Airtel yawazawadia 500% bonus ya Muda wa Maongezi kwa wateja wake
· Wateja wa Airtel kupata mara tano ya muda wa maongezi
· Hakuna haja ya kujiunga kwenye “ Jipatie Mara 5”
Dar es salaam Octoba 2012 Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel leo imezindua promosheni mpya kabambe itakayowazawadia wateja wake nchi nzima. Promosheni hii ijulikanayo kama “Jipatie Mara 5” itawawezesha wateja wa Airtel kupata MARA TANO ya wastani wa matumizi ya kupiga simu kwa siku nzima.
Akiongea wakati wa uzinduzi wa promosheni hiyo Mkurugenzi wa Airtel Sam Elangalloor alisema” Airtel tunayofuraha kuwazawadia wateja wetu nchi nzima mara tano ya wastani wa kiwango cha pesa watakayotumia kila siku promosheni hii ya “Jipatie Mara 5”. Promosheni hii itawazawadia wateja wa Airtel mara 5 ya matumizi yao kama bonus ya muda wa maongezi itakayowawezesha kupiga simu kwenda namba yoyote ya Airtel kwa siku hiyo , hii ni sawa na asilimia 500 ya bonus.
”Tumefanya hivi ili kuendelea kuboresha huduma zetu na pia kuendeleza kudhibitisha dhamira yetu ya kuwapatia wateja wetu nchini nzima uhuru wa kuongea aliongeza Elangalloor .”
Akifafanua juu ya promosheni hiyo Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano Airtel Beatrice Singano Mallya alisema” kila mteja wa Airtel tayari ameshaunganishwa katika promosheni hii, kinachotakiwa kufanya ni kupiga simu upate bure salio mara 5 ya wastani wa matumizi yako ya siku kadri mteja anavyotumia simu yake kwa kupiga simu ndivyo anajipatia nafasi zaidi ya kuzawadia asilimia 500 ya bonus ya muda wa maongezi
“Jipatie Mara 5” ni promosheni kwa ajili ya wateja wa malipo ya awali, kila mteja atapata ujumbe utakaomjulisha wastani wake kwa siku na kisha kupokea ujumbe mara atakapopokea asilimia 500% kutoka Airtel. Kwa maelezo zaidi juu ya huduma hii piga 0783001001 bure na kuunganishwa moja kwa moja na taarifa mbalimbali za huduma zetu”aliongeza Mallya.
Airtel inaendelea kuboresha huduma za mawasiliano nchini. kwa kupitia huduma ya Airtel money, Airtel imewawezesha watanzania kupata huduma za kifedha kirahisi katika maeneo mbalimbali nchini. Kwa kuthibitisha uwezeshaji wa upatikanaji wa huduma za kifedha Airtel imewawezesha wateja wake kutuma na kupokea pesa chini ya shilling 100,000/= bure bila makato yoyote. Vile vile Airtel imeendelea kupanua zaidi huduma za internet kwa kuwezesha miji zaidi ya 30 nchini kupata internet yenye kasi ya 3.75G .