NA VICTOR MASANGU MKURANGA
Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Pwani imeamua kujikita katika kuboresha sekta ya afya kwa kutoa msaada wa vifaa mbali mbali katika Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga ikiwemo kitanda maalumu kwa ajili ya kujifungulia wakinama pamoja na magodoro 20.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa TRA Mkoa wa Pwani Masawa Masatu wakati wa halfa fupi ya kukabidhi msaada huo ikiwa ni ni mwendelezo ya wiki ya kutoa shukrani kwa mlipa kodi wake pamoja na kufanya matendo ya huruma.
Meneja huyo ambaye katika halfa hiyo pia aliambatana na maafisa wengine wa TRA ikiwa sambamba na viongozi wa serikali ambao waliweza kufika katika hospitali hiyo kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha huduma ya afya.
Kadhalika Meneja Masawa alibainisha kuwa pia wamesherekea siku hiyo kwa kutoa pia mashuka 50,Magodoro 20 taupo za kike,pamoja na mahitaji mengine mbali mbali ya msingi vyote vikiwa na zaidi ya milioni tano.
"TRA Mkoa wa Pwanin tupo katika maadhimisho ya wiki ya shukurani Kwa walipa kodi wetu na leo tumepata fursa ya kutembelea katika hospitali ya Wilaya ya Mkuranga na tumekabidhi misaada mbali mbali ambayo pia itasaidia kwa wagonjwa hasa kwa wakinamama,"alibainisha Masawa.
Pia aisema kwamba wana tambua kwamba sekta ya afya ni muhimu sana hivyo wana imani misaada hiyo ambayo wameitoa itaweza kupunguza baadhi ya changamoto ambazo zilikuwa zikiikabili hospitali hiyo ya Wilaya ya Mkuranga kwani wagonjwa wataweza kutibiwa katika mazingira rafiki.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Angelus Mtewa,alisema kwamba wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya upungufu wa vitanda hasa katika wodi ya mama na mtoto.
Alisema kuwa wakati mwingine kutokana na uhaba huo inawalazimu baadhi ya wakinamama muda mwingine kulala wagonjwa watatu katika kitanda kimoja hali ambayo inasababisha msongamano.
Mganga huyo hakusita kuishukuru TRA Mkoa wa Pwani kwa kutumia wiki ya mlipa kodi kwenda kutoa msaada wa vifaa mbali mbali ambavyo vitakuwa ni chachu katika kuongeza ufanisi ya kutoa huduma ya matibabu kwa wananchi.
Alisema, jengo la mama na mtoto lilipo katika hosptali hiyo linauwezo wa kuhudumia wanawake 70 Kwa mwezi lakini huudumia wanawake zaidi ya 500 Kwa mwenzi Hali ambayo imesababisha upungufu wa vitanda na baadhi ya vifaa tiba.
"Jengo letu Lina uwezo wa kuhudumia wanawake 70 tu Kwa mwezi lakini tunahudumia wanawake zaidi ya 500 tofauti na mahitaji hivyo wengi wanalala watatu katika kitanda kimoja na unakuta mama amejifungua Kwa upasuaji"alisema Mtewa
Aidha alisema mahitaji ya vitanda vya kuwalaza wanawake baada ya kujifungua ni zaidi ya 50 na kwamba vilivyopo ni vitanda 18 pekee huku vitanda vya kujifungulia vikiwa nane na mahitaji yakiwa vitanda 20.
"Changamoto nyingine ni jengo letu ni dogo halitoshelezi mahitaji, wanawake wengine wanalala chini na tena wamefanyiwa upasuaji, hivyo tunaishikuru TRA Kwa kutupatia msaada Ila bado tunahitaji misaada zaidi kutoka kwa wadau wengine,"alisema
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga, Arafa Halifa,aliongeza kwamba msaada ambao wamepatiwa na TRA Mkoa wa Pwani utakuwa ni mkombozi katika kusaidia kupunguza changamoto ya wakinama kujifungua hasa katika wodi ya wazazi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.