MAENEO YA KATIKATI YA JIJI LA MWANZA KUNA'HAPPEN ILE MBAYA YAANI NI NOuMAA! UKIKOSA STONE CLUB UJUE UMEPISHANA NA RAHA! @MUZIKI SAFI! @ENEO SAFI! @WATU SAFI! #####UKIJICHANGANYA PALE KATI INALETA MAANA ZAIDI.######
MH. ANNA MAKINDA ambaye alikuwa ni Naibu Spika wa bunge lililopita na pia ni mbunge wa jimbo la Njombe kusini mkoani Iringa,ameshinda nafasi ya kugombea kiti cha Uspika kupitia CCM baada ya kujizolea idadi ya kura 265 na kumbwaga mpinzani wake Mabere Marando (CHADEMA) ambaye amejinyakulia kura 55 katika uchaguzi huo uliofanyika leo asubuhi mjini Dodoma.
IDADI YA KURA ZILIZOPIGWA KATIKA UCHAGUZI HUO ZILIKUWA 307, ZILIZOHZRIBIKA NI 9. MH. ANNA MAKINDA ANACHUKUWA NAFASI YA KITI CHA SPIKA ALIYEPITA MH.SAMWEL SITTA.
HIVI SASA SPIKA HUYO MPYA ANASIMAMIA ZOEZI LA KUAPA KWA WABUNGE WAPYA WA BUNGE HILO LA 10. BUNGE LA TISA LILIMALIZA MUDA WAKE JUAI 16, 2010. ZOEZI LA KUAPA WABUNGE WAPYA LINATARAJIWA KUCHUKUA SIKU ZAIDI YA 2.
BI. ANNA MAKINDA AME - CHAGULIWA NA WAJUMBE WA CHAMA CHA MAPINDUZI KWA KURA 211 KWA AJILI YA KUWANIA USPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
WALIOBWAGWA KATIKA KINYANG'ANYIRO HICHO CHA AKINA MAMA WATATU WALIOTEULIWA NA KAMATI KUU YA CCM HAPO JANA KUWANIA KITI HICHO NI BI KATE KAMBA ALIYEPATA KURA 15 NA BI ANNA ABDALAH ALIYEPATA KURA 14.
KINYANG'ANYIRO HICHO KINATIA TAMATI KESHO KWA ANNA MAKINDA (CCM) KUPAMBANA NA MABERE MARANDO (CHADEMA).
MLINDA MLANGO WA TIMU YA TAIFA YA TOGO KODJOVI OBILALE ATAPATIWA DOLA 100,000 KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA DUNIANI- FIFA BAADA YA KUJERUHIWA VIBAYA KWA RISASI KABLA YA KUANZA FAINALI ZA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA NCHINI ANGOLA MWEZI WA JANUARY.KODJOVO OBILALE. Rais wa Fifa Sepp Blatter, alimwambia Obilale mwezi wa Septemba kwamba malipo ya dola 25,000 zitatolewa kutoka mfuko wa Fifa wa misaada ya kibinadamu.
Hata hivyo Shirikisho hilo la soka Duniani kwa sasa limeamua kuongeza kiwango hicho cha pesa.
Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 25 alifanyiwa upasuaji kutokana na majeraha ya risasi alizopigwa mgongoni na tumboni kufuatia shambulio hilo.
Shambulio hilo lililotokea katika jimbo la Cabinda nchini Angola, lilisababisha watu wawili waliokuwemo katika kikosi cha Togo kupoteza maisha pamoja na dereva wa basi lililokuwa limewachukua.
Obilale bado hawezi kutembea ikiwa ni miezi minane tangu lilipotokea shambulio la risasi lililofanywa na waasi wanaotaka kujitenga kwa jimbo la Cabinda na bado anaendelea kutibiwa nchini Ufaransa.
Togo ilijitoa katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Angola baada ya shambulio hilo na ilifungiwa na Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf) kwa miaka minne kushiriki mashindano hayo.
Hata hivyo Fifa ilitengua adhabu hiyo.
Akiwa amekatishwa tamaa kwa kukosa msaada kutoka Caf na Angola ambao waliandaa mashindano hayo, Obilale alimwandikia barua Rais wa Fifa Blatter mwezi wa Agosti akimuomba msaada.
Blatter akamuahidi msaada kutoka mfuko huo wa Fifa wa misaada ya kijamii, pamoja na kumueleza Fifa haina dhamana na mashambulio ya Cabinda.
Obilale alieleza hadhari kukatishwa tamaa kwa kukosa msaada wa Caf na maafisa wa Angola baada ya shambulio hilo ambalo limekatisha matumaini yake ya kucheza soka.
Mlinda mlango huyo aliyekuwa akichezea klabu moja ya daraja la chini huko Ufaransa, hawezi kusogeza mguu wake wa kuume chini ya goti, pia mguu wake umekufa ganzi, lakini ana matumaini ataweza kutembea siku za baadae.
Kwa sasa anatumia kiti maalum cha kutembelea kuzunguka hapa na pale na amesema angekuwa na jina kubwa katika soka, basi matibabu yake yangekuwa tofauti na anayopatiwa sasa..
SIKU MBILI TU BAADA YA MBUNGE WA BARIADI MAGHARIBI KUMTUHUMU VIKALI SPIKA ANAYEMALIZA MUDA WAKE, SAMWEL SITTA KUWA NI KIONGOZI ASIYEFAA NAYE AKIWA TAYARI KESHA CHUKUWA FOMU KUWANIA KITI HICHO CHA USPIKA NA NDANI YAKE AKITOA AHADI KIBAO ZILIZOZUA MASWALI MENGI KWA WADADISI NA WACHAMBUZI WA MASUALA YA SIASA. MZIGO KABAAA! HATIMAYE KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI KIMETEUA MAJINA MATATU AMBAPO HUMO YALE MAJINA YALIYOKUWA YAYATOKI MIDOMONI MWA WATU LIKIWAMO HILO LA MH. CHENGE YAMETUPILIWA MBALI (USWAHILINI TWASEMA TUPA KAPUNI). HIVYO MAJINA YALIYOPITA NI KAMA KAMA IFUATAVYOMH.ANNA ABDALAH,
MH.KATE KAMBA
NA MH.ANNA MAKINDA.
NAO WADADISI WA MAMBO WALIOKO MAENEO YA KARIBU NA SHUGHULI HIYO INAPOFANYIKA WANADAI KUWA KUANGUKA KWA BWANA SAMUEL SITTA NI KAMPENI ZA BAADHI YA VIGOGO KADHAA WA CHAMA HICHO AKIWEMO KATIBU MKUU BW. YUSUF MAKAMBA, ANAYEDAIWA KUWA ALIFANYA KAMPENI ZA CHINI CHINI KUMWANGUSHA BW. SITTA.
WAKATI VIGOGO HAO WAKIDAIWA KUSHIRIKI KUMWANGUSHA BW. SITTA, BAADHI YA WABUNGE AMBAO WALIKUWA WAKIAFIKI UTENDAJI WA SPIKA HUYO ALIYEMALIZA MUDA WAKE WAMEANZA KUJITENGA, NAKUAHIDI A, B, C, D MPAKA KIELEWEKE KATIKA SIKU YA USHINDI IJUMAA HIYO KESHO AMBAPO VILEVILE MWANASHERIA MAARUFU NCHINI NA MUASISI WA SIASA ZA VYAMA VINGI NCHINI, MABERE MARANDO, AMEJITOSA KUWANIA KITI HICHO KUPITIA CHADEMA.
ZOEZI LA UCHUNGUZI WA AFYA YA MACHO NA UPASUAJI WA MACHO KWA WATOTO MIKOA YA KANDA YA ZIWA NA MAGHARIBI UMEENDELEA TENA LEO KATIKA HOSPITALI YA SEKOU TOURE JIJINI MWANZA.
HOSPITALI YA MKOA WA MWANZA SEKOU TOURE.
UPASUAJI HUO UNAOFADHILIWA NA KAMPUNI YA MTANDAO WA SIMU NCHINI TIGO UMEFANYIKA KWA AWAMU YA PILI LEO UKIWASHIRIKISHA MADAKTARI BINGWA KUTOKA CCBRT KWA KUSHIRIKIANA NA MADAKTARI WA HOSPITALI YA SEKOU TOURE MKOA WA MWANZA, UMEONEKANA KUHITAJI MUDA ZAIDI KWANI IDADI KUBWA YA WATOTO WAKIWA NA WAZAZI WAO WAMEONEKANA KUENDELEA KUMIMINIKA HOSPITALINI HAPO TENA WENGINE KUTOKA MBALI WAKIWA NA MATATIZO YA MTOTO WA JICHO NA MAGONJWA MENGINE YA MACHO.
AIDHA MPANGO HUO ULIOANZA JANA TAREHE 8 NA KUPANGWA KUHITIMISHWA LEO TAREHE 9 NOV 2010 UKIWAHUSISHA WATOTO WA CHINI YA MIAKA 16 UMEONEKANA KUWAVUTA PIA WATU WENYE UMRI ZAIDI YA UMRI ULIOTAJWA HALI INAYOPELEKEA KUWAPA CHANGAMOTO WAHUSIKA WA MPANGO HUO KUFIKIRIA TENA ZAIDI JUU YA MATIBABU AWAMU NYINGINE KWA WAKAZI WA KANDA YA ZIWA NA MIKOA YA MAGHARIBI.
WANANCHI WAKIWA WAMEJIPUMZISHA KUSUBIRI HUDUMA.
TIGO IMEAMUA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA CCBRT ILI KUONGEZA UGUNDUZI WA TATIZO LA MTOTO WA JICHO KWA WATOTO NA PIA KUFADHILI MAFUNZO YA WIKI MBILI YA KOZI YA HUDUMA ZA UZAZI KWA WAKUNGA 10, IKIWEMO PIA NA UFADHILI WAO WA KLINIKI ZA MACHO AMBAZO HUTOA HUDUMA ZA UCHUNGUZI NA TIBA YA MATATIZO YA MACHO KWA WATOTO HASA TATIZO LA MTOTO WA JICHO.
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Thomas Kashililah akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mpangilio mzima wa shughuli za bunge katika mkutano wa kwanza wa Bunge Utakaoanza Tarehe 8-17 Novemba 2010 mjini Dodoma.kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha sheria anaitwa Oscar Mtenda.
Dk Dr. Thomas Kashililah amesema kwamba leo tarehe 8-11-2010 amepoka barua rasmi kutoka wa Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Jakaya Kikwete akilitisha kikao cha bunge la jamhuri la Muungano wa Tanzania ambapo wabunge wataanza kuelekea Mkoani Ddodoma tayari kabisa kuanza kikao kipya cha bunge kwanzia Tarehe 9-11-2010 na kazi ya kuanza kusajili wabunge wateule itaanza rasmi mpaka tarehe 10-11-2010
Na siku ya alhamisi kutafanyika mikutano ya kamati za vyama vya siasa kupokea majina ya wagombea uspika wa bunge la jamhuri la muungano wa Tanzania na siku ya ijumaa tareeh Tarehe 12-11-2010 utaanza mkutano wa kwanza wa bunge la jamhuri la muungano wa Tanzania na kusomwa Tangazo la Rais Jakaya kikwete kuliita bunge na kufanya uchaguzi wa Spika na baada ya kuchaguliwa spika atakula kiapo ambapo wabunge nao wataanza kuapishwa rasmi Jumamosi Tarehe 13-11-2010 na 15-11-2010 hadi jumanne ya 16-11--2010 asubuhi kikifatiwa na tukio la kuthibitishwa kwa jina la Waziri Mkuu na Waziri Mkuu huyo kutoa Neno la Shukrani na Kumalizia na Uchaguzi wa Naibu Spika.
Tarehe 17-11-2010 Waziri Mkuu ataapishwa katika ikulu ya chamwino saa nne na saa kumi jioni ni tukio la Rais Jakaya Kikwete kulihutubia Bunge katika Ukumbi wa Bunge na Baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza kulihutubia Bunge Waziri Mkuu atatoa Neno la Shukrani na kutoa hoja na kuahirisha Bunge.
MAAFISA WA SERIKALI YA KENYA WAMESEMA ASKARI POLISI ALIYEHAMAKI AMEWAPIGA RISASI NA KUWAUWA WATU KUMI. MKUU WA JESHI LA POLISI WA MJI WA SIAKAGO, MARCUS OCHOLE AMESEMA MAAFISA WA POLISI WANACHUNGUZA TAARIFA ZA MAUAJI HAYO YALIYOTOKEA USIKU WA KUAMKIA JUMAPILI KATIKA MJI HUO, KASKAZINI MASHARIKI MWA NAIROBI.
MWANADISHI WA HABARI KATIKA ENEO LA HILO TUKIO AMESEMA ASKARI HUYO ALIFYATUA RISASI HOLELA KATIKA BAA TATU TOFAUTI NA KUUWA WATU WAWILI KATIKA BAA MBILI NA WENGINE WANANE KATIKA BAA YA TATU.
NYAGA MANUNGA JAMAA AMBAYE BINTI YAKE NI MOJA KATI YA WALIOUAWA KWENYE TUKIO HILO ANASEMA TUKIO HILO LIMETOKEA KARIBU KABISA NA KITUO HICHO CHA POLISI NA KUONGEZA KWA KUSEMA KUWA "HAPA SIAKAGO HAKUANA KABISA ULINZI, MTU ANAWEZA KUWATWANGA RISASI WATU HATA 20 HADI 30 BILA KUCHUKULIWA HATUA NA JESHI LA POLISI".
TAARIFA ZAIDI ZINAENDELEA KUSEMA KUWA MAMIA YA WATU WALIFANYA MAANDAMANO NJE YA KITUO HICHO CHA POLISI MJINI SIAKAGO, KULISHUTUMU JESHI HILO KWA KUSHINDWA KUCHUKUA HATUA ZOZOTE NA KULIACHA TUKIO HILO LIKAFANYIKA MITA CHACHE TOKA KITUONI HAPO.
MWASITI FROM TANZANIA. November 8th 2010 Malaria No More are holding their annual Benefit in New York where stakeholders, supporters and investors of Malaria No More come together to celebrate their achievements thus far and motivate further contributions to the fight against malaria.
YOUSSOU N'DOUR FROM SENEGAL. Mwasiti Almas is invited to the Benefit and perform alongside Senegal Ambassador Youssou N’Dour. This is through recognition of her dedication and hard work and commends her for her efforts in the fight against malaria in Tanzania.
As a great contributor to the music and entertainment industry and a passionate advocate of Tanzanian humanitarian causes, Malaria No More are truly honored to have Mwasiti Almas serve as one of the first Good Will Ambassadors for the Zinduka-malaria haikubaliki campaign in Tanzania.
It is a blessing to be born with talent and a true gift when people appreciate her art. These good fortunes provide her with an amazing advantage that many others do not have – to speak and be heard, to inform and see results, to be a leader who can inspire 44 million people.
SI WAWILI TENA BALI NI MWILI MMOJA, HILO ANDIKO LIMEJIDHIHIRISHA TENA NA SAFARI HII NI KWA VIJANA WAWILI JORAM NGAIZA NA GRACE MTONGOLE AMBAO WAMEFUNGA PINGU ZA MAISHA MWISHONI MWA WIKI KATIKA KANISA LA KIKATOLIKI NYAKAHOJA MJINI MWANZA.
BWANA HARUSI AKIMLISHA KEKI BI HARUSI NDANI YA SHEREHE SAFI YA KUWAPONGEZA ILIYOFANYIKA JIONI YA SIKU HIYO HIYO YA NDOA PALE YATCH CLUB.
NI MGENI GANI WA KWANZA UNGEPENDA AWE MGENI WA KWANZA KUTEMBELEA NYUMBA YENU? JORAM AKAMCHAGUA BINTI HUYU MDOGO. WATU WAKAGONGANISHA VIGANJA PWAAH! PWAAH! PWAAaa!
HATUA ZA MINATO KUELEKEA KWENYE MENUz. PLIZ UTANISAMEHE MISOSI SINTOKUONYESHA USIJE JILAUMU KWANINI HUKUPATA MWALIKO.
SI MCHEZOo!
HAPA JEH!
BURUDANI PALE KATI WOW! THE WACO J. FROM UGANDA.
MARA ZOTE KATIKA FAMILIA FURAHA YA KILA MMOJA HUPIMWA KWA MIZANI YAKE, LAKINI USHAPIMA KIWANGO CHA FURAHA ANAYOKUWA NAYO DADA PINDI KAKA ANAPOPATA JIKO? MBALI NA KUJITAHIDI KILA KITU KIENDE SAWA, FURAHA YA DADA HAITOFAUTIANI NA YA MAMA. PICHANI MWENYE GAUNI SAFI NA POCHI AINA YA KIPIMA JOTO NI DADA WA BWANA HARUSI ANAITWA....(msaada jamani)
KILA LA KHERI KWA MR&MRS JORAM NGAIZA. NA BURUDANI IENDELEE!!!!
Vita vya Gaza: Mamia waandamana Gaza dhidi ya Hamas
-
Mamia ya watu wameandamana Gaza, wakitaka vita vikomeshwe na Hamas ijiuzulu
kutoka madarakani, katika maandamano makubwa zaidi dhidi ya vuguvugu la
Wapales...