ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 8, 2016

SAIDA KAROLI "NINA JINA KUBWA LAKINI SINA KITU" + "WALINITUMIA KUJINUFAISHA"

Mwanamuziki nguli wa muziki wa asili toka nchini Tanzania Saida Karoli amesema kwamba asingekuwa hapo alipo (katika umasikini) zaidi ya kuwa mtu mkubwa mwenye msaada kwa jamii ya sasa kwani katika zama zake za kuwika mapromota wote aliofanya kazi nao walimtumia kujinufaisha huku wakimuacha yeye akiambulia patupu kwa kupewa visenti vidogo visivyo na tija kwenye maisha yake ya baadae.


Akizungumza na Kipindi cha Hit Zone kinachorushwa kila siku za jumatatu hadi ijumaa ndani ta Jembe Fm Mwanza wakati akihojwa na Natty E Saida Karoli alifunguka hivi. BOFYA PLAY KUMSIKILIZA.

AMUUA MKEWE KWA SULULU SONGEA.

Mwanamume mmoja wilayani Songea amuua mke wake kwa Sululu kwasababu zinazotajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.

MSANII CHEGE AADHIMISHA SIKU YAKE YA KUZALIWA KWA KUTOA MSAADA KWA HOSPITALI YA TEMEKE JIJINI DAR.

 Msanii wa Muziki wa kizazi kipya kutoka kundi la Wanaume Family, Chege Chigunda akiweka sawa baadhi ya zawadi alikuwa ameziandaa kwa ajili ya Wagonjwa Temeke Hospitali.
 Msanii wa Muziki kutoka kundi la Wanaume Family, Chege Chigunda akizungumza jambo na mmoja ya wauguzi wa Temeke Hospitali jijini Dar.
 Chege na Temba wakiteta jambo mara baada ya kuwasili katika Hospitali ya Temeke
 Chege Chigunda akizungumza na Waandishi wa habari
 Chege Chigunda na baadhi ya Wasanii kutoka kundi la Mkubwa na Wanawe wakielekea wodini.
 Chege Chigunda akiwasiliana na baadhi ya watu kabla ya kuingia wodini
 Msanii wa Muziki wa Bongofleva Mheshimiwa Temba  akitoa zawadi kwa wagonjwa
 Chege Chigunda akitoa baadhi ya Zawadi kwa wagonjwa
 Mh Temba akiingia wodini  kupeleka zawadi kwa Wagonjwa
 Mhe. Temba akigawa zawadi kwa wagonjwa
 Baadhi wasanii kutoka kundi la Mkubwa na Wanawe akitoa zawadi kwa wagonjwa
 Chege Chigunda akiwa amembeba mtoto Hadija Abdalah akiwa na Mama yake Mwanahawa Juma.
Na. Humphrey Shao, blog ya Jamii MSANII wa Muziki wa Bongo Fleva kutoka kundi la Wanaume Family Chege Chigunda , leo ameadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kutembelea hospitlai ya Rufaa ya Temeke na kugawa zawadi mbalimbali katika wodi ya Watoto waliozwa hapo kutokana na matatizo mbalimbali. 

Akizungumza na Mwandishi wa blog hii Mapema leo Hospitalini hapo chege alisema kuwa imekuwa tofauti sana kwa watu kupenda kusheherekea katika nyumba za starehe lakini yeye ameamua kukaa na watoto hao wagonjwa hili kurudisha kile ancho kipata kwa jamii.

“Chege Chigunda aezaliwa leo hivyo ndio maana nipo hapa motto wa Mama Said kushherekea siku yangu ya kuzaliwa na wagonjwa kwa kutoa zawadi mbalimbali kama mnavyoziona Pampers , Dawa za Mswaki na Dawa kwa ajili ya wagonjwa ambao awana uwezo wa kujijinunuli a hivyo katika siku ya leo wamepata fursa ya kununuliwa madawa na mimi” anasema Chege. 

Anasema kuwa maisha yamebadilika sana na inapaswa watu kurudi nyuma na kufanya yale yaliyoa mazuri yanayompendeza Mungu kwa kusheherekea siku zao za kuzaliwa na watu ambao wanamatazo na wenye uhitaji hili kuweza kuwapa faraja ambayo wakuwa wameikosa kwa muda kutokana na matatizo yaliyowakuta. 

Alimaliza kwa kutoa wito kwa wasanii na watu maharufu kuwa na utamaduni wa kuwakumbuka watu wenye mahitaji mablimbali kila wanapopata nafasi na kiasi kidogo kwani kutoa akuhitaji kuwa na utajiri mkubwa bali ni moyo tu.

RAYMOND AKA RAYVANNY KATUA MWANZA ASUBUHI HII TAYARI KUKISANUKISHA USIKU WA WCB NDANI YA VILLA PARK.

💯.... Eh banaeEeeh @rayvanny ndiyo hivyo keshatua jiji la Sato na Sangara... MWANZAaaaaa kwaajili ya usiku wa leo 8/10/2016 #WasafiClassicParty itakayopigwa Villa Park Resort... Vuta picha @rayvanny + @wcb_wasafi & + UTAMBULISHO WA #jembedjZ + @jj_band + @zarryedosha + Super Kamanyola =🔥💯💯💯🔥 Tupia ile kinowmerNowmer kwani kutakuwa na Red Carpet la WCB pale langoni. Mwambie rafiki awaambie marafiki kwamba #VyumaVimekaza Ili panukie kinowmerNowmer usisahau unyunyu kujimwagia CC:- @jembenijembe @rick_juniour @mkuryamstarabu @gijegije @rama.maganga BILA KUSAHAU MAPISHI YA SAMAKI AINA ZOTE TOKA ZIWA VICTORIA 💯

MAGAZETI YA LEO:- ALIYETOBOLEWA MACHO NA SCORPION KUTOONA TENA, WALIMU KATILI KUIBUA MAZITO, KIPIGO CHA MWANAFUNZI MBEYA CHAIBUA MAPYA,.

YALIYOJIRI MAGAZETINI LEO October 8, 2016.

Aliyetobolewa macho na Scorpion kutoona tena,walimu katili kuibua mazito,kipigo cha mwanafunzi Mbeya chaibua mapya,pata dondoo hapa: 

Magendo yafanywa kwa mbinu mpya,sembe dona si salama,Polisi Lushoto waua majambazi wawili,Pata dondoo za magazeti hapa; 

  Mwalimu Babati ampa mimba mwanafunzi,aliyetobolewa macho na Scorpion aliza wengi,Mkasa wa Scorpion Makonda amwaga machozi; 

MD KAYOMBO ABAINI UBADHILIFU WA MAPATO KATIKA DUKA LA DAWA HOSPITALI YA SINZA

 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alipotembelea wodi ya wanawake
Watumishi, wauguzi na madaktari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo alipozuri katika hospitali ya Manispaa ya Ubungo kwa ziara ya kikazi.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akiwasili Ofisi za Manispaa ya Ubungo

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo Akitoa maelekezo wakati akikagua ufanisi wa kazi katika Hospitali ya Manispaa ya Ubungo
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisikiliza kwa makini maelezo ya jinsi wanawake wanavyohudumiwa katika wodi ya wanawake

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Duka la Dawa za Binadamu lililopo katika Hospitali ya Manispaa ya Ubungo iliyopo katika Mtaa wa Sinza Jijini Dar es salaam limekutikana na unadhilifu wa fedha za Umma kinyume na utaratibu wa matumizi ya fedha hizo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo ameyabaini hayo baada ya kukagua mapato na matumizi ya Duka hilo na kugundua uwapo wa ubadhilifu huo mdogo mdogo ambao ameahidi kutuma mkaguzi wa ndani ili kukagua hesabu za duka hilo.

MD Kayombo amebainisha hayo wakati wa kikao cha kazi na watumishi wa Hospitali hiyo mara baada ya kuzuru na kuwa na kikao cha pamoja ili kukumbushana majukumu ya kazi ikiwa ni pamoja na kujitambulisha ili kisikiliza kero za watumishi hao na kuzitafutia ufumbuzi.

Kayombo amebaini kuwa Duka hilo la Dawa za binadamu katika Hospitali ya Manispaa ya Ubungo lina Account mbili zilizofunguliwa kwa ajili ya matunzo ya fedha za mauzo jambo ambalo sio sahihi kisheria katika Taasisi moja ya serikali kuwa na Account mbili za Bank.

MD Kayombo ameahidi kubadilisha Mfumo wa kukusanya Mapato katika Hospitali hiyo kuhamia mfumo wa kisasa ili Serikali iweze kukusanya fedha za kutosha ambapo mfumo wa sasa mapato mengi yanapotea kwani kufanya hivyo itarahisisha Hospitali hiyo kuweza kujisimamia katika maswala ya matumizi madogo madogo na kuweza kuongeza uwezo wa kunua dawa za kutosha kwa mahitaji husika.

Kuhusu kutoa na kupokea Rushwa MD Kayombo amesema kuwa hakuna asiyetambua kuwa jambo hili linawanyima haki wananchi wengi wanyonge hivyo watumishi wote katika Hospitali hiyo wameonywa kujihusisha na kadhia hiyo kwani endapo mtumishi yeyote atabainika kufanya hivyo atachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo ili kuwa fundisho kwa wengine.

"Watumishi wote mnatakiwa kuwa Clean Officials katika mazingira ya kazi hivyo ni lazima kujiepusha na ubadhilifu wa fedha za Umma kwani kila mmoja anapaswa kuridhika na kipato anachopata, Pia nawaahidi kila mmoja kumpatia Extra Duty Allowance kulingana na Bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017.

MD Kayombo ametembelea Wodi zote Hospitalini hapo na kujionea hali halisi ya utoaji huduma ambapo pia ametembelea Ofisi zote zinazotoa huduma na kukutana na wataalamu mbalimbali ambapo wameelezea changamoto zao jambo ambalo Mkurugenzi huyo ameahidi kulifanyia kazi haraka iwezekanavyo kwani lipo ndani ya uwezo wake.

Md Kayombo Amewaonya Wakuu wa Idara kuacha tabia ya kuwanyanyasa na kuwagawa watumishi katika sehemu za kazi ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi katika kuwahudumia wananchi.

Kwa upande wao baadhi ya watumishi katika Hospitali hiyo wamempongeza Mkurugenzi huyo wa Manispaa ya Ubungo kwa ziara yake katika Hospitali hiyo kwani amekuwa Mkurugenzi wa kwanza kuzuru Hospitalini hapo na kujionea hali halisi ya utoaji huduma na sio kusimuliwa.

MD Kayombo ametoa namba ya simu kwa ajili ya matumizi ya dharura kwa watumishi hao ili waweze kuripoti matukio ya haraka ambayo yanakuwa nje ya uwezo wao.

RAIS DKT MAGUFULI AKUTANA NA MABALOZI WANAOWAKILISHA TANZANIA NCHI ZA NJE

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga alipowasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam kwa minajili ya kuzungumza na Mabalozi wanaowakilisha Tanzania nchi za nje
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Eng. John Kijazi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akingia kwenye ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam kwa minajili ya kuzungumza na Mabalozi wanaowakilisha Tanzania nchi za nje
 Sehemu ya makatibu wakuu na mabalozi wanaowakilisha Tanzania nchi za nje wakiwa ukumbini
 Sehemu ya mabalozi wanaowakilisha Tanzania nchi za nje wakiwa ukumbini
 Mnadhimu Mkuu wa JWTZ  Luteni Jenerali Venance Mabeyo (kati) na  Bw. Alphayo Kidata, Kamishna Mkuu wa TRA (kulia) na maofisa wengine waandamizi wakiwa ukumbini
  Sehemu ya mabalozi wanaowakilisha Tanzania nchi za nje wakiwa ukumbini
  Sehemu ya maofisa Ubalozi wanaowakilisha Tanzania nchi za nje wakiwa ukumbini
 Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Cliford Tandari (kulia) na maofisa wengine ukumbini hapo
  Sehemu ya maofisa Ubalozi wanaowakilisha Tanzania nchi za nje wakiwa ukumbini
 Kaimu  Mkurugenzi  Idara ya Itifaki Bw.. James Bwana akiwa na mabalozi wakurugenzi wa Idara mbalimbali Wizarani
 Balozi wa Tanzania nchini Urusi Luteni Generali Wyjones Kisamba akisimama wakati mabalozi wakitambulishwa 
  Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Mhe,Wilson M.Masilingi akitambulishwa
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe Angela Kairuki, Katibu mkuu wake Dkt. Laurian  Ndumbaro, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Juma Assad na viongozi wengine wakiwa ukumbini

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Ponary Mlima akiwatambulisha mabalozi
 Sehemu ya mabalozi hao
 Wajumbe wa mkutano huo
 Mabalozi
 Wajumbe wa mkutano
 Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa
 Maofisa toka Sekretarieti ya Maadili,
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akisoma risala yake
 Wajumbe wakifuatilia kwa makini
 Waziri Mkuu Mhe Kasssim Majaliwa akiongea na wajumbe
  Waziri Mkuu Mhe Kasssim Majaliwa akiongea na wajumbe
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na wajumbe
 Sehemu ya Mabalozi ambao ni wakurugenzi wa Idara mbalimbali
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wajumbe
 Sehemu ya mabalozi wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Mabalozi wakifuatilia hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua jambo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea na hotuba
 Mabalozi wakinakiri kwa makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Mabalozi wakinakiri kwa makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Mabalozi wakinakiri kwa makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Mabalozi wakinakiri kwa makini hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Kila mtu alikuwa makini wakat wa hotuba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Kila mtu alikuwa makini wakat wa hotuba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Kila mtu alikuwa makini wakat wa hotuba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua jambo