urais yafutwe.

Bolsonaro alipoteza kura ya marudio kwa ushinde mwembamba mnamo Oktoba 2022, kwa mpinzani wake Luiz Inacio Lula da Silva, almaarufu "Lula," ambaye anatazamiwa kuapishwa rasmi kuwa rais mnamo Januari 1. 

Kufuatia ushinde huo, Bolsonaro alionekana kukiri wazi kuwa anakubali kushindwa akisema ataendelea kutimiza amri zote za katiba. Kauli yake iliwafanya waangalizi kuamini kuwa atamwachia Lula madaraka kwa amani. 

Hata hivyo, mnamo Jumanne, Novemba 22, Bolsonaro na kiongozi wa chama chake cha mrengo wa Liberal waliwasilisha malalamishi wakidai kuwa baadhi ya mashine za kupigia kura zilikumbwa na hitilifu na kura zote zilizopigwa kupitia mashine hizo zinapaswa kubatilishwa. 

Akirejelea ripoti ya ukaguzi uliofanywa na kampuni iliyoajiriwa na chama cha Bolsonaro, walalamishi wanadai kuwa iwapo kura hizo zitafutwa, basi Bolsonaro angeibuka mshindi.

 Wakijibu ombi la Bolsonaro, maafisa wa tume ya uchaguzi walisema kwa kuwa mashine hizo ndizo zilizotumika katika duru ya kwanza ya uchaguzi, Bolsonaro na chama chake lazima warekebishe malalamiko yao ili kujumuisha matokeo hayo kupitia mahakama. 

Mahakama ya Upeo ya Uchaguzi ya Brazil, imempa Bolsonaro na walalamishi wenzake saa 24 kurekebisha maombi yao. Uchaguzi mkuu wa Oktoba ulikumbwa na ushindani mkali na ulikujia wakati kulikuwa na hali ya wasiwasi na mgawanyiko wa kisiasa nchini humo, ambayo imekuwa ikikabiliwa na mfumuko wa bei, na kuongezeka kwa umaskini. 

 Lula da Silva alipata zaidi ya kura milioni 60 kulingana na matokeo ya mwisho ya halmashauri ya kusimamia uchaguzi Brazil. Kura hizo zilikuwa nyingi zaidi katika historia ya Brazili na kuvunja rekodi yake mwenyewe kutoka 2006. 

Ushindi wake unakujia baada ya kufungwa jela mnamo 2018, na alikaa gerezani kwa zaidi ya miezi 18 kwa tuhuma za ufisadi. Lula alipoteza urais mara tatu na hatimaye akafanikiwa kushinda mnamo 2002 na tena miaka minne baadaye.