ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 19, 2012

AGIZO LA NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI LA KUHAMISHA KIVUKO CHA MV SAMAR LALETA BALAA, WANANCHI WAKERWA WAILALAMIKIA SERIKALI, MMILIKI ASIMAMISHA HUDUMA YA USAFIRI HUO.


Mkurugenzi wa Kampuni ya Meli ya MV. SAMAR Salum Ally akizungumza na vyombo vya habari. 
 ABIRIA na wananchi wanaotumia kivuko cha MV. SAMAR wamepinga vikali agizo la Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt. Charles Tizebar la kuamuru kusitishwa kwa huduma ya usafiri wa kivuko hicho kinachotoa huduma kati ya Mwanza mjini na Kamanga Wilayani Sengerema hali iliyopelekea wananchi kupinga vikali hatua hiyo ya Naibu Waziri na Serikali.


Wananchi na abiria hao wamesema kwamba kauli hiyo ya Naibu Waziri Dkt.Tizebar aliyoitoa hivi karibuni wakati wa kuipokea treni ya abiria ya kutoka Jijini Dar es salaam hadi Jijini Mwanza kuwasili kwa mara ya kwanza tangu kuanza kazi Desemba 9 mwaka huu baada ya kusitisha safari zake kwa miaka mitatu kwa madai kuwa wamezuia njia ya reli iendayo bandarini huku madai hayo yakionekana kupingana na Mamlaka ya Bandari ya Mwanza Kaskazini waliodai kuwa kwa sasa hawahitaji huduma ya Treni kufika Bandari hiyo na ni miaka zaidi ya kumi Treni kupita na kufika Bandari hiyo ya Mwanza Kaskazini.

Akizungumza na vyombo vya Habari Mkurugenzi wa Kampuni ya Meli ya MV. SAMAR Salum Ally alisema kwamba agizo la kusimamisha huduma na kuhamia eneo la maegesho ya Meli za Marine Service huku kukiwa hakuna matayarisho ya barabara ya magari kuingia na kutokea,abiria na daraja la meli hiyo kuweka nanga ili kuruhusu abiria na magari kupita kirahisi kama ilivyo kwenye eneo kilipokuwa kikitolea huduma awali.

Salum amesema kwamba alipokea barua ya kwanza ya Mamlaka ya Bandari ya Kaskazini (PTA) Desemba 11 mwaka 2012 yenye kumb.MN/2/3/04 iliyosainiwa na Mkuu wa Bandari hiyo Mhandisi Josephat Mutalemwa  huu ikisomeka kwamba  ‘AGIZO LA NAIBU WAZIRI LA KUHAMISHA HUDUMA YA KIVUKO KUTOKA HAPO ULIPO NA KUELEKEA NDANI ZAIDI YA BANDARI YA KASKAZINI’ ikiwa ndani ya wiki tatu za kutekelezwa kwa agizo hilo.

Barua ya kwanza.
Ameongeza kuwa wakati akitafakali juu ya uamuzi huo wa barua hiyo na Agizo la Naibu Waziri Dkt.Tizebar,Kabla ya wiki moja kumalizika ghafla akapokea barua nyingine tena ya pili ambayo pia ikitolewa na PTA Desemba 19 mwaka huu na ikisainiwa na Kaimu Mkuu wa Bandari T.S.Akile iliyosemeka 'KUSITISHA HUDUMA YA KIVUKO KUTOKA HAPO ULIPO NA KUELEKEA ZAIDI NDANI YA BANDARI YA KASKAZINI' Mamlaka ya usimamizi wa Bandari (PTA) inakutaka kusitisha mara moja shughuli za kupakia na kushusha abiria na mizingo kuanzia sasa hivi (Leo Desemba 19 mwaka huu).

Kufatia hatua hiyo hali ilikuwa tofauti kwa wananchi na abiria na kuanza kurusha mameno na kauli kali za kupinga hatua ya PTA,Serikali na Agizo la Naibu Waziri Dkt. Huku Mkurugenzi wa SAMAR alidai kuwa ameheshimu kauli ya Waziri na agizo la barua za PTA, akidai kuwa amekuwa akiilipa PTA kiasi cha shilingi milioni 2 kwa mwezi ikiwa ni makubaliano baada ya kuomba kutumia eneo hilo na kupitia Meli zake amekuwa pia akiliingizia shirika hilo kiasi cha zaidi milioni 70 kwa mwezi kwa huduma ya Bandari ya Mwanza Kaskazini na Kusini.

Mbali na kuiingizia PTA mapato hayo, kampuni hiyo imekuwa akisaidia wanawake wajane zaidi 60 kiasi cha shilingi 600,000 kwa mwezi waliopo eneo la Kamanga huku serikali ya Kijiji hicho cha Kamanga kikiingiza kila siku kiasi cha elfu 40,000/= ikiwa ni huduma za wananchi wanaotumia vyoo katika eneo la kugota Meli ya MV. SAMAR huku wanafunzi wote wakipita bure katika kivuko hicho wakiwemo wazee wa zaidi ya miaka 70 na mama wajawazito na watoto walio chini ya miaka 8 kila siku ya huduma wa Meli hiyo.

Kivuko hicho cha MV.SAMAR.
Kivuko hicho cha MV.SAMAR kinacho beba abiria wapatao 390  kwa wakati mmoja,mizigo tani 320 kwa kila safari moja ifanyayo ambapo kwa kutwa nzima ni zaidi ya abira zaidi ya 3,500 kwa siku nzima ya safari 12 za abiria na mizigo kutoka Jijini Mwanza hadi Kamanga Wilayani Sengerema tangu kukubaliwa na Uongozi wa Mamlaka ya Bandari ya Mwanza Kaskazini Septemba 17 mwaka huu hadi Septemba 17 mwaka 2013 ikiwa ni mkataba wa majaribio wa  mwaka mmoja kabla ya kusainiwa mkataba mwingine.



Njia ya reli ndani ya eneo ambayo kimsingi kwa upande wa wamiliki wa eneo la kivuko cha MV. SAMAR ambao wao wameacha nafasi ya kutosha kwa reli hiyo kupitika zaidi ya kutumia eneo la reli kama sehemu ya barabara ikatishayo kwa ajili ya magari.

 Baadhi ya abiria walikuwa wakitakiwa kupanda kivuko husika wakirejea kwenye siti zao kufanya mgomo wa kulazimisha safari ziendelee.

Ghati ya eneo ambalo huduma inapaswa kuhama kufuatia agizo la kusimamisha huduma na kuhamia eneo la maegesho ya Meli za Marine Service

Mishemishe za biashara eneo la Kamanga ferry. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.