ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, April 2, 2022

MOTO WATEKETEZA MADUKA 520 SOMALILAND

 


Mamlaka ya jimbo lenye kutaka kujitenga la Somalia, Somaliland imesema moto uliozuka ghafla jana jioni umeteketeza maduka 520, maghala na ofisi za masoko ya jumla. 

Moto huo ulioliteketeza soko kubwa la Waheen, mjini Hergeisa, ulisambaa umbali wa kilometa 5.Ulishindikana kuzimwa hadi mapema leo. 
Akielezea mkasa huo, Meya wa mji wa Hargeisa, Abdikarim Ahmed Mooge alisema hilo ni tukio baya zaidi la moto kuikumba Somaliland.

Somalind ilijitangazia uhuru wake kutoka kwa Somalia 1991 lakini halijatambuliwa kuwa taifa na jumuiya ya kimataifa.

MAREKANI YAAHIDI NYONGEZA YA DOLA MILIONI 300 YA ULINZI KWA UKRANE.

 


Wizara ya Ulinzi ya Marekani metangaza kutenga kiasi cha kitita cha dola milioni 300 ukiwa "msaada wa usalama" kwa Ukraine ili kuimarisha uwezo wa ulinzi wa nchi hiyo, kikiwa ni nyongeza ya kiasi kingine cha dola bilioni 1.6 ambacho taifa hilo lilikiahidi kukitoa tangu Urusi ilipoanza uvamizi Februari.

Taarifa ya msemaji wa wizara hiyo John Kirby inasema hatua hiyo inaonesha usisitizwaji wa dhamira isiyotetereka ya Marekani kwa taifa la Ukraine katika kulinda uhuru wake wa kimipaka baada ya kuvamiwa.


Jumatano iliyopita Rais Joe Biden wa Marekani na yule wa Ukraine, Volodymyr Zelensky walijadiliana juu ya nyongeza ya msaada wa ziada katika kulisaidia jeshi la Ukraine. 

Taarifa hiyo ilitolewa na Ikulu la Marekani baada ya mazungumzo hayo kwa njia ya simu.

WAKUU WA SHULE ZA SEKONDARI WAONYWA WEREDI WIZI WA MITIHANI.

 


Afisa elimu mkoani Mara, Benjamini Oganga amewataka wakuu wa shule za sekondari kufanya kazi kwa nguvu zote weledi,bidii,ujuzi zaidi ili watoto wetu na ndugu zetu wapete kupata elimu bora na kuinua ufaulu bila kuiba mitihani.


Afisa huyo aliongeza kusema kuinua ufaulu kuanzia shuleni hadi ngazi ya mitihani ya Taifa lengo lake ni pale ambao wataende kufuta matokeo ya alama ya ufaulu ya Division (0) na (4).


Katika hatua nyingine Afisa huyo alisema kuwa walimu wakuu wanapaswa kuwa na mbinu za kuhakikisha wanafunzi wanakaa kwenye mfumo wa elimu na kuwa wanaanza kupima wakuu wa shule kwa usimamizi wa wanafunzi na walimu ambapo amesisitiza lugha ya Kingereza katika shule za sekondari Mkoani hapa.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa wakuu wa Shule TAHOSSA Mkoani hapa,Magudira Mugeta amezitaja sababu baadi zinazowakabili wakuu wa shule kadhaa na pia kuchangia kwa ufaulu wa watahiniwa kushuka madaraja kwa shule za sekondari mkoani hapa.


“Mheshimiwa mgeni rasimi pamoja na kufanya kazi kwa bidii yapo mambo machache yanayoleta changamoto na kurudisha nyuma juhudi za kuinua kiwango cha cha elimu mkoani hapa kama vile wakuu wa shule kutochangia ada za TAHOSSA kwa wakati kwa ngazi zote,baadhi ya wakuu wa shule kutohudhuria vikao hivi ambavyo ni vya mhimu katika usimamizi wa shule maana maelezo na maelekezo mbalimbali ya serikali hutolewa katika vikao hivi na kukosekana kwa semina(Orientation/workshop)kwa wakuu wa shule ambao niwateule wa hivi karibuni”alisema Mageta.


Mkurugenzi wa Taasisi ya Professor Mwera Faundation,Hezeboni Mwera ambao pia ni wadau wa elimu alisema wameanzisha mpango wa kutoa tuzo kwa shule ndani ya mikoa kumi hapa Tanzania.


Mwera aliongeza katika kikao hicho kuwa  wamefadhili chakula cha wageni ikiwemo kutoa ukumbi wa mkutano bure na kuongezakuwa wakuu wahao shule za sekondari wajihadhari na matapeli wanaofika mashuleni wakitaka wanafunzi kujiunga na vyo mbalimbali vya veta ambavyo havikusajiliwa kisheria.


Nasisitiza kuweni makini na watu wanakuja kweny shule kwani baadhi ya vyuo havijasajiriwa na sasa tunashukuru serikali imeunganisha vyuo vyote kuingia katika mfumo wa NACTE alisema Mwera.


Katika kikao hicho cha TAHOSSA kilichokalia ukumbi wa Taasisi ya Professor Mwera Faundation ilitajwa kuwa asilimia 69 ya wanafunzi wakike mkoani hapawanashindwa kumaliza masomo.


Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Mara,Ayubu Mbilinyi alisema kuwa Idadi kubwa ya wanafunzi katika Mkoa wa Mara wanatajwa kutomaliza masomo yao ya sekondari tangu pale wanapoandikishwa hususani wasichana.


ambapo wanafunzi zaidi ya elfu tisa wanatajwa kupotea ambapo asilimia 69 ni wasichana.

Wednesday, March 30, 2022

RC MALIMA AAGIZA HALMASHAURI KUWEKA SHERIA ZA KULINDA VYANZO VYA MAJI

 

MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza wakati akifungua Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Wadau wa Bonde la
 Mto Pangani kulia ni Mkurugenzi  Msaidizi wa Wizara ya Maji Pamela Temu na kushoto ni Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Tanga Kasunzu
Mkurugenzi  Msaidizi wa Wizara ya Maji Pamela Temu akizungumza wakati wa Jukwaa hilo
Mkurugenzi wa Bonde la Maji Pangani Segule Segule akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika mkutano huo
MKUU wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo akizungumza wakati wa Jukwaa hilo
MKURUGENZI wa Bonde la Mto Pangani Segule Segule katika akiwa na Meneja wa Ruwasa Mkoa wa Tanga Mhandisi Upendo Omari na kulia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Jukwaa la Watumiaji Maji
Sehemu ya washiriki wa kikao hicho wakufuatilia matukio

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima ameziagiza Halmashauri za mkoa huo kutengeneza sheria za ndogo ambazo zitalinda mazingira na vyanzo vya maji ikiwemo kuwataka kutokuruhusu watu kuvichezea .

Malima aliyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Pili wa Jukwaa la Wadau Bonde la Mto Pangani ambalo limefanyika Jijini Tanga ambapo alisema lazima wahakikishe wanakuwa wakali sana kwani mambo mazuri hayataki kubembelezana

Alisema pia suala la mazingira na maji ni kama vile uji na mgonjwa hivyo ukiwaona watu wanachafua vyanzo vya maji kwa kutia zebaki kwenye vyanzo vya maji na kuvichafua lazima wachukuliwe hatua kali za kisheria.

“Suala la Mazingira na Maji ni kama vile uji na mgonjwa hivyo ukiona watu wana weka zebaki kwenye vyanzo vya maji halafu anasimama mbele za watu anasema hao wanapiga kelele bure yeye anachangua mapato kwenye Halamshauri sio sawa chukueni hatua “Alisema

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwa sababu mtu huyo atakuwa anachangia magonjwa kwa watumiaji wa maji na jumuiya zenu hivyo wawe wakali kwa wachafunzi wa vyanzo vya maji kuhakikisha wanazibiti .

“Ndugu zangu wadau wa Jukwaa hili kuweni wakali kwenye vyanzo vya maji msikubali watu waingie wachezee hakuna cha Tanga,Arusha wala Moshi mkifanya masishara vyanzo vitakauka heshimuni masharti ya matumizi ya maji yaliyopo kwa kila mmoja”Alisema

Mkuu huyo wa mkoa alisema kwamba watu wakifanya mchezo kwenye vyanzo vya maji vinaweza kukauka na hivyo kupelekea changamoto ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu kwa maisha

“Ndio maana tumeamua kuanzisha Jukwaa hilo tujadili lakini ukichezea vyanzo vya maji mito itakauka kuna miradi ya maji watu wanapiga sana lakini tunamshukuru Rais Samia Suluhu miradi ya maji imeinginia heshima kubwa kutokana na usimamizi mzuri”Alisema

“Mkiona mradi wa maji hauna maelezo na kila mwaka unaambiwa unaishi lakini hauishi ukimuangalia mkandarasi kanawiri,wakina mama wana beba maji hii sio sawa mradi wa maji lengo lake ni kutoa maji”Alisema

Hata hivyo amelipongeza Bonde la Pangani kwa kuwashirikisha wadau kwenye rasiliamali za maji na kuimarisha jumuiya za watumiaji wa maji huku akiwataka waendelee kufanya jitihada za makusudi kutunza vyanzo vya maji.

“Lakini muelewe kwamba hakuna mtu mahususi mwenye dhamana ya usimamizi wa maji ukiona mtu anachafua vyanzo vya maji ukasirike muwafichue msiwafumbie macho”Alisema RC Malima.

Awali akizungumza wakati wa Jukwaa hilo Mkurugenzi wa Bonde la Maji Pangani Segule Segule alisema bonde la linahusisha ukubwa wa kilomita 58600 katika mikoa ya Kilimanjaro,Arusha,Tanga na sehemu Manyara,

Alisema kazi kubwa ni kuhakikisha rasilimali za maji zinatunzwa ipasavyo na kusimamia vyanzo kwa kuhakikisha wanafanya shughuli za urudishaji uoto asili katika vya vyanzo vya maji ikiwemo upandaji miti,kutumia njia mbalimbali kupelekea uelewa kwa jamii na wananchi.

Alisema lengo la Jukwaa hilo la wadau ni kujadiliana kuhusu rasilimali za maji changamoto za vyanzo na kukabiliana nazo kwa kuchukua ili kuweza kukabiliana nazo.

“Changamoto za bonde ni ya watu wa madini kuchimba madini kwenye vyanzo vya maji maeneo ya Lushoto Muheza lakini pia ukataji wa miti kwenye eneo la hifadhi,uchafuzi vyanzo watu kutupa taka kwenye vyanzo vya maji kugeuza vyanzo vya maji kuwa sehemu uya kutupia taka”Alisema

Tuesday, March 29, 2022

IGP SIRRO AMBADILISHA ACP WANKYO KUPISHA UCHUNGUZI.


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amefanya mabadiliko ya Makamanda wa Jeshi la Polisi katika mikoa miwili ya Kagera na Rukwa.


Taarifa ya Jeshi la Polisi imeeleza kuwa mabadiliko hayo ni kupisha uchunguzi wa kauli za aliyekuwa RPC wa Kagera ACP Wankyo Nyigesa alizozitoa wakati anaaga baada ya kuhamishwa kutoka Pwani kwenda Kagera.


Katika mabadiliko hayo, Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amemhamisha aliyekuwa RPC mkoa wa Rukwa William Mwampagale kwenda kuwa RPC mkoa wa Kagera, kuchukua nafasi ya aliyekuwa RPC wa mkoa huo ACP Wankyo Nyigesa ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma.


Aidha IGP Simon Sirro  amempandisha aliyekuwa Afisa Mnadhimu wa mkoa wa Rukwa ACP Theopista Mallya kuwa RPC wa mkoa huo, akichukua nafasi ya ACP William Mwampagale ambaye amekwenda kuwa RPC mkoa wa Kagera.


Sunday, March 27, 2022

ZITAMBUE ATHARI 5 ZA KUKOPESHA PESA NA BIDHAA KWA WATEJA.

 

Katika jaamii zetu za kiafrika suala la mikopo ya bidhaa au fedha kutoka kwenye biashara kwenda kwa wateja limezoeleka sana. Ingawa jambo hili linaweza kuwa na manufaa kwa upande fulani, hata hivyo kutokana na kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa watu wengi jambo hili limekuwa na athari nyingi kuliko faida.

Inawezekana umekuwa ukiwakopesha wateja wako wa maana sana, au umekuwa ukitumia mikopo kama njia ya kuuza huduma au bidhaa zako, lakini karibu nikushirikishe athari tano za mikopo hiyo.

1. Kumpoteza mteja

Kuna usemi usemao kumkopesha mteja ni kumfukuza. Nimesikia mara kadhaa wafanyabiashara wakisema tangu ni mkopeshe haji tena dukani kwangu, au tangu nimkopeshe anapita mbali tu. Mara nyingi mteja akishakopeshwa pesa au bidhaa haji tena kwenye biashara husika ili kukwepa kulipa deni. 

Kuliko umpoteze mteja kwa kumkopesha ni bora umueleze ukweli kwa kutumia busara; ingawa hatofurahi kwa wakati ule lakini baada ya muda atakuelewa na ataendelea kuwa mteja wako.

2. Ugomvi au kuharibu mahusiano

Kuna msemo usemao kukopa harusi kulipa matanga. Mara nyingi watu huja kwa uso mzuri uliojaa furaha na uaminifu wakati wa kukopa. Mara tu baada ya kukopa maisha ya shari na kusumbuana yanaweza kutokea hasa kwa wale wateja wasio waaminifu kulipa deni.

Kuna wafanyabiashara walioishia kugombana vibaya au hata kuvurugika kabisa kwa mahusiano yao na baadhi ya wateja wao kutokana na kuwakopesha bidhaa au pesa kutoka kwenye biashara zao.

Hivyo basi, kuliko uishie kugombana na wateja wako au watu wako muhimu, ni vyema ukaepuka suala hili la mikopo katika biashara yako.

3. Athari katika mzunguko wa pesa

Pesa za biashara zinatakiwa kuzunguka na si kukaa eneo moja. Mtaji wa biashara unapokuwa bidhaa katika biashara, bidhaa hizo zinapaswa kuuzwa; baada ya bidhaa hizo kuuzwa tunatakiwa kupata mauzo ambayo hujumuisha sehemu ya mtaji na faida. Mtu anapokopa pesa au bidhaa kutoka kwenye biashara yako, moja kwa moja anavuruga mzunguko huu.

Hili husababisha matatizo kama vile kukosa pesa timilifu kwa ajili ya manunuzi au gharama nyingine. Tatizo hili limewasababishia wengine kuchukua pesa zao binafsi au zilizoko nje ya biashara ili kuzipa pengo lililotokana na mikopo ili biashara isiyumbe.

4. Kupoteza fedha na mali

Kwa hakika hakuna hakikisho la asilimia mia moja kuwa pesa au bidhaa ulizomkopesha mteja zitalipwa. Ikizingatiwa kuwa watu wengi hukopeshana pesa na bidhaa kienyeji bila kufuata taratibu za kisheria zinazoweza kuwalinda baadaye iwapo mkopaji hatokuwa mwaminifu.

Hivyo basi, mikopo inaweza kukusababishia kupoteza fedha na mali ulizowakopesha wateja iwapo wateja hao hawatakuwa waaminifu kulipa, jambo ambalo linaweza kukuathiri pia kibiashara. 

5. Kufilisika au kufa kwa biashara

Hoja hii ni hitimisho tu la hoja zilizotangulia; ikiwa mikopo haitalipwa kwa wakati au haitolipwa kabisa, biashara yako inaweza kufilisika au kufa kabisa. Imeshuhudiwa wafanyabiashara wakiwa na mikopo wanayodai kutoka kwa wateja wao ambayo inazidi hata nusu ya mitaji yao; huku wakiwa hawana uhakika kama watalipwa pesa hizo au laa. Ni muhimu sana kulichukulia swala la mikopo kwa tahadhari kubwa lisije likasababisha biashara yako  kufa.

Je kuna lolote unaloweza kufanya? Ndiyo, Mueleze mteja ukweli kwa njia ambayo ni ya busara na hekima ili aelewe lengo lako. Hatakama hatokuelewa kwa wakati huo, usihofu, kadri muda unavyokwenda ataelewa hata kupitia mfanyabiashara mwingine mwenye msimamo kama wa kwako. Kumbuka uhai wa biashara yako ni muhimu kuliko mikopo ya wateja. 

RAIS JOE BIDEN AKOSOA UTAWALA WA PUTIN NCHINI URUSI

 


Rais wa Marekani Joe Biden amesema rais wa Urusi Vladimir Putin hawezi kusalia mamlakani baada ya kuivamia Ukraine huku akiyaonya majeshi Urusi kutojaribu kusogeleea eneo la jumuiya ya kujihami ya NATO. 


Biden amesisitiza katika hitimisho la ziara yake ya siku mbili nchini Poland kwamba Putin hawezi kubakia madarakani na kuongeza kuwa vita vyake dhidi ya Ukraine ni mkakati wa Moscow ulioshindwa.


Matamshi yake makali na yasiyo ya kawaida hata hivyo yalidhoofishwa na ikulu ya Washington ambayo ilisema hakumaanisha kutoa mwito wa serikali ya Putin kuondolewa madarakani. Na baada ya ikulu ya Kremlin kuulizwa kuhusu matamshi hayo ya Biden msemaji alisema tu kwamba huo sio uamuzi wa Biden kwa kuwa rais wa Urusi alichaguliwa na raia wa Urusi.

WAZIRI UMMY APIGIA CHAPUO VIVUTIO VYA UTALII TANGA

 

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza mara baada ya Kufungua Tamasha la Tanga Utalii Festival leo Jijini Tanga lililofanyika viwanja vya Urith Jijini humo ambalo liliandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa
MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa Tamasha hilo
Naibu Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Calvas Joseph akizungumza wakati wa Tamasha hilo
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu kulia akipata maelezo kutoka kwa Bandari ya Tanga mara baada ya kutembelea banda lao
WAZIRI wa Afya akipata maelekezo kwenye Banda la Benki ya Tanzania Comercial Benki wakati alipotembelea Banda lao
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu kulia akimsikiliza kutoka kwa Benki ya NMB wakati alipotembelea Banda lao
WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu kushoto akipata maelezo kwenda Banda la Magoroto
WAZIRI wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu  kushoto akimkabidhi cheti cha ushiriki mshiriki kutoka Kivutio cha Utalii cha Magoroto kilichopo wilayani Muheza Aisiana Mero wakati alipofungua tamasha la Tanga Utalii Festival kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo katikati ni Mkuu wa wilaya ya Mwanga Abdallah Mwaipaya
WAZIRI wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu  kushoto akimkabidhi cheti cha ushiriki mshiriki kutoka Kivutio cha Utalii cha Magoroto kilichopo wilayani Muheza Aisiana Mero wakati alipofungua tamasha la Tanga Utalii Festival kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo akifuatiwa na Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga (DAS) katikati ni Mkuu wa wilaya ya Mwanga Abdallah Mwaipaya
WAZIRI wa Afya na Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu  akipokea tisheti wakati wa tamasha hilo

NA OSCAR ASSENGA,TANGA

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amefungua Tamasha la Tanga Utalii Festival huku  akipigia chapuo vivutio vya utalii vilivyopo Jijini Tanga kwa kuwashauri watalii wanapokwenda kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi waunganishe na Tanga kuona vuvutio vingine ikiwemo Beach nzuri,Visiwa vya Toten na Mapango ya Amboni.


Amesema pia Tamasha hilo la Tanga Utalii Festival litafungua fursa na kuongeza za kipato kwa wananchi wa mkoa wa Tanga na hivyo kuchochoe ukuaji wa uchumi kwa mkoa huo.


Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) aliyasema hayo leo wakati akifungua Tamasha la Tanga Utalii Festival ambalo limefanyika kwa mara ya kwanza ambalo limeandaliwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa na kushirikisha wadau kutoka maeneo mbalimbali.


Alisema upo umuhimu wa watalii wanapokwenda kutembelea hifadhi ya Taifa ya Mkomazi wanapomaliza badala ya kurudi uwanja wa ndege Kia watumia fursa hiyo kuja mkoani Tanga ili kuweza kuona vivutio adimi vilivyopo ikiwemo beach,visiwa na eneo la magoroto lenye vipepeo ambavyo havipatikani mahali pengine popote duniani.


Waziri Ummy alisema kwamba wanaweza kutumia jukwaa hilo ambalo kwa sasa litakuwa likifanyika kila mwaka kuhakaikisha wakuza fursa za ajira na uchumi kwa watu wa Tanga.


“Tunataka kulifanya Jiji la Tanga kuwa la Mahaba watu wa Mwanga na Same wanapokuja kutalii Mkomazi tuna maombi yetu watu wasiiishie mkomazi waje na Tanga tuwapeleke visiwa vya toten,beach Usongo Pangani ambapo kuna mchanga mzuri halafu waende Magoroto Muheza wanaona vipepeo”Alisema


Hata hivyo alisema jambo hilo ni nzuri na wao wataendelea kumuunga mkono Mkuu wa wilaya ya Tanga huku akieleza kwamba Rais Samia Suluhu ametoa Milioni 500 kwa Jiji la Tanga kwa ajili ya kujenga Machinga Complex.


“Kwa kweli nimpongeza Dc Mgandilwa kwa kuandaa Tanga Utalii Festival ni jambo nzuri lengo lake ni kutaka kuonyesha utamaduni wa Tanga uzuri mila za Tanga nitoe wito kwa wakazi wa Tanga na nje ya Tanga kutembelea vivutio vilivyopo katika mkoa wa Tanga yakiwemo Mapango ya Amboni tunashukuru Mamlaka ya Ngorongoro wanayaboresha kila siku”Alisema


“Lakini Tanga pia tuna kisima cha maji Moto,Beach nzuri za kutembelea,kisiwa cha Toten tunaposema tunataka kulifanya Jiji la Tanga kuwa la mahabaa ukarimu na maendeleo ni kuonyesha mambo mazuri tulionayo ni jambo nzuri na sisi viongozi wenye asili ya Tanga tutakuunga mkono kuhakikisha tunaliboresha kila mwaka”Alisema


Awali akizungumza wakati wa tamasha hilo Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa alisema waliona watumie jukwaa hilo kutangaza fursa za utalii uliopo Jijini Tanga ikiwemo Visiwa,Mapango na Makaburi ya Shabani Robert kwani waliona bado hayajatangaza ipasavyo.


Alisema sambamba na kutangaza vivutio hivyo lakini pia kutangaza Utalii uliopo eneo la Magoroto wilayani Muheza ikiwemo na baadhi ya samaki silikant huku akieleza kuanzishwa kwa tamasha hilo ni kutangaza vivutio vilivyopo kwa wadau.


Mkuu huyo wa wilaya alisema lengo lengine ni kuhamasisha wananchi kupata chanjo na kuhamasisha sensa ya watu na makazi kwa wananachi na wanaamini tamasha hili litakuwa endelevu lengo ni kutangaza utalii .


Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Same Edward Mpogolo alisema wamekuja kumuunga mkono Waziri Ummy kutokana na kazi nzuri anayoifanya nchi na jimbo na wilaya ya Same umekuja kufanya kazi kubwa na nzuri hivyo pia niwahamasisha wananchi kutembelea vuvutio vya utalii vilivyopo nchini.


Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Mwanga Abdallah Mwaipaya Alisema wao kama wakuu wa wilaya za mkoa wa Kilimanjaro wameona kuna umuhimu wa kuja kuunga mkono tamasha hilo.