ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, March 9, 2023

MALALA AWALAUMU RAILA NA UHURU KWA HALI NGUMBU YA KIUCHUMI WANAYOPITIA WAKENYA

 

Katibu Mkuu wa UDA Cleophas Malala.

Katibu Mkuu wa chama cha UDA Cleophas Malala amesema kuwa wanostahili kulaumiwa kwa hali ngumi ya uchumi nchini ni Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta na Kinara wa Azimio Raila Odinga. 

 Malala aliyezungumza wakati wa mahojiano na runinga ya Citizen amesema kuwa ukiritimba katika biashara wanazozifanya Kenyatta na Odinga ndicho chanzo cha bei za bidhaa muhimu kuongezeka. "Hawa ndio viongozi wenye ukiritimba wa biashara nchini Kenya na ni wao wanaolalama kuhusu bei ya bidhaa kuwa juu. 

Wanalalama kuhusu bei ya juu ya chakula ilihali wanajuwa anayemiliki kampuni ya maziwa ya Brooksie, wanalalama kuhusu hali ngumu ya maisha wakati wanajua nani anayemiliki biashara ya gesi nchini.

 Iwapo viongozi hawa ni wa kweli kwa nini wasianze na kupunguza bei ya gesi," Malala alisema.

 Sababu ya Ababu Namwamba Kutengana na Pris... Malala Jumatano akihutubia wanahabari alidai kuwa bei ya unga ilikuwa juu kwa sababu fedha zilizotolewa kugharamia ruzuku ya bidhaa hiyo katika serikali ya Kenyatta hazikuwafikia wazalishaji kwani fedha hizo zilifujwa. 

"Tunataka kabla ya maandamano watu wote wanaoenda maandamao wakuje na gunia Raila awawekee ile mahindi ambayo ameficha katika magala," Malala alisema katika hotuba yake ya Jumatano. 

Hili si tukio la kwanza kwa kiongozi wa Kenya Kwanza kuwarushia lawama viongozi wa Azimio na maafisa wakuu waliohudumu katika serikali ya Rais mstafuu Uhuru Kenyata. 

Azimio inapoendeleza shinikizo zao za kutaka serikali kuwakwamua Wakenya kutoka kwa hali ngumu ya kiuchumi baadhi ya viongozi serikalini wameendelea kulaumu uongozi wa serikali ilioondoka kama chanzo cha matatizo wanayopitia Wakenya. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.