|
Mkurugenzi wa Kampuni ya Meli ya MV. SAMAR Salum
Ally akizungumza na vyombo vya habari. |
ABIRIA na wananchi wanaotumia kivuko cha MV. SAMAR
wamepinga vikali agizo la Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizebar la
kuamuru kusitishwa kwa huduma ya usafiri wa kivuko hicho kinachotoa huduma kati
ya Mwanza mjini na Kamanga Wilayani Sengerema hali iliyopelekea wananchi
kupinga vikali hatua hiyo ya Naibu Waziri na Serikali.
Wananchi na abiria hao wamesema kwamba kauli hiyo ya
Naibu Waziri Dkt.Tizebar aliyoitoa hivi karibuni wakati wa kuipokea treni ya
abiria ya kutoka Jijini Dar es salaam hadi Jijini Mwanza kuwasili kwa mara ya
kwanza tangu kuanza kazi Desemba 9 mwaka huu baada ya kusitisha safari zake kwa
miaka mitatu kwa madai kuwa wamezuia njia ya reli iendayo bandarini huku madai
hayo yakionekana kupingana na Mamlaka ya Bandari ya Mwanza Kaskazini waliodai
kuwa kwa sasa hawahitaji huduma ya Treni kufika Bandari hiyo na ni miaka zaidi
ya kumi Treni kupita na kufika Bandari hiyo ya Mwanza Kaskazini.
Akizungumza na vyombo vya Habari Mkurugenzi wa
Kampuni ya Meli ya MV. SAMAR Salum Ally alisema kwamba agizo la kusimamisha
huduma na kuhamia eneo la maegesho ya Meli za Marine Service huku kukiwa hakuna
matayarisho ya barabara ya magari kuingia na kutokea,abiria na daraja la meli
hiyo kuweka nanga ili kuruhusu abiria na magari kupita kirahisi kama ilivyo
kwenye eneo kilipokuwa kikitolea huduma awali.
Salum amesema kwamba alipokea barua ya kwanza ya
Mamlaka ya Bandari ya Kaskazini (PTA) Desemba 11 mwaka 2012 yenye kumb.MN/2/3/04
iliyosainiwa na Mkuu wa Bandari hiyo Mhandisi Josephat Mutalemwa huu ikisomeka kwamba ‘AGIZO LA NAIBU WAZIRI LA KUHAMISHA HUDUMA
YA KIVUKO KUTOKA HAPO ULIPO NA KUELEKEA NDANI ZAIDI YA BANDARI YA
KASKAZINI’ ikiwa ndani ya wiki tatu za kutekelezwa kwa agizo hilo.
|
Barua ya kwanza. |
Ameongeza kuwa wakati akitafakali
juu ya uamuzi huo wa barua hiyo na Agizo la Naibu Waziri Dkt.Tizebar,Kabla ya
wiki moja kumalizika ghafla akapokea barua nyingine tena ya pili ambayo pia
ikitolewa na PTA Desemba 19 mwaka huu na ikisainiwa na Kaimu Mkuu wa Bandari
T.S.Akile iliyosemeka 'KUSITISHA HUDUMA YA KIVUKO KUTOKA HAPO ULIPO NA KUELEKEA
ZAIDI NDANI YA BANDARI YA KASKAZINI' Mamlaka ya usimamizi wa Bandari (PTA)
inakutaka kusitisha mara moja shughuli za kupakia na kushusha abiria na mizingo
kuanzia sasa hivi (Leo Desemba 19 mwaka huu).
Kufatia hatua hiyo hali ilikuwa tofauti kwa wananchi
na abiria na kuanza kurusha mameno na kauli kali za kupinga hatua ya
PTA,Serikali na Agizo la Naibu Waziri Dkt. Huku Mkurugenzi wa SAMAR alidai kuwa
ameheshimu kauli ya Waziri na agizo la barua za PTA, akidai kuwa amekuwa
akiilipa PTA kiasi cha shilingi milioni 2 kwa mwezi ikiwa ni makubaliano baada
ya kuomba kutumia eneo hilo na kupitia Meli zake amekuwa pia akiliingizia
shirika hilo kiasi cha zaidi milioni 70 kwa mwezi kwa huduma ya Bandari ya
Mwanza Kaskazini na Kusini.
Mbali na
kuiingizia PTA mapato hayo, kampuni hiyo imekuwa akisaidia wanawake wajane zaidi 60 kiasi
cha shilingi 600,000 kwa mwezi waliopo eneo la Kamanga huku serikali ya Kijiji
hicho cha Kamanga kikiingiza kila siku kiasi cha elfu 40,000/= ikiwa ni huduma
za wananchi wanaotumia vyoo katika eneo la kugota Meli ya MV. SAMAR huku
wanafunzi wote wakipita bure katika kivuko hicho wakiwemo wazee wa zaidi ya
miaka 70 na mama wajawazito na watoto walio chini ya miaka 8 kila siku ya huduma
wa Meli hiyo.
|
Kivuko hicho cha MV.SAMAR. |
Kivuko hicho cha MV.SAMAR kinacho beba abiria
wapatao 390 kwa wakati mmoja,mizigo tani
320 kwa kila safari moja ifanyayo ambapo kwa kutwa nzima ni zaidi ya abira
zaidi ya 3,500 kwa siku nzima ya safari 12 za abiria na mizigo kutoka Jijini
Mwanza hadi Kamanga Wilayani Sengerema tangu kukubaliwa na Uongozi wa Mamlaka
ya Bandari ya Mwanza Kaskazini Septemba 17 mwaka huu hadi Septemba 17 mwaka
2013 ikiwa ni mkataba wa majaribio wa
mwaka mmoja kabla ya kusainiwa mkataba mwingine.
|
Njia ya reli ndani ya eneo ambayo kimsingi kwa upande wa wamiliki wa eneo la kivuko cha MV. SAMAR ambao wao wameacha nafasi ya kutosha kwa reli hiyo kupitika zaidi ya kutumia eneo la reli kama sehemu ya barabara ikatishayo kwa ajili ya magari. |
|
Baadhi ya abiria walikuwa wakitakiwa kupanda kivuko husika wakirejea kwenye siti zao kufanya mgomo wa kulazimisha safari ziendelee. |
|
Ghati ya eneo ambalo huduma inapaswa kuhama kufuatia agizo la kusimamisha huduma na kuhamia eneo la maegesho ya Meli za Marine Service |
|
Mishemishe za biashara eneo la Kamanga ferry. |