ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, November 16, 2012

MAJAMBAZI WAKUTANA NA JOTO YA POLISI KILIMAHEWA 'BIG BITE' ILEMELA MWANZA

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Bi. Lilian Matola akionyesha silaha (SMG) aliyokutwa nayo mmoja wa majambazi aliyeuawa, aliyekuwaakiwashambulia kwa risasi polisi katika eneo la Big Bite Kilimahewa wilayani Ilemela jijini Mwanza.
JESHI la Polisi mkoani Mwanza limefanikiwa kuwaua kwa kuwapiga risasi watuhumiwa wawili wa ujambazi na kufanikiwa kukamata bunduki moja aina ya Sub Machine Gun (SMG), ikiwa na risasi 43.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Lilian Matora, alisema  tukio hilo lilitokea  saa 5 usiku wa kumkia jana katika eneo la Kilimahewa Big Bite, Nyamanoro jijini hapa.

Polisi wakiwa katika doria ya kawaida, walishambuliwa kwa risasi na majambazi watano waliokuwa katika harakati za kupora wananchi mara baada ya polisi hao kupita katika mtaa husika na kugundua kuwa kuna hali ya utata isiyoeleweka.

Alisema polisi walijipanga vizuri na kufanikiwa kujibu mapigo ambapo majambazi wawili waliuawa papohapo kwa kupigwa risasi ambapo katika tukio hilo, majambazi wengine watatu walifanikiwa kutoroka.
 Baada ya polisi kuipekua miili ya majambazi hayo, walifanikiwa kukamata risasi 43 zikiwa katika magazine mbili tofauti pamoja na bunduki aina ya SMG yenye namba T 1964 TB 8799.


Miili ya majambazi hayo, imehifadhiwa mochuwari katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando.

“Jeshi la Polisi mkoani Mwanza liko imara na haya ni mafanikio makubwa katika harakati za kutokomeza ujambazi…nawaomba wananchi waendelea kutoa taarifa muhimu ambazo zitasaidia kukamatwa kwa majambazi kabla hayajafanya uhalifu,” alisema kaimu kamanda Lilian Matora, .

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.