
Kama uko home jumamosi ya leo basi mida hii ya jioni kupitia TBC 1 umetoka kucheki mavituuuuZzz ya hawa majamaa katika kipindi chao 'Ben and mai' ila leo sijamwona kabisa kwenye chupa mwanadada Mai... Where is she bhana?

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. E Ndikilo akifungua mkutano MZFA.
Ongezeko la idadi ya watu na huduma mbalimbali za kijamii ile hali idadi ya viwanja inabaki palepale huku vingine vikibadilishwa matumizi imekuwa ni changamoto kubwa kwa mkoa wa Mwanza na wilaya zake.
Pia Mh Ndikilo hakuacha kuwapasha makocha wanaogeuza vyeti vyao mapambo ile hali walishiriki mafunzo ya Ukocha na fedha nyingi kutumika
Ili kurejesha heshima ya historia ya soka Mkoa wa Mwanza umeweka mikakati ya kuhakikisha unaingiza timu zaidi ya mbili katika ligi kuu zoezi ambalo litakwenda sambamba na uendelezaji wa vipaji vinavyochipukia.
Stori za ziada baina ya wajumbe wa MZFA na mkuu wa mkoa.
Picha ya pamoja.
Jumla ya wajumbe 33 kati ya 36 toka wilaya mbalimbali za jiji la Mwanza wamehudhuria mkutano huo wa mwaka uliofanyika katika ukumbi wa mikutano ukliopo ndani ya uwanja wa michezo CCM Kirumba Mwanza.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Jaji Joseph Sinde Warioba, kuwa Mwenyekiti wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Said Elmaamri, kuwa Mjumbe wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo katika Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Jaji Agustini Ramadhan, kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Jaji Salim Ahmed Salim, kuwa Mjumbe wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Mbunge wa Viti Maalum, Al-shymaa Kwegiyr, kuwa Mjumbe wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Said Elmaamri, kuwa Mjumbe wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete na Makamu wake Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakiwapongeza wajumbe wa Tume hiyo baada ya kuapishwa rasmi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete, akimuapisha Said Elmaamri, kuwa Mjumbe wa Tume ya mchakato wa kutafuta maoni ya Katiba Mpya, wakati wa hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Picha na Muhidin Sufiani. OMR
Baada ya kutabiri kifo cha mmoja wa rais wa bara la Afrika, mtumishi wa Mungu Nabii na Mtume TB Joshua ametabiri kifo cha mwigizaji mwingine wa kiume wa Nollywood na ameomba ukiwa kama MwafriKa anaomba maombi yako kumwombea mungu amuepushie na kifo else basi mapenzi ya Mungu yatimizwe akasema muigizaji huyo ni wa kiume hivyo sala zaidi zinaombwa kwa waigizaji wafanye maombi ya kufunga na kuomba.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. Ernest Ndikilo leo ameongoza Umma aliojitokeza kutoa salamu za rambirambi kwa mwili wa aliyewahi kuwa mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kiaro aliyefariki dunia siku ya Jumanne wiki hii akiwa na umri wa miaka 87 ambaye ameagwa rasmi leo jijini Mwanza.
Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kiaro alizaliwa mnamo tarehe 1/01/1923 nakufariki dunia 10/04/2012.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Ernest Ndikiro akimfariji mke mdogo wa marehemu Zainab Kiaro.
Mmoja wa wanafamilia (Kushoto) akimfariji mke wa kwanza wa marehemu Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kiaro aitwaye Penina Kiaro (Kulia).
Makamanda wakijadiliana.
Makamanda wakizidi kufurika eneo la tukio kutoa salamu zao za mwisho kwa mwili wa marehemu.
Makamanda wakiwa eneo la juu katika kilima kidogo cha mawe ili kushuhudia ibada ya salamu za mwisho jijini Mwanza.
Safu ya Makamanda wengine.
Mwili huo ulitoka katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando mchana na hatimaye majira ya saa saba ukaagwa hapa katika nyumba yake ya kikazi maeneo ya Kapripoint kabla ya kusafirishwa kuelekea wilayani Tarime mkoani Mara kwaajili ya Mazishi.
Kwa mwendo wa pole mwili ulipelekwa eneo rasmi.
Moja kati ya wanajeshi akiongoza moja ya vifungu kwenye ibada hiyo.
Mapaparazi.
Wakati wa kutoa heshima za mwisho uliwadia.
Jeshi la polisi usalama barabarani nao walikuwepo kutoa heshima zao.
Heshima...
Heshima ziliendelea kutolewa.
Makamanda wakipanga mikakati.
Mzee Gachuma katikati akifanya majadiliano na baadhi ya maafisa wa Jeshi.
Msafara.
Mwili wa marehemu aliye kuwa mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Jenerali Mstaafu Ernest Mwita Kiaro umesafirishwa leo kuelekea wilayani Tarime mkoani Mara kwaajili ya Mazishi ambayo yatafanyika kesho.
Wakazi wa mkoa wa Dar es salaam nchini Tanzania kupitia Mamlaka ya hali ya hewa wamepewa taarifa ya tahadhari kukaa mbali na maeneo ya mwambao wa bahari kupitia tishio la Tsunami kulikumba eneo la pwani ya bahari ya Hindi.
Hofu nchini Indonesia
According to the USGS, the 2004 quake struck about 155 south-southeast of Banda Aceh at a depth of 18.6 miles. Some 227,898 people were killed or missing presumed dead and about 1.7 million were forced out of their homes after the tsunami affected 14 countries in Asia and East Africa.
Vice President Mohammed Gharib Bilal pays his last respects at Leaders Club grounds. Dressed in white in the background is First Lady Salma Kikwete. PH/SAID POWA
Aliyewahi kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini, Jenerali mstaafu Ernest Mwita Kiaro (Pichani), amefariki dunia jana asubuhi akiwa na umri wa miaka 87.
Mgeni rasmi Afisa Usalama wa Mkoa Bwana Mutash akiongea na wachezaji wa mpira wa pete kabla ya ufunguzi wa bonanza. Bonanza hili lilifanyika katika viwanja vya CCM Kirumba na baadae sherehe fupi ndani ya Shooter’s Pub ambayo ilidhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania.
Maveteran wa Mwanza na Dodoma wakilisakata kabumbu katika mchezo wa kwanza wa mpira wa miguu, timu hizo zilitoka sare ya bao 2-2.
Haya ndo mambo yalivyokua katika bonanza la sikukuu ya Pasaka, hapa ilikua mechi kati ya Mwanza na Isaka ambayo pia matokeo yalikua sare ya 1-1.
Baadhi ya mashabiki wakifuatilia kwa umakini bonanza la maveterani huku wakichati kwa nafasi.
Wadau wakiwa ndani ya Shooter’s Pub wakisherehekea baada ya bonanza la Pasaka kuisha majira ya jioni hivi.