ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 19, 2010

MAONESHO YA WATUMISHI WA UMMA YANAYOENDELEA JIJINI MWANZA.

KITI HIKI KILIANZA KUTUMIKA TANGU ENZI ZA UTAWALA WA WAJERUMANI NA KIKATUMIKA NA CHIFU KWA SASA KINATUMIKA KWA HAKIMU MFAWIDHI MAHAKAMA YA MWANZO KATUMBA.

MPANGILIO WA MABANDA CCM KIRUMBA.

KAMA NI UELIMISHAJI, UHAMASISHAJI NA BURUDANI UKO HAPA MWENGE JAZZ BAND.

HAPO JE! CHEZA KAMA UNAMLIA TAIMING NYOKA!!

CHAMA CHA WADAU WA NGOZI.

RAMANI YA SOKO KUU JIPYA LITAKALOJENGWA JIJINI MWANZA.

UBUNIFU NA UFUNDI NDANI YA JKT.

FURNITURE.

BW.CARTHBERT BOMA KAIMU AFISA WANYAMA PORI SERENGETI AKITOA MAELEZO KWA MDAU ALIYETEMBELEA BANDA LAKE.

AFISA UTALII YUSUPH IMORI.

Friday, June 18, 2010

TUHESHIMIANE KATIKA KAZI NA HAYA NDIYO MAJINA SAHIHI.


NA HUU NDIYO UTARATIBU:-

GARDEN BOY - Landscape Executive and Animal Nutritionist

HOUSE MAD - Domestic Operations Specialist

TYPIST - Printed Document Handler

MESSENGER - Regional Business Communications Conveyer

WINDOW CLEANER - Transparent Wall Technician

TEMPORARY TEACHER - Associate Tutor

TEA BOY - Refreshments Overseer

GARBAGE COLLECTOR - Public sanitation Technician

WATCHMAN - Area Theft Prevention and Surveillance Officer

THIEF - Wealth Redistribution Officer

DRIVER - Automobile propulsion Specialist

RECEPTIONIST - Office Access Control Specialist

COOKER - Food Technician and Preparation Officer

NAOMBA KUWAKILISHA
AKSANTENI.

Thursday, June 17, 2010

WIKI YA UTUMISHI WA UMMA JIJINI MWANZA.

HUYU NDIYE MKURUGENZI WA KIHELYA AUTO PARTS WAKALA WA SERIKALI WAUZAJI WA PEMBEJEO ZA KISASA ZA KILIMO.

UNAYO KILA SABABU YA KUFIKA NDANI YA UWANJA WA CCM KIRUMBA, TAFADHALI UTAKAPO TEMBELEA KIHELYA KUJIONEA MAPINDUZI KTK KILIMO.

MAPOKEZI MAZURI UTAYAPATA TOKA KWA WAJUZI WENYE UTAALAMU WA PEMBEJEO.

BIDHAA ADIMU.

KTK MAONESHO HAYA MAGONJWA YA MIMEA YANAYAAINISHA KISHA DAWA GANI KUTUMIKA INABAINISHWA.

NI ZAIDI YA MAONESHO.

NI MASWALI YAKO TU! MAJIBU NA MAELEZO NA MAELEKEZO YANAKUSUBIRI.

KUNA MENGI MAZURI YANAYOENDELEA KATIKA UWANJA WA CCM KIRUMBA JIJINI MWANZA NAYO YANAIHUSU WIKI YA MAADHIMISHO YA UTUMISHI WA UMMA. PICHA NA HABARI ZAIDI ZAJA....

Wednesday, June 16, 2010

HAPPY BIRTHDAY MTOTO MARIAM.

Nimepokea picha toka kwa mdau wa blog hii mamaa Ester wa paleee... za borzdei ya mwanae ENDELEA:-
MTOTO MARIAM KHERI MCHUME AMETIMIZA MWAKA AMBAPO ALIFANYIWA SHEREHE SAFI. PICHANI AKIWA AMESHIKILIWA NA MAMA YAKE ESTER.

MARIAM AKIWA NA RAFIKIYE BRITNEY

RAFIKIZE MARIAM WAKIMWIMBIA KALE KA WIMBO.

HAYA NDO MAMBO, FURAHIA UTAMU WAKE!

MARIAM NA BABA YAKE.

HONGERA MTOTO MARIAM KWA KUTIMIZA MWAKA MMOJA MUNGU AWAPE NGUVU, HEKIMA NA BUSARA WAZAZI WAKO, WAKULEE KATIKA MAADILI MEMA SAMBAMBA NA KUIZINGATIA ELIMU.

SARAKASI ZA LUCH YA MUJINI.

MJOMBA AKITIA MAJI SUFURIANI.


MJOMBA AKITIA UNGA MARA BAADA YA MAJI KUCHEMKA


AMJOMBA AKISONGA NGUNA.

JIPANGUSEEE... KISHA MEZA MATE!

BAADA YA MITIKASI YA JANA HATIMAYE KUTIZAMA SOKA LINALOPIGWA KTK ARDHI YA AFRIKA NA KUHUSIKA NA SHANGWE ZAKE (SIUNAJUA TENA DUBAIII') ASUBUHI ILIKAA SAWA ZAIDI PALE NILIPOSTUA NA KITU CHA SILINDER HEAD YA FISH AINA YA SATO. PAAAP! NIKAFUNGUKA MZAZI.

Tuesday, June 15, 2010

SHANGWE!

KATIKA POZI LA FURAHA BWANA HARUSI KIZITO I. BAHATI ALMAARUFU KWA JINA LA SOSHO KIZITO NA BI. BERNADETA K. CYRIL WA JIJINI MWANZA.

NDOA TAKATIFU ILIFUNGWA TRH 29 MAY 2010 KTK KANISA LA RC BUGANDO.

PICHA YA KUPENDEZESHA ZAIDI.

KUNA VITU VYA KUSAHAU LAKINI SIO WIMBO WA KWANZA WA MAHARUSI WA KUFUNGULIA MZIKI, KWANI HUWA UNACHAGULIWA NA WAHUSIKA WENYEWE KAMA WIMBO MAALUM NA MARA ZOTE UNA UJUMBE KWAO.

MAHARUSI PEMBEZONI MWA RASLIMALI ZA KITALII. LAKO JICHO CHUNGUZA!

TWAP! BWANA NA BIBI HARUSI WAKIUKATA UTEPE KUASHIRIA UFUNGUZI RASMI WA SHEREHE ILIYOFANYIKA KTK UKUMBI WA NEW MWANZA HOTEL.

NILISHE NIKULISHE NI ISHARA YA UPENDO.

RAHA YA SHEREHE NGOMA, WACHA WATU WALIZUNGURUSHE PALE KATI.

MAHARUSI NA WAZAZI.

KAMA MAUA YAPENDEZAYO BUSTANINI, MAHARUSI NA SAFU NZIMA.

NO PARKING!

IMEZOELEKA KWA WENGI KTK MATEMBEZI,MASHOPING NA KADHALIKA KUTEMBEA NA MBWA & PAKA au BATA (niliishuhudia ktk Fiesta). SASA HII KALI NILIIFUMA JANA KWA JAMAA MMOJA ALIYEKUJA KWA MKWARA BENKI KUWEKA FEDHA. AKIHOFU KUFANYA USUMBUFU NDANI YA BENKI (ILE MEEE! MEEE!) AKATINGA ENEO HILO, KISHA AKAMFUNGA MBUZI WAKE PALE PALE KWENYE KIBARAZA CHA UZIO TUNAPOPENDA KUKAA WAKATI TUKISUBIRI FOLENI YA ATM TUKAPIGWA STOP.

Monday, June 14, 2010

SIKU YA WACHANGIA DAMU DUNIANI KITAIFA MWANZA YAFANA.

WORLD BLOOD DONORS DAY.
WAKAZI WA JIJI LA MWANZA LEO WAMEKUTANA KATIKA VIWANJA VYA GHAND HALL KUADHIMISHA SIKU HII PAMOJA NA KUSHIRIKI ZOEZI LA UTOAJI DAMU SALAMA. PICHANI MC WA MAADHIMISHO HAYO YALIYOFANYIKA KITAIFA MWANZA AFISA UHUSIANO WA JIJI BW JOSEPH MLINZI AKIHUSIKA NA RATIBA.

VIONGOZI WA SIASA, KAMATI YA MAANDALIZI, VIONGOZI WA DINI NA WAGENI WAALIKWA MEZA KUU.

KAULI MBIU YA MAADHIMISHO YA MWAKA HUU NI "WACHANGIAJI DAMU VIJANA, DAMU MPYA KWA DUNIA YA LEO" NAO VIJANA WALIWAKILISHA KISAWA SAWA.

BURUDANI NAYO ILIKUWA NA SEHEMU YAKE.

MSTARI KUELEKEA KATIKA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU. TAKWIMU ZINAONESHA KUMEKUWEPO NA ONGEZEKO LA UKUSANYAJI WA DAMU MWAKA HADI MWAKA HALI INAYOPELEKEA UHAKIKA WA KUWAPO KWA DAMU YA KUTOSHA MAHOSPITALINI.

KABLA YA MWANANCHI KUCHANGIA DAMU, SAMPLE YA DAMU HUCHUKULIWA NA KUPIMWA NDIPO MAAMUZI YA KUTOA AU KUTOTOA HUFANYIKA.

WAWEZA KUWA NA DAMU SAFI LAKINI AFYA IKAWA NA UTATA, HIVYO LAZIMA TUPIME PRESHA NA MENGINE...

NCHINI PETU VIFO VINGI HUTOKEA KUTOKANA NA UKOSEFU WA DAMU, MOJA YA MAKUNDI YANAYOATHIRIKA ZAIDI NI AKINA MAMA WAJAWAZITO WAKATI WA MIMBA NA KUJIFUNGUA. KWA ZOEZI KAMA HILI VIFO VINAWEZA KUZUILIKA.

ASKARI WA JESHI LA WANANCHI TANZANIA (JWTZ) NAO WALIJITOKEZA. WAKATI NIKICHUKUWA PICHA NIKAULIZA SWALI KIMTINDO:-
"AKITOKEA MKUU HAPA YALE MAMBO YETU YA SALUTI INAKUWAJE?"
"HA-HA-HA-HAAAA!!!!" (WAKAANGUA KICHEKO)


BAADHI YA VIJANA WENYE SIFA ZA KUCHANGIA DAMU WALIO HUDHURIA ZOEZI HILO WAKIPONGEZANA KWA STORI HUKU WAKILAMBA CLUCOSE.

PAMOJA INAWEZEKANA CHANGIA DAMU MARA KWA MARA, OKOA MAISHA.