ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 26, 2025

HUDUMA YA MAJI IMEREJEA - RC MTANDA

 

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema huduma za maji mkoani humo zimeanza kurejea katika hali yake ya kawaida tangu jana tarehe 25 September 2025, baada ya wataalamu kutoka Mamlaka ya Maji na Usafi na Usafi wa Mazingira (MWAUWASA) na Shirika la Ugavi (TANESCO) kurekebisha tatizo.


Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ametoa kauli hiyo jana kwenye Chanzo cha Maji cha Butimba wilayani Nyamagana alipofika kufanya ukaguzi kwenye mitambo ya kuzalisha na kusambaza maji ambayo ilipata hitilafu takribani siku nne zilizopita.


Mhe. Mtanda amesema mafundi wamefanya kazi mchana na usiku kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji kama kawaida na wamefanikisha hilo kwa kurejesha mawasiliano ya umeme kwenye pampu ya kusambaza maji kutoka kwenye chanzo hicho kwenda kwenye matenki.


“Changamoto iliyojitokeza hapa ni umeme kutofika kwenye pampu yaani kilichokua kimekwama ni mawasiliano ya umeme kufika kwenye pampu lakini kwa juhudi na ushiriniano wa wataalamu wetu napenda niwaambie wananchi kwamba tayari kazi ya matengenezo imekwisha.” Mhe. Mtanda.

Aidha, ametumia wasaa huo kuwashukuru wataalamu wa Mamlaka hiyo ya Maji pamoja na TANESCO kwa kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha mitambo inarejea katika hali ya kawaida na kwa kuweka mfumo ambao hautoruhusu mitambo ya maji kuathirika na hitilafu ya umeme endapo litatokea.


Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri amewashukuru wataalamu kutoka wizara hiyo kwa kushirikiana na MWAUWASA pamoja na TANESCO kwa kufikisha nishati ya umeme kwenye pampu kama awali.

“Mhe. Mkuu wa Mkoa, kwakweli mafundi na wataalamu wetu wamefanya kazi kubwa na niwakikishie tu wananchi kuwa tumewasha pampu na sasa wananchi tayari wameanza kupata huduma ya maji kama ilivyokua siku za nyuma.” Katibu Mkuu

Mbali ya hayo Mhe. Mkuu wa Mkoa akiwa ameambatana na Katibu Mkuu pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA walihitimisha ziara kwa kuwatembelea Kiwanda cha Dawa, Zahanati na kwenye Makazi ya wananchi wa Buhongwa ambapo wamejiridhisha kwamba Maji yanatoka tena kwa kasi inayotakiwa.



Sunday, September 21, 2025

BUKOBA JIANDAENI KUIPOKEA NEW MV MWANZA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo tarehe 21 Septemba, 2025 amekuwa mmoja kati ya mashuhuda wa jaribio la mwisho la safari ndefu kwa Meli ya MV New Mwanza kwenye bandari ya Mwanza Kusini iliyopo jijini Mwanza ilipoondoka kuelekea kwenye Bandari ya Bukoba mkoani Kagera.
Akizungumza na wananchi waliojitokeza kushuhudia hafla hiyo ya kihistoria Mhe. Mtanda amesema kukamilika kwa meli hiyo ni ishara ya juhudi za Serikali katika kuimarisha sekta ya usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo katika ukanda wa ziwa Victoria.



Meli ya MV New Mwanza ikiianza safari yake ya kwanza ndefu kwenye bandari ya Mwanza Kusini iliyopo jijini Mwanza kuelekea kwenye Bandari ya Bukoba mkoani Kagera.

Ndani ya maji ya Ziwa Victoria Meli ya MV New Mwanza ikiianza safari yake ya kwanza ndefu kwenye bandari ya Mwanza Kusini iliyopo jijini Mwanza kuelekea kwenye Bandari ya Bukoba mkoani Kagera.





AĹLY HAPI AZINDUA RASMI KWA KISHINDO KAMPENI ZA UBUNGE JIMBO LA KIBAHA VIJIJINI

VICTOR MASANGU, KIBAHA

Katibu mkuu wa jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi (CCM) ndugu Ally Hapi (MNEC) amezindua rasmi kampeni  katika Jimbo la Kibaha vijini na kuwaomba wanachama na wananchi kumpa ridhaa  ya kuweza kuwatumikia  mgombea  wa  wa Jimbo la  Kibaha mjini Hamoud Juma kwa  kura nyingi za kishindo  ili aweze kutekeleza ilani kwa vitendo na  kwa  kuwaletea chachu ya maendeleo chanya katika nyanja mbali mbali.

Hayo ameyasema wakati mkutano wa uzinduzi rasmi wa kampeni katika Jimbo la Kibaha Vijijini ambapo amesema kwamba  wanachama wa CCM wanapaswa kuungana kwa pamoja na kuwa na mshikamano katika kuhakikisha Octoba 29 kura zote kuanzia ngazi za udiwani, Ubunge pamoja na nafasi ya Rais lengo ikiwa ni kuhakikisha wagombea wote ambao wamechaguliwa wanakwenda kusikiliza keo na changamoto za wananchi.


Hapi amebainisha kwamba lengo kubwa la chama ni kuhakikisha inatekeleza ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025 hadi 2030 katika kuekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo katika Mkoa wa Pwani  ikiwemo mradi mkubwa wa ujenzi wa viwnda vya dawa vitatavyo saba viwanja vya chuma tisa, mbolea saba, viwandavya sukari, viwanda vya sukari vitatu pamoja na viwanda vya  mafuta kumi lengo ikiwa ni kutoa fursa za ajira kwa wananchi.
 

"Ndugu zangu wanachama na wa ccm pamoja na wananchi katika utekelezaji wa ilani ya chama chetu Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye ni mgombea pekee ya nafasi ya Urais  kwa hivyo kitu kikubwa ninawaomba tumpe kura nyingi za kishindo ikiwemo pamoja na mgombea wetu Hamoud Jumaa pamoja na madiwani wenzake lengo ikiwa ni kuwaletea wananchi maendeleo katika sekta mbali mbali,"amebainisha Katibu Hapi.

Kwa upande wake Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Hamoud Juma amehahakikisha wananchi  endapo wakimchagua katika uchaguzi mkuu wa Octoba 29 mwaka huu ataleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo katika nyanja mbali mbali ikiwemo ujenzi wa soko jipya la kisasa ambalo litaweza kuwasaidia kwa kiwango kikubwa katika kujikwamua kiuchumi.

Hamoud amebainisha kwamba katika serikali ya awamu ya sita Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweza kufanya mambo makubwa katika miradi ya kimkakati ambayo kwa kiwango kikubwa imeweza kuwapa fursa wananchi  kuweza kujikimu kimaisha pamoja na kupambana na wimbi la umasikini.

Hamoud amesema kwamba lengo alke kubwa ni kuhakikisha anawaletea wananchi maendeleo ikiwemo mradi mkubwa wa ujenzi huo wa soko ambao ana imani utakuwa ni mkombozi mkubwa katika suala zima la kungoeza kazi ya kukuza uchumi pamoja na kujiongezea kipato ambacho kitaweza kuleta mabadiliko katika suala zima la kimaendeleo.

Naye  Mgombea ubunge wa jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amewataka wanachama na wananchi wasifanya makosa hata kidogo na badala yake wawe kumpa kura nyingi Rais Dkt. Samia Suluhu Hasssan, madiwani pamoja na mgombea ubunge wa Jimbo la Kibaha vijiji Hamoud Juma kwa ajili ya kuweza kuwatatulia changamoto mbali mbali zinazowakabili.

Aidha Mgombe ubunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani kupitia chama cha mapinduzi Hawa Mchafu amesema kwamba Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan ameweza kufanya mambo makubwa katika jimbo la Kibaha vijiji kutokana na kutenga fedha nyingi amabzo zimekwenda kuleta mageuzi katika miradi  mbali mbali ya maendeleo hivyo wanachama wanapsawa kumpa kura nyingi za kishindo yeye pamoja na Hamoud Juma pamoja na madiwani wenzake.

Uzinduzi wa kampeni katika jimbo la Kibaha Vijinini  ambao umefanyika katika viwanja vya shule ya msingi mtongani Mlandizi  umezinduliwa rasmi Katibu mkuu wa jumuiya ya wazazi wa chama cha mapinduzi (CCM) ndugu Ally Hapi na kuhudhuliwa na  wanachama wa CCM, viongozi mbali mbali, wananchi, wenyeviti wa mtaa , sambamba na wagombea ubunge pamoja na madiwani.
                           MWISHO

MWANA FA KUSHUGHULIKIA MAWASILIANO YA SIMU JIMBO LA MUHEZA

 







Na Mwandishi Wetu, Muheza

MGOMBEA ubunge Jimbo la Muheza kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamis Mwinjuma maarufu MwanaFA amesema katika miaka mitano ijayo atahakikisha anaongeza minara ya simu ili Jimbo la Muheza liweze kuwa na mawasiliano katika maeneo ambayo yana changamoto hiyo.



Akizungumza katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika kata ya Kwezitu tarafa ya Amani, MwanaFA alikiri kwamba yapo maeneo katika Jimbo hilo, yana changamoto ya ukosefu wa mawasiliano.



"Katika miaka mitano ijayo tutaimarisha mawasiliano ya simu...Moja ya mambo yanayonisikitisha ni kufika baadhi ya maeneo kwenye Jimbo la Muheza ikawa simu haiwezi kushika mawasiliano, huwezi kupigiwa simu," alisema na kuongeza,

"Tunachotaka kufanya ni kuhakikisha tunaongeza minara ya simu ili kuongeza kiwango cha upatikanaji wa mawasiliano kwa wananchi wetu,".



MwanaFA ambaye ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, alisema kuwa katika kipindi cha mwaka 2020-2025 Jimbo hilo lilipata minara Saba ambayo kutokana na jiografia ya Jimbo hilo, bado haijakidhi mahitaji ya mawasiliano katika maeneo mengi kutokana na hali hiyo.

Hivyo, alisema anakwenda kuzifanyia kazi kuhakikisha minara ya simu inaongezeka na hali ya mawasiliano inazidi kuimarika katika Jimbo hilo.



"Sitaki kuahidi mambo mengi na nikashindwa kuyatekeleza lakini niwahakikishie jambo moja changamoto zote za kata ya Kwezitu, Jimbo la Muheza kwangu ni kipaumbele...Miaka mitano hii nimejua kona zote za kutatua changamoto zilizopo katika Jimbo letu," alisema.




Aliwaomba wananchi wa Kwezitu kufanya kazi mbili ambazo ni kwenda kupiga kura Oktoba 29 na kuwachagua wagombea wa CCM ili waweze kumalizia kazi ambazo wamezifanya katika miaka mitano iliyopita.



Alisema wananchi wa Kwezitu wanakila sababu za kumchagua Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwakuwa ameleta fedha nyingi katika kata hiyo na Jimbo zima la Muheza.




Rais ameleta fedha nyingi katika miradi ya afya, elimu, maji, barabara na miradi mingine hivyo anastahili kupigiwa kura nyingi katika Jimbo letu.

"Nichagueni na Mimi miaka mitano hii nimeisema wilaya hii, hatuwezi kusema matatizo yetu yote tumeyamaliza bali dhamira yetu ni ya dhati kwakuwa kila sekta tumeigusa," alisema na kuwaomba wananchi wa kata hiyo kumchagua Mch. John Mzalia awe diwani wa kata hiyo.



Akiomba kura kwa wananchi wa kata hiyo Mgombea udiwani Mch Mzalia alisema kuwa kata hiyo imepata miradi mingi kuliko wakati wowote ule ikiwemo miradi ya Elimu, afya, barabara na huduma za jamii.




"Tumepata mradi wa Boost ambao shule yetu ya Kwezitu imekuwa nzuri mno hadi watoto wetu wanasoma kwenye shule ya vioo wakati mwingine wanachungulia kwenye madirisha hayo kama watoto wa Kihindi," alisema na kuwaomba wananchi hao wawachague wagombea wa CCM.




Katibu wa CCM wilaya ya Muheza Simon Leng'ese amewataka viongozi wa CCM wa ngazi zote za kata hiyo kuhakikisha wanatoka na kwenda kwa wananchi kuomba kura za wagombea wa CCM ili kukifanya chama hicho wagombea wake kupata kura za kishindo.



"Viongozi wa kata, matawi, mashina, mabalozi mtoke kwenda kuomba kura kwa wananchi katika maeneo yenu, haya ni maagizo nawapa mwende kukifanya chama chetu na wagombea wetu waweze kupata kura nyingi," alisema Leng'ese.




Meneja wa kampeni wa mgombea wa Jimbo la Muheza Aziza Mshakang'oto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM wilaya ya Muheza (UVCCM), amewataka wananchi wa kata ya Kwezitu wasifanye makosa kwa kuwachagua wagombea wa upinzani kwakuwa hawana jipya.




Alisema CCM imekuja na ilani ambayo kwa wilaya ya Muheza imekuwa na miradi mingi ya maendeleo katika Jimbo hilo hivyo wasifanye makosa katika uchaguzi huo.

Mwisho