ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, December 7, 2023

MBUNGE KOKA ASHUKA NA NEEMA YA SERIKALI AKABIDHI GARI HOSPITALI YA RUFAA TUMBI


VICTOR MASANGU/PWANI/TUMBI HOSPITALI teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi iliyokuwa inakabiliwa na changamoto ya usafiri wa uhakika kwa watumishi wake hatimaye imepata msaada wa gari jipya ambalo limetolewa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuboresha sekta ya afya. Hayo yamebainishwa na Mganga mfawidhi wa hospitali ya Tumbi wakati wa halfa fupi ya kukabidhiwa gari hilo na mgeni rasmi Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji Silvestry Koka kwa niaba ya serikali ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya CCM kwa vitendo.  

Amani Malima ni Mganga Mfawidhi hospitali ya Rufaa ya Tumbi.

Benedicto Ngaiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani. 

Silvester Koka ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini.

Robert Shilingi ni Mkurugenzi wa Shirika la Elimu Kibaha.

HOSPITALI teule ya rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi iliyopo Wilayani Kibaha ilianzishwa mnamo mwaka 1967 ambapo kwa sasa inawahudumia wagonjwa zaidi ya 500 kwa siku kutoka maeneo mbali mbali.

KOKA AKABIDHI GARI JIPYA LILILOTOLEWA NA RAIS SAMIA HOSPITALI YA RUFAA TUMBI


NA VICTOR  MASANGU KIBAHA

Mbunge wa jimbo la Kibaha mjini katika kuendelea kuboresha sekta ya afya kwa wananchi wake leo amekabidhi rasmi gari maalumu aina ya Land cruser kwa ajili ya kusaidia shughuli mbali mbali katika Hospitali teile ya rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
Koka amekabidhi gari hilo kwa niaba ya serikali ya awamu ya sita ikiwa zimetolewa na Rais DKt. Samoa Suluhu Hassan kwa lengo la kuweza kusaidia masuala mbali mbali ya afya katika hospitali hiyo ya Tumbi.

Alisema kuwa gari hiyo ambayo imetolewa na Rais itaweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika kuongeza ufanisi zaidi katika suala zima la kuwahudumia wananchi pamoja na kutimiza wajibu wao

Pia alisema katika hospitali ya Tumbi bado inskabiliwa na changamoto ya usafiri kwa wagonjwa  wanaokwenda kutibiwa hivyo amesema atalivalia njuga na kulipambania jambo hilo kwa kushirikiana na serikali.

Katika sherehe hiyo ya makabidhiano ambayo  imehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali,madaktari pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) sambamba na wananchi.

Pia Koka alibainisha kwa kipindi cha miaka miwili na nusu wamepokea shilingi bilioni 6.8 ambazo zimeletwa katika kibaha mji kwa ajili ya kuboresha huduma ya afya na kuweza kufanya mambo mbali mbali ikiwemo ununuzi wa vifaa tiba pamoja na kufanya ukarabati wa miundombinu ya majengo ya dharura na wagonjwa mahututi.


"Kwa kweli napenda kumshukuru kwa dhati Rais wa awamu ya sita DKt kwa kutoa fedha ambazo kwa kiasi kikubwa zimeweza kusaidia mambo ya kuboresha huduma katika hospitali ya Tumbi,"alisema Koka.

Kadhalika alisema Rais wa awamu ya sita ameweza kupambana kwa ajili ya kutoa fedha kwa lengo kufanikisha kujenga miradi mbali mbali ikiwemo  zahanati na vituo vya afya.
Alisema kuwa ili kuweza  kuleta mafanikio makubwa katika huduma ya afya ni lazima kufanya kazi kwa bidii kuanzia ngazi za chini  lengo ikiwa ni kuwapatia wananchi huduma bora ya afya.

 Mbunge huyo alisema lengo lake kubwa ni kuhakikisha anaboresha zaidi huduma ya afya na kwamba alishawahi kuchangia vifa tiba mbali mbali kwenye kituo cha afya mkoani vilivyogharimu milioni 700.

Kwa upande wake Mganga mfawidhi wa Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi Amani Malima alisema kwamba gari hilo litaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuendeshea shughuli mbali mbali za kuwahudumia wagonjwa.


Aidha Mganga huyo alisema kuwa Hospitali hiyo ya tumbi ambayo ilianzishwa mnamo mwaka 1967 imekuwa ikiwaudumia zaidi ya wagonjwa 500 kwa siku hivyo kunahitajika magari zaidi ya kutolea huduma.

"Tunamshukuru sana Rais wetu kwa juhudi zake kwa kuweza kutoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa gari hii ambayo itasaidia kumaliza changamoto mbali mbali  za usafiri kwa watumishi na wagonjwa.

Kadhalika alimpongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha kwa kuweza kuwa mstari wa mbele kuwatumikia wananchi na kuwapambania kwa hali na mali katika kuwawekea mazingira mazuri ya kupata matibabu.
Naye Mkurugenzi wa Shirika la elimu Kibaha Robert Shilingi alibainisha uwepo wa huduma wa gari hilo jipya ni moja ya hatua kubwa ya kuchochea kasi ya huduma ya usafiri kwa wagonjwa na watumishi.

Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani tumbi ilianzishwa mnano mwaka 1967 ambapo mwakw 2011 ilipandishwa hadhi ambapo kwa sasa inahudumia wagonjwa zaidi ya 500 kwa siku na kwa sasa ina jumla ya magari 6 ya kutolea huduma.

RC KINDAMBA AWATAKA WANANCHI KUACHA TABIA YA KUWANYANYAPA NA KUWABAGUA WANAOISHI NA VVU

 






Na Oscar Assenga, TANGA

MKUU wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amewaasa wananchi wa mkoa huo kucha tabia ya kuwanyanyapaa na kuwabagua watu wanaoishi na Ugonjwa wa Ukimwi kwenye ngazi ya familia na jamii kwa ujumla.

Wito huo uliotolewa katika Hotuba yake iliyosoma kwa niaba yake Mkuu wa wilaya ya Mkinga Kanali Maulid Surumbu wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani ambapo kimkoa ilifanyika kwenye viwanja vya Tangamano.

Alisema kwamba jamii inapaaswa kuacha kufanya vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vinachangia maambukizi mapya ya VVU.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwamba lazima Watumishi Idara ya Afya waendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa afuasi mzuri wa dawa na kufuatilia kiwango cha VVU kwa wanaopokea huduma wanaowahudumia.

Aidha pia Mkuu huyo wa Mkoa aliitaka Idara ya Afya na Maendeleo ya Jamii kuendelea kuwashauri wananchi ambao hawajui afya zao umuhimu wa kupima afya .

“Lakini pia shirikianeni na wadau waliopo mkoani kufanya kampeni maalumu kwenye maeneo yenye viashiria vya uhatarishi wa maambukzi ya VVU sambamba na kuimarisha utendaji wa kamati shirikishi za Ukimwi katika ngazi za vijii,mitaa,kata na wilaya ili ziweze kuratibu vyema huduma za ukimwi kwenye maeneo yetu”Alisema

Mkuu huyo wa Mkoa alimshukuru Rais Dkt Samia Suluhu kwa kuendelea kujali makundi yote yenye uhitaji maalumu nchini ikiwemo wale walioathirika na ugonjwa wa ukimwi.

“Tumeona kwenye mabanda tuliotembelea jinsi walivyosaidiwa na kuweza kujikita kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi ili waweze kujikimu mahitaji yao ya kila siku na jinsi huduma zinavyotolewa za kuondoa unyanyapaa katika Jamii”Alisema

Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya Ukimwi Kitaifa yamefanyika Mkoani Morogoro yaliobeba kauli Mbiu ya mwaka huu Jamii iongoze kutokomeza Ukimwi na hiyo inahimiza umuhimu wa kutoa nafasi kwa jamii kushika hatamu katika jitihada za kutokomeza ukimwi.

Hivyo ni Rai yangu kwa Asasi za Kiraia ambazo zinashirikisha makundi mbalimbali ya kijamii hasa zenye hatari ya kupata maambukizi ya VVU kuwa mstari wa mbele kwenye kupambana na kutekeleza afua mbalimbali za ukimwi kwenye mkoa huo.

Mratibu wa Ukimwi Mkoa wa Tanga Dkt Suleiman Msangi alisema kwamba maambukizi ya Ukimwi bado ni makubwa katika mkoa huo hivyo wanahitaji wadau wote waongeze mikakati ya kukabiliana na hali hiyo ikiwemo utoaji wa elimu kwenye majukwaa mbalimbali, muhadhara, kiasiasa na dini.

Alisema mkoa wa Tanga wanaendelea na mapambano mbalimbali ya kuhakikisha wanatokomeza maambukizi ya VVU ikiwemo upimaji wa VVU ambao unaendelea kwa wananchi kwenye vituo vya Serikali na Binafsi.

Dkt Msangi alisema kwamba mkoa huo umepata mdau anayefuatilia ndugu mwenye kifua kikuu anayegundulika na ukimwi na dawa za kupunguza makali ya VVU na Ukimwi zinaendelea kutolewa bila malipo kwa mtu yeyote anayegundulika na kuishi navyo.

Wednesday, December 6, 2023

TRA TANGA YAKAMATA MIZIGO YENYE THAMANI YA BILIONI 2.59

 

  Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kanali Maulid Surumbu akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya Shukrani kwa Mlipakodi iliyofanyika kwenye Hotel ya Tanga Beach Resort Jijini Tanga


 Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kanali Maulid Surumbu akizungumza wakati wa maadhimisho ya wiki ya Shukrani kwa Mlipakodi iliyofanyika kwenye Hotel ya Tanga Beach Resort Jijini Tanga







Na Oscar Assenga,TANGA

MAMLAKA ya Mapato Tanzania TRA Mkoa wa Tanga imefanikiwa kukamata mizigo yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.59 Kufuatia doria mbali mbali za kiforodha ziliyofanywa na mamlaka hiyo.

Doria hizo ni moja ya mikakati kabambe ya mamlaka hiyo kuhakikisha wafanyabiashara wanapita njia halali na kulipa kodi ya Serikali.

Akizungumza wakati wa wiki ya shukrani kwa Mlipakodi Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Thomas Masese alisema kwamba miongoni mwa bidhaa zilizokamatwa ni pamoja na vitenge maroba 180 ambayo yalipigwa mnada na kiasi cha Milioni 328.2 kilikusanywa.

Masese alisema kwamba kwa mwaka wa fedha 2022/2023 wamekusanya kiasi cha shilingi Bilioni 214.39 lakini pia kuna changamoto mbali mbali ikiwemo wafanyabiashara kukwepa kodi.

Awali akizungumza katika maadhimishio ya wiki hiyo Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Kanali Maulid Surumbu aliipongeza mamlaka hiyo kwa kuweka utaratibu huo wa siku ya shukrani kwa mlipa kodi kurejesha shukrani kwao.

Alisema walipa kodi ni muhimu kwa Taifa huku akiipongeza mamlaka hiyo kwa ukusanyaji wa kiwango hicho cha kodi kwani kila mwaka wamekuwa na ongezeko la mapato.

“Nikupongeze Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga kazi isingeweza kufanikiwa bila kusimamia vizuri wafanyakazi ambao nao wamefanya kazi kwa waledi kuhakikisha kodi inakusanywa “Alisema

Mwakilishi huyo wa Mkuu wa Mkoa aliwahamasisha waongeze kasi ya kuvuka lengo la kila mwaka ikiwemo kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi zaidi .

“Kwa lengo la kuhakikisha mnaendelea na ongezeko la ukusanyaji wa mapato lakini pia kusanyeji kodi kwa waledi,uwajibikaji uadilifu na kujenga mahusiano ya karibu ya mazuri na walipa kodi”Alisema

Hata hivyo alisema nchi nyingi duniani zinategemeaa kodi kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wake hivyo ni muhimu watanzania watambue kwamba ulipaji wa kodi una manufaa makubwa .

Maadhimisho hayo ya siku y,a mlipa kodi yamekwenda sambamba na utoaji wa vyeti vya kuwatambua wafanyabiashara ambao wanajituma kulipa kodi.

Tuesday, December 5, 2023

TRA PWANI YAIPIGA JEKI HOSPITALI YA WILAYA MKURANGA YATOA KITANDA, MAGODORO,MASHUKA



NA VICTOR MASANGU MKURANGA

Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani imeamua kujikita katika kuboresha sekta ya afya kwa kutoa msaada wa vifaa mbali mbali katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga ikiwemo kitanda maalumu kwa ajili ya kujifungulia wakinama pamoja na magodoro 20.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Pwani Masawa Masatu wakati wa halfa fupi ya kukabidhi msaada huo ikiwa ni ni mwendelezo ya wiki ya kutoa shukrani kwa mlipa kodi wake pamoja na kufanya matendo ya huruma.

Meneja huyo ambaye katika halfa hiyo pia aliambatana na maafisa wengine wa TRA ikiwa sambamba na viongozi wa serikali ambao waliweza kufika katika hospitali hiyo kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha huduma ya afya.

Kadhalika Meneja Masawa alibainisha kuwa pia wamesherekea siku hiyo kwa kutoa pia mashuka 50,Magodoro 20 taupo za kike,pamoja na mahitaji mengine mbali mbali ya msingi vyote vikiwa na zaidi ya milioni tano.

"TRA Mkoa wa Pwanin tupo katika maadhimisho ya  wiki ya shukurani Kwa walipa kodi wetu na leo tumepata fursa ya  kutembelea katika hospitali ya Wilaya ya Mkuranga na tumekabidhi misaada mbali mbali ambayo pia itasaidia kwa wagonjwa hasa kwa wakinamama,"alibainisha Masawa.

Pia aisema kwamba wana tambua kwamba sekta ya afya ni muhimu sana hivyo wana imani misaada hiyo ambayo wameitoa itaweza kupunguza baadhi ya changamoto ambazo zilikuwa zikiikabili hospitali hiyo ya Wilaya ya Mkuranga kwani wagonjwa wataweza kutibiwa katika mazingira rafiki.

Kwa upande wake  Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Angelus Mtewa,alisema kwamba wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upungufu wa vitanda hasa katika wodi ya mama na mtoto.

Alisema kuwa wakati mwingine kutokana na uhaba huo inawalazimu baadhi ya wakinamama muda mwingine kulala wagonjwa watatu katika kitanda kimoja hali ambayo inasababisha msongamano.

Mganga huyo hakusita kuishukuru TRA Mkoa wa Pwani kwa kutumia wiki ya mlipa kodi kwenda kutoa msaada  wa  vifaa mbali mbali ambavyo vitakuwa ni chachu katika kuongeza ufanisi ya kutoa huduma ya matibabu kwa wananchi.

Alisema, jengo la mama na mtoto lilipo katika hosptali hiyo linauwezo wa kuhudumia wanawake 70 Kwa mwezi lakini huudumia wanawake zaidi ya 500  Kwa mwenzi Hali ambayo imesababisha upungufu wa vitanda na baadhi ya vifaa tiba.

"Jengo letu Lina uwezo wa kuhudumia wanawake 70 tu Kwa mwezi lakini tunahudumia wanawake zaidi ya 500 tofauti na mahitaji hivyo wengi wanalala watatu katika kitanda kimoja na unakuta mama amejifungua Kwa upasuaji"alisema Mtewa

Aidha alisema mahitaji ya vitanda vya kuwalaza wanawake baada ya kujifungua ni zaidi ya 50 na kwamba vilivyopo ni vitanda 18 pekee  huku vitanda vya kujifungulia vikiwa nane na mahitaji yakiwa vitanda 20.

"Changamoto nyingine ni jengo letu ni dogo halitoshelezi mahitaji, wanawake wengine wanalala chini na tena wamefanyiwa upasuaji, hivyo tunaishikuru TRA Kwa kutupatia msaada Ila  bado tunahitaji misaada zaidi kutoka kwa wadau wengine,"alisema
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga, Arafa Halifa,aliongeza kwamba msaada ambao wamepatiwa na TRA Mkoa wa Pwani utakuwa ni mkombozi katika kusaidia kupunguza changamoto ya wakinama kujifungua  hasa katika wodi ya wazazi.