ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 7, 2018

JEMBE FM, METDO NA WADAU WAKE WAMUENZI KARUME KWA KUTEMBELEA NA KUTOA CHAKULA KWA KITUO CHA KULEA WAZEE BUKUMBI.

Leo ni Tarehe 7 April 2018, tunaadhimisha Kumbukumbu ya Kifo Cha Rais wa Kwanza wa Zanzibar Abeid Aman Karume @Jembefm 93.7 kupitia kipindi chake cha muziki wa Injili yaani #JembeGospel kwa Kushirikiana na wanamuziki wa muziki huo, Wachungaji wa makanisa kadhaa ya Kipentekoste pamoja na METDO, wameitumia siku hii muhimu ya #KarumeDay kwa kuwatembelea ndugu zetu wa kituo cha Wazee wasiojiweza kilichopo Bukumbi wilayani Misungwi mkoani Mwanza na kutoa mahitaji mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 'First Lady' Mama Janeth Magufuli.

Vilevile kuipa thamani Kazi ya utumishi uliotukuka na Kuuenzi Upendo na Msisitizo wa Mshikamano aliokuwa nao Hayati Mzee Karume.

Mshikamano ulipo baina ya Tanzania na Zanzibar umeendelea kudumu sasa yapata miaka 46. 

Ni takribani miaka miwili sasa imepita tangu Mama Janeth Magufuli alipodhuru kwenye kituo hicho (mwezi March 7 mwaka 2016) ambapo aliteuliwa rasmi kuwa Mama Mlezi Mkuu wa Kituo hicho  baada ya kuhamasisha mashirika mbalimbali, watu binafsi na taasisi za kifedha kutoa michango ya vitu mbalimbali vilivyofikia thamani ya shilingi milioni 54 na kukiwezesha kituo hicho kwa chakula, malazi na mavazi.

Hivyo mpango huu umekuja kama sehemu ya kuitikia wito wa Fist lady. 

CC:- #JembeGospel @nzwallajr @gsengo @jembenijembePICHA ZAIDI ZAJA.................

CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA KAGERA (KCU) CHAFAFANUA KUHUSU MALIPO YA AWALI YA KAHAWA YA WAKULIMA


Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa ufafanuzi kuhusu malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd, Leo 7 Aprili 2018, Mwingine ni Kaimu meneja Mkuu wa Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg John kanjagaile. Picha Zote Na Mathias Canal, WK 

Waandishi wa habari wakifatilia Mkutano wa Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila wakati akitoa ufafanuzi kuhusu malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd, Leo 7 Aprili 2018, Katika Ukumbi wa Ofisi za Wizara ya Kilimo (Kilimo 4).

Na Mathias Canal, WK-Dodoma

Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha ushirika cha Kagera (KCU) Ndg Onesmo Niyegila ametoa ufafanuzi kuhusu malipo ya awali ya kahawa ya wakulima wa Chama Kikuu cha Kagera KCU (1990) Ltd kama ilivyojadiliwa kwenye Mkutano wao Mkuu tarehe 27/03/2018.

Amebainisha hayo wakati akizingumza kwenye mkutano na waandishi wa habari Mjini Dodoma na kusema kuwa Chama Kikuu cha Ushirika cha Kagera si Kampuni ya kununua kahawa bali ni ushirika wa wakulima wadogo wadogo wenye lengo la kuunganisha nguvu zao kwa  pamoja katika kuhudumia zao la  kahawa na kuliwasilisha sokoni kwa utaratibu wenye tija endelevu na kisha kugawana mapato  baada ya kufanya mauzo.

Alisema bei halisi ya mkulima kwa upande wa Ushirika inapatikana mara baada ya mauzo ya kahawa kufanyika ambapo  wakulima hulipwa malipo ya mwisho kwa kadri ya bei ya kuuzia iliyopatikana sokoni na hesabu ya mwisho kuwasilishwa kwenye mkutano mkuu.

Hivyo kwa vile mchakato wa mauzo huchukua si chini ya kipindi cha mwezi mmoja tangu mkulima awasilishe kahawa yake kwenye ushirika hadi malipo ya mwisho kufanyika, basi ili kumuondolea mkulima adha ya kusubiri malipo yake yote baada ya mauzo wakati anahitaji kujikimu na kukidhi mahitaji yake muhimu, wakulima wenyewe kwa utashi wao kupitia  Mkutano Mkuu, wanajadili malipo ya awali atakayotanguliziwa mkulima wakati anasubiri malipo ya mwisho.

Niyegila alibainisha kuwa mnamo tarehe 27/03/2018, Chama Kikuu cha Kagera kilifanya Mkutano wake Mkuu ambao pamoja na mambo mengine wanachama walijadili malipo ya awali ya mkulima (Advance Payments). Katika makisio hayo,  Menejimenti na Bodi ya KCU (1990) Ltd walipendekeza malipo ya awali yawe ni TZS 1,000 kwa kilo moja ya kahawa ya maganda.

Alisema kuwa baada ya mjadala, wanachama waliagiza kupitiwa upya kwa makisio hasa katika upande wa malipo ya awali na kuangalia namna ya kupandisha kiwango cha malipo ya awali. Aliongeza kuwa Kiwango kipya pendekezwa kitawasilishwa kwa Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini kwa ajili ya kuidhinishwa.

Alisisitiza kuwa kile kilichojadiliwa kwenye Mkutano Mkuu wa wanachama si tangazo la bei bali ni malipo ya awali kwa mkulima ambapo Kwa mujibu wa sheria, bei elekezi ya zao la kahawa inatolewa na Bodi ya Kahawa Tanzania kwa utaratibu wa ushirika, bei halisi itajulikana mara baada ya mauzo ya kahawa kufanyika sokoni na si vinginevyo.

Niyegila aliongeza kuwa kwa utaratibu wa sasa wa Serikali, kahawa yote itakusanywa kupitia kwenye Vyama vya Ushirika na kupelekwa sokoni Manispaa ya Moshi Mkoani Kilimanjaro ambapo wanunuzi wote watanunulia hapo mnadani.

Kwa mantiki hiyo, hakuna mkulima yeyote atakayeruhusiwa kuuza kahawa nje ya mfumo wa ushirika

KUTOA HAKI SAWA KWA WOTE NDIYO MSINGI MKUU WA MAHAKAMA NCHINI TANZANIA


KATIKA kufikia malengo ya utoaji Haki sawa kwa wote na kwa wakati Mahakama ya Tanzania kupitia Kanda zake nchini, imeendesha mafunzo kwa watendaji wake wa vitengo mbalimbali.

Mkoani Mwanza Mkutano wa kujadili mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania 2015 – 2020 umefanyika ijumaa hii ya Tarehe 6 April 2018 katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mkuu wa mkoa wa Mwanza aliopo wilayani Nyamagana ukijumuisha wadau wa Mahakama kutoka wilaya mbili za Ilemela na Nyamagana pamoja na Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Mwanza.

Licha ya kuwa na changamoto ya uhaba wa vifaa na watumishi Mahakama nchini Tanzania imeendelea na ujenzi na uboreshaji wa Mahakama zake za Mwanzo,Wilaya na hata zile za  Mkoa na hivi karibuni ujenzi utakamilika nao mkoa wa Mara kukabidhiwa Mahakama Kuu ya Kanda.

"Kwahiyo itapunguza gharama na usumbufu wa ule umbali wa mtu kusafiri mwendo mrefu kuja mkoani Mwanza kwaajili ya kusikilizwa shauri lake" Alisema Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe. Robert Vicent. CHEKI VIDEO.

Mkutano huo wa mafunzo umeandaliwa na Ofisi ya hakimu Mkazi mfawidhi mkoa wa Mwanza ambapo Watoa maada au wawezeshaji wakiwa ni Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi mkoa wa Mwanza Mh Wilbert M.Chuma na Mtendaji wa Mahakama kuu Moses Minga.

"Mafunzo hayo ni endelevu na tunatarajia kuendesha pia mafunzo hayo kwa wilaya zilizobaki ndani ya mkoa wa Mwanza  kama vile Magu , Sengerema , Misungwi  , Ngudu Kwimba na Ukerewe lengo likiwa ni kuhakikisha kila mtumishi anauishi mpango mkakati husika" Alisema Mhe. Chuma.

Friday, April 6, 2018

VIDEO: MASHABIKI MWANZA WALIA NA MBAO FC.


JINAMIZI la kutoka sare  limezidi kuiandama Timu ya Mbao Fc ya jijini Mwanza baada ya kutoka sare na timu ya Lipuli kutoka mkoani Iringa katika mtanange wa Ligi kuu Soka Tamzania Bara uliopigwa Uwanja wa CCM Kifrumba jijini hapa.

Katika vipindi vyote vya mchezo timu zote zilionekana kuwa na safu butu hasa Mbao Fc iliyoonekana kuingia mara kadhaa langoni mwa timu ya Lipuli lakini uwezo wa washambuliaji wake kufumania nyavu ulikuwa mdogo.

Lipuli walionekana kucheza kwa tahadhri `ili wasifungwe wakiwa ugenini huku wakicheza kwa kujihami zaidi kuliko kushambulia wakihakikisha washambuliaji wa Mbao wasipenye na kuleta madhara.

Hadi mwisho wa mchezo Mbao FC imelazimishwa sare ya 0-0 na Lipuli FC ya Iringa.

Kwa sare hiyo, Mbao FC inabaki kwenye eneo la hatari ya kushuka daraja, ikifikisha pointi 20 baada ya kucheza mechi 23 na kuendelea kukamata nafasi ya 14 katika ligi hiyo yenye timu 16, mbele ya Njombe Mji FC yenye pointi 18 za mechi 22 na Maji Maji FC pointi 16 za mechi 22.


Lipuli FC yenyewe inayofundishwa na wachezaji wake wa zamani wa Simba SC, Suleiman Matola na Amri Said imefikisha pointi 28 baada ya kucheza mechi 23 na kuendelea kukamata nafasi ya saba, ikiwa juu ya Mbeya City na Ruvu Shooting ya Pwani zenye pointi 25 kila moja baada ya kucheza mechi 22 pia. 

HAYA NDIYO YALIYOJITOKEZA KWENYE MKUTANO WA KUJADILI MPANGO MKAKATI WA MAHAKAMA YA TANZANIA 2015-2020 JIJINI MWANZA

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe. Robert Vicent ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo.
KATIKA kufikia malengo ya utoaji Haki sawa kwa wote na kwa wakati Mahakama ya Tanzania kupitia Kanda zake nchini, imeendesha mafunzo kwa watendaji wake wa vitengo mbalimbali.


Mkoani Mwanza Mkutano wa kujadili mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania 2015 – 2020 umefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mkuu wa mkoa wa Mwanza aliopo wilayani Nyamagana ukijumuisha wadau wa Mahakama kutoka wilaya mbili za Ilemela na Nyamagana pamoja na Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Mwanza.

Pia Mkutano huo umelenga kupitia mpango mkakati huo, kuujadili utekelezaji wake mpaka sasa, kubaini changamoto, mafanikio lakini pia na kuona nini kifanyike kwaajili ya kuendeleza na kutekeleza utoaji maamuzi ya haki na kwa umakini zaidi kwa manufaa ya wadau wanaohudumiwa.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe. Robert Vicent ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo amewaasa washiriki hao kufanya kazi kwa weredi, kwa kuzingatia uwajibikaji, maadili, nidhamu huku wakitambua kuwa Serikali imewapa dhamana kubwa watumishi ngazi mbalimbali za mahakama  katika kuhakikisha kuwa haki inatendeka katika utoaji maamuzi.

Yote haya yamefanyika yakilenga dira ya Mahakama inayosema HAKI SAWA KWA WOTE NA KWA WAKATI.

Kwa mujibu wa Mhe. Robert, ni matarajio yake kwamba kila mdau wa Sheria atashiriki ipasavyo katika kutekeleza mpango uliowekwa kwenye mpango mkakati wa Mahakama kwa kuzingatia nguzo tatu muhimu za mpango mkakati huo ambazo amezitaja kuwa ni  pamoja na:- 
1.UTAWALA BORA UWAJIBIKAJI NA USIMAMIZI WA RASILIMALI.
2.UPATIKANAJI NA UTOAJI HAKI KWA WAKATI.
3.KUIMARISHA IMANI YA JAMII NA USHIRIKISHWAJI WA WADAU KATIKA SHUGHULI ZA MAHAKAMA.

MATEGEMEO
Baada ya Mkutano na Majadiliano yake kila mmoja atatekeleza  mpango huo kwa uadilifu, uwajibikaji, uwazi pamoja na kuzingatia weredi.

Mkutano huu wa mafunzo umeandaliwa na Ofisi ya hakimu Mkazi mfawidhi mkoa wa Mwanza ambapo Watoa maada au wawezeshaji wakiwa ni Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi mkoa wa Mwanza Mh Wilbert M.Chuma na Mtendaji wa Mahakama kuu Moses Minga.


"Mafunzo hayo ni endelevu na tunatarajia kuendesha pia mafunzo hayo kwa wilaya zilizobaki ndani ya mkoa wa Mwanza  kama vile Magu , Sengerema , Misungwi  , Ngudu Kwimba na Ukerewe lengo likiwa ni kuhakikisha kila mtumishi anauishi mpango mkakati husika" Alisema Mhe. Chuma.

Jumla ya washiriki 68 wamehudhuria Mkutano huo ambao ni Mahakimu, Makarani, Wahudumu wa Mahakama pamoja na Madereva.
GAUDENTIA KABAKA: WANAWAKE MSIONE FAHARI KUITWA 'DUME JIKE'

Mwenyekiti ya Jumuiya ya Wanawake wa Tanzania (UWT) Gaudentia Kabaka akizungumza na Waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, Suwata Kariakoo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa UWT Bara Eva Kihwelo (Picha na Bashir Nkoromo).

NA BASHIR NKOROMO

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudentia Kabaka amewataka Wanawake kote nchini  wasione fahari kuitwa 'Dume-Jike' bali wawe wanawake wenye msimamo imara na jasiri kwa maendeleo yao na ya nchi kwa jumla.

Gaudentia ameto mwito huo, wakati akiwasilisha salaam maalum za pole kwa ndugu jamaa, marafiki na hasa wanawake wote hapa nchini na duniani kote kufuatia kifo cha Winnie Mandela aliyemwelezea kuwa alikuwa amwanamke shupavu katika kupigania haki na vita dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.


"Tazama Winnie Mandela alikuwa mpambanaji hata kabla ya kuwa mke wa Rais Nelson Mandela, kwa hiyo tukiangalia historia yake tunabaini kuwa hakuhitaji msukumo wa nguvu za mwanaume katika kuonyesha ushupavu wake", alisema.


Alisema Winnie Mandela aliyefariki dunia Aprili 2, mwaka huu, aliendelea kuonyesha ushupavu wake katika kupambana na udhalimu na ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini hata wakati Mandela akiwa gerezani


"Winnie atakumbukwa na Watanzania na dunia nzima kwa ujasiri wake pia atakumbukuwa kwa umaarufu alioupata hata akiwa bado mwanafunzi, msichana kabla ya kuolewa. Alichukia kuona Mwafrika anabaguliwa, anatengwa asifike kwenye maeneo walipokuwa weupe. Kwa hiyo umaarufu wa Winnie haukutokana tu kwa kuwa ni mke wa Rais yaani “First lady “ lakini umarufu wake ulikuwa wa kwake mwenyewe. Alijitambua, akajiamini, akatimiza wajibu wake kama Binadamu, kama Mwafrika, baadaye kama Mke, Mama, Mwanasiasa na Kiongozi" alisema Gaundetia 


"Wanawake wa Tanzania hasa wanasiasa tuna mengi ya kujivunia na kujifunza kutoka kwa mwana mama huyu mtoto wa Afrika. Tumejifunza kuishi sisi wenyewe na sio kutegemea tufanyiwe, tupendelewe ndipo tuonekane tunaweza. 


Tunatambua uwezo tulionao wanawake lakini pia tuwe wastahimilivu tunapokumbana na magumu tupambane hadi mwisho. Kama Winnie Madikizela Mandela aliweza kutetea Waafrika wenzake hata baada ya mume wake kufungwa; kwa sababu hiyo kwa nini sisi wengine tusiweze kujitokeza waziwazi na kuiunga Serikali na Rais wetu Dk. John Magufuli katika juhudi zake za kupiga vita ufisadi, wizi wa mali ya umma, kutowajibika", Alisema Gaudentia. 


"Wanawake wa Tanzania na wa Afrika nzima tunapomlilia Winnie Mandela kwa nini tusiige ujasiri wake kwa kukemea bila woga tabia mbaya kama mahusiano ya jinsia moja, ubakaji na utumiaji dawa ya kulevya, katika jamii yetu. Wanawake wa Tanzania tumapomlilia Winnie Mandela kwanini tusijitokeze waziwazi kupinga mfumo dume unaoendelea kwenye baadhi ya maeneo hapa nchini kwetu na kusababisha kina mama kutojiamini", alisema.


Alisema, kama Winnie Mandela alivyotimiza wajibu wake katika harakati za Waafrika kuing’oa Serikali dhalimu ya kibaguzi nchini Afrika kwa nafasi yake kama mwanamama, na wanawake wa Tanzania  kila mmoja kwa nafasi yake wanaweza kuwa chachu ya kuleta mabadiliko ya kweli hapa nchini.


"Tunafahamu kuna wanawake wa nchi yetu ambao wameonyesha ujasiri  kama huo wa Winnie Mandela wakiiwakilisha nchi yetu Kimataifa. Sisi UWT tunajiandaa kuwatambua hivi karibuni, nia yetu ni kutambua michango yao wakiwa wanafanya kazi nje ya nchi yetu na hivyo wametuleta sifa wanawake wa Tanzania, lakini pia kuwatia moyo wengine watimize wajibu wao, Alisema Gaudentia.", alisema Gaudentia.


Akizungumzia mrejesho wa ziara aliyoifanya hivi karibuni aliwapongeza wanawake wanaowajibika ipasavyo Mijini na Vijijini hapa nchini akisema yeye na timu yake walitembelea Mikoa na Wilaya zote za Kanda ya Nyanda ya Juu Kusini na kubaini kuwa wanawake ni wajasiriamali wazuri, ni wakopaji na walipaji wazuri na kuzitaka Halmashauri kuwapa mikopo wanawake hao ili wapanue shughuli zao za ujasiriamali na kwamba hicho ndicho kilio chao kikubwa, akihimiza halmashauri hizo kutenga asilimia kumi ya mapato ya ndani.


"Tunapenda ifahamike kwamba Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Mwelekeo wa Sera zake kwa Mwaka 2010 - 2020 na Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2015-2020 kwa pamoja zimeweka msisitizo wa kuyawezesha makundi Maalum ikiwemo Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu na katika kutekeleza maelekezo CCM, Serikali imeshatoa Maelekezo kwa Halmashauri za Majiji, Manispaa, Wilaya na Miji Midogo kutenga asilimia kumi za makusanyo yao ya ndani kwa ajili ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu Alisema Gaudentia na kungeza;


"Tunapenda kuwakumbusha wale wote wenye dhamana katika Mamlaka hizi kwamba ni Maelekezo ya CCM kutoa bila kukosa fedha hizi ili kuwawezesha wananchi katika makundi haya muhimu. Kuanzia sasa UWT itafuatilia kwa ukaribu suala hili na hatutasita kupendekeza kwa Mamlaka za uteuzi kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa wale wote wanaosuasua au kutenga kutoa fedha hizi ili kujihakikishia kuwa wanawake hawa wachapakazi wapate mahali pa kupata mikopo kwa bei nafuu kwa maana ya riba nafuu".


"Tunawaomba Maafisa Maendeleo ya Jamii watimize wajibu wao wa kutembelea vikundi vya wakina mama ili kuwapatia elimu ya kujisajili, Kuendesha shughuli zao, Kupata mikopo ya Halmashauri,  Kupata mikopo kutoka benki kwa wale watakaoweza. Tunawapongeza Wakurugenzi na Maafisa wa Maendeleo ya Jamii ambao tulikuta wanatimiza wajibu wao kikamilifu, kwa mfano, Mkurugenzi wa Maendeleo Halmashauri ya Chunya ambayo inaongozwa na Wanawake (Mkuu wa Wilaya, Mkurugenzi wa Halmashauri, Afisa Maendeleo ya Jamii) ndiyo Halmashauri ya mfano kwa kutenga asilimia kwa wanawake, pia Halmashauri ya Njombe (V) inaongozwa na Mwanamke na ina fanya vizuri ikifuatiwa na Halmashauri ya Mufindi", alisema Daudentia.


Kuhusu Maadili, Gadentia alisema UWT wataendelea kukemea maadili yaliyoporomoka kwa vijana wa kike na wa kiume jambo ambalo ni hatari kwa kizazi kijacho na kuhumiza wazazi na walimu kukemea uvunjaji wa Maadili na hasa mimba za utotoni.


"UWT inashauri kwenye maeneo tunakoishi ambako kuna Kamati mbalimbali kama vile polisi jamii na nyingine, Jamii iongeze Kamati ya za Maadili zitakazosimamia maadili kwa vijana wa kike na wa kiume kwa kila Kata, ambazo zitakuwa na wajumbe wafuatao, Viongozi wa Dini zote, Madiwani wa Kata na Viti Maalum, Wazee na watu wazima wanaoishi ndani ya Kata hizo, Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Kata. Kamati hizo zisimamie kikamilifu zoezi hilo na viongozi waliotajwa hapo juu na ikibidi watakaokiuka wachukuliwe hatua za kinidhamu kama wahalifu wengine", alisema Gaudentia 


Alisema, baada ya kukamilisha ziara hiyo UWT iliandaa Mafunzo ya kuwajengea uwezo na uelewa wa pamoja Viongozi na Watendaji wa UWT wa ngazi ya Wilaya na Mikoa hiyo ya Nyanda za Juu Kusini. Mafunzo hayo yalifanyika tarehe 26 – 27/03/2018 katika Mkoa wa Mbeya na kwamba ziara na mafunzo haya yataendelea kufanyika katika Mikoa yote.

WANANCHI WAJITOLEA KULIMA BARABARA


WAKAZI  WA MTAA WA IBISABAGENI KATA YA IBISABAGENI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA SENGEREMA WAMEAMUA KUJITOLEA KULIMA NA KUFUNGUA BARABARA IKIWA NI KATIKA JUHUDI ZA KUJILETEA MAENDELEA NA KUONDOA KERO ZA MAWASILIANO KATIKA  MTAA HUO

Akizungumza wakati wa zoezi hilo leo lililofanyika mapema asubuhi mwenyekiti wa mtaa wa IBISA BAGENI MH STANNRY KAKERE amesema kuwa kupitia mikutano mbali mbali wameadhimia kulima barabara ili kujiletea maendeleo katika  mtaa wao.

Pamoja na hayo mwenyekiti huyo wamewashauri baadi ya viongozi kusimamia maendeleo katika maeneo yao hasa katika swala la ulinzi na usalama na wananchi na atakayeshindwa  hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.

Kwa upane wawao  wananchi wa kata hiyo wao wamesema kufunguliwa kwa barabara  hizo kutachochea maendeleo yao  na kusaidia kuondoa kero ya kuzunguka umbali mrefu kwenda hospitali teule ya MISSION iliyopo karibu kata jirani ya MISSION.

MGUNDUZI WA TANZANITE AANGUKIWA NA NEEMA YA MAGUFULI.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi kumpatia pesa kiasi cha Tsh. Milioni 100, Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite, mzee Jumanne Ngoma imsaidie katika matibabu ya ugonjwa wake unaomsumbua wa kupooza.

magufuli amesema hayo leo, Aprili 6, 2018 katika eneo la Simanjiro ambako anazindua Ukuta uliojengwa kuzungushiwa Migodi ya Tanzanite, Mirerani ili kuzuia utoroshwaji wa madini hayo.


“Madini haya yalivumbuliwa na mzee Jumanne Ngoma mwaka 1967, na kupeleka sampuli kwa Geologist (mtaalam wa miamba) kwenda kuyapima, pamoja na kutambuliwa na Baba wa Taifa, Mwl Julius Kambarage Nyerere kwenye barua aliyoisani Oktoba 8, 1980 akitambua kazi nzuri ya mzee Ngoma.

“Hata alipoyavumbua hakujua yatakuwa na thamani kubwa kiasi hicho, lakini mzee Ngoma hakufaidika chochote, sasa naambiwa amepooza, nitampatia shilingi milioni 100 zikamsaidie katika matibabu,” alisema Magufuli.

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MPWAPWA.


Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Mohamed Maje kuanzia leo kwa kilichoelezwa kushindwa kutimiza majukumu yake.
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Tamisemi Mussa Iyombe inasema Maje amesababishia hasara serikali ikiwamo kushindwa hata kukusanya mapato ya serikali.

"Hata makusanyo ya mwaka huu hatujui anayapeleka wapi hadi leo amekusanya asilimia 24 tu katika Halmashari ya Kongwa na Mpwapwa licha ya kuwa na vyazo vingi vya mapato.


 Iyombe amesema Mkurugebnzi huyo kwa sasa yupo chini ya uchunguzi.

Thursday, April 5, 2018

KHALIGRAPH JONES AKIRI KIU YAKE KUFANYA COLLABO NA DIAMOND PLATNUMZ


Mwanamuziki namba moja wa Hip Hop toka nchini Kenya Khaligraph Jones amesema kuwa moja kati ya wakali anaowakubali kwenye kiwanda cha muziki barani Afrika ni Mwanamuziki kutoka nchini Tanzania Diamond Platnumz.

Khaligraph anakiri kuwa mafanikio aliyofikia Diamond ni alama tosha ya uwakilishi wa muziki wa Afrika Mashariki, amesema hayo katika mahojiano na Mtangazaji wa kipindi cha Hot Stage cha  93.7 Jembe Fm Mwanza John Jackson (JJ) kinachoruka kila siku za wiki yaani Jumatatu hadi Alhamisi. majira ya saa moja kamili jioni hadi saa tatu usiku. 

RAIS MAGUFULI ASIKITISHWA NA AJALI YA TABORA.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ajali iliyotokea usiku wa jana Mkoani Tabora na kusababisha vifo vya takribani watu 12.

Dkt. Magufuli ameeleza hayo kwenye salamu zake za rambirambi alizozitoa leo Aprili 05, 2018 baada ya kupita siku moja tokea basi la kampuni ya City Boy lililokuwa limebeba abiria kutoka Karagwe Mkoani Kagera kuelekea Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso lililokuwa linatoka Singida kuelekea Igunga.

“Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya vifo vya watu 12 waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyotokea jana usiku katika wilaya ya Igunga mkoani Tabora, nawapa pole wafiwa wote, ndugu, jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu mkubwa. Nalitaka Jeshi la Polisi, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na Wilaya na Mamlaka zote zinazohusika na usalama wa barabarani kujitathmini, na kutafuta majawabu ya kwa nini ajali za barabarani zinaendelea kutokea kwa kusababishwa na uzembe na uvunjaji wa sheria za barabarani?”, amesema Dkt. Magufuli.

Pamoja na kutoa pole kwa wafiwa, Dkt. Magufuli amewataka viongozi wote wanaohusika na usimamizi wa usalama wa barabarani kutafakari kwa nini ajali nyingi zimekuwa zikitokea katika maeneo yaleyale na kutafuta ufumbuzi ili kuepusha madhara ya watu kupoteza maisha, kupata ulemavu wa kudumu na kupoteza mali.

“FEDHA ZA UPANUZI WA VITUO VYA AFYA ZIFANYE ZAIDI YA KAZI ILIYOTARAJIWA”, RC GALLAWA.

 Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akizungumza na mafundi wanaojenga katika kituo cha Afya Isansa Wilaya ya Mbozi, kituo hicho cha Afya kimepokea shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa akizungumza na baadhi ya watendaji na wananchi wa kijiji cha Iyula waliojitokeza katika eneo la ujenzi katika kituo cha Afya cha Iyula Wilaya ya Mbozi, kituo hicho cha Afya kimepokea shilingi milioni 400 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho.
Grace Gwamagobe-Songwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Gallawa amesema atahakikisha anasimamia kwa ukaribu fedha zilizotolewa na serikali Mkoani hapa kwa ajili ya upanuzi wa vituo vya afya ili zifanye kazi zaidi ya ile iliyopangwa awali kutokana na kuongezeka kwa nguvu za wananchi.
Gallawa ameyasema hayo mapema jana wakati wa ziara yake Wilaya ya Mbozi alipokagua maendeleo ya upanuzi wa vituo vya afya vya Isansa kilichopokea milioni 500 na kituo cha Afya cha Iyula Kilichopokea milioni 400, kwa ajili ya ujenzi wa maabara, nyumba ya daktari, chumba cha upasuaji, jengo la mama na mtoto na chumba cha kuhifadhia maiti.
“Fedha hizi lazima zifanye kazi iliyopangwa vizuri na pia tuongeze kazi nyingine ya ziada kutokana na kuwa tumepata nguvu ya wananchi lakini pia mafundi wetu hawa tunaowatumia ni wazawa na wenyeji wa maeneo ya kwetu kwahiyo gharama zao zitatupa unafuu ambao tunatakiwa kuutumia kuongeza kazi nyingine”, amesema Gallawa.
Ameongeza kuwa licha ya upanuzi wa vituo vya afya kuchelewa kuanza bado ana Imani kuwa wataweza kumaliza ndani ya muda uliopangwa kutokana na uchapakazi wa mafundi wazawa wa maeneo hayo.
Gallawa amesema kukamilika upanuzi wa vituo hivyo vya afya kutavifanya vituo hivyo vivutie na hata mgonjwa akifika apate matumaini ya kupona na sio kukatishwa tamaa na hali mbovu ya mazingira.
“Tiba ya kwanza ya mgonjwa akifika kituo cha afya akute mazingira yanavutia na sio majengo mabovu na uchafu hivyo vitamfanya akate tamaa ya kupata matibabu sahihi, tukimaliza ujenzi wa hayo majengo tutahakikisha tunapaka rangi paa za majengo yote zifanane ili vituo vyetu vya afya vivutie”, amefafanua Gallawa.
Aidha Gallawa amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mbozi Lauteri Kanoni kuhakikisha anaweka mfumo wa maji safi katika vituo hivyo hasa mfumo wa kuvuna maji ya mvua ili vituo vikikamilika maji yawepo kwa ajili ya matumizi.
Naye Mkazi wa kijiji cha Isansa Wilaya ya Mbozi Bi Stela Mkeya ameonyeshwa kufurahishwa na upanuzi wa kituo cha Afya Isansa huku akieleza baadhi ya kero walizokuwa wakizipata awali.
“Tunaishukuru sana serikali ya Magufuli kwakweli wametusaidia, tulikuwa tunapata shida kufuata huduma za upasuaji wa akina mama wajawazito huko hospitali ya Wilaya iliyopo Vwawa lakini pia hapa kwenye kituo cha afya mzazi akijifungua hata mazingira ya kwenda kujisafisha vizuri kama vile mabafu yakiwa hayatoshi kabisa”, ameeleza Bi Mkeya.
Kwa upande wao mafundi waliokabidhiwa kazi ya upanuzi wa vituo hivyo vya Afya wameonyesha ari ya kufanya kazi hiyo kwa ufanisi na haraka huku wakimuomba Mkuu wa Mkoa Chiku Gallawa awasaidie upatikanaji wa taa ili waweze kufanya kazi mchana na usiku naye Mkuu wa Mkoa amekubaliana na mapendekezo hayo.

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YAZINDUA UGAWAJI ENDELEVU WA VYANDARUA VYENYE DAWA YA MUDA MREFU.

Na Ferdinand Shayo,Arusha .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amekanusha vikali maonyesho ya Jeshi la polisi yanayoambatana na mazoezi  ya jeshi hilo yanayoendelea  katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid vilivyoko jijini Arusha  kuhusishwa na maandalizi ya kukabiliana na maandamano yanayohamasishwa kwenye mitandao na kudaiwa  kufanyika april 26.

Mkumbo amesema kuwa  maonyesho hayo ni ya kawaida na jeshi hilo limekua likijiweka imara kwa ajili ya kulinda raia na  mali zao na taifa kwa ujumla na si maandamano ambayo ni ya kusadikika .

Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake amesema kuwa maonyesho hayo yatafanyika April 7 baada ya kuzindua nyumba za kuishi za jeshi la polisi zitakazozinduliwa na Raisi John Pombe Magufuli.

Aidha amewakaribisha wananchi wa Jiji la Arusha kujitokeza kwa wingi kuona maonyesho ya kazi za jeshi hilo lenye jukumu la kulinda raia na mali zao.

Kamanda amesema kuwa licha ya uzinduzi wa nyumba hizo wanatarajia kuzindua kituo cha utalii na diplomasia ambacho kitasaidia shughuli za utali na kuchochea ari ya watalii kutembelea mkoa wa Arusha wenye vivutio vingi.

Alisema kuwa mpaka sasa maandalizi yako vizuri ya kumpokea Raisi na wanatarajia hakutakua na msongamano wa magari kwani shughuli za kila siku zitaendelea kama kawaida.

Hata hivyo ametoa onyo kali kwa wanaoharibu miundombinu ya barabara ikiwemo alama za barabarani na kusababisha adha kwa watumiaji wa barabara kwani jeshi hilo halitawavumilia  na hatua kali zitachukuliwa .

Wednesday, April 4, 2018

RONALDO AIPAISHA TENA MADRID YAIADHIBU JUVE NYUMBANI KWAO 0-3 UCL 2018


Juventus wamepoteza mchezo wa kwanza katika uwanja wao wa nyumbani Allianz katika mashindano ya Ulaya baada ya miaka mitano.

Mashabiki wa Juve waliokuwa wakimzomea Ronaldo awali katika mchezo walilazimika kuanza kumpigia makofi na kumshangilia mara baada ya goli la pili, naye Ronaldo alishangilia goli lake huku akiwashukuru.

Juve's misery was further compounded by Paulo Dybala's red card and Marcelo bundling in a third, with Ronaldo later hitting the crossbar – as Toni Kroos had done in the opening period – and spurning two more opportunities to register yet another hat-trick.

The headlines were already his, though, his exploits leaving Juve with a mountain to climb in the Spanish capital next week.

Ronaldo on his amazing overhead kick

Key player: Cristiano Ronaldo (Real Madrid)
Who else? Two more goals, more sheer brilliance, another match-winning performance. Ronaldo's most memorable moments are plentiful, but that bicycle kick is right up there. The records keep on coming.

Tuesday, April 3, 2018

MBUNGE ROSE TWEVE AMBANA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA JUU YA FIDIA ZA MAJERUHI WA AJALI ZA BARABARANI Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiuliza swali la nyongeza kwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba juu ya idadi ya vifo na majeruhi wa ajali barabani na hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo ili kupunguza ajali hizo 
 Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve akiwa makini kuandika hoja ambazo anajibiwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba.


Na Fredy Mgunda,Dodoma.

Mbunge wa viti maalum mkoa wa iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve amelibana jeshi la polisi nchini kupitia kikosi cha usalama barabani kwa kutaka kujua idadi ya vifo na majeruhi wa ajali barabani na hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo ili kupunguza ajali hizo

Mbunge Rose Tweve mapema hii leo bungeni aliuliza swali kwa wizara ya mambo ya ndani ya nchi kwa kutaka kujua idadi ya vifo na majeruhi wa ajali barabani na hatua zinazochukuliwa na jeshi hilo.

Akijibu swali la mbunge Rose Twelve Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mh. Mwigulu Nchemba alisema kuwa jeshi la polisi nchini kupitia kikosi cha usalama barabani limeweza kupunguza ajali za barabarani kwa asilimia 43 kwa mwaka 2017

Mwigulu alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2016-2017 kulitokea ajali 9856 ambazo zilisababisha vifo 3256 na majeruhi 2128 ambapo kwa mwaka 2017 kulitokea ajali 5310 na kusababisha vifo 2533 na majeruhi 5355.

Waziri Mwigulu ameongeza kuwa kwa kipindi cha januari hadi februari 2018 kumetokea ajali 769 na kusababisha vifo 334 na majeruhi 698.

Akiuliza swali la nyongeza mbunge Rose Tweve alimtaka waziri kutoa idadi ya wahanga wa ajali waliolipwa fidia na mwaka 2009 bunge ilipitisha sheria ndogo namba 10 ya bima ya kuwalinda wahanga wa ajali hizo,sasa mheshimu waziri hawa wenzetu wa TIRA wanaonyesha wanamapungufu mengi na watanzania wamekuwa wanahanga wakubwa kwenye swala hilo na kwanini tusianzishe idara maalum ambayo itakuwa inatoa elimu kwa wahanga wa ajali pindi inapotekea na kujua nini cha kufanya.

Akijibia swali la Nyongeza la Mbunge Rose Tweve la kuhusu idadi ya wahanga wa ajali waliolipwa fidia, Waziri Nchemba amebainisha kuwa katika kipindi cha mwaka 2016-2018 jumla ya wahanga wa ajali 1583 wakilipwa fidia takribani Bilioni  7 kutoka makampuni mbalimbali ya bima.

Katika hatua nyingine Mwigulu Nchemba amekiri kuwepo kwa matukio ya ajali 1500 yanayosababishwa na uzembe wa madereva huku serikali ikipanga kuwachukulia hatua madereva wenye tabia hizo.

“Ni kweli serikali itahakikisha inawachukulia hatua madereva wazembe ikiwemo kuwanyang’anya leseni ili kupunguza idadi ya madereva ambao wamekuwa wakisababisha ajali zinazoweza kuepkukika” alisema Mwigulu nchemba.

FAINI YAMUEPUSHA KUTUPWA JELA MASOGANGE

Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ ameachiwa huru katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mara baada ya kulipa faini ya Shilingi Milioni 1.5.

Masogange alihukumiwa miaka 3 jela ama alipe faini ya Milioni 1.5 baada ya kutiwa hatiani kwa makosa ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.

MHE BITEKO AANZA KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU LA KUKOMESHA UTORO MASHULENI, ACHANGIA MATOFALI 10,000 UJENZI WA MAABARA

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua majengo ya maabara za shule ya sekondari ya Kata ya Busonzo katika Kijiji cha Nampalahala akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe, Leo 2 Aprili 2018. Picha Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua nyumba ya walimu katika shule ya sekondari ya Kata ya Busonzo katika Kijiji cha Nampalahala, Leo 2 Aprili 2018. 
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Nampalahala, Kata ya Busonzo wakifatilia mkutano wa hadhara ukiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe, Leo 2 Aprili 2018.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Nampalahala, Kata ya Busonzo wakati akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe, Leo 2 Aprili 2018.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua ujenzi wa nyumba za madaktari wa kituo cha afya cha Uyovu akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe, Leo 2 Aprili 2018.

Na Mathias Canal, Geita

Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko Leo 2 Aprili 2018 amechangia matofali 10,000  kwa ajili ya ukamilishaji Wa vyumba vya maabara ili kurahisisha uanzisha Wa shule ya sekondari Kata ya Busonzo Wilayani Bukombe.

Shule ya sekondari Busonzo inahitaji kukamilisha maabara tatu ili iweze kufunguliwa ambapo serikali imetoa milioni 40 kwa ajili ya kazi hiyo.

Mhe Biteko amechangia matofali hayo Mara baada ya maagizo ya Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa aliyoyatoa wakati Wa dhifa ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2018 katika uwanja wa Magogo mkoani Geita kwa kuwataka viongozi wa mikoa ya Tabora, Geita, Mtwara na Shinyanga ambayo inaongoza kwa utoro wa wanafunzi kwa shule za msingi na kwa sekondari wahamasishe umuhimu wa elimu na mahudhurio endelevu shuleni.

"Mkoa wetu tumepata aibu kubwa kwa kuwa namba mbili kwa utoro kati ya mikoa yote nchini, utoro huu hapa wilayani kwetu unachangiwa na umbali wa kwenda shuleni, hapa Busonzo watoto wetu wanasoma Runzewe ambapo ni mbali sana. Umbali huo unachangia utoro" alisisitiza Mhe. Biteko

Katika sherehe hizo zilizonakshiwa na Kaulimbiu ya mbio za mwenge kwa mwaka huu ambayo ni ‘Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu.’ Waziri Mkuu alisema kuwa utoro wa wanafunzi wa Sekondari ni mkubwa zaidi kwa Mikoa husika kuliko shule za msingi. 

Mara baada ya uzinduzi Wa Mwenge huo wa Uhuru kabla ya kuelekea Mjini Dodoma kwa ajili ya shughuli za Bunge zinazotarajiwa kuanza kesho 3 Aprili 2018 Mhe Doto Biteko amezuru Kijiji cha Nampalahala kilichopo Kata ya Busonzo na kujionea jinsi ujenzi Wa maabara unavyoendelea.

Mara baada ya kubaini kuwa kuna upungufu wa matofali 10,000 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo, Naibu Waziri huyo amechagiza ujenzi huo kwa kuchangia gharama za ununuzi wa matofali hayo ili ujenzi huo ukamilike kwa wakati.

"Mheshimiwa Waziri Mkuu ameshatoa maelekezo ya kukomesha utoro naomba tukimbie kulitekeleza hilo na ninaomba wazazi tuhakikishe watoto wote wanakuwa shuleni ni aibu mno sisi kuwa vinara wa utoro". Aliongeza Mhe. Mbunge Na Naibu Waziri huyo.

Mhe Biteko amewaeleza wananchi hao jinsi ambavyo utoro kwa shule za sekondari Mkoani Geita umekithiri jambo ambalo limepelekea Mkoa huo kushika nafasi ya pili kwa utoro Kitaifa kwa asilimia 8.1, ambapo Mtwara imekuwa nafasi ya tatu kwa asilimia 6.4, Shinyanga asilimia 6.3 huku nafasi ya kwanza ikishikiliwa na Mkoa Wa Tabora kwa asilimia 9.7 

Aidha, Mhe Biteko ameonyesha kusikitishwa na takwimu za Mkoa Wa Geita kushika nafasi ya pili pia katika kwa utoro kwa shule za msingi kwa kwa asilimia 3.1 nyuma ya Mkoa Wa Rukwa unaoongoza kwa asilimia 3.2

Aliongeza kuwa anatamani kuona  Wilaya ya Bukombe inahakikisha inafikia viwango bora vya elimu. Serikali ya awamu ya tano inyoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, imedhamiria kuboresha elimu katika ngazi zote nchini, kuanzia Elimu ya Awali hadi Elimu ya Juu hivyo wananchi wanapaswa kuitumia fursa hiyo kwa maendeleo ya wilaya hiyo na Taifa kwa ujumla aliwaomba pia wananchi wa  kata ya Busonzo kumuombea Rais Magufuli na kuunga mkono juhudi za serikali.