ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 17, 2012

MSTAHIKI MEYA WA JIJI LA MWANZA AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA MWILI WA MAREHEMU MMACHINGA ALIYEUAWA KWA RISASI, MWILI WASAFIRISHWA LEO KUELEKEA KIBONDO.


Mstahiki meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula ambaye pia ni diwani wa kata ya Mkolani (CCM) akizungumza na wakazi wa Isegege 'A'  kata ya Mahina jijini Mwanza wakati wa ibada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Daudi Balenga Patrick (28) maarufu kwa jina la 'Greda' mmachinga aliyeuawa kwa risasi hivi majuzi kwenye purukushani za wamachinga na mgambo wa jiji la Mwanza. Ipate sauti Bofya Play.


Wakazi wa Isegege 'A'  kata ya Mahina jijini Mwanza waliokusanyika wakimsikiliza mheshimiwa Mstahiki Meya wakati wa ibada ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Daudi Balenga Patrick (28) maarufu kwa jina la 'Greda' mmachinga aliyeuawa kwa risasi hivi majuzi kwenye purukushani za wamachinga na mgambo wa jiji la Mwanza.


Diwani wa kata ya Igoma Adam Chagulani (CHADEMA) akiongoza safu ya viongozi nyuma yake akifuatiwa na Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula kwenye hatua za wanajamii kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Daudi Balenga Patrick (28) maarufu kwa jina la 'Greda' mmachinga aliyeuawa kwa risasi hivi majuzi kwenye purukushani za wamachinga na mgambo wa jiji la Mwanza.


Bi. Flora Michael ambaye ni mke wa marehemu akilia kwa uchungu wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu mumewe Daudi Balenga Patrick (28) maarufu kwa jina la 'Greda' mmachinga aliyeuawa kwa risasi hivi majuzi kwenye purukushani za wamachinga na mgambo wa jiji la Mwanza.


Akina mama wakishiriki kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Daudi Balenga Patrick (28) maarufu kwa jina la 'Greda' mmachinga aliyeuawa kwa risasi hivi majuzi kwenye purukushani za wamachinga na mgambo wa jiji la Mwanza.


Ibada ya kutoa heshima za mwisho ikiendelea ambapo halmashauri ya jiji la Mwanza pamoja na kutoa usafiri (gari) kuusafirisha mwili wa marehemu hadi kijijini kwao Kumuhasha wilaya ya Kibondo kata ya Murungu mkoani kigoma, pia imetoa kiasi cha shilingi 500,000/= kama ubani kwa msiba huo uliotokea.


Marafiki wakiuaga mwili wa mpendwa wao.


Vijana wa kata hiyo nao wamehudhuria ...


Utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu Daudi Balenga Patrick (28) maarufu kwa jina la 'Greda' ukiendelea.


Bi. Flora Michael ambaye ni mke wa marehemu akilia kwa uchungu huku akisaidiwa na nduguze.


Msemaji wa familia Bw. Onesmo Birago ambaye ni babu wa Marehemu akitoa utaratibu wa ndugu na jamaa watakao ambatana kuusafirisha mwili huo hadi  kijijini kwao Kumuhasha wilaya ya Kibondo kata ya Murungu mkoani kigoma kwaajili ya mazishi.
Mzee Patrick Balenga ambaye ni baba wa marehemu (wa tatu kutoka kushoto mwenye koti) akiwa na watoto wake sita waliobakia. Marehemu Daudi 'Greda'alikuwa ni mtoto wa kwanza.

BADO ELIMU INAHITAJIKA KUPAMBANA NA UNYANYASAJI WA WENYE ULEMAVU WA NGOZI

Majuzi kamera ya blogu hii ilikuwa sehemu ya kipindi cha Radio Maria kilichorushwa hewani live kutoka Mwanza toka Parokia ya Kirumba, Mada kuu ilikuwa kujadili ni namna gani ya kuwanususru ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi toka kwenye lindi la manyanyaso linalowakabili toka kwa baadhi ya familia hapa nchini.

  Tanzania kwa muda mrefu imekuwa ikisomeka kuwamiongoni mwa nchi ambazo zimefanikiwa kulinda amani na utulivu wa nchi, lakini baada ya kutokea kwa mauaji ya ndugu zetu hawa wenye ulemavu wa ngozi maeneo ya kanda ya ziwa, taswira imebadilika kwa kuchafua uhalisia wa amani ya nchi.

Ingawa kwa sasa lile wimbi la mauaji yenye nia ya kuchukuwa viungo vya miili ya albino limedhibitiwa lakini bado ndugu zetu hawa wanakabiliana na tatizo jingine la unyanyapaa, suala ambalo limekuwa sugu na kuwaathiri wengi kulingana na maeneo wanayoishi watu hao.

Unyanyapaa umekuwa na viwango vyake na uko kwenye madaraja.. kwani kwa maeneo ya mijini suala la unyanyapaa limedhibitiwa kupitia usambaaji wa elimu itolewayo kupitia radio mbalimbali, majarida, makongamano na mitandao ya kijamii tofauti na ngazi ya wilayani na vijijini ambako mijadala imekuwa michache na upashaji habari hauna nyenzo za kuwafikia wananchi.

Walemavu wengi wa ngozi, ngozi zao kushindwa kuhimili mionzi ya jua hivyo kushambuliwa na maradhi ya kansa ya ngozi na kadhalika, pamoja na kuwa na uoni hafifu unaowapa shida kujisomea au kupata elimu darasani wamejikuta wakitengwa na ndugu zao na hata jamii zinazo wazunguka kutokana na jamii hizo kutopewa elimu ya kutosha inayowawezesha kuwatambua.

Wengi bado wana fikra potofu kwamba kuwa albino ni laana.

Elimu bado inahitajika ndugu zangu. 

Friday, November 16, 2012

MADUKA 10 MTAA WA LIBERTY JIJINI MWANZA YAKAMATWA YAKIUZA NYEMBE FEKIAskari polisi jijini Mwanza wakiwa na wakaguzi kutoka FCC kuhakiki ubora wa bidhaa ya nyembe zinazotengenezwa na kampuni ya Super Max.
 BIDHAA zinazotengenezwa na Kampuni ya Super Max ya nchini Dubai imegudua bidhaa zake za Nyembe kuchakachuliwa na kuuzwa katika baadhi ya maduka ya jumla katika mikoa mbalimbali hapa nchini huku Jijini Mwanza maduka kumi yakikutwa yakiuza bidhaa feki za wembe wa Super Max.

Msako wa kushitukiza kutoka kwa maafisa wa Taasisi ya Fear Competition Commission (FCC) na maasifa watatu wa Kampuni ya Super Max wakiwa na mwanasheria wao sanjari na askari polisi walifanya msako huo na kukuta bidha hizo zisizo na ubora zikiuzwa huku zikiwa na jina la Kampuni ya Super Max ambapo pia nembo ikiwa tofauti kabisa na ile ya bidhaa zenye ubora kutoka kampuni ya super max ya nchini India.
Mmoja wa wafanyabiashara katika mtaa wa Liberty baada ya kukutwa akiuza bidhaa feki na orijino, (Super Max yenye rangi ya njano na kijani ndiyo orijino na ile ya blue ni magumashi aka feki)  
 Zoezi hilo lilionekana kuwa na mafanikio makubwa pia liliwapa changamoto baadhi ya wafanyabiashara kuanza kuzikagua bidha wanazokuwa wananunua na kuziuza kwa wateja wao endapo zina nembo ya shirika la viwango nchini (TBS) ili kuepuka usumbufu na madhala kwa wateja wao wanaovitu vitu hivyo.
Mmoja kati ya maafisa wa FCC walioongoza zoezi hilo akitoa wito kwa wafanya biashara.
Afisa wa Kampuni ya Super Max Bw.Emmanuel Shija alieleza kuwa kufanyika kwa msako huo kunatokana na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wateja wao wakidai kuwa bidhaa za super max zimekuwa hazina ubora hususani wembe ambazo zinapotumiwa na wateja wao hazina makali na zimekuwa zikikatika hali ambayo iliwalazimu kufanya uchunguzi na kukungundua kuwepo kwa bidhaa feki sokoni zenye nembo ya kampuni hiyo.

“Tumekuwa tukiwaelimisha wateja wetu ambao ni wafanyabiashara wa bidhaa zetu kuwa makini na bidhaa ambazo huingizwa nchini kwa njia za panya na hata wakati mwingine kubadilishiwa makasha huku yakiwa hayana hata mhuri wa TBS ili kuepuka kuwauzia wananchi kwa kutambua kuwa bidhaa hizo hazina ubora  unaotakiwa huku pia vikiwa havijatengenezwa na kampuni yetu”alisema.

Mzigo wa nyembe feki uliokutwa kwenye baadhi ya maduka mtaa wa Liberty jijini Mwanza.
 Naye Afisa mdhibiti wa vifaa bandia toka FCC Bw.Emmanuel Ndyetabula alieleza kuwa wamekuwa wakifanya ukaguzi wa mara kwa mara hasa pale wanapotaarifiwa kuwepo bidhaa bandia sokoni pamoja na kufanya ukaguzi wa kawaida katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mkoa wa Mwanza na Wilaya zake bila kujali kuwa bidhaa hizo zimegaramiwa fedha nyingi na wafanyabiashara hao.
 Bidhaa za Super Max  zenye ubora na orijino ndiyo hizi ambapo kuna Green na Blue Diamond.
 “Lengo kubwa ni kuhakikisha bidhaa zote zinazoingizwa sokoni na kutumiwa na wateja ni zile tu zenye ubora unaotakiwa na si vinginevyo ili kuepuka madhala kwa watumiaji pamoja na Taifa kuwa na bidhaa ambazo hazina ubora na zisizo faa kwenye matumizi ya binadamu mbali na kukamata bidha hizo wanaokutwa nazo pia tumekuwa tukiwalipisha faini ili kusaidia kutoendelea kuzifanyia biashara bidhaa hizo kwa vile watakuwa wanatambua hasara watakazopata baada ya kukutwa nazo”alisisitiza.
Hizi ni bidhaa feki kuwa wangalifu.
 Bw.Ndyetabula alisema kuwa baada ya maafisa wa Kampuni ya Super max kuleta malalamiko yake kwetu na tulipo hoji iwapo anao ushahidi wa kutosha walitueleza kuwa wamefanya uchunguzi wa kina na kugundua kuwa bidhaa nyingi za kampuni hiyo zimechakachuliwa na zinauzwa kwa wingi katika maduka mengi ya Jijini Mwanza ndiyo hasa bado yalikuwa yanauza bidhaa hizo feki.
Msako ukiendelea kwa maduka ya Mwanza.
Kwa upande wake Meneja masoko na mauzo wa Kampuni ya Super Max Bw.Kartesh Patil kutoka nchini Dubai alisema kuwa soko kubwa la usambazaji wa bidhaa hizo lina ofisi zake nchini humo hivyo kuja kufanya ukaguzi wa kugundulika kuwa bidhaa hizo zimechakachuliwa na kuingizwa sokoni kwa lengo la kuharibu jina la kampuni limewagarimu kuja kupigania haki yao ya kibiashara ili bidhaa zao ziendelee kuwepo sokoni lakini kwa ubora unaotakiwa na kuendelea kutoa elimu na mifano ya bidha zao zenye ubora na nembo halisi ya kampuni hiyo.
Super Max yenye rangi ya njano na kijani ndiyo orijino na ile ya blue ni magumashi aka feki.  
Bw.Patil ametoa wito kwa wafanyabiashara kuendelea kuuza bidhaa za kampuni yake zilizo na ubora na zenye nembo halisi badala ya kukubali kuingizwa mkenge na kutumia bidhaa zenye nembo ambayo haifanani kabisa na ile ya kampuni kuepuka usumbufu kama walioupata wa kuchukuliwa bidhaa zao hizo na kutozwa faini hali itakayoweza kuwayumbisha kibiashara kutokana na garama kubwa wanazozitumia.

"Haya-hayaaaa.. Kazi kwenu wanyoaji na wanyolewaji, wito kuweni makini.... Feki zinamadhara zaweza kukupa tetenasi....Tehe-teh!!"

CCM NYAMAGANA YATOA TAMKO MAUAJI YA MACHINGA

Katibu wa Siasa na Uenezi wilaya ya Nyamagana, Mustapha A. Banigwa.
Kufuatia kuawa hapo jana kwa risasi mmoja kati ya wafanyabiashara wadogo jijini Mwanza (Machinga) na wengine wawili kujeruhiwa,  Chama cha mapinduzi wilayani Nyamagana hatimaye leo majira ya saa 7:30 mchana kimetoa Tamko lake rasmi juu ya mauaji hayo yaliyoleta taharuki kubwa kwa watanzania.

Akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari vya jijini Mwanza, Katibu wa Siasa na Uenezi wilaya ya Nyamagana (wilaya ambako tukio hilo lilitokea) Bwa. Mustapha Athuman Baningwa, amesema kuwa chama chake kinalaani vitendo vya Raia ama Askari yeyote kujichukulia sheria mkononi hivyo wameiomba serikali kufanya uchunguzi zaidi kubaini tatizo......


Zaidi msikilize katibu wa siasa na uenezi kwa kubofya play...


MAJAMBAZI WAKUTANA NA JOTO YA POLISI KILIMAHEWA 'BIG BITE' ILEMELA MWANZA

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Bi. Lilian Matola akionyesha silaha (SMG) aliyokutwa nayo mmoja wa majambazi aliyeuawa, aliyekuwaakiwashambulia kwa risasi polisi katika eneo la Big Bite Kilimahewa wilayani Ilemela jijini Mwanza.
JESHI la Polisi mkoani Mwanza limefanikiwa kuwaua kwa kuwapiga risasi watuhumiwa wawili wa ujambazi na kufanikiwa kukamata bunduki moja aina ya Sub Machine Gun (SMG), ikiwa na risasi 43.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Lilian Matora, alisema  tukio hilo lilitokea  saa 5 usiku wa kumkia jana katika eneo la Kilimahewa Big Bite, Nyamanoro jijini hapa.

Polisi wakiwa katika doria ya kawaida, walishambuliwa kwa risasi na majambazi watano waliokuwa katika harakati za kupora wananchi mara baada ya polisi hao kupita katika mtaa husika na kugundua kuwa kuna hali ya utata isiyoeleweka.

Alisema polisi walijipanga vizuri na kufanikiwa kujibu mapigo ambapo majambazi wawili waliuawa papohapo kwa kupigwa risasi ambapo katika tukio hilo, majambazi wengine watatu walifanikiwa kutoroka.
 Baada ya polisi kuipekua miili ya majambazi hayo, walifanikiwa kukamata risasi 43 zikiwa katika magazine mbili tofauti pamoja na bunduki aina ya SMG yenye namba T 1964 TB 8799.


Miili ya majambazi hayo, imehifadhiwa mochuwari katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando.

“Jeshi la Polisi mkoani Mwanza liko imara na haya ni mafanikio makubwa katika harakati za kutokomeza ujambazi…nawaomba wananchi waendelea kutoa taarifa muhimu ambazo zitasaidia kukamatwa kwa majambazi kabla hayajafanya uhalifu,” alisema kaimu kamanda Lilian Matora, .

MEYA WA JIJI LA MWANZA ATOA TAMKO JUU YA VURUGU ZA JANA ZILIZO SABABISHA CHINGA KUUAWA.

Sikiliza kilichosemwa na Mstahiki meya wa jiji la Mwanza (Nyamagana) Stanslaus Mabula (wa pili kutoka kulia) kwa kubofya Play..


TAARIFA RASMI

BALOZI WA KINYWAJI CHA HENNESSY KUKUTANA NA WAFANYABIASHARA, WANAMUZIKI NA WANAMITINDO WA TANZANIA

Balozi wa kinywaji cha Hennessy, Cyrile Gautier Auriol, akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na mikakati yake ya kufanya mazungumza na wafanya biashara mbali mbali wa hapa nchini.
Viongozi wa kinywaji cha Hennesy pamoja na waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.
Waandishi wakiwa makini kufuatilia.

Waandishi wakiwa makini kufuatilia.
---
Na Mwandishi wetu.
Balozi wa kinywaji cha Hennessy, Cyrile Gautier Auriol, yupo nchini kwa ajili ya shughuli mbali mbali pamoja na kukutana na wafanyabiashara wa jiji la Dar es Salaam.

Auriol aliwasili jijini juzi na kufanya mazungumza na wenyeji wake kabla ya kuelezea nia ya safari yake ambayo lengo kubwa ni kutanua soko la kinywaji hicho maarufu duniani kwa Watanzania nan chi za Afrika Mashariki.

Alisema kuwa pamoja na kukutana na wafanyabiashara, pia atakutana na watu wa sekta tofauti, miongoni mwao ni wanamuziki na wanamitindo. Ziara ya balozi huyo itakuwa ya siku tano.

Alifafanua kuwa ujio wake ni mara ya pili kwa ukanda wa Afrika Mashariki na ameona kuna mafanikio makubwa kwa wafanyabiashara na hasa katika soko la vinywaji vikali.

Alisema kuwa kinywaji cha Hennessy kwa sasa ndicho kinatamba katika ukanda huu na hivyo kuna haja kwa Watanzania kuanza kupartavradha kwa ajili ya kujenga mwili na afya bora. Ikiwa na zaidi ya historia ya miaka 250, Hennessy inatajwa kuwa kinywaji (Cognac) bora zaidi duniani.

Pia Auriol atakutana na wapenzi wa Hennessy katika matukio mbalimbali maalumu ikiwemo chakula cha mchana katika hoteli ya Hyatt Regency ambapo baadhi ya wanawake watakaochaguliwa watapata fursa ya kujifunza historia ya kinywaji cha Hennessy lakini pia kuonja aina mbalimbali za kinywaji hicho lengo likiwa kuwafundisha wanawake namna ya kufurahia kinywaji hicho wakiwa majumbani mwao.

Balozi Auriol pia atahudhuria chakula cha jioni na wafanyabiashara wa hapa nchini katika mgahawa wa Akemi uliopo katika ghorofa la Diamond Jubilee. Balozi Auriol atatoa elimu kuhusu Hennessy ikifuatiwa na uonjaji wa kinywaji hicho pamoja na chakula kitakachoandaliwa na mpishi mkuu wa hotel hiyo.

Ziara ya balozi Auriol inaenda sambamba na juhudi nyingine za kutangaza kinywaji hicho hapa nchini, mojawapo ikiwa ni kampeni ya mabango ya ‘Flaunt Your Taste’ yaliyosambaa jiji zima pamoja na ukamilishaji wa chumba cha Hennessy kilicho katika Club 327, ambacho balozi Auriol atakizindua.

Balozi Auriol atakuwa na kikao maalumu pia na wapenzi wakubwa wa kinywaji hicho, na pia atawazawadia mialiko maalumu ya kuingia kwenye klabu ya wapenzi wa kinywaji hicho ya Afrika mashariki.

Pia atatoa mafunzo maalumu kwa baadhi ya wahudumu kutoka katika bar kubwa za jijini. Lengo kuu la mafunzo hayo yatakayofanyika katika hoteli ya Southern Sun na George & Dragon ni kuwapa wahudumu ujuzi utakao wawezesha kutoa huduma bora na ya kipekee kwa wateja wao wakati wakiburudika na kinywaji cha Hennessy kwenye bar au hotel wanazozipendelea.

SHUJAA MPYA WA KIBONGO

Urban Pulse na Freddy Macha wanakuletea kidokezo ("trailer") cha filamu kuhusu shujaa mpya wa Kitanzania Wilfred Moshi, aliyejitolea kwa hali na mali kuupanda Mlima Everest. Ameweka rekodi ya kuwa Mwafrika wa tatu na Mtanzania wa kwanza kupanda mlima mrefu kushinda yote duniani...

BONDIA KING CLASS 'MAWE' AENDELEA KUJIFUA KUMKABILI SAIDI MUNDI DESEMBA 9

Bondia Mohamed Hemedi 'Kadogo Ninja' kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika Kambi ya Ilala Dar Es salaam Class anajiandaa na mpambano wake na Said Mundi utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.Bondia Mohamed Hemedi 'Kadogo Ninja' kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakati wa mazoezi yanayoendelea katika Kambi ya Ilala Dar Es salaam Class anajiandaa na mpambano wake na Said Mundi utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba Dar es salaam.


Bondia Ibrahimu Class 'King Class mawe' akioneshana ufundi wa kutupiana masumbwi na Mohamed Hemedi 'Kadogo Ninja' wakati wa mazoezi yao yanayoendelea Katika Kambi ya Ilala Dar es salaam Class anajiandaa na mpambano wake na Said Mundi wa Tanga utakaofanyika Desemba 9 katika ukumbi wa PTA Sabasaba.
Picha zote na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Thursday, November 15, 2012

MMOJA AUAWA NA WENGINE KUJERUHIWA KUFUATIA VURUGU ZA WAMACHINGA NA ASKARI WA JIJI MWANZA. HALI TETE, MADUKA YAFUNGWA HADI SASA

Polisi wakiwa kwenye doria eneo la tukio.
 Mtu mmoja ameuawa na wengine wawili kujeruhiwa kufuatiaa vurugu zilizotokea leo majira ya saa tano asubuhi  katika eneo la barabara ya Pamba karibu na soko kuu la jijini Mwanza katika vurugu baina ya wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga na askari wa Halmashauri ya jiji la Mwanza.

Mtu huyo ambaye jina lake kamili halikupatikana badala yake ametambuliwa kwa jina moja tu la Greda.

Taarifa zaidi zinasema kuwa leo mnamo majira ya saa nne na nusu asubuhi askari wa halmashauri ya jiji la Mwanza wakiwa katika maeneo yao ya kazi eneo la barabara ya Pamba kwenye stendi ya zamani ya mabasi ya Tanganyika karibu na soko kuu la jiji hilo, wakiwa katika operesheni zao za kawaida za kusafisha jiji walikamata bidhaa zilizokuwa zimepangwa katika maeneo ambayo hayaruhusiwi kisheria wakiwa kwenye eneo hilo mtu mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni mmachinga alimrukia mgambo wa jiji shingoni na kumtolea silaha ya jadi aina ya sime kwa nia ya kumdhuru.

Maganda  ya risasi zilizo tumika.
 Baada ya tukio hilo wamachinga waliokuwa eneo la tukio walianza kuwarushia mgambo hao wa jiji mawe ndipo wale mgambo wa jiji katika kujihami wakaanza kurusha risasi hewani kuwatawanya wamachinga hao  waliokuwa wakiongezeka kadri kuanza kwa seleka hilo, kwa bahati mbaya moja kati ya risasi hizo zikampiga mpiga debe mmoja upande wa kushoto na kufariki papo hapo.

 Machinga mwingine amejeruhiwa kwenye mkono wa kushoto katika kiwiko, naye dereva wa magari ya  biashara za kusafirisha mizigo wa gari aina ya Kenta, magari ambayo hupaki katika eneo hilo amejeruhiwa upande wa kushoto kichwani na kukimbizwa hospitali ya rufaa Bugando kwa matibabu. Mmoja wa viongozi wa akiwatuliza wamachinga wenzake kupata kumsikiliza mkuu wa polisi (OCD) wa wilaya ya Nyamagana Ally Kitumbu. .

Msikilize kwa kubofya play..
Mkuu wa polisi (OCD) wa wilaya ya Nyamagana Ally Kitumbu. akizungumza na wafanyabiashara hao wadogo (wamachinga) kuendelea na kazi kwa kufuata sheria wakati jeshi hilo likifanya uchunguzi wa tukio hilo.

Msikilize kwa kubofya play...
Maduka mengi hususani yaliyo karibu na eneo la tukio yamefungwa kufuatia seleka hilo.

Makutano ya barabara za Liberty na Nyerere ambalo muda wote huwa na pilikapilika za kibiashara likionekana tupu kutokana na vurugu hizo zilizo sababisha wafanyabiashara kukimbia na kufunga biashara zao kuhofia vurugu hizo.

Mmoja kati ya viongozi wa wamachinga akizungumza na wenzake kuwasihi kulinda utulivu ili haki yao isipotee.Wednesday, November 14, 2012

TAIFA STARS YAIDUNGUA HARAMBEE STAR 1-0 CCM KIRUMBA MWANZA

Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo imeibika na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Harambee Stars ya Kenya katika mchezo wa Kimataifa uliokwenye kalenda ya FIFA uliofanyika leo katika uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza.

Kikosi cha Harambee Stars ya Kenya katika mchezo wa Kimataifa uliokwenye kalenda ya FIFA uliofanyika leo katika uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza ambacho kimefungwa 1-0 na Tanzania.
Mgeni rasmi wa pambano la kimataifa la kirafiki kwa mujibu wakalenda ya FIFA, Mkurugenzi wa jiji la Mwanza (wa tatu kushoto) akiwa katikapicha ya pamoja na viongozi wa TFF, FKF, MZFA, IDFA na kamishna mechi wakati nyimbo za mataifa hayo mawili zikipigwa.

Mgeni rasmi wa mchezo huo mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe akisalimiana  na wachezaji wa timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars'

Mgeni rasmi wa mchezo huo mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe akisalimiana  na wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'.

Kapteni wa Harambee Stars Denis Oliechi akiwaongoza wachezaji wenzake kukisalimiana na wenyeji wao Taifa Stars katika mechi ya kirafiki inayotambuliwa na FIFA iliyochezwa leo dimba la CCM kirumba Mwanza, Mbwana Samata ndiye alikuwa wa mwisho kusalimiwa pichani. Matokeo Taifa Stars waliibuka na ushindi wa 1-0.

Salaam muhimu.. ni baina ya Taifa Stars na Harambee Stars.

Mgeni rasmi wa mchezo huo mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe akisalimiana na Kocha mkuu wa Taifa Stars Kim Poulsen kabla ya mchezo kuanza.

Ilikuwani kona ndogo iliyochezwa vyema na Amir Maftah wakigongeana na Thomas Ulimwengu kisha mpira ukarudi kwa Maftah akamimina fupi ya juu ikamkuta beki wa timu ya Taifa ya tanzania 'Taifa Stars' Aggrey Moris (aliyeruka juu) aliyekuwa katikati ya mabeki wa Harambee Stars akatumia ufundi kuukwamisha mpira wavuni.

Bao la Stars lilipatikana mapema tu katika dakika ya 5 na sekunde kadhaa kipindi cha kwanza mfungaji akiwa ni Agrey Moris na kufanya timu hizo zikienda mapumziko Stars ikiwa mbele matokeo yaliyodumi hadi kumalizika kwa mchezo huo. 


Wachezaji wa Tanzania na sherehe  za goli.

Mfungaji wa goli la ushindi kwa Tanzania Aggrey Morris (6) akiserebuka na wachezaji wenzake mara baada ya kuipatia timu yake goli dakika ya tanotu ya mchezo.

Mchezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania Simon Msuva akijaribu kutafuta mbinu za kumtoka mlinzi wa timu ya taifa ya Kenya Christopher Wekesa katika mechi ya kirafiki ya kimataifa ambapo Taifa Stars iliibuka na ushindi wa bao 1- 0.

Wanahabari wakitimiza wajibu wao wa kuripoti nao walijikuta wakipigwa picha ya matukio mbalimbali yaliyokuwa yakijiri katika uwanja wa CCM Kirumba katika mechi ya kirafiki ya kimataifa baina ya Taifa Stars 'Tanzania' na Harambee stars 'Kenya'.

Muosha huoshwa...! Mpiga picha wa kituo cha televisheni cha Star TV akiweka sawa na hatimaye kunaswa na blogu ya G. Sengo.

Mashabiki wa Taifa Stars waliokuwa wameketi katika jukwaa la mashabikiwa wa Simba wakifuatilia mtanange huo ambapo ushirikiano ulikuwa asilimia mia. 

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' akizungumza na waandishi wahabari mara baada ya mchezo kumalizika kwa timu yake kuibuka na ushindi.. Kumsikiliza Bofya Play...
Nyomi na shangwe zake.......baada ya goli.