NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
MKUU wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda leo tarehe 21 Septemba, 2025 amekuwa mmoja kati ya mashuhuda wa jaribio la mwisho la safari ndefu kwa Meli ya MV New Mwanza kwenye bandari ya Mwanza Kusini iliyopo jijini Mwanza ilipoondoka kuelekea kwenye Bandari ya Bukoba mkoani Kagera. Akizungumza na wananchi waliojitokeza kushuhudia hafla hiyo ya kihistoria Mhe. Mtanda amesema kukamilika kwa meli hiyo ni ishara ya juhudi za Serikali katika kuimarisha sekta ya usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo katika ukanda wa ziwa Victoria.Meli ya MV New Mwanza ikiianza safari yake ya kwanza ndefu kwenye bandari ya Mwanza Kusini iliyopo jijini Mwanza kuelekea kwenye Bandari ya Bukoba mkoani Kagera.
Ndani ya maji ya Ziwa Victoria Meli ya MV New Mwanza ikiianza safari yake ya kwanza ndefu kwenye bandari ya Mwanza Kusini iliyopo jijini Mwanza kuelekea kwenye Bandari ya Bukoba mkoani Kagera.
Tupe maoni yako







0 comments:
Post a Comment