|
Meneja bia chapa Serengeti Primium Lager, Rugambo Rodney akiongea kwa njia ya simu na mshindi wa Limo bajaj na fedha taslim Tsh 100,000/= katika Shindano la Tutoke na Serengeti linaloendeshwa na kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kushirikiana na BPESA kushoto ni msimamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Bw. Bakari Majjid , ambapo Godfrey Longino Mpiruka mkazi wa Dar ameibuka na ushindi mnono. Droo hiyo ilifanyika makao makuu ya Serengeti-Chang’ombe jijini Dar es Salaam. |
|
Meneja bia chapa Serengeti Primium Lager, Rugambo Rodney akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kuchezesha droo ya Shindano la Tutoke na Serengeti linaloendeshwa na kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kushirikiana na BPESA. Kushoto ni msimamizi toka bodi ya michezo ya kubahatisha, Bw. Bakari Majjid na kulia ni Meneja Vipoozeo na mwonekano, Baraka Mandara, ambapo Bw.Godfrey Longino Mpiruka mkazi wa Bunyokwa, Segerea Dar es salaam ameibuka mshindi wa Limo Bajaj yenye uwezo wa kubeba watu 7 na fedha taslim Tsh. 100,000/=. Droo hiyo ilifanyika makao makuu ya Serengeti-Chang’ombe jijini Dar es Salaam. |
|
Meneja bia chapa Serengeti Primium Lager, Rugambo Rodney akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa kuchezesha droo ya Shindano la Tutoke na Serengeti linaloendeshwa na kampuni ya Bia ya Serengeti kwa kushirikiana na BPESA |
RE:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MKAZI WA
DAR AIBUKA NA USHINDI MNONO KWENYE KAMPENI YA TUTOKE NA SERENGETI
7th Dec 2015, Dar-Es-Salaam
Mwaka 2015 umeanza vizuri kwa Bwana Godfrey Longino Mpiruka baada ya kutangazwa mshindi wa nne wa bajaji
mpya aina ya Limo sambamba na fedha taslim Tsh. 100,000/= zinazotolewa kila
wiki katika kampeni inayoendelea ya “Tutoke na Serengeti” .
Godfrey mwenye
umri wa miaka 47 na mkazi wa Bunyokwa Segerea-Dar es salaam ameibuka na ushindi
huo mnono baada ya kuwashinda washiriki kutoka mikoa ya Moshi na Morogoro ambayo
mpaka sasa imeongoza kwa kutoa washindi
mbalimbali katika kampeni hii ya miezi mitatu inayodhaminiwa na kampuni ya bia
ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha Serengeti Premium lager kwa
kushirikiana na BPESA.
“Wakati nashiriki
katika kampeni hii, lengo langu lilikuwa ni kushinda shilingi 100,000/= bila
kujua kwamba ushiriki wangu ungenipelekea kushinda pia Limo Bajaj mpya..ninashukuru
sana Serengeti” alisema Bw.Godfrey kwa njia ya simu mara baada ya kuibuka
mshindi wa nne wa Limo Bajaj. Godfrey aliongeza kwamba, Bajaji hiyo yenye uwezo
wa kubeba watu 7 ambayo imeigharimu SBL kiasi cha Tsh. 9,000,000/= itamsaidia
kwa kiasi kikubwa kuongeza kipato katika maisha yake na pia kukabiliana na
changamoto mbalimbali za kifedha ambazo amekua akikabiliana nazo.
Baadhi ya washindi
waliofaidika na kampeni hii na kupata zawadi zao ni pamoja na: - Bi. Rukia
Almasi ambaye ni mama wa nyumbani na mkazi wa Kihonda aliyeshinda bajaji ya
kwanza, wakati Peter Emmanuel, dereva wa
bodaboda aliibuka mshindi wa pili, na Isaack
Edward Maro mwalimu wa shule ya awali kutoka mkoa wa Kilimanjaro aliibuka
mshindi wa tatu. Kwa upande mwingine, Hassan Mfaume na Deogratias Masenga kwa
pamoja walishinda safari ya siku mbili na wenza wao ya kutembelea mbuga ya
wanyama ya Serengeti National park na zaidi ya washindi saba walijinyakulia
kitita cha shilingi 100,000/= kila mmoja
zilizokuwa zikitolewa kila wiki baada ya droo.
Akiongea na waandishi
wa habari Bw. Rugambo Rodney, Meneja wa bia chapa Serengeti Premium Lager
alisema….“ Promosheni ya Tutoke na Serengeti bado inaendelea na kama ilivyo
ada, SBL kwa kushirikiana na BPESA wanaendelea kuwazawadia wateja wao zawadi
mbalimbali zikiwemo Limo Bajaj, safari za bure za kutembelea mbuga za wanyama, fedha za papo
kwa hapo kiasi cha shilingi 100,000/=
kila wiki, punguzo la bei la shilingi 300/= katika bei halisi ya bia aina ya
Serengeti, pamoja na bia za bure ambazo zinatolewa nchi nzima.” Rodney aliendelea
kueleza kuwa promosheni imeendelea kufanya vizuri tangu kuanza kwake kwa muda
wa miezi miwili iliyopita na hivyo basi uongozi umeona ni vema kuongeza mwezi
mmoja wa promosheni ili wateja waendelee kujinyakulia zawadi mbalimbali.
Promosheni hii ya nchi
nzima ilizinduliwa na SBL pamoja na B-Pesa miezi miwili iliyopita ikiwa na
lengo la kuwazawadia wateja wake katika kila droo itakayokuwa ikifanywa kila wiki
na SBL chini ya uangalizi wa bodi ya michezo ya bahati nasibu Tanzania.
Ili kushiriki katika promosheni hii, mteja anatakiwa
awe na umri wa zaidi ya miaka 18, na anunue bia ya Serengeti Premium Lager na
kuangalia chini ya kizibo ambapo atakuta namba zinazotakiwa kutumwa kwa njia ya SMS kwenda 15317. Kadiri mteja
anavyoshiriki zaidi ndivyo anavyojiweka katika nafasi nzuri ya kushinda zaidi.