Friday, November 12, 2010
SIASA
MH. ANNA MAKINDA ambaye alikuwa ni Naibu Spika wa bunge lililopita na pia ni mbunge wa jimbo la Njombe kusini mkoani Iringa,ameshinda nafasi ya kugombea kiti cha Uspika kupitia CCM baada ya kujizolea idadi ya kura 265 na kumbwaga mpinzani wake Mabere Marando (CHADEMA) ambaye amejinyakulia kura 55 katika uchaguzi huo uliofanyika leo asubuhi mjini Dodoma.
IDADI YA KURA ZILIZOPIGWA KATIKA UCHAGUZI HUO ZILIKUWA 307, ZILIZOHZRIBIKA NI 9. MH. ANNA MAKINDA ANACHUKUWA NAFASI YA KITI CHA SPIKA ALIYEPITA MH.SAMWEL SITTA.
HIVI SASA SPIKA HUYO MPYA ANASIMAMIA ZOEZI LA KUAPA KWA WABUNGE WAPYA WA BUNGE HILO LA 10. BUNGE LA TISA LILIMALIZA MUDA WAKE JUAI 16, 2010. ZOEZI LA KUAPA WABUNGE WAPYA LINATARAJIWA KUCHUKUA SIKU ZAIDI YA 2.
Tupe maoni yako
Mimi nimependa ukomavu wa kisiasa unaooneshwa na Nchi yetu pia chama tawala cha mapinduzi- CCM, nampongeza pia Mhe; Anne Makindakwa kushinda uspika lakini namuomba sana asiwe mstari kuwabeba viongozi wazemb. Ajue wananchi wanaelekeza macho yao katika bunge hili jipya juu ya kuwawajibisha Mafiasdi.
ReplyDeleteTunataka tuone hatma yao. awape nafasi wabunge wetu kujadili miswada inayokwamisha maendeleo ya nchi yetu.
Ni mimi Yahya Mnung`a wa DSM