Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, Mhe. Robert Vicent ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo. |
Mkoani Mwanza Mkutano
wa kujadili mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania 2015 – 2020 umefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Mkuu
wa mkoa wa Mwanza aliopo wilayani Nyamagana ukijumuisha wadau wa Mahakama
kutoka wilaya mbili za Ilemela na Nyamagana pamoja na Mahakama ya Hakimu mkazi
mkoa wa Mwanza.
Pia Mkutano huo umelenga kupitia
mpango mkakati huo, kuujadili utekelezaji wake mpaka sasa, kubaini changamoto,
mafanikio lakini pia na kuona nini kifanyike kwaajili ya kuendeleza na
kutekeleza utoaji maamuzi ya haki na kwa umakini zaidi kwa manufaa ya wadau
wanaohudumiwa.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya
Mwanza, Mhe. Robert Vicent ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mkutano huo amewaasa washiriki
hao kufanya kazi kwa weredi, kwa kuzingatia uwajibikaji, maadili, nidhamu huku
wakitambua kuwa Serikali imewapa dhamana kubwa watumishi ngazi mbalimbali za
mahakama katika kuhakikisha kuwa haki
inatendeka katika utoaji maamuzi.
Yote haya yamefanyika yakilenga dira
ya Mahakama inayosema HAKI SAWA KWA WOTE NA KWA WAKATI.
Kwa mujibu wa Mhe. Robert, ni
matarajio yake kwamba kila mdau wa Sheria atashiriki ipasavyo katika kutekeleza
mpango uliowekwa kwenye mpango mkakati wa Mahakama kwa kuzingatia nguzo tatu
muhimu za mpango mkakati huo ambazo amezitaja kuwa ni pamoja na:-
1.UTAWALA BORA UWAJIBIKAJI NA
USIMAMIZI WA RASILIMALI.
2.UPATIKANAJI NA UTOAJI HAKI KWA
WAKATI.
3.KUIMARISHA IMANI YA JAMII NA
USHIRIKISHWAJI WA WADAU KATIKA SHUGHULI ZA MAHAKAMA.
Baada ya Mkutano na Majadiliano yake
kila mmoja atatekeleza mpango huo kwa
uadilifu, uwajibikaji, uwazi pamoja na kuzingatia weredi.
Mkutano huu wa mafunzo umeandaliwa na Ofisi ya hakimu Mkazi mfawidhi mkoa wa Mwanza ambapo Watoa maada au wawezeshaji wakiwa ni Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi mkoa wa Mwanza Mh Wilbert M.Chuma na Mtendaji wa Mahakama kuu Moses Minga.
"Mafunzo hayo ni endelevu na tunatarajia kuendesha pia mafunzo hayo kwa wilaya zilizobaki ndani ya mkoa wa Mwanza kama vile Magu , Sengerema , Misungwi , Ngudu Kwimba na Ukerewe lengo likiwa ni kuhakikisha kila mtumishi anauishi mpango mkakati husika" Alisema Mhe. Chuma.
Jumla ya washiriki 68 wamehudhuria
Mkutano huo ambao ni Mahakimu, Makarani, Wahudumu wa Mahakama pamoja na Madereva.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.