NA IGENGA MTATIRO, MARA.
MRADI wa kutokomeza ukatili wa kijinsia na ukeketaji kwa watoto wa kike na akina mama ulioanzishwa na mwaka 2010 na Jumuiya ya Kikiristo [CCT] Tanzania, wilaya ya Rorya, umeendelea kuzaa matunda.
Waratibu wa mradi huo katika maeneo ya wilaya hiyo yanayoendekeza ukatili wa kijinsia na ukeketaji kwa watoto wa kike Isack Salasala na Ilibariki Raphael wanaendelea kuibua vitendo vya ukatili huo wakishirikiana na madawati ya Polisi katika vituo vikuu vya Rorya [Utegi], Kinesi na Shirati.
Mbali na uibuaji wa vitendo hivyo na kufikishwa katika vyaombo vya sheria kuchukuliwa hatua za kisheria kwa lengo la kuomesha hali hiyo, pia kunaendeshwa mafunzo kwa jamii ya uelewa wa madhala ya kuendekeza ukeketaji huo kwa watoto wa kike.
Desemba 3, mwaka huu usiku wa Alfajiri, saa 11.00 Ngaliba Wankyo Mwikwabe [65-70] alitiwa mikononi mwa Askari polisi wa kituo cha Kinesi alipokutwa akiwakeketa watoto wa kike katika maficho ya nyumba Anna Magoigwa [14] na Ghati Mwita [15].
Ngaliba huyo alifanya tendo hilo katika nyumba ya mji wa Magoigwa Matiku majira hayo katika kitongoji cha Mlimani Kijiji cha Marasibora kata ya Kisumwa, ambapo alipatwa na viungo vya vipande vya miili ya sehemu za siri zilizonyofolewa vya watoto hao wa kike akiwa tayari amevihifadhi na miti shamba kwa pamoja.
'' Tulimkuta akiwakeketa watoto hao wa kike tukiwa na Askari Polisi wa kituo cha Kinesi usiku wa Alfajiri saa 11.00, desemba 3, mwaka huu katika nyumba moja ya mji wa mzee Magoigwa Matiku katika Kitongoji cha Mlimani kijiji cha Marasibora, Wankyo Mwikwabe alipotushutikia tumeingia ndani alikimbilia uvunguni kujificha na vifaa vyake na wale watoto aliokuwa akiwakeketa'' alisema Mratibu Isack Salasala.
Aidha oparesheni hiyo pia ilifanikiwa kuwapata watoto waliokeketwa na ngaliba huyo siku hiyo waliokuwa wamekeketwa siku ya desemba 2 mwaka huu waliofahamika kwa majina yao kuwa ni Veronica Msangya [14] na Bhoke Msangya [12] ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano [v] katika shule ya msingi ya Marasibora wote wakaazi Kitongoji cha Senta kijiji cha Marasibora.
Watoto hao walifanyiwa tohara hiyo kwa siri na ngaliba huyo katika nyumba moja ya mji wa Msangya Nyabange mbinu ambayo iliyopo ailiyogunduliwa na kuibuliwa na waratibu wa CCT na kuwasilisha katika Jeshi la Polisi chini ya kamanda wake Lazaro Mambosasa.
Wararibu hao walifanikiwa pia kukamatwa kwa wazazi wa watoto hao waliofanyiwa tohara na Askari polisi wa kituo hicho siku hiyo waliofahamika majina yao ni Nchagwa Magoigwa [35] na Robi Chacha [60] waliofikishwa katika kituo cha Polisi na kufunguliwa majalada ya jinai hiyo.
Gazeti hili lilifanikiwa kulinyaka tukio hilo, na kuweka picha zake za kuhusiana na tukio hilo wakati zoezi hilo likifanyika chini ya Askari polisi hao muda mfupi, aliposika ngaliba akisema kuwa hawezi kuacha kukeketa watoto wa kike hadi hapo akipata kazi nyingine ya kumpatia ujira.
'' Siwezi kaucha kazi hii hadi hapo nikipata kazi ya kunipatia ujira kwani hapa ninafanya kazi hii ninajipatia fedha kutoka kwa wazazi wa watoto hawa'' alisema Ngaliba Bibi Wankyo Mwikwabe.
Bi Wankyo alisema kuwa yeye anafanya kazi hiyo kwa kukubaliwa na wazazi ama walezi wa watoto wanaofikishwa kwake na kuwakeketa na yeye anafurahia wakifishwa na kazi hiyo kuendelea kuwepo ajipatie riziki.
Wazazi wa watoto hao walikiri kuwahusisha watoto wao kwa hiali yao kufanyiwa mila hiyo ili kutekeleza jadi hiyo bila kujali kutokwa baadae na madhala watoto wao hao.
Watoto hao walipoulizwa juu ya hilo walidai kuwa wanafurahishwa na kutendewa na mila hiyo kupitia wazazi na walezi wao na kwamba wao hawana mamlaka ya kuonga kufanyiwa hivyo na hawajui madhala yake.
'' Sisi wazazi na walezi wetu ndio walituhamasisha kufanyiwa ukeketaji kwa kurejea mifano ya wakubwa waliofanyiwa mila hiyo na aliyetufanyia ukeketaji huu ni huyu bibi Wankyo na tuliletwa usiku na kuingizwa kwenye nyumba kwa siri bila watu kujua'' walisikika wakisema watoto hao walipohojiwa na Askari Polisi.
Watoto hao baada ya kuchukuliwa maelezo yao katika kituo cha Polisi cha Kinesi baada ya kumalizika uchunguzi wa kitabibu katika kituo cha Afya cha Kinesi na kubaini kuondolewa sehemu zao a siri kwa kukatwa, waliachiwa mikononi mwa Askari Polisi walipowasafirisha na kuwarusisha majumbani kwao katika Kijiji cha Marasibora.
Tukio hilo ni moja ya matukio yanayopingwa na mradi huo ukikumbwa na changamoto mbali mbali katika jamii kushindwa kubadilika na kuachana na mila hiyo kwa visingizo mbali mbali visivyo na msingi.
Waratibu hao katika msimu huu wa tohala wanaendelea kuibua na kufikishwa katika vituo vya polisi kuchukuliwa hatua za kisheria yaliyoshamili na kutukuzwa katika makabila na koo zinazotekeleza mila hiyo muda wote.
Isacka Salasala na Ilibariki Raphael mapema mwaka huu waliibua tukio la kunyanyaswa mjane Pili Samwel Elphas [24] wa Kijiji cha Omuga wilayani Rorya, aliyepigwa na shemeji yake Isaya Elphas Mei 19, mwaka huu na kumuingizia mti sehemu za siri.
M,jane huyo alifanyiwa hayo na shemeji yake huyo majira ya saa 5.00 asubuhi alipotetea haki yake na mume wake marehemu Samwel Elphas aliponyang'anywa Ardhi [mashamba] na kutimuliwa kutoka nyumbani kwake alipokwenda kuishi na mikononi mwa baba yake mzee Alex Allal.
Waratibu hao katika kumsaidia mjane huyo waliungana na baba mzazi wa mjane huyo na babu yake Mzee Alselemus Raphael Ondieki na kufanikiwa kukamatwa na mtu huyo aliyemfanyia kitendo hicho.
'' Sisi waratibu wa CCT wilayani hapa tuliibua tukio la mjane Pili Samwel Elphas aliyepigwa na shemeji yake hadi kuingiziwa mti katika sehemu zake za siri zilizopata vidonda Mei mwaka huu na mtuhumiwa Isaya Elphas alifikishwa mahakama ya wilaya ya Tarime'' alisema Salasala.
Tukio hilo lilinukuliwa RB yake UTE/RB/256/2014 katika kituo cha Polisi Utegi ilifunguliwa kesi yake ya jinai CC191/2014 ambapo bado inaendelea na hatua zake changamoto ambayo ilidaiwa na wararibu hao kuwa ipo katika jamii kuchukua muda mrefu kuelewa na kubadilika.
Salasala ambaye ni mchungaji wa kanisa la AIC wilayani Rorya, anasema kuwa licha ya k,utumia mafunzo ya kiroho kwa waumini wake kupinga matendo hayo bado ni kazi ngumu.
'' Kwa mfano bibi Wankyo,muda wote tumekuwa tukimwambia aachane na kukeketa watoto wa kike tukimuelimisha zaidi bado alisimamia msimamo wake wa kuendelea na kukeketa watoto wa kike, kisa eti hana kazi nyingine labda tumpatie kazi nyingine ya kumuwezesha kupata fedha 200, 0000 kwa mwezi sio vinginevyo'' alisema Salasala.
Ukatili wa kijinsia na ukeketaji wa watoto wa kike katika makabila yanayotekeleza mila hiyo hadi sasa nchini licha ya kudaiwa kupungua kutokana na juhudi za kubadilishwa na mashirika ya kijamii ya TAMWA, KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU [LHRC] na TGNP MTANDAO, bado unaendekezwa na jamii.
Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia na watoto anayo kazi kubwa ikiwa ni pamoja na kuyawezesha mashirika hayo binafsi ruzuku na k,uacha kutegemea fedha za wafadhili wa ndani na nje kutekeleza miradi hiyo ili kuharakisha kukomesha ukatili katika jamii wanaofanyiwa watoto, akina mama.
'' Ipo haja kazi hii serikali itambue kuwa ni ngumu kufanikiwa hili, kwani ni mila na ni utamaduni ulioshamili muda mrefu tusiachiwe tu mashirika tu, serikali kuanzia ngazi ya kitongoji [ mtaa] hadi ngazi ya kitaifa, wizara yake kutengwa bajeti ya kutosha katika kufanikiwa haya'' alisema Salasala.
Ukatili wa kijinsia na ukeketaji wa watoto wa kike na akina mama wilaya za mkoa wa mara, kwa makabila yaliyoendekeza tabia hizo, umekuwa sugu na kuwafanya wanajamii wakae kando na wengine wanashiriki moja kwa maoja wakitambua wengine kutotambua madhala yake kiafya na kiuchumi wakiacha mashirika ya kijamii na viongozi wa serikali kupata changamoto zake.