ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, January 6, 2024

DKT. BITEKO APONGEZA JUHUDI ZA RAIS DKT. SAMIA KUSTAWISHA DEMOKRASIA NCHINI


📌 Asema amekuwa mfano Kitaifa na Kimataifa


📌 Apongeza  Baraza la Vyama vya Siasa kukusanya maoni Miswada ya Sheria za Uchaguzi


📌 Awasisitiza kwenda bungeni kutoa maoni ya miswada


Dar es Salaam

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati,  Mhe. Dkt. Doto Biteko amempongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan  kwa juhudi zake za kustawisha ustawi wa kidemokrasia nchini, sambamba na kuimarisha miundombinu ya kiuchumi na kijamii ili kuwaletea Maendeleo watanzania.


Dkt. Biteko amesema  hayo  tarehe 4 Januari, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akifunga Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini ulioshirikisha wadau wa Demokrasia ya Vyama vingi vya Siasa ili  kujadili miswada ya Sheria za Uchaguzi na Muswada wa Sheria za Vyama vya Siasa.Mkutano umeandalilwa na  Baraza la Vyama vya Siasa.


Miswada iliyokuwa ikijadiliwa ni muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani  wa mwaka 2023, Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wa mwaka 2023 na  Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa wa mwaka 2023.


“ Rais wetu amekuwa ni mfano wa kuigwa, kitaifa na kimataifa kwa kuhakikisha kuwa demokrasia yetu inazidi kustawi na kuifanya Serikali kuendeshwa kwa misingi ya haki, utawala bora na kwa mujibu wa sheria tulizojiwekea na bila kusahau kuzingatia maoni ya watu ambao ni muhimu katika kuboresha utendaji wetu.” Amesema Dkt. Biteko


Dkt. Biteko amepongeza Baraza la Vyama vya Siasa kwa kuandaa mkutano huo ambao ni muhimu kwa maslahi ya Taifa na kueleza kuwa Baraza hilo kwa kwa mujibu sheria linajukumu pia la  kuishauri Serikali kuhusu utekelezaji wa sheria ya vyama vya siasa na masuala mengine yanayohusu vyama vya siasa na demokrasia.


Amesema kuwa, mkutano huo umekuwa wenye tija kwani washiriki  wameweza kutoa maoni yao kwa kuzingatia maslahi ya nchi.


Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko  amewaasa wajumbe wa Mkutano huo kuitikia wito wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson wa kwenda bungeni kuanzia tarehe 6 hadi 10 Januari ili kutoa maoni kuhusu miswada ya sheria za uchaguzi na mswada wa sheria ya vyama vya siasa.


Amewashukuru wajumbe hao kwa kutoa maoni ambayo ni bora na kwa kujadiliana kwa uungwana kuhusu miswada hiyo, kwani hakuna chama kilichoonesha kuwa kina umiliki wa kutoa mawazo bali wote walisikilizana huku akieleza kuwa yale  waliyojadiliana itakuwa ni muendelezo wa kujenga maridhiano ya kitaifa.


Kuhusu sheria zilizopo nchini amesema kuwa, endapo kuna sheria inaonekana ina changamoto baada ya kuitumia kwa muda mrefu, “wito wa Dkt. Samia Suluhu Hassan ni sote kukaa na kuridhiana kama Taifa  wapi tuboreshe na Bunge ni Taasisi mahiri yenye uongozi mahiri ambao watapokea maoni yetu na kuyafanyia kazi na mahali ambapo Serikali itapaswa kupeleka muswada sheria ya marekebisho bungeni itafanya hivyo.”


Awali, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama, amesema kuwa, lengo la mkutano huo lilikuwa ni kukutanisha wadau wengi  wanaohusika na masuala ya demokrasia ya mfumo wa vyama vingi nchini ili kutoa maoni yatayoboresha miswada kwa kupitia utaratibu utakaozingatia sheria na kanuni  za upitishwaji wa miswada katika Bunge la Tanzania.


Amesema kuwa, mkutano huo umekuwa na mafanikio makubwa na wadau wametoa maoni yao kwa amani na ushirikiano mkubwa, hivyo amepongeza Baraza la Vyama vya Siasa, kwa kuandaa mkutano huo na kusema kuwa, Serikali itaendelea kuliunga mkono Baraza hilo katika utekelezaji wa mipango yake.


Kwa upande wake, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Fransis Mutungi amesema kuwa, zao la mkutano huo ni muongozo uliotolewa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati alipopokea taarifa ya kikosi kazi alichokiunda cha kuratibu maoni ya wadau wa Demokrasia ya vyama vingi vya siasa ambapo moja ya masuala aliyoelekeza ni  kufanyika kwa maboresho ya sheria za uchaguzi na sheria za vyama vya siasa.


Amemshukuru Rais kwa jitihada zake katika kukuza na kuendeleza demokrasia nchini kwani kukutana kwa Baraza hilo kunatokana jitihada hizo za uwepo wa demokrasia nchini.


Viongozi mbalimbali waliohudhuria Mkutano huo ni  pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hamza Hassan Duma, Mkuu wa Mkoa wa Da es Salaam, Albert Chalamila na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mgeni Hassan Juma.

DKT. BITEKO AANZA ZIARA YA KIKAZI ZANZIBAR.


Leo tarehe 6 Januari 2024, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili Zanzibar, Mkoa wa Kusini Pemba kwa ajili ya ziara ya kikazi.

Katika Uwanja wa Ndege wa Pemba, Dkt. Biteko amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba,  Mhe. Mattar Zahoro,  Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,  Mhe. Jumanne Sagini na viongozi wengine wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM).


Leo tarehe 6 Januari 2024, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili Zanzibar, Mkoa wa Kusini Pemba kwa ajili ya ziara ya kikazi.

Friday, January 5, 2024

VIDEO:- WAZIRI JAFO AUNGURUMA KWA WATAALAMU NA VIONGOZI JUU YA KUSIMAMIA MIRADI YA MAENDELEO

 

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Dkt. Seleman Jafo amewaagiza viongozi na wataalamu kusimamia na kukamilisha kwa wakati miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuwaondolea changamoto zinazowakabili wananchi.

Thursday, January 4, 2024

JAFO APANIA UWEPO WA UJENZI WA ZAHANATI KILA KIJIJI IFIKAPO MWAKA 2025

 


NA VICTOR MASANGU,KISARAWE


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Raisi Muungano na Mazingira Dkt.Seleman Jafo amewataka viongozi na watendaji kujikita zaidi katika kusimamia na kukamilisha  ipasavyo miradi mbali mbali ya maendeleo lengo ikiwa ni kuwahudumia wananchi.

Jafo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe ameyasema hayo wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kutembelea miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na wananchi ili kubaini changamoto zinazowakabili.




Waziri Jafo katika ziara hiyo ameweza kupata fursa ya kuwatembelea na kuzungumza na  wananchi wa maeneo ya  vijiji katika Kata za Marui,Vikumburu pamoja na Chole  na kuwahakikishia kuwaboreshea huduma za kijamii kama vile maji safi na salama,afya  elimu na mambo mengi ya msingi.


Jafo alibainisha kwamba lengo lake kubwa katika Amesema katika jimbo hilo ni kuweka mikakati ya kila kijiji kuwa na zahanati ifikapo mwaka 2025 ili kuwaondolea adha wananchi ya kutembea umbari mrefu ya kufuata huduma ya maji.


Alisema endapo miradi inayopelekwa kwa wananchi viongzi wataisimamia kama ilivyopangwa itaondoa vikwazo kwa jamii na wataendelea na shughuli nyingi e za maendeleo kuinua uchumi wao.

Katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa Zahanati ngazi ya Vijiji zaidi ya milionin 50 zimetolewa kutoka mfuko wa Jimbo kujenga miradi hiyo na kwamba ifikapo Machi mwaka huu zipo ambazo zitaanza kutoa huduma.

"Nimetembelea miradi ya  nyumba ya mwalimu Ngongere shule ya Msingi na nimeelekeza kupitia fedha za mfuko wa jimbo ikamilike kwa wakati hawa walimu wapate sehemu ya kuishi" alisema.

Kadhalika alisema wataalamu wanatakiwa kubadilika na kuzingatia fedha zinazotengwa zinafika kwa wakati maeneo ya miradi ili wanufaika waondokane na vikwazo .

Katika hatua nyingine Waziri Jafo alipongeza mradi wa ujenzi wa Zahanati ya Mafumbi  iliyopo kata ya Chole  ambapo alisema uongozi wa Kijiji hicho unatakiwa kuigwa kutokana na usimamizi mzuri wa fedha wanazopatiwa.

MBUNGE LUGANGIRA ATAKA MATUMIZI YA MITANDAO KATIKA UCHAGUZI YAINGIE KATIKA SHERIA

 



MBUNGE wa Viti Maalumu, Neema Lugangira ameshauri Mswada wa Sheria ya Tume Huru ya Uchaguzi uwe na Ibara inayoongelea masuala ya Matumizi ya Mitandao katika Uchaguzi ikiwemo (Akili Mnemba - AI).

Lugangira ametoa ushauri huo leo jijini Dar es Salaam wakati akichangia kwenye mkutano maalum wa Baraza la Vyama vya Siasa unaoshirikisha wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa kujadili miswada ya sheria za uchaguzi na mswada wa sheria za vyama vya siasa.

Alisema Novemba 2023, Jumuiya ya Tume za Uchaguzi Afrika (Association of African Election Authorities) ilipitisha Mwongozo wa Matumizi ya Mitandao katika Uchaguzi barani Afrika na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania ni Mjumbe katika Jumuiya hiyo, hivyo itakuwa sio jambo jema kutunga Sheria ambayo inakinzana na maazimio hayo.

"Mswaada wa Sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi haijagusia kabisa suala la Matumizi katika Uchaguzi, jambo ambalo limeshathibika kuwa moja ya maeneo yenye changamoto kubwa katika chaguzi zetu," alisema

Alisema ni lazima kuangalia pia athari za teknolojia mpya kama akili mnemba “artificial intelligence” katika Uchaguzi kwa kuwa tayari dunia imekwenda huko.

"Napenda kushauri na kusisitiza Sheria hii ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi uhakikishe inaongezwa Ibara Mpya katika eneo hili la Matumizi ya Mitandao katika uchaguzi sababu Jumuiya ya Tume za Uchaguzi Afrika ambapo Tume yetu ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania ni Mjumbe, alisema.

MAKTABA YA KIJAMII YA MARTHA ONESMO YAFUNGULIWA WILAYANI MWANGA.

 

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda akiongea katika hafla hiyo.

Mwakilishi wa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Abdala Mwaipaya, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga,akizungumza katika hafla hiyo.

Mwanzilishi wa Maktaba jamii ya Martha Onesmo, Jennifer Dickson, (kushoto mwenye Tshirt nyeupe) akitoa maelezo jinsi maktaba hiyo itakavyohudumia wananchi kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda (katikati) na viongozi wengine wa Serikali na Dini wakati wa uzinduzi wa maktaba hiyo uliofanyika katika viwanja vya usharika wa Kisangeni, wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.

Mwanzilishi wa Maktaba jamii ya Martha Onesmo, Jennifer Dickson, (kulia mwenye Tshirt nyeupe), akitoa maelezo jinsi maktaba hiyo itakavyohudumia wananchi kwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda, (wa pili kutoka kulia) wakati wa uzinduzi wa maktaba hiyo uliofanyika katika viwanja vya usharika wa Kisangeni, wilayani Mwanga mkoani Kilimanjaro.wengine pichani ni Askofu wa Dayosisi ya Mwanga Chediel Sendoro na Mbunge wa Jimbo la Mwanga Joseph Tadayo (kushoto).
Baadhi ya wageni waliohudhuria katika hafla hiyo wakifuatilia matukio .

Na Mwandishi Wetu

Maktaba mpya ya kijamii inayojulikana kwa jina la Martha Onesmo, iliyoanzishwa kwa ajili ya kuwahudumia wakazi wa wilaya ya Mwanga, imezinduliwa katika kata ya Msangeni, ambapo hafla ya uzinduzi ilifanyika katika katika viwanja vya kanisa la KKKT usharika wa Kisangeni na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali na wananchi wa eneo hilo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda. Maktaba hiyo imeanzishwa na kijana wa kitanzania anayesoma Chuo Kikuu nchini Rwanda, Jennifer Dickson.

Akiongea katika hafla hiyo,Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, alimpongeza mwanzilishi wa mradi huo Bi. Jennifer Dickson, ambapo alisema maono yake, (ya Jennifer) yatachangia maendeleo ya watu wengi watakaotumia maktaba hiyo.

“Maktaba hii imekuja wakati muafaka ambapo Serikali imekuja na mabadiliko ya mfumo wa elimu yenye lengo la kuboresha elimu ya Watanzania kwa kuwa maktaba itatumiwa na wanafunzi, walimu na wakazi wengine kujiongezea maarifa”. alisema.

Aliongeza, "Jennifer maono yako yametupa matumaini kwa serikali kuwa mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu ni salama kwa sababu ina vijana wabunifu kama wewe; nikuhakikishie wewe na waliohudhuria hafla hii kuwa serikali itafanya kila linalowezekana ili kuhakikisha maktaba hii inakuwa endelevu".
Alisema Serikali imeanza kutekeleza mpango unaolenga kuboresha maktaba zote nchini ili kutoa fursa kwa wanafunzi, walimu na wakazi wengine wa ndani na wanaoishi nje ya nchi kupata ujuzi wa ziada na tayari imetenga takribani shilingi bilioni 2 kutekeleza suala hilo sambamba na kuboresha maktaba 22 katika maeneo mbalimbali nchini lengo likiwa ni kuhakikisha wananchi wanapata maarifa zaidi kupitia maktaba hizo.

Naye Mwanzilishi wa maktaba hiyo, Bi. Jennifer Dickson, alisema ameanzisha maktaba hiyo ili kutimiza ndoto yake ya muda mrefu aliyokuwa nayo kwa miaka mingi ya kuhakikisha wakazi wa vijijini wanafikiwa huduma za maktaba ili waweze kupata maarifa.

"Maktaba hii inayoitwa Martha Onesmo, ni kwa ajili ya kumuenzi bibi yangu, ni ndoto niliyoota tangu nasoma kidato cha sita, ninafuraha kuwa ndoto hiyo imetimia. Maktaba hii pia ni mchango wangu na wale walioniunga mkono, katika kuunga mkono juhudi za serikali zinazolenga kuboresha sekta ya elimu nchini".alisisitiza.

Bi Jennifer, aliendelea kusema kuwa maktaba hiyo ambayo alisema pia ina baadhi ya michango kutoka kwa wanajumuiya wa Msangeni itakuwa kituo cha mafunzo ya ujasiriamali na elimu ya aina nyingine kwa ujumla itakayochangia maendeleo ya taifa na kutoa wito kwa Watanzania wote kujenga tabia ya kutumia huduma za maktaba kujisomea ili waweze kupata maarifa na kuachana na dhana potofu kuwa maktaba ni za wanafunzi, walimu na wasomi pekee.

Alitoa shukrani kwa wafadhili mbalimbali waliomwezesha kutimiza ndoto yake baadhi yake akiwataja kuwa ni pamoja na Bayport Tanzania, Barick Gold Tanzania, Dayosisi ya Mwanga ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT-MD).
Akizungumza katika hafla hiyo Askofu wa KKKT wa Dayosisi ya Mwanga Askofu Chediel Sendoro, alimpongeza Bi Jennifer, kwa ubunifu wake ambao alisema utachangia maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

“Maktaba hii ijapokuwa ipo kwenye jengo la Kanisa itatumika kwa watu wote bila kujali imani zao za kidini, lengo ni kuhakikisha kila mtu anapata fursa ya kujiendeleza na kupata maarifa ya ziada kwa ajili ya maendeleo yake binafsi na taifa kwa ujumla,” alisema.

Aidha aliwapongeza wazazi wa Bi Jennifer Dickson na Dk. Linda Ezekiel, kwa malezi mazuri ya wazazi waliyompa binti yao ambayo yalimwezesha yeye (Jennifer) kuja na maono yenye lengo la kuchangia maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

"Nichukue fursa hii kuwataka wazazi wengine kuiga mfano wa wazazi wa Jennifer; pia niwasihi watoto wengine kuiga mfano wa Jennifer ili taifa liendelee kupiga hatua kupitia vijana wetu", alisema.

Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof Bonaventure Rutinwa, amesema kuwa maktaba hiyo ni miundombinu ya kielimu inayomwezesha mtu wakiwemo watoto wadogo kupata elimu ya ziada kupitia usomaji wa vitabu, ambapo alisema ni vyema watoto wakaanza kusoma. kufahamishwa kuhusu umuhimu wa kutumia maktaba mapema katika hatua za utotoni.

"Tunasoma sio kupata elimu ya shule pekee bali kuboresha maisha yetu kwa ujumla na hii ni moja ya maana halisi ya kuwepo kwa maktaba kuwa;maktaba zimekusudiwa kwa ajili ya watu wote na si kwa ajili ya wanafunzi na walimu pekee",alisisitiza.

Wednesday, January 3, 2024

MBUNGE KOKA APIGA JEKI YA VIFAA VYA MICHEZO MICHUANO YA KIBAFA VIJANA CUP

 


VICTOR MASANGU,KIBAHA


KATIKA kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta ya michezo Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ametoa vifaa  vya michezo ikiwemo jezi 16 na mipira 20  kwa ajili ya michuano ya vijana wenye umri  chini ya miaka 25.


Akikabidhi msaada huo  kwa viongozi wa Chama cha soka Wilaya ya Kibaha (KIBAFA)  katibu wa  Mbunge wa Jimbo la Kibaha mji Method Mselewa  alibainisha  kwamba lengo kubwa la kutoa vifaa hivyo ni kutoa fursa kwa  kuonyesha vipaji na kukuza mchezo wa  soka.

Katika halfa hiyo ya makabidhiano ambayo  imehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Kibafa,pamoja na baadhi ya viongozi wengine wa chama cha mapinduzi (CCM ) kwa lengo la kushuhudia utekelezaji wa ilani katika nyanja ya michezo


"Leo kwa niaba ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini tumekuja kukabidhi vifaa vya michezo kwa uongozi wa soka Wiaya ya Kibaha na tumetoa mipira 20 pamoja na jezi seti  16 ambazo zimegharimu kiasi cha shilingi milioni 3.5 na zitapewa timu ambazo zitashiriki katika michuano hiyo," alisema Mselewa.
Aliongeza kuwa lengo la Mbunge ni kuendea kusaidia vijana wa jimbo lake katika kuendeleza na kukuza michezo mbali mbali katika kata zote 14  ikiwemo mchezo wa soka kwa vijana  wa Jimbo lake la Kibaha mjini.

Mselewa katika hatua nyingine alisema kuwa michuano hiyo ambayo mdhamini wake mkuu ni  Mbunge na kwamba wataendelea kushirikiana bega kwa bega na viongozi wa mpira wa miguu ili kutimiza malengo ya michuano hiyo.

Pia katika hatua nyingine aliwahimiza wacheza na timu zote kuwa na nidhamu na kuzingatia sheria na taratibu zote za mashindano ikiwemo kuzingatia suala la kutozidisha umri.


Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama cha soka Wilaya ya Kibaha (KIBAFA) Robert Munisi  amempongeza Mbunge Koka kwa kuweza kuunga jitihada za serikali katika kukuza sekta ya michezo hususan kwa vijana katika jimbo lake.

"Kiukweli napenda kwa dhati kabisa kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Kibaha kwa kuweza kusaidia sekta ya michezo na amesaidia vifaa hivi kwa lengo la kufanikisha michuano hii ya vijana wenye umri chini ya miaka 25,"alisema Munisi.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji  amesema kwamba kite do alichokifanya Mbunge ni moja kati ya utekelezaji wa ilani kwa vitendo katika nyanza  ya michezo husan kwa vijana.


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha soka Wilaya ya Kibaha (KIBAFA) David Mramba  ambaye pia ni Katibu mwenezi wa Chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani alisema kwamba dhamira ya Mbunge ni kuendeleza vipaji kwa vijana hivyo ni vema kumuunga mkono kwa dhati.


Mashindano hayo yaliyopewa jina la Kibafa vijana Cup  yanatarajiwa  kuanza kutimua vumbi lake rasmi kuanzia Januari 6 mwaka huu katika kiwanja cha Mwendapole  kwa kuzishirikisha time  16 kutoka Jimbo la Kibaha mjini.