ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, March 11, 2023

RAIS SAMIA AMUAPISHA NAIBU KATIBU MKUU, OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Dkt. Wilson Mahera Charles kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 11 Machi, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimuapisha Dkt. Wilson Mahera Charles kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 11 Machi, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 11 Machi, 2023

KAMANGA HOSPITAL YAKABIDHI VYOO VITANO & MABAFU MATANO KWA KITUO CHA WATOTO WAISHIO MAZINGIRA MAGUMU

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

#KamangaHospital #mwanza #UpendoDaima

WANAWAKE WA SHOKA TANESCO WATISHA WATOA MSAADA KITUO CHA AFYA MKOANI PWANI.



Na Victor Masangu,Pwani


Wafanyakazi Wanawake wa shirika la ugavi wa umeme (Tanesco) Mkoa wa Pwani wametoa msaada wa mahitaji mbali mbali katika kituo cha afya mkoani kilichopo Wilaya ya Kibaha.


Wanawake hao wa Tanesco wameamua kufanya ziara katika kituo hicho kwa ajili ya kuwatembelea wanawake 40 ambao walikuwa wamejifungua katika wodi ya wazazi na kuwapatia msaada wa vitu mbali mbali ikiwemo miche ya sabani,pampasi za watoto na mahitaji mengine.
Mwenyekiti wa wanawake hao wa Tanesco Selina Tarimo alisema kwamba wameamua kwenda kufanya matendo ya huruma katika wodi ya wazazi kwa lengo la kuweza kuwasalimia wakinamama ambao wamejifungua ikiwa pamoja na kuwapatia zawadi mbali mbali.
"Mimi pamoja na wafanyakazi  wenzangu wa Tanesco tumeamua kuja katika kituo hiki cha afya mkoani lengo ikiwa ni kuwatembelea wakinamama 40 ambao wamejifungua na tumewapatia sabuni za unga.sabuni za miche,pampasi za watoto na mahitaji mengine muhimu,"alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha Mwenyekiti huyo alisema wao Kama wanawake wataendelea kushirikiana kwa umoja wao katika kuendelea kufanya matendo ya huruma pamoja na kuwasaidia wakinamama wengine ambao wanakabiliwa na changamoto mbali mbali.

Nao baadhi ya wakinamama ambao wamepatiwa msaada huo wamewashukuru wafanyakazi Wanawake wa Tanesco kwa upendo wao wa kwenda kuwatembelea pamoja na kuwapatia msaada wa mahitaji yao tofauti.

Friday, March 10, 2023

VIJANA MWANZA WAONGOZA KUTAKA KUUZA FIGO 'WAKALE BATA'

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

VIJANA jijini #Mwanza wametajwa kuongoza katika biashara ya kuuza figo kutokana na hali ya ugumu wa maisha. Hayo yamebainishwa na Dr. Bingwa na mbobezi wa magonjwa ya figo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya #Bugando Said Kanenda katika maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani hii leo ambapo amesema wakazi saba kati ya mia moja wa vijijini wanasumbuliwa na ugonjwa figo. Kutokana na uwepo wa takwimu hizo Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando imesema wagonjwa 150 wanapatiwa matibabu katika kliniki ya magonjwa ya figo kila wiki sawa na wagonjwa 600 kwa mwezi ambao hawajaanza atibabu ya kutoa taka mwili.

TASAC YATOA MAFUZO KWA WADAU WA SERIKALI JUU YA MABADILIKO YA KANUNI KATIKA KUDHIBITI VIVUKO VYA SERIKALI

 

Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limeanza kutoa Mafunzo kwa wasimamizi wa Sheria Mkoani Mara ikiwa ni Mkakati wa kujua Mabadiliko ya Sheria mbalimbali za Shirika hilo ambalo kwasasa limepewa jukumu la kusimamia vivuko hapa nchini.

Mkuu wa wilaya ya Musoma Dkt Khalfan Haule amefungua mafunzo hayo na kusema juu ya umuhimu wa kujua Mabadiliko hayo ni ili kutekeleza Majukumu ya usimamizi wa Sheria kwa Haki katika usalama wa Wananchi na Vyombo vya usafiri Majini.





Aidha, Afisa Mfawidhi TASAC Mkoa wa Mara na Simiyu Abed Mwanga amesema zamani vivuko hivyo vilikuwa chini ya sheria ya SUMATRA lakini kwasasa vitasimamiwa na TASAC kwa mujibu wa Sheria na TASAC itaendelea kutoa mafunzo hayo kwa wadau mbalimbali.

SHOTI YA UMEME YAUA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA NYUMBA IKIUNGUA SHINYANGA

 

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Old Shinyanga Rashid Mashaka miaka 14 amefariki dunia baada ya nyumba aliyokuwa amelala kuungua moto.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Machi 10 majira ya saa 6 usiku katika kitongoji cha Senyenge kata ya Old Shinyanga baada ya shoti ya umeme kutokea katika nyumba hiyo kisha moto kuwaka na kuunguza vitu mbalimbali wakati kijana huyo akiwa amelala ndani.

Mama mzazi wa mtoto huyo Fatuma Rajab ambaye hakuwepo nyumbani wakati wa tukio hilo amesema mvua zilizonyesha jana zilisababisha umeme kukatika na uliporejea majira hayo ndipo shoti hiyo ilipotokea kisha nyumba yake kushika moto.

Kamanda wa kikosi cha zimamoto na uokoaji wilaya ya Shinyanga Inspekta Stanley Luhwago amesema kuwa chanzo cha moto huo ni shoti ya umeme iliyoanzia kwenye mita ya nyumba hiyo.

Kijana huyo alikuwa akisoma kidato cha kwanza shule ya sekondari Old Shinyanga.

DR CHINGUILE BILIONI 120 KUTATUA KERO YA MAJI NACHINGWEA.

Mbunge wa Jimbo la Nachingwea DR Amandus Chinguile akifurahia jambo na mwananchi wa Jimbo hilo baada ya kusikia neema ya maji kuwa itawafikia

Na Fredy Mgunda, Nachingwea.


MBUNGE wa Jimbo la Nachingwea Dr Amandus Chinguile Mkoani Lindi amedhamilia kutatua changamoto za maji na afya kwa wananchi wa Jimbo hilo.

Akizungumza wakati wa ziara ya kuwasikiliza wananchi,Dkt Chinguile alisema kuwa Wananchi wamekuwa wanatafuta maji mbali na maeneo wanayoishi


Dkt Chinguile alisema kuwa lengo ni kuhakikisha anawatua ndoo akina mama wa Jimbo la Nachingwea ili kuwawezesha kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo na sio kwenda kutafuta maji mbali au kutumia maji yasiyofaa kwa matumizi ya binadamu

Alisema kuwa suala la maji limekuwa likimuumiza kichwa ndio maana akashirikiana na serikali kuhakikisha wanatafuta mradi mkubwa wa kutatua kero hiyo ya wananchi iliyodumu kwa miaka mingi.

Dkt Chinguile alisema mradi wa maji vijiji 21 utasiaidia kumaliza kabisa kero za wananchi kwenye vijiji hivyo ambavyo vimekuwa vinachangamoto toka kuumbwa kwa dunia.

Alisema kuwa mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 120 kwa vijiji vya Nachingwea na Ruangwa mkoani Lindi ambapo tayari mkandarasi ameshasaini mkataba ambao utatekelezwa kwa muda wa miezi 26.

Dkt Chinguile alimazia kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kimaendeleo anayowaletea wananchi wa Jimbo la Nachingwea na Tanzania kwa ujumla.

Thursday, March 9, 2023

"KAZI YA POLISI SIKU YA MAANDAMANO NI KUCHUNGA RAIA" ASEMA RAILA

 

Raila Odinga amesema kazi ya polisi siku ya maandamano ni kulinda raia. Amesema hayo baada ya kuitisha maandamano kote nchini ya kushinikiza serikali ya Rais Rais William Ruto kuondoka mamlakani. 

Raila alisema siku hiyo polisi wanafaa kuhakikisha kuwa kila mwandamanaji ana usalama wa kutosha. 

 Kiongozi wa Azimio la Umoja Raila Odinga ameitisha maandamano ya umma kote nchini katika kile amesema ni mkondo wa kuiondoa mamlakani Kiongozi huyo amewataka wafuasi wake kujiandaa kwa makabiliano na serikali ya Ruto kwenye maandamano Ametaja kupanda kwa gharama ya maisha, kuteuliwa kwa jopo la kuwatafuta makamishna wa IEBC na kutofunguliwa kwa server za IEBC kama sababu ya kuanza makabiliano na Ruto.

Kiongozi wa Azimio la Umoja Raila Odinga sasa ameitisha maandamano kote nchini kushinikiza serikali ya Rias William Ruto kuondoka mamlakani.

 Kwenye kikao na wanahabari, Raila alisema sasa wafuasi wa Azimio wako huru kuandamana wakilia kuhusu machungu ya serikali ya Ruto. 

"Kuanzia leo Wakenya wanaweza kugoma, au kuandamana na kuenda katika nyumba yoyote ya serikali kupelekea malalamishi yao," alisema Raila. Raila amewataka wafuasi wake kuanza kazi rasmi leo ili kufanikisha ajenda yao. 

"Movement for Democratic Defence inaanza kufanya kazi leo," alisema kiongozi huyo wa Azimio la Umoja. Ametaja kupanda kwa gharama ya maisha, kuteuliwa kwa jopo la kuwatafuta makamishna wa IEBC na kutofunguliwa kwa server za IEBC kama sababu ya kuanza makabiliano na Rais Ruto. 

Azimio wametangaza kwamba kutakuwa na maandamano makubwa jijini Nairobi Machi 20. "Wafuasi wote wa Azimio Kenya yote watakutana jijini Nairobi Machi 20 kwa maandamano ya kukataa Ruto," alisema Raila. 

MALALA AWALAUMU RAILA NA UHURU KWA HALI NGUMBU YA KIUCHUMI WANAYOPITIA WAKENYA

 

Katibu Mkuu wa UDA Cleophas Malala.

Katibu Mkuu wa chama cha UDA Cleophas Malala amesema kuwa wanostahili kulaumiwa kwa hali ngumi ya uchumi nchini ni Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta na Kinara wa Azimio Raila Odinga. 

 Malala aliyezungumza wakati wa mahojiano na runinga ya Citizen amesema kuwa ukiritimba katika biashara wanazozifanya Kenyatta na Odinga ndicho chanzo cha bei za bidhaa muhimu kuongezeka. "Hawa ndio viongozi wenye ukiritimba wa biashara nchini Kenya na ni wao wanaolalama kuhusu bei ya bidhaa kuwa juu. 

Wanalalama kuhusu bei ya juu ya chakula ilihali wanajuwa anayemiliki kampuni ya maziwa ya Brooksie, wanalalama kuhusu hali ngumu ya maisha wakati wanajua nani anayemiliki biashara ya gesi nchini.

 Iwapo viongozi hawa ni wa kweli kwa nini wasianze na kupunguza bei ya gesi," Malala alisema.

 Sababu ya Ababu Namwamba Kutengana na Pris... Malala Jumatano akihutubia wanahabari alidai kuwa bei ya unga ilikuwa juu kwa sababu fedha zilizotolewa kugharamia ruzuku ya bidhaa hiyo katika serikali ya Kenyatta hazikuwafikia wazalishaji kwani fedha hizo zilifujwa. 

"Tunataka kabla ya maandamano watu wote wanaoenda maandamao wakuje na gunia Raila awawekee ile mahindi ambayo ameficha katika magala," Malala alisema katika hotuba yake ya Jumatano. 

Hili si tukio la kwanza kwa kiongozi wa Kenya Kwanza kuwarushia lawama viongozi wa Azimio na maafisa wakuu waliohudumu katika serikali ya Rais mstafuu Uhuru Kenyata. 

Azimio inapoendeleza shinikizo zao za kutaka serikali kuwakwamua Wakenya kutoka kwa hali ngumu ya kiuchumi baadhi ya viongozi serikalini wameendelea kulaumu uongozi wa serikali ilioondoka kama chanzo cha matatizo wanayopitia Wakenya. 

WAFANYAKAZI SF GROUP WAFANYA MATENDO YA HURUMA KIBAHA KWA WANAFUNZI WA KIKE NA WATOTO YATIMA.

 


Na  Victor Masangu,Kibaha 
Baadhi ya wanafunzi  wa kike wanaosoma katika shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya mji Kibaha bado wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia pamoja na ukosefu wa mahitaji muhimu ikiwemo taulo za kike.

Kwa kuliona hilo wafanyakazi wanawake wa kampuni  ya SF Group ya Jijini Dar es Salaam wameamua kutumia maadhimisho siku ya wanawake duniani kufanya matendo ya huruma katika kata ya sofu kwa baadhi ya maeneo.


Wafanyakazi hao wa  SF group ambao wameona kuna haja ya kuitumia siku hiyo hivyo kuungana kwa pamoja na kwenza kutoa misaada mbali mbali kwa wanafunzi wa shule ya Koka sekondari  pamoja na kituo Cha watoto yatima na wanaishi katika mazingira magumu.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi wenzake katika ziara hiyo Aisha Kanyika alisema kwamba wametoa msaada wa vitu mbali mbali katika shule ya Koka sekondari ikiwemo taulo kwa ajili ya wanafunzi wa kike ili ziweze kuwasaidia kusoma katika mazingira rafiki.


"Mimi pamoja na wenzangu tupo hapa kwa ajili ya kutoa msaada wa vitu mbali mbali katika shule hii ya Koka sekondari na pia tunamshukuru Mwenyekiti wetu wa SF mheshimiwa Koka pamoja na mkewe ambao wameweza kuhakikisha wanafanikisha shughuli hii,"Alibainisha Aisha.

Aidha Aisha alisema kwamba lengo lao ni kuendelea kuisaidia jamii katika nyanja mbali mbali na kuwahasa wanafunzi wa kike kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza malengo ambayo wamejiwekea katika siku za baadae na kuwa ni nidhamu kwa walimu wao.


Pia katika ziara hiyo wafanyakazi hao walitembelea kituo Cha watoto yatima na ambao wanaishi katika mazingira magumu ambapo walitoa msaada wa vyakula mbali mbali ikiwemo unga,mafuta ya kupikia,madaftari,maji ya kunywa,miswaki na mahitaji mengine muhimu pamoja na fedha.

Naye Kaimu mwalimu mkuu wa shule ya Koka Sekondari Godwin Magoha aliwashukuru wafanyakazi hao kwa moyo wa kujitolea na kwenda kutoa msaada wa vitu mbali mbali ambavyo vitakuwa ni msaada hasa kwa watoto wa kike.

Kwa upande wake Mkurugenzi ambaye pia ni mmiliki wa kituo cha Buloma  Anna Kiando amebainisha kwamba amefurahishwa sana na kitendo cha wafanyakazi hao wa SF Group kutenga muda wao na kutoa msaada kwa watoto hao ambao kwao ni mkombozi mkubwa kulingana na mahitaji waliyopatiwa.

Elina Mgonja ni Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mji naye hakusita kuwapongeza wafanyakazi hao kwa kuonyesha uzalendo kwa watu wenye mahitaji pamoja na kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji Silvestry Koka pamoja na mke wake kwa kusaidia makundi ya watu wenye mahitaji.


Ziara ya wafanyakazi wanawake wa kampuni ya SF Group katika kata ya sofu imeleta neema kubwa kwa wanafunzi wa kike katika shule ya Koka sekondari pamoja na kituo cha watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu cha Buloma kutoka na misaada waliyopatiwa.

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ahutubia katika Baraza la Wanawake CHADEMA, Moshi Mkoani Kilimanjaro


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi mbalimbali wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) pamoja na Wanachama wa Chama hicho kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 08 Machi, 2023. 




 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe pamoja na viongozi wengine wa Baraza la Wanawake la Chama hicho BAWACHA mara baada ya kuhutubia kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 08 Machi, 2023. 

 


 viongozi mbalimbali pamoja na Wajumbe wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan Moshi mkoani Kilimanjaro katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani tarehe 08 Machi, 2023.

 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Tuzo ya Maridhiano kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe aliyeikabidhi kwa niaba ya Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) mara baada ya kuwahutubia kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 08 Machi, 2023. 

 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe, pamoja na viongozi mbalimbali wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) mara baada ya kuwahutubia kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Moshi Mkoani Kilimanjaro tarehe 08 Machi, 2023. 


Wednesday, March 8, 2023

MWANAMKE JEMBE - MAFANIKIO YAMO NDANI YAKO

 


Heri ya siku Wanawake Dunia, Ewe #Mwanamkejembe Tambua  #Mafanikioyamondaniyako2023 Simama Imara kama ambavyo Rais wetu Mh.Dkt @samia_suluhu_hassan amekuwa Mwanamke wa Mfano Tanzania, Afrika na Dunia nzima Hakika ni Mwanamke Jembe.

.

.

#Mwanamkejembe 

#Mafanikioyamondaniyako2023 

#jembefm2023kimewaka🔥🔥🔥

MHE. RAIS SAMIA AKISHIRIKI KONGAMANO LA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI - MOSHI, KILIMANJARO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Kongamano la Siku ya Wanawake Duniani lilioandaliwa na Baraza la Wanawake wa CHADEMA ( BAWACHA) katika Ukumbi wa Kuringe - Mkoa wa Kilimanjaro leo tarehe 08 Machi, 2023.

TANZIA TANZIA


Klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC) inasikitika kutangaza kifo cha Mwanachama wake Richard Makore kilichotokea jana lwenye ajali ya gari (Min bus) iliyotokea Mkoani Geita.


Makore alikuwa anafanya kazi na Gazeti la Nipashe Mwanza na pia ni Mwanachama hai wa MPC.


Kwa sasa mwili wake upo kwenye chumba cha kuhifadhi Maiti hospitali ya Geita.


MPC inawaomba wanachama wake wote kuwa watulivu kwenye wakati huu mgumu kwetu.


Pia MPC inaendelea kuwajuza kila hatua ya inayoendelea.


Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihidimiwe.


 Edwin Soko 

 Mwenyekiti 

 MPC 

 8.03.2023








Tuesday, March 7, 2023

ACT WAZALENGO YAITAKA SERIKALI KUPITIA UPYA MFUMO WA TAASISI ZA MIKOPO NCHINI

 

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Tanzania Bara Dorothy Samu  ambaye pia ni Waziri Mkuu Kivuli akizungumza leo wakati wa Kongamano la Kitaifa la Wanawake wa ACT lililofanyika Jijini Tanga ambapo alisema mikopo hiyo badala ya kuwa mkombozi kwa wanawake imekuwa mizigo kwao.


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Tanzania Bara Dorothy Samu ambaye pia ni Waziri Mkuu Kivuli akizungumza leo wakati wa Kongamano la Kitaifa la Wanawake wa ACT lililofanyika Jijini Tanga ambapo alisema mikopo hiyo badala ya kuwa mkombozi kwa wanawake imekuwa mizigo kwao.

aziri Kivuli wa Wizara ya Wanawake,Watoto na Makundi Maalumu Janeth Rite akizungumza wakati wa kongamano hilo

Na Mwandishi Wetu,TANGA
 

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo Tanzania Bara Dorothy Samu ameitaka Serikali kupitia upya mfumo  mzima wa Taasisi zisizo za Kiserikali zinazotoa mikopo na kuangalia riba zao kutokana na kuwa zimekuwa mzigo kwa wanawake na kupelekea kushindwa kurejesha na wakati mwengine kukimbia familia zao

Dorothy ambaye pia ni Waziri Mkuu Kivuli aliyasema hayo leo wakati wa Kongamano la Kitaifa la Wanawake wa ACT lililofanyika Jijini Tanga ambapo alisema mikopo hiyo badala ya kuwa mkombozi kwa wanawake imekuwa mizigo kwao.

Alisema kwa lazima Serikali iangalie kwa umakini riba ambazo zimetolewa na taasisi hizo ambayo sio himilivu na sio rafiki kwa wanawake ambao ndio wakopaji wakubwa katika kuendeleza biashara zao za ujasiriamali.

“katika hili tunaitaka Serikali kuangalia kwa umakini taasisi za mikopo ambazo zimekuwa riba kubwa na kupelekea kushindwa kurejesha na kukimbia familia zao hili ni tatizo liangalie hasa ile inayoitwa Kausha Damu “Alisema

Awali akizungumza Waziri Kivuli wa Wizara ya Wanawake,Watoto na Makundi Maalumu Janeth Rite aliitaka Serikali kuhakikisha Halamshaueri zinakuwa na uwiono sawa katika utoaji wa fedha za mikopo asilimia 10 zinazotokana na mapato ya ndani.

Alisema kwa sababu hali ilivyo hivi sasa imekuwa ikiwabagua baadhi ya wananachi kutokana na itikadi ya vyama vyao jambo ambalo sio nzuri kwa ustawi wa maendeleo hapa nchini.

“Suala hilo la mikopo zinazotoka kwenye Halmashauri lazima kuwepo na usawa pamoja na kuondosha upendeleo ambao umekuwa ukipelekea manunguniko kwa wanawake kutokana na itikadi zao za kiasiasa”Alisema

Waziri huyo alisema kwamba kwa mujibu wa takwimu zilizopo ni asilimia 80 ya wanawake wapo kwenye  sekta ya kilimo ambao wanalima kwa kutumia jembe kilimo ambacho hakina tija kwao kutokana na kupata mazao hafifu.

Alisema kwa sababu hakina tija ndio maana Chama hicho katika mipango tyao watakapo pata ridhaa ya kuongoza nchi watawaondoa kwenye ujasiriamali usiokuwa na tija ikiwemo kuwapeleka wenye tija ambao wanaweza kukopesheka.

“lakini pia Serikali iweze kuona namna nzuri ya kutoa mikopo kwa wakina mama ili waweze kuongeza wigo mpana wa uzalishaji mazao ya chakula ndipo itapoondosha  changamoto zao za kiuchumi “Alisema

Hata hivyo alisema wakina mama wakiendelea kutumia jemnbe la mkono wasahau mafanikio yao kupitia sekta ya kilimo kutokana na kwamba kuna haja ya kubadilika kwa kulima kisasa

MTOTO ALIYEKUWA AKIUGUA MALARIA AFARIKI DUNIA AKIOMBEWA NA PASTA ILI APONE.


Hali ya huzuni ilighubika kijiji cha Magamba Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, Tanzania kufuatia kifo cha mtoto mwenye umri wa miaka 16.

 Consolata Charles amefariki dunia wakati alipokuwa akipokea huduma ya maombi nyumbani kwa mchungaji. 

Inaripotiwa kwamba kuwa vipimo vya awali vya hospitali vilionesha kuwa mtoto huyo alikuwa akiugua Malaria pamoja na UTI. 

Alipewa rufaa ya kwenda hospitali kubwa lakini aliruhusiwa kurejea nyumbani ambapo mlezi wake alipoamua kumpeleka kwa mchungaji kuombewa.

Kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini humo, wazazi wa mtoto huyo pamoja na ndugu na majirani walisema marehemu alilazwa hospitalini mara kadhaa na baadaye kuruhusiwa kurudi nyumbani. 

Lakini baada ya muda alianza kuugua tena na hali yake kudhoofika hivyo kuwalazimu wazazi wakewake kumpeleka kwa mchungaji kuombewa.